Wednesday, 9 September 2015

Re: [wanabidii] Siyo lazima kubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo

Kwa asiyeangalia CCM wamefanya nini, bali anaangalia hawakufanya nini tu atakubaliana nawewe. najua wapo ambao wanaadika humu lakini isingekuwa CCM wasingepata nafasi ya kuandika hata humu. Nenda nchi jirani utawakuta. Hatuitetei wala hatusemi haina makosa au haikuharibu lakini si sahih kusema miaka 54 haikufanya kitu. Tafakari hilo kwanza.
--------------------------------------------
On Sun, 9/6/15, 'Flano' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Siyo lazima kubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, September 6, 2015, 11:36 PM

Kwa Tanzania na tulipofikia noooo big
noooo impractical. ccm wameshindwa kufanya vzr miaka 54
unasema wabaki? haipogo

'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

>
>-Nchi ambayo UKAWA wataleta mabadiliko kwa  kuondoa
kodi zote kwa kuwa tuna gas, madini makaa ya mawe,
tanzanite, gold, almasi, mbuga za wanyama, ruby, no kodi.
>
>-Mishahara ya walimu haitokatwa kodi.
>
>-Mkulima ambaye mpaka achuke madaraka Oct 25 atakuwa
hajalipwa hela zake za mazao stakabadhi gharani atalipwa
mara 2. Kwa mfano wapo wakulima mia kila kijiji Tanzania
zidisha huyu milioni 20 mara mbili yule mil 30 mara 2 kama
fidia na hakuna kuwatoza kodi.
>
>-Kuukataa masikini na nyumba za nyasi ambapo nyumba za
kaya au maboma za aina ya manyata Monduli, manyara ni za
fito zilizokandikwa kwa udongo uliochanganywa na kinyesi cha
ng'ombe na kuelekwa kwa nyasi lakini hazijaondolewa karne.
Kuukataa umasikini ambapo gender NGOs zinapambana na elimu
na ufuatiliaji kutokomeza ndoa za utotoni kuoza mtoto wa
miaka 12 kwa jibaba la miaka 60 ili wazazi wapate mifugo ya
kulimbikiza. Wanafunzi kukosa uji shule mpaka kupata misaada
ya World Food Progeam unga wa USAID ulaya ulilimwa kulishia
mifugo. Leo hauondoi umasikini uliopo ndani ya utajiri wa
kulimbikiza mifugo iletayo land degradation, kukausha mito
lakini anaukataa umasikini kimaneno sio kimatendo jimboni
ambalo sio la mfano kitaifa ktk maendeleo wakati mbunge wa
miaka kenda plus anamwaga mindoo ya hela.
>
>-Urafiki na mama, baba ntilie na bodaboda-kaeni popote
mtakako hakuna wa kuwasumbua na kodi msitoe nchii tajiri ni
CCM ndio wabadhirifu.
>-Mkulima lima na uuze mazao yako kokote utakako ndani na
nje ya nchi hakuna masharti ya serikali. Kukukataza na
kukutoza kodi ni uonevu.
>
>Ama kweli kuleta maendeleo kwa sasa hakuhitaji
Economists. Rais mtarajiwa ameachwa kuongea haya ya
economists wapo hata kumshauri. Public health specialists na
wanasheria wapo kusema Ruksa kila kitu kaa popote fanya
utakalo hakuna bugha wala kodi. Sio tu kipindupindu
kitamaliza watu, malori yatapata raha ya kukanyaga miili ya
wafanyabiashara barabarani. Kihamo kutoka vijijini kuja
mijini kufanya biashara kitaongezeka. Ujenzi holela utapaa
300% plus kwani uhuru bila kuzingatia sheria ni ukichaa.
Misaada yetu toka nje ni kodi za walipakodi huko itokako.
kama hapa TZ matajiri waliopewa viwanda, mashamba
hawaendeshi; wanaziona sekta za uchumi wao wanauza soda za
rangi na kuingiza mitumba malori kwa malori na used
cars-hela ya kila kitu bure itatoka wapi iwapo local
investors wenyewe ni dhulumati katika kuendesha uchumi na
kulipa mishahara ni magumashi tu?
>
>Kuleta mabadiliko si lazima kubadilisha chama. Wote
tunahusuka wananchi, watumishi wa umma na makampuni binafsi
y wabongo. Kufanya efficiently na effectively yale ya wajibu
wetu bila udugu, ukabila, urafiti na tamaa ya kutajirika
haraka haraka bali kuzingatia wajibu wa kazi, sera, mikakati
na sheria ya sekta husika.Tubadilike kiakili na kimatendo
tusitegemee vishuke kama mvua. Wanaoahidi vya
kusadikika-tusiwape kura. Hata kama nchi tajiri ina kila
kitu KODI lazima ikusanywe, ikatwe katika mauzo na biashara
ili huduma za bure zipatikane. Bure ilikuwa wakati ule
China, Urusi, Scandinavian countries, UK inatulipia wakitaka
aidha tuwe wajamaa (ujamaa-Socialism) au tuwe capitalists
wakipambara. Sasa ni liberal economy ili tujitegemee budi
tugharimie maendeleo yetu kwa juhudi zetu. Bure aghali!!
Budi uwe mtumwa wa mtu ndani au nje ya mnchi. Wagombea
wengine Tabula Rasa!!
>--------------------------------------------
>On Sun, 6/9/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>
> Subject: [wanabidii] Siyo lazima kubadilisha chama ili
kuleta mabadiliko ya Maendeleo
> To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Sunday, 6 September, 2015, 22:28
>
>
>
>  Siyo
> lazima kubadilisha chama ili kuleta
> mabadiliko ya Maendeleo
>
>
>
> Dhana ya
> baadhi ya sisi Wantania ya kwamba kuondoa Mfumo wa
utawala
> wa nchi ni lazima
> kubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo
ya
> Kiuchumi na maisha bora
> kwa kila mwanachi siyo sahihi. Dhana hii imekuwa
ikitolewa
> mfano wa Kenya na
> kwamba imeondoa tabaka la uongozi wa KANU.
>
>
>
> Kiuhalisia Kenya haijawahi kubadilisha mfumo wa Utawala
ulio
> nje ya KANU. MWAI
> KIBAKI amekuwa ndani ya KANU tangu Kenya ilipopata
uhuru
> mpaka mwaka 2002
> alipogombea Urais kupitia National Alliance Rainbon
> Coalition NARC. Kabla ya
> hapo alikuwa Makamu wa Rais wa serikali ya KANU ya
Rais
> mstaafu DANIEL ARAP MOI.
> Rais mstaafu MWAI KIBAKI alidumu na NARC hadi 2005
ambapo
> alipokuwa akigombea
> kiti hichocha Urais 2007 alipolazimika kupitia chama
cha
> PNU( Party of National
> Unity).
>
>  Pia ikumbukwe kwamba wakati MWAI
> KIBAKI akiwa
> Rais UHURU KENYATTA alikuwa mmoja wa viongozi ndani ya
> serikali hiyo. Aidha
> viongozi wengine tofauti tofauti ambao ni KANU
kiundakindaki
> walikuwemo RAILA
> ODINGA . ODINGA ambaye hajawahi kuwa KANU.
>
>
>
> Mwaka 2013 UHURU KENYATTA alishinda uchaguzi kupitia
chama
> cha The National
> Alliance (TNA). Hivyo mlolongo huu wa uongozi
hauonyeshi
> moja kwa moja ya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment