pole zake, R.I.P
On Tuesday, September 22, 2015 6:58 AM, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
Innaillah wainnaillah rajuun. Kiwasila ikiwa ni kweli imefikia hatua hiyo ya kutokwa na haja ktk hadhara huo ni mtihani tena mkubwa. Yarrabi tunusuru waja wako na mrehemu huyu mzee kwa kumpa siha njema.
On Sep 22, 2015 12:41 AM, "Jovias Mwesiga" <ngonzy@gmail.com> wrote:
-- Huu utumwa wa mzungu ndo mwenye kuwaza sahihi mtoa Mada umenitoa hamu ya kusoma ulichotaka kuandika.Utumwa wa fikra ni kitu kibaya basi katuletee wazungu watusaidie kutupa rais .On Sep 21, 2015 9:57 AM, "fadhil fadhil" <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:--KiwasilaWanakuelewa ila njaa wameitoa tumboni na kuipeleka kichwani wameharibu akiritukutane october 25On Sep 21, 2015 1:35 PM, "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:--
Wampumzishe tu Lowasa. Kama ningekuwa nduguye-ningeomba UKAWA na Chadema wampumzishe alinde afya yake. Wanampa shinikizo la mwili na akili wakati ni mgonjwa. Haya sasa Video zimezagaa mitandaoni jinsi mgombea alivyopata haja jukwaani akakimbizwa toilet kubadilishwa nguo. Mkewe yupo wapi asitetee huyu baba akapumzika. Stress wampayo ni kubwa wao mradi mkono uende tumboni-wachukue nchi. WaTZ ni nduma kuwili sisi. Si unaona wananchi wanavyouza majumba kariakoo, magomeni na maeneo mengi kwa mabilioni, kuvamia mabwawa ya kinyesi na maeneo hatarishi na wanatesa familia hasa watoto. Kutwa vijiweni na kutupa malundo ya uchafu katika mitaro ya wazi na kuingiza ndani ya mifereji waliyoiba mifuniko. Maji machafu ya kinyesi yanatoka majumbani kwao na kuzalisha mainzi na kipindupindu kinazidi kupamba moto. Tunalaumu serikali kwa uchafu huo tutupao mchana na usiku, kwa kukataza biashara ya vyakula maeneo machafu na katika hali ya uchafu. Tunakufa sisi na jamaa zetu
lakini hatubadiliki tunalaumu third part kwa kipindupindu. huyo Sumaye hajitambui alisema nini huko nyuma na sasa anasema nini.Bila ya shaka wamempora mashamba aliyojilimbikizia alipokuwa kiongozi sasa hasira zake anaziweka kumuunga mkono yule aliyemshutumu zamani mradi tu aipinge serikali ya CCM. Inakuwa kama ile moja niliyoiona 1974 kijiji cha Mhenda Kilosa-mume alimpiga mke kisha akamvua nguo na kumpanua miguu pande mbili kumdhalilisha. Tuliokuwepo tulishangaa na kusikitisha sana lakini wakati ule mambo ya haki za wanawake, jinsia na deski maalum hayakuwepo. Mila na ujamaa ulishika hatamu. Cha kushangaza-kesho yake tuliwaona wakiwa wameongozana kama mume na mke baada ya kumfedhehesha vile mpaka watu kumuona utupu wake mke. Leo katika siasa ndio hii. Ulimtukana au kumkashifu ila ili uishi (survival) unamkubatia. Ni kama wafanyavyo ISIS na Al gaeda-Choma makanisa, kata vichwa wakistru na wasiokuunga mkono kisha unapokuwa umezidiwa nawe nyoa madevu,
vibadili mavazi-kimbilia Itali na Roma kwa Papa, Greece, Australia, Hungary, Ujerumani for survival!!-Huko kuna bendera na katiba zenye misalaba. Lakini wanasema- We want goodlife, education, peace!!-Survival!! Hapa ni survival tu Ukawa iwe na liwe. jamaa wanamtesa. Muoneenu huruma akina Mollel huyo EDO.
--------------------------------------------
On Mon, 21/9/15, 'Mpambo R.' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Upatu, Deci, Babu Loliondo na sasa Edward Lowassa!
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>, "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 21 September, 2015, 12:34
Sent
from Yahoo Mail on Android From:"'mpombe
mtalika' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date:Mon, Sep 21, 2015 at 12:30
Subject:[wanabidii] Upatu, Deci, Babu
Loliondo na sasa Edward Lowassa!
Upatu, Deci, Babu
Loliondo na sasa Edward Lowassa!
Johnson
Mbwambo
Kwa nini nisiamini
tuwavivu wa kufikiri?
NIANZE kwa
kuomba radhi wasomaji wangu kwamba katika sehemu
ya mwisho ya makala yangu ya toleo lililopita nilifanya kosa
la kiufundi kwa
kukitaja chama cha Zitto Kabwe kuwa ni ADC Wazalendo.
Nilichomaanisha ni ACT
Wazalendo. Nakiomba pia radhi chama hicho kwa kosa
hilo.
Mengine yote
niliyozungumza kuhusu chama hicho kipya kwamba
kama hakitatetereka kimwelekeo miaka si mingi kitakuwa chama
mbadala wa Chadema
katika siasa za Tanzania, yanabaki kama yalivyo.
Hayo pembeni,
naomba leo nirejee makala niliyopata kuandika
huko nyuma kuhusu utafiti uliowahi kufanywa ulioonyesha ya
kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi duniani ambazo watu wake wana bongo zenye
uwezo mdogo wa
kufikiri (IQ).
Nakumbuka
makala ile iliibua mjadala mkubwa mitandaoni; huku
baadhi wakinitumia sms za matusi na kejeli kana kwamba mimi
ndiye niliyefanya
utafiti huo. Nilichokieleza wakati huo, na ninachotaka
kukirudia leo ni kwamba,
kwa namna Watanzania tunavyoenenda, yawezekana Wazungu
waliofanya tafiti hizo
hawakuwa mbali sana na ukweli!
Hebu tafakari
yafuatayo: Miezi miwili na ushee iliyopita
Edward Lowassa aliulizwa na wahariri wa magazeti iwapo
ataihama CCM kama
haitamchagua kugombea urais mwaka huu. Jibu lake lilikuwa
kwamba hatahama CCM
kamwe kwa sababu ilimlea, na kwamba huyo ambaye hamtaki
ndani ya CCM ndiye
akihame chama hicho!
Hata hivyo,
kabla hata mwezi haujakatika Lowassa akakihama
chama hicho na kujiunga na chama cha Upinzani cha Chadema,
na kikamteua
kugombea urais, na sasa maelfu ya vijana wanamshabikia!
Kimsingi, Lowassa
aliongopa katika jibu lake lile na taswira aliyojijengea ni
ya mtu asiyeaminika
katika anayosema na ambaye ni kigeugeu.
Ingekuwa ni
Wazungu au ingekuwa sisi ni watu wenye kufikiri
sawasawa, tusingemshabikia Lowassa kwa maelfu katika mbio
zake za urais kwa
sababu ni mtu mwongo, kigeugeu na asiyeaminika – mtu
asiyeweza kusimamia maneno
yake mwenyewe.
Lakini kwa
uwezo wetu mdogo wa kufikiri, baadhi yetu
Watanzania 'tunamzawadia' mtu huyo kwa kumuunga mkono
kwenye kampeni yake ya
kuusaka urais kwa udi na uvumba!
Uongo na
ukigeugeu kama huo pengine ungevumilika kama nafasi
yenyewe anayowania si urais. Lakini urais ni kazi yenye
heshima, utukufu,
uadilifu nk. Ni kazi ambayo haimfai mtu mwongo na
asiyesimamia maneno yake
mwenyewe.
Lakini kwa
hapa Tanzania hilo halionekani kuwa ni upungufu
nyeti kwa mtu anayewania kuingia Ikulu. Vijana wetu
hawajiulizi: Kama huyu
alidiriki kutudanganya jana, kwa nini asiendelee
kutudanganya hata leo au hata
baada ya kuingia Ikulu. Tutamwini vipi katika hayo anayodai
kuwa atatutendea
akiingia Ikulu kama huko nyuma aliwahi kutudanganya kwa
kushindwa kusimamia
maneno yake mwenyewe?
Kule Uingereza
kuna waziri mmoja wa zamani (simkumbuki jina)
alishinikizwa na umma kujiuzulu uwaziri kwa kutokuaminika.
Waziri huyo alikuwa
akiusifia mno mfumo wa elimu wa shule za umma za Uingereza
uliokuwa ukikosolewa
na wananchi, lakini baadaye ikagundulika kwamba licha ya
kuusifia sana, wanawe
walikuwa wakisoma kwenye shule binafsi (private school).
Ilibidi ajiuzulu.
Lakini hapa
kwetu Tanzania hali ni tofauti kabisa. Mtu
(Lowassa) anadanganya waziwazi na anaonyesha si mtu wa
kusimamia maneno yake
mwenyewe, lakini maelfu ya Watanzania wanamuona kuwa ndiye
anayefaa kuwa rais
wao! Bado wanaamini maneno yake kuwa atawaondolea umaskini!
Kama huo sio uwezo
mdogo wa kufikiri wa Watanzania, ni nini?
Katika hilo,
Lowassa anao 'wasanii' wengine wawili wa
kisiasa wanaokamilisha ile listi ninayoweza kuiita The Three
Musketeers –
nawamaanisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri
Mkuu mstaafu,
Frederick Sumaye.
Nianze na
Mbowe. Mbowe huyu ni miongoni mwa viongozi wa
Chadema ambao walizunguka nchi nzima wakimtuhumu Lowassa
kuwa ni fisadi mkubwa.
Mara ya mwisho Mbowe kufanya hivyo ilikuwa wakati Lowassa
akitafuta saini za
kuungwa mkono ili CCM imteue kugombea urais. Mbowe akasema
Lowassa ni fisadi na
wananchi hawastahili kumchagua kuwa
rais wao!
Leo hii, Mbowe
huyo huyo anapita mikoani akiwa na Lowassa
akiwahamasisha
Watanzania wamchague Lowassa kuwa rais
mpya wa nchi. Tena
anamkampenia bila soni wala kupepesa macho - anajitia
hayakumbuki maneno yake
hasi aliyoyahubiri huko nyuma dhidi ya Lowassa.
Na Watanzania,
kwa uwezo wetu mdogo wa kufikiri,
tunamshangilia huyo Mbowe bila hata kujali kuwa ni mtu
mwongo, laghai wa
kisiasa asiyeweza kusimamia maneno yake mwenyewe
anayoyatamka! Na wala
hatujiulizi: Kama alitudanganya jana kuhusu Lowassa, kwa
nini tusiamini kuwa
hata leo anatudanganya pia kuhusu huyo huyo Lowassa?
Hadithi ni
hiyo hiyo kwa Frederick Sumaye. Miezi kadhaa
iliyopita aliuambia umma wa Watanzania kwamba kama Lowassa
(aliyemwita fisadi)
atapitishwa na CCM kuwania urais, yeye Sumaye ataondoka CCM.
Sasa, ni kweli
aliondoka CCM lakini mbona sasa anampigia kampeni Lowassa;
ilhali alimwita
fisadi asiyestahili kupitishwa na CCM kugombea urais?
Na sisi
wananchi katika uzuzu wetu na IQ zetu ndogo
tunampigia makofi Frederick
Sumaye wakati akimnadi Lowassa; ilhali
tunajua yeye
Sumaye ni mtu aliyetuongopea kuhusu Lowassa. Badala ya
kumkasirikia na kumzomea
kwa ulaghai wake wa kisiasa, tunamshangilia kama vile ni
shujaa eti tu kwa
sababu kahama CCM!
Jamani, si
Sumaye huyo huyo ambaye alipokuwa waziri mkuu
aliwaambia wafanyabiashara wa Moshi kama wanataka mambo yao
yawanyookee wahamie
CCM! Leo Sumaye kama atakwenda Moshi kumkampenia Lowassa,
safari hii atawaambia
nini tena wafanyabiashara wale wa Moshi? Atajipa ujasiri wa
kuwaambia kwamba
wakitaka mambo yao yawanyookee wahamie Chadema?! Na
wanapaswa wamwamini kama
alishawadanganya mwanzoni?
Ndugu zangu,
ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba 'The Three
Musketeers' – Lowassa, Mbowe na Sumaye ni watu waongo na
wasioaminika katika
wasemayo, na kwa mujibu wa Rais wa zamani wa Marekani,
Dwight Eisenhower,
hawastahili kuongoza hata genge la wahuni.
Eisenhower
alipata kutamka hivi: The supreme quality for
leadership is unquestionably integrity. Without it, no real
success is possible
whether it is on a section gang, a football field, in an
army or in an office
(sifa kuu ya uongozi ni uadilifu, unyoofu na usema kweli
usio na shaka. Bila
hivyo hakuna mafanikio yoyote ya maana yanayoweza kupatikana
iwe ni katika
genge la wahuni, viwanja vya michezo, jeshini au
ofisini.)
Kwa mujibu wa
Eisenhower, hata genge la wahuni linamhitaji
kiongozi mkweli anayesimama katika maneno yake mwenyewe
anayoyatamka! Sasa,
kama hata genge la wahuni halimhitaji kiongozi mwenye
udhaifu huo, sembuse
Ikulu yetu? Ndo maana naamini uwezo wetu wa kufikiri una
walakini.
Lakini si
hivyo tu. Lowassa na Sumaye tunawashangilia pia
wakisema kwamba wataleta mabadiliko Tanzania. Ni kwa sababu
ya uvivu wetu wa
kufikiria tunasahau ya kuwa wote wawili walikuwa na nyadhifa
za juu serikalini
kwa zaidi ya miaka 20 ikiwa ni pamoja na kuwa mawaziri
wakuu, na hakuna
mabadiliko yoyote waliyoyapigania wakiwa madarakani.
Katika miaka
yote hiyo zaidi ya 20 ya utendaji kazi wao
serikalini (walianza wakiwa vijana mpaka wakazeekea humo
humo serikalini)
hakuna mabadiliko yoyote waliyoyapigania na wakakwamishwa,
lakini leo
wameshazeeka na wameshaondoka serikalini baada ya
kujitajirisha, na ndiyo
wanaahidi kuwa wataleta mabadiliko, na sisi
tunawaamini!
Kama ni uozo
wa CCM na serikali yake mbona nao kwa zaidi ya
miaka 20 walikuwa sehemu ya uozo huo walipokuwa viongozi
waandamizi serikalini?
Kwa nini leo baada ya juhudi zao za kuutaka urais kugonga
mwamba ndio
wanakumbuka kwamba kuna mabadiliko yanahitajika kuletwa
Tanzania? Walikuwa wapi
miaka yote hiyo? Kwa nini hatuuoni ulaghai ndani ya ahadi
zao hizo za kuleta
mabadiliko nchini!?
Kwa hakika,
hili la Lowassa ndilo linalonitia shaka zaidi
kuhusu viwango vya IQ zetu. Baadhi yetu tumejitahidi mno
kuwaelemisha vijana wa
nchi hii juu ya nakisi kubwa ya uadilifu ya Lowassa
inayomfanya asistahili kuwa
rais wetu, lakini vijana badala ya kuzipembua hoja hizo wao
hukimbilia kwenye
kutukana tu na kudai kuwa tumehongwa na CCM.
Dk. Slaa, kwa
mfano, amejaribu mno kuanika hadharani kila
kitu (tena kwa data na ushahidi kibao) kuhusu tuhuma za
ufisadi wa Lowassa
ikiwa ni pamoja na kuidanganya Tume ya Maadili ya Viongozi
kuhusu mali anazomiliki,
lakini vijana wetu kwa IQ zao ndogo, hawana hata muda wa
kupembua na kutafuta
ukweli juu ya hoja za Slaa. Badala yake wanachokimbilia wao
ni matusi na kudai
eti kahongwa na CCM!
Kwa miaka
kadhaa sasa Lowassa ameandamwa na kashfa ya
mkataba wa Richmond ambao unailazimisha Serikali kuilipa
Dowans (kampuni hewa)
kiasi sha Shilingi takriban bilioni 93 – fedha za
walipakodi.
Utetezi wake
ni kwamba alijua kuwa huo ni mkataba wa
kifisadi lakini aliutia saini eti kwa kulazimishwa na
mamlaka za juu (bila
shaka akimaanisha Rais Kikwete). Kama hivyo ni kweli, mbona
hakukataa kuusaini,
na kisha kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu?
Angeweza
kumwambia Rais hivi: "Mheshimiwa Rais, huu ni
mkataba wa kifisadi utakaowaumiza Watanzania, na kama
unanilazimisha kuutia
saini, mimi najiuzulu uwaziri mkuu, na hivyo teua waziri
mkuu mwingine
atakayetia saini mkataba huu wa kifisadi."
Kama Lowassa
angefanya hivyo, hadithi leo ingekuwa tofauti;
maana angelionekana kama shujaa aliyekubali "kufa
kidogo" kutetea maslahi ya
Watanzania. Lakini sivyo alivyofanya; kwani aliusaini na
akaendelea na uwaziri
mkuu wake. Ni hivi karibuni tu baada ya kutemwa na CCM
kugombea urais ndipo
alipoanza kudai eti alilazimishwa na Kikwete kuusaini! Uongo
mtupu!
Ni Watanzania
wenye IQ ndogo ndiyo wanaouamini utetezi wake
huo, lakini wasio wavivu wa kufikiri wanajiuliza: mbona
hakujiuzulu uwaziri
mkuu wakati huo kama ni kweli alilazimishwa na Rais Kikwete
kutia saini mkataba
huo wa Richmond?
Historia ya
chama alichojiunga nacho cha Chadema inaonyesha
kuwa mwasisi wake, Edwin Mtei alijiuzulu uwaziri wa fedha
wakati Mwalimu
Nyerere alipomshurutisha ayakatae mapendekezo ya Benki ya
Dunia ya kurekebisha
uchumi wa Tanzania.
Mbona Lowassa
hakufuata nyayo za Mtei kwa kujiuzulu uwaziri
mkuu siku alipolazimishwa na Kikwete kusaini mkataba wa
Richmond? Hivi kweli
vijana wetu hawauoni ulaghai uliomo kwenye utetezi huo wa
Lowassa kuhusu kashfa
hiyo ya ufisadi ya Richmond?
Kuna hili
suala jingine analowadanganya maelfu ya vijana
wanaomshabikia kwamba eti akiwa rais ataendesha
'mchakamchaka' wa maendeleo
nchini. Hivi hao vijana hawaoni (hata kwenye TV) kuwa
Lowassa ana matatizo ya
kiafya kiasi kwamba hawezi kuhutubia mkutano wa kampeni kwa
muda mrefu, na hata
kushika tu kipaza sauti kwake ni tatizo?
Hivi mtu
mwenye umri mkubwa na mwenye matatizo ya afya ya
kiasi hicho anawezaje kuahidi 'mchakamchaka' wa
maendeleo? Mbona huo
'mchakamchaka' hatukuuona katika miaka zaidi ya 20 ya
utumishi wake serikalini
hasa alipokuwa kijana na mwenye afya nzuri? Mbona hata kule
Monduli alikokuwa
mbunge kwa miaka 20 hatujaona 'mchakamchaka' wa
maendeleo alioufanya? Hivi hata
hilo vijana wetu hawalioni?
Sumaye naye ni
hivyo hivyo. Anasimama majukwaani na
kuzungumza lugha ya
Chadema na ya Ukawa ya
'kuwakomboa' vijana kiuchumi. Hivi
hawa vijana wetu hawajui kwamba Sumaye anamiliki hekta
40,000 za ardhi kule
Mvomero alizozitwaa akiwa waziri mkuu na mpaka leo
hajaziendeleza; ilhali
vijana wa Mvomera hawana mashamba?
Kama kweli
dhamira yake ni ya kweli, mbona haanzi kwa
kutangaza kwamba anazitoa hizo hekta 40,000 za ardhi
anazozimiliki ili
zigawanywe kwa vijana wasio na ajira nchini na wanaotafuta
maeneo ya kulima?
Angeanza na hilo, tungemuamini; maana angekuwa amekubali
"kufa kidogo" kwa
ajili ya vijana wa Tanzania! Kinyume cha hicho, anachofanya
ni usanii mtupu, na
ni wavivu tu wa kufikiri ndiyo wanaoweza kumwamini.
Hivi taifa
hili la kesho (tunaambiwa vijana ni taifa la
kesho) litakuwa taifa la namna gani kama lina vijana wenye
IQ ndogo kiasi hicho
cha kutouona ulaghai wa watu kama hao? Yaani hatuna vijana
ambao hawana uwezo
wa kuchanganya akili za kuambiwa na akili zao wenyewe na
kuung'amua ulaghai
uliomo katika ugombea urais wa Lowassa?
Kwa ufupi
ndugu zangu, japo si jambo jema kulisema lakini ni
lazima lisemwe. Jambo hilo ni kwamba sisi Watanzania ni
wavivu wa kufikiri, na
tunapenda kufuata mambo kwa pupa na kwa mkumbo bila
kufikiri, na mwisho wake
mara nyingi hauwi mwema kwetu.
Kinachosikitisha na kukatisha tamaa ni
kwamba hata wenzetu
wengine wanapojaribu kuchokonoa bongo zetu na kutushawishi
tufikirie kidogo
kabla ya kuchukua maamuzi, tunawapuuza na kuwakejeli lakini
mwishowe hatima
inakuwa ni wao "kulizwa".
Labda msomaji
nikukumbushe mambo mawili au matatu hivi
kuthibitisha hicho ninachokisema. La kwanza ni lile suala la
moto wa Upatu (pyramid
scheme) uliowaka Tanzania mwaka 1992. Mtakumbuka kuwa baadhi
ya Watanzania
wachache waliona mapema ulaghai ndani ya mpango huo na
walijaribu kuwaelemisha
wananchi kuwa watapoteza pesa zao.
Nini
kilitokea? Kilichotokea ni kwamba wananchi walikataa kupima
hoja zilizotolewa, na badala yake wakamiminika kwa maelfu
kuwekeza pesa za
akiba zao za maisha katika Upatu ule. Na mwisho wa yote
mpango huo uliporomoka
kama ilivyobashiriwa, na maelfu ya Watanzania wakapoteza
fedha zao hizo!
Katika hali ya
kawaida ya wananchi wenye IQ nzuri,
usingelitaraji ulaghai kama huo ujitokeze tena baadaye na
kushabikiwa tena na
maelfu ya watu. Lakini ndivyo ilivyotokea tena hapa Tanzania
kwani mwaka 2012
'upatu mpya' kwa jina la DECI uliibuka, na Watanzania
kwa maelfu wakawekeza
tena fedha zao licha ya kuonywa tena na wachambuzi walioona
ulaghai wa mpango
huo sawa na ule wa upatu wa mwanzo.
Nini
kilitokea? Maelfu ya Watanzania 'wakalizwa' tena kwa
kuibiwa pesa zao chini ya upatu huo mpya kwa jina la DECI.
Yaani Watanzania wale
wale 'waliolizwa' kwa kupoteza fedha zao kwenye Upatu
'wakalizwa' tena fedha
zao kwenye DECI. Ni kwa nini tusihoji kwanza mambo, na
badala yake tukimbilie
kwa maelfu kwa kufuata mkumbo tu? Kama sababu si IQ zetu
kuwa ndogo, ni nini?
Mfano wa tatu
ni suala lile la Kikombe cha Babu wa Loliondo
mwaka 2011. Binafsi nilijitahidi sana, kupitia safu hii,
kuwatahadharisha
Watanzania juu ya ulaghai uliokuwemo katika 'tiba' ya
kikombe hicho cha Babu wa
Loliondo aliyedai kaoteshwa na Mungu.
Juhudi zangu
hizo zilipokewa na matusi na kejeli kama
ninayoyapokea hivi sasa ninapojaribu kuwatahadharisha
Watanzania juu ya urais
wa Edward Lowassa. Maelfu kwa maelfu ya Watanzania, wakiwemo
viongozi, wakaenda
Loliondo kufuata kikombe cha Babu.
Nini kilitokea
baadaye? Kilichotokea baadaye ni kwamba
maelfu ya wagonjwa wa sukari na ukimwi walipoteza maisha yao
kwa kuacha sindano
za insulin na vidonge vya ARVs baada ya kunywa kikombe cha
Babu. Baadaye,
ikadhihirika kwamba kumbe Kikombe cha Babu kilikuwa ulaghai
mtupu! Wale walionikejeli
na kunitukana mpaka leo wanaona haya nikikutana nao!
Kwa ufupi,
kama Watanzania wasingekuwa wavivu wa kufikiri
wangelizichambua hoja zilizotolewa na Watanzania wenzao
dhidi ya pyramid
schemes za Upatu na DECI na pia tiba ya kikombe cha Babu wa
Loliondo. Na kama
wangefanya hivyo, wangeliona ulaghai uliomo ndani yake na
"wasingelizwa" kwa
maelfu kama "walivyolizwa".
Sasa, nakiona
kile kilichotokea kwenye Upatu, DECI na
Kikombe cha Babu wa Loliondo – yaani kufuata mambo kwa
mkumbo bila kutafakari
kikitokea pia katika suala hili la mbio za urais za Edward
Lowassa. Maelfu
wanamfuata bila kujihoji na kujitambua.
Yaani, pamoja
na juhudi zote za kina Slaa na kina sisi
(ambao wala si wana CCM) kujaribu kuwatahadharisha
Watanzania kuhusu hatari ya
urais wa Lowassa, bado maelfu ya vijana wanamfuata kwa
maelfu ki- mkumbo bila
kwanza kufikiri, kutafiti au kuusaka ukweli wa hoja
zinazotolewa dhidi yake.
Kuanzia Upatu,
DECI, kikombe cha Babu wa Loliondo, na sasa
Lowassa, Watanzania tunadhihirisha kwamba sisi ni watu wa
kufanya mambo kwa
kufuata mkumbo, na hatima ya watu wanaofuata mkumbo bila
kwanza kutafakari ni
"kulizwa" . Je, hiyo inathibitisha kwamba IQ zetu
Watanzania ni ndogo kama
tafiti za Wazungu zinavyodai?
Rais mstaafu
Benjamin Mkapa aliwahi kutamka maneno
yaliyowaudhi Watanzania wengi ambayo leo nikiyatafakari
naona yalikuwa na
ukweli wa kiasi fulani ndani yake. Alisema sisi Watanzania
ni wavivu wa
kufikiri. Rais Kikwete alikuja baadaye kuiboresha kauli hiyo
ya Mkapa kwa
kutupa changamoto hii: "Akili za kuambiwa changanya na
zako za kuzaliwa ndipo
ufanye maamuzi."
Mimi
nimechanganya akili za kuambiwa na akili zangu
mwenyewe, na ndiyo maana nilikataa na nitaendelea kukataa
kuifuata sauti ya
mlio wa mpiga filimbi wa Hamelin (Lowassa), kwa sababu sina
hakika na
anakotupeleka Watanzania.
Kwa akili za
kuambiwa na nikichanganya na za kwangu za
kuzaliwa, nauona wazi ulaghai na uongo unaoenezwa na hawa
Three Musketeers –
Mbowe, Sumaye na Lowassa. Ndugu zangu, tusiifanyie Ikulu
yetu upatu – ni mahali
patakatifu! Tafakari.
Chanzo Raia
Mwema
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment