Thursday, 3 September 2015

Re: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA

Mama Nkya na wengine,

Kwa maoni yangu hakuna kipya alichoongea Dr Slaa kuhusu Lowassa. Dr Slaa huyuhuyu amemnanga Lowassa kwa maneno yale yale aliyoyatumia pale Serena kwa miaka yote na wewe ni moja ya watu waliomsifu kwa 'ujasiri' wake. Baadhi yetu ambao tuliandika kuonyesha shaka kuhusu tuhuma za Lowassa tulitukanwa na kuambiwa tumenunuliwa na Lowassa. Alichofanya Dr Slaa ni kuwa consistent vile amekuwa siku zote. Kwa maneno mengine amekataa kula matapishi yake kama ambavyo wenzake wameyala kwa furaha! Au niseme amekataa kuwa MNAFIKI na kuwa KIGEUGEU kama wenzake. Kwa hivyo, kwa maoni yangu, Dk Slaa KAJISAFISHA na kamrudisha Lowassa kulekule walipomuweka miaka na miaka!! 

Tatizo ambalo linaikumba CHADEMA ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wake, akiwemo Dr Slaa, walijijengea uhalali na umaarufu kwa sababu ya kutuhumu na kufitinisha wapinzani wao na viongozi wenzao ndani ya chama ambao hawakuwapenda. Tulipoandika mkakati wetu wa ushindi katika uchaguzi ndani ya chama wa mwaka 2013 tuliligusia hili, tukasema kuna haja ya kuwa na uongozi utakaojikita katika kuhubiri misingi na sera za chama ili tujenge taswira ya serikali mbadala. Bahati mbaya tukaambiwa ni wahaini kwa sababu ya kutaka kushiriki kugombea uongozi ndani ya chama na nyie mkashangilia kwa bidii.

Sasa kama wanavyosema wazungu what goes around comes around au kama tunavyosema waswahili mwiba huingilia ulipotokea na kwamba ukweli hupanda polepole lakini hatimaye fufika. Dr Slaa ametusaidia  kuanika ulaghai wake na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA. Ametuambia kwamba viongozi hawa wamekuwa wakiwadanganya watanzania na kuchafua watu kwa miaka mingi ili kujijengea uhalali na umaarufu kisiasa. Hii hatusemi kwamba Lowassa na CHADEMA/UKAWA hawawezi tena kuchaguliwa. Lakini tunajua kwamba kuna uwezekano wa kweli wa kuchagua ufisadi (CCM) au kuchagua ufisadi + Ulaghai (CHADEMA/UKAWA) au msingi/sera (ACT). Uamuzi ni wa wapiga kura.  Kama mabadiliko ni kung'oa CCM basi Lowassa na UKAWA wanaweza wakawa ni mawakala wazuri sana wa mabadliko. Lakini kama mabadiliko ni pamoja na kung'oa mizizi ya ufisadi, ulaghai, uwongo na ubabaishaji, ni wazi kuwa Lowassa/CHADEMA/UKAWA ni mawakala wakubwa wa mambo haya. Lakini bado uamuzi na uchaguzi ni wa wapiga kura wenyewe. 

Kila la heri!

Kitila





2015-09-03 17:03 GMT+03:00 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
 Ndugu De kleinson Kim. Nashukuru kwa maswali yako. Tafadhali soma makala yangu niliyoandika Lowassa karafa CCM kuzuia mabadiliko. Ina majibu ya maswali yako. Baada ya kusoma kama una swali lingine tafadhali usisite kuniuliza.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 9/3/15, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

 Subject: RE: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Thursday, September 3, 2015, 8:13 AM

 Mama
 Nkya,
 Nisaidie, kama wewe ndio ungekuwa Dr Slaa, na
 leo unapanda majukwaani kumnadi Edo. ukakutana na swali
 hili;

 "juzi tu ulimtukana siku chache kabla hajahamia kwako,
 leo unamtetea na kusema anafaa? hebu tuelezee
 tukuelewe"
 Nipe jibu utakalompa

 1, Mtu ambaye hana elimu wala uelewa wowote ila alikuwa
 anakusikiliza wewe tu.

 2. Mtu mwenye uelewa mzuri na elimu yake ambaye anataka
 reasoning, facts e.t.c.
 Natanguliza shukrani.



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment