1. Shein azungumza na Magufuli Ikulu ya Dar es Dar Salaam
Hii ni habari kubwa na inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wahttp://mjengwablog.com
Katika hali inayoendelea ya mtanzuko wa kisiasa visiwani inaposemwa, kuwa Maalim Seif ameridhia Dr Shein awe mwenyekitini wa Kamati Maalum iliyoanza mazungumzo Novemba 9 huku naye Seif akiwa Makamu wake, basi, ni tumaini kwa Zanzibar- Hope For Zanzibar.
Maana, kamati hiyo ni jopo la viongozi wenye busara na hekima- Eminent persons. Ni viongozi aina ya Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu, Abeid Karume, Rais Mstaafu, Dr Salmin Amour, Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu. Watanzania wana imani kubwa, kuwa sasa, kupitia Kamati hiyo maalum, kutapatikana muafaka utakaoifanya Zanzibar isonge mbele kutoka ilipo sasa, kama visiwa vya watu wamoja na walio kwenye Muungano na ndugu zao wa Bara.
Ni habari njema na yenye kuonyesha mfano kwa dunia, kuwa Watanzania tunaweza kuyamaliza ya kwetu kwa njia ya mazungumzo bila hata kuwaita wapatanishi kutoka nje. Na kwamba hayo mataifa ya Magharibi yasitumie kutoelewana kwetu kupenyeza hila zao za kutugawa, na wakati mwingine bila soni, kutumia karata yao ya misaada kushinikiza matakwa yao, kwa maslahi yao.
2. " Mwakyembe akianza Katiba tu, nitasema".
Hii ni habari inayopewa nafasi ya pili. Ni kwa vile inarudisha mezani ajenda ya Katiba Mpya.
3." Msimtwishe Magufuli mzigo wa wauza ' unga'"- Askofu Chengula.
Ni habari inayochukua nafasi ya tatu. Tatizo la madawa ya kulevya ni janga kwa taifa, na hapa Askofu Chengula wa Jimbo la Mbeya anawahimiza wananchi kushiriki mapambano na kwa kwamba kupambana na wauza unga si jukumu la Rais peke yake.
Hizo ni habari tatu kubwa kwa siku ya leo kwa mujibu wa mtandao wahttp://mjengwablog.com , ukitembelea mjengwablog.com, utakutana pia na habari kubwa ya michezo kwa siku ya leo, na katuni bora kwa siku ya leo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment