Thursday, 3 September 2015

Re: [wanabidii] DR SLAA KAJICHAFUA

Ujio wa Lowasa upinzani sikupenda niliona kama dhihaka kwa watu waliopambana miaka nenda rudi kuleta mabadiliko.

Kwa sasa ajenda imebadilika, ni kuondoa ccm madarakani sasa linakuja hili ambalo linanishangaza.

Utumikaji kila kona ni utumikaji nimejiuliza kama kweli Kuna utapanyaji hela namna hii nchini kwanini haziwekezwi vyema tukawapa ajira Hawa wazurulaji wanaoleta mafuriko kwenye mikutanoni.

Ukweli ni mmoja unapokuwa na taifa lenye kuwa na watu wengi wasio na shuguli watatumika tu. Nachokiona sasa ni upuuzi kupiga kelele kwa mtumikaji mmoja wakati Kuna watu mamilioni wametumika miaka nenda rudi sasa wako barabarani wanasababisha mafuriko. Mabadiliko hayakwepeki baada oktoba 25 nchi itakuwa na sura mpya tuombe amani na busara tu

On Sep 3, 2015 12:14 AM, "emmbaga" <emmbaga@hotmail.com> wrote:
Mama Nkya wewe ndio unazidi kujichafua. yaani mtu aseme ukweli wake ndio anajichafua. kisa anaawaumbua!!... time will tell
ernest




Sent from Samsung mobile

Neatness Msemo <nmuzeh@gmail.com> wrote:

Unajua mtu akikosa anasema lolote sasa sungura alipokosa alisema sizitaki mbichi hizi lakini hata kama lowasa ni mchafu hakuna msafi lakini Mungu anaweza kumbadiliaha Lowasa awe msafi watakavyo sema watanzania wamechoka kwani CCM wanataka watawale milele

On Sep 3, 2015 6:10 AM, "fadhil fadhil" <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:

Mama nkya kazi ya moyo ni kusukuma damu kupenda ni kiherere chako. Tunajuaa una mahaba mgombea wako lkn wakati mwingine kupenda sana ni ugonjwa.

On Sep 3, 2015 2:18 AM, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Dk SLAA  KAJICHAFUA

Na Ananilea Nkya

Nimeisikiliza  hotuba Dr Slaa  kwenye youtube--nimeungana na wananchi ambao wamesema  Dr Slaa kwa kujua au kwa kutokujua amekubali  kutumika kuyumbisha maelfu ya wananchi wanaotaka  mabadiliko nchini na kwa hiyo amejichafua mbele ya Watanzania.

Dr Slaa anapaswa kujua kwamba mabadiliko ni lazima kwa sasa  na hayazuiliki tena maana  nchi ilipofikia  sasa  Septemba 2015,  wenye ari kubwa ya kuleta mabadiliko  ni wananchi wenyewe    kupitia sanduku la kura hapo tarehe 25 Oktoba.

Pengine Dr Slaa hakujua kuwa wananchi wanaotaka mabadiliko  ya uongozi nchini walikuwa wameshamsahau maana tangu alipoacha kuonekana hadharani  hasa wakati wa  kumtambulisha Edward Lowassa kama mgombea Urais wa UKAWA--muungano wa vyama vinavyopigania kuingia madarakani vikiwa na ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi, wengi walishajua kuwa  Dr Slaa  hayupo tena upande wa wananchi.

Alichokisema   Dr Slaa  kwenye hotuba yake  ya kile alichokiita 'kuachana na siasa za vyama' ni  kajichafua yeye mwenyewe na kuharibu heshima aliyojijengea  kwenye jamii.

Kwa mfano Dr Slaa alisema  eti aliweka msingi kwamba angemkubali Edward Lowassa kugombea  Urais iwapo angeondoka CCM  na mtaji wa  wabunge 50  kuhamia  UKAWA   ili wagombee ubunge  kwa tiketi ya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD-  vyama vinavyounda   UKAWA.

Hivi Dr Slaa aliona vijana wanaochakarika kwenye vyama vinavyounda UKAWA  wao hawataki kuwa wabunge? Hawastahili nao  kufaidi  mshahara wa shilingi milioni 10 kila mwezi na kiinua mgongo cha zaidi ya shilingi milioni 200 baada ya miaka mitano ?

Hebu fikiria wabunge wa CCM ambao wengi wamekuwa bungeni miaka kumi, ishirini wengine  miaka thelathini na zaidi. Ni matajiri kiasi gani leo hii? Hivi watu  wa aina hiyo kweli wanaweza  kuondoka kwenye chama chao  kwa wingi kiasi hicho na kuamua  sasa kupigania  kuondoa mfumo unaowatajirisha wao ili  wananchi  wengi masikini nao watajirike?

Watakuwa na shida gani wakati kwenye chama chao hata kama mtu umekosa kuteuliwa kugombea ubunge malofa wakishaichagua CCM  serikali ya CCM  inawagawia kazi za ulaji watu waliokosa ubunge? Kwani wewe hujamsikia  Mgombea Urais wa CCM  Dr Magufuli akiwatangazia wale walioanguka kwenye kuwa za maoni  ubunge CCM  kwamba wasijali anazo kazi tele za kuwapa akichaguliwa Rais?

Kwa mtazamo wangu--walioamua kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA  kama kweli dhamira yao  ni kushirikina na UKAWA kupigania kuingiza serikali ya UKAWA madarakani ili kuandika Katiba Mpya ya wananchi--watu hao wanastahili pongezi maana watakuwa wamefanya maamuzi magumu na muhimu ya kuwezesha wananchi wengi kuondoka kwenye umaskini unaosababishwa na serikali ya CCM.

Hivi Dr Slaa kweli anadhani mabadiliko ya  kuchagua  serikali  itakayoandika  Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi yatatokea nchini kwa wabunge wengi  wa CCM  kuondoka CCM –kujiunga   UKAWA--wabunge ambao waliizika Rasimu ya Katiba ya wananchi pale Dodoma 2014  huku wakiwa  wanalipw akila mmoja shilingi laki tatu kila siku kwa  takriban miezi mitatu?

Hivi Dr Slaa hajui kwamba wanaotaka mabadiliko ni mamilioni ya Watanzania  wakiwepo wanachama wa CCM wanaoumizwa na umaskini ambao chimbuko lake ni mifumo iliyowekwa na serikali ya CCM--mifumo  inayotajirisha watawala wachache huku mamilioni ya wananchi wakiwa mafukara?

Kwa mtazamo  wangu, wananchi wengi wakitafakari hatua aliyochukua Dr Slaa na maneno aliyoyazungumza hadharani watabaini kuwa  Dr Slaa amejidhihirisha kuwa ni  mtu  mbinafsi.
Zaidi watabaini kuwa Dr Slaa  pengine aliingia kwenye upinzani akidhani  siasa ni kama kazi nyingine. Kumbe  siasa  hasa kuwa kwenye chama cha upinzania  ni  kujitoa  hata kama kuna kuumia kiasi gani –hadi lengo  la ukombozi wa pili wa taifa hili--ukombozi wa kuondoa mifumo inayowafukarisha wananchi  ing'olewe.

Kwa maoni yangu, kama Dr Slaa angekuwa ameingia kwenye siasa kupigania ukombozi wa wananchi--kamwe asingekubali kukaa pembeni sasa--tena baada ya yeye mwenyewe kukubali Lowassa aingie UKAWA mradi awe ni mtaji na si hasara.   Kibaya zaidi asingekuwa upande wa watawala wanaofukarisha wananchi eti kwa sababu Lowassa  alishindwa kuleta UKAWA  mtaji  wa watu wa kugombea ubunge.

Pengine Dr Slaa amekuwa na tafsiri finyu kuhusu mtaji  wa siasa.  Siamini kuwa  vyama vinavyounda UKAWA  vina  uhaba wa  watu wenye uwezo wa kuwa wabunge. Hivyo  mtaji  muhimu  ambao Dr Slaa angeutaka kwa  Lowassa  ni  wapiga kura.  Angejiuliza je huyu Lowassa anakubalika kwa wapiga kura?

Jibu kama Lowassa  anakubalika kwa wapiga kura au la Watanzania wenyewe wanalo jibu na hadanganyiki mtu hapo.  Watanzania wanaomuona Lowassa  anafaa kuongoza Tanzania  mafuriko.  Huyo mtaji wa wapiga kura ambao  Lowassa  ameongeza UKAWA  ndicho kinachowasumbua watawala.

Tena Watanzania wanaomuunga mkono Lowassa  hawajakosea maana hata Mwalimu Nyerere  alitamka  hadharani mwaka 1995 kwamba Lowassa  ni mtu mwenye  dhamira  na uwezo  wa kuiongoza Tanzania.

Isitoshe  wananchi wanamuona Lowassa kuwa ni mtaji muhimu maana kwa kuhama CCM  amehamasisha nguvu kubwa ya umma  katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi.

Dr Slaa alisema eti kwenye familia yake wanakula mhogo na maharage. Hivi familia  inayokula mhogo na maharage (yaani kwa sababu ya umaskini wa kikwelikweli) inaweza kumruhusu baba ambaye alijibainisha kuwa ni kamanda wa mapambano ya wanyonge awageuke mamilioni ya Watanzania ambao hata mhogo na maharage hawapati  na hivyo siku nyingine hulazimika kulala njaa?

Kama Lowassa angeingia CHADEMA na asigombee Urais badala yake  CHADEMA  na UKAWA wangemteua  Dr Slaa kugombea  Urais, je Dr Slaa angetamka maneno aliyoyatamka?  Hata kama Dr Slaa angekuwa na uadilifu kama malaika angetoa kauli zinazofanana na zile  wanazotoa  watalawa wa CCM dhidi ya   mamilioni ya Watanzania wanaotaabika kwa umaskini?

Hivi Dr Slaa ameamua kuungana na  serikali ya CCM kudanganya wananchi  kwamba tatizo la umaskini unaosumbua mamilioni ya  Watanzania  chanzo chake siyo serikali ya CCM bali  ni Lowassa na hivyo Lowassa akiingia madarakani uma ufisadi  utaongezeka nchini?

Kimsingi Watanzania wa leo HATUDANGANYIKI. Zaidi sana Mungu wa wanyonge ni mnyofu  sana  hatawaacha Watanzania   mwaka huu—mwaka wa mabadiliko.

Ninawatia moyo Watanzania wote mkiwepo wana CCM  mnaoumizwa  na hali  ya umaskini miongoni mwa  wananchi wengi nchini kwetu  msikate tamaa  wala kuogopa kama akitokea  kiongozi mwingine wa   UKAWA  akageuka wananchi kama   Dr Slaa na  Prof Lipumba kabla ya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015 ninyi songeni mbele, mabadiliko yanawezekana.

Kimsingi ni  kila mtu kutambua kuwa kuna njama nyingi   zinazofanyika kwa lengo  la kuvuruga  wananchi  ili waogope au wapuuze  kufanya mabadiliko.

Sote tuwe macho, hakuna  kuchoka, hakuna kuogopa .Mabadiliko ni lazima hayazuiliki.   Mungu ibariki Tanzania.

Narudia kusema mimi sina chama chochote cha siasa ninachofungamana nacho. Ninachopigania  ni maslahi ya  mamilioni ya Watanzania masikini (malofa)  kwa utawala mbovu wa  serikali ya CCM.

Ninaruhusu mwenye kutaka kuchapisha makala hii  afanye hivyo maana historia itatuhukumu mmoja mmoja na kama kundi linalopigania mabadiliko Tanzania.

Kwa maswali  niandikie: ananilea_nkya@yahoo.com



Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Wed, 9/2/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Mtikisiko
 To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Wednesday, September 2, 2015, 2:29 PM

 Mtikisiko







                                        Waandishi Wetu



 ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
 (Chadema),
 Dk. Wilbrod Slaa, amevunja ukimya kwa kueleza kile
 kilichomsukuma
 kujiuzulu wadhifa huo, sambamba na kujivua uanachama wa
 chama hicho.
 Katika kuvunja kwake ukimya huo, Dk. Slaa aliweka hadharani
 namna
 viongozi wenzake ndani ya Chadema, akiwamo mwenyekiti wao,
 Freeman
 Mbowe, Makamu Mwenyekiti Profesa Abdallah Safari
 walivyoyumbisha
 kusimamia misingi ya namna ya kumpokea Waziri Mkuu
 aliyejiuzulu kwa
 kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, Edward
 Lowassa.



   Mbali na hayo, mengine aliyoweka wazi ni namna Lowassa
 alivyoratibu
 mipango yake ya kuhamia Chadema akiwa bado CCM, akifanya
 hivyo kwa
 kumtumia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
 Gwajima.



   Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Gwajima ndiye "mshenga" wa
 Lowassa kwa Chadema
  na kati ya hoja alizozitumia kumshawishi Dk. Slaa kumkubali
 Lowassa ni
 kwamba, mwanasiasa huyo aliyeokosa urais CCM, anaungwa mkono
 na Kanisa
 la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na ndani ya Kanisa
 Katoliki,
 maaskofu 30 kati ya 34, wamehongwa na wamemkubali
 Lowassa.



   Ilivyokuwa na Kama ambavyo wahenga wanasema kimya kingi
 kina mshindo,
 ndivyo ilivyokuwa kwa kimya cha Dk. Slaa. Mshindo wa kimya
 hicho ulianza
  kujidhihirisha mapema, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar
 es Salaam,
 alikofanyia mkutano huo, ambapo mpaka saa saba mchana idadi
 kubwa ya
 waandishi wa habari walikuwa tayari wamefika katika eneo
 hilo, kushiria
 kuwa tukio hilo litakuwa na ukubwa wa aina yake.



 Dk. Slaa aliyewasili ukumbi wa mkutano saa 8:05 mchana,
 jana, Jumanne,
 aliweka bayana uamuzi wake wa kuzungumza na waandishi wa
 habari,
 akisema, kwa kuwa ikifika mahali ukweli unatakiwa kusemwa ni
 lazima
 usemwe, kutokana na upotoshwaji uliofanywa na watu
 mbalimbali wakiwamo
 baadhi ya viongozi wakuu wa Chadema, kwamba alikuwa
 amepumzishwa
 (likizo) na viongozi wa chama hicho.



   "Nataka nianze na kusema mimi sikuwa likizo, sikupewa na
 mtu yeyote,
 niliamua kuachana na siasa Julai 18, 2015 usiku saa tatu,
 baada ya kuona
  yanayofanyika ndani ya chama changu sikubaliani nayo,"
 alisema Dk.
 Slaa.



   Alisema alishiriki katika majadiliano ya kumakribisha
 Lowassa ndani ya
  Chadema lakini kwa kuweka misingi ambayo chama kilitakiwa
 kwanza
 kuizingatia kabla ya kufikia uamuzi wa kumkaribisha, baada
 ya kukatwa
 katika mbio za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi
 (CCM).



   "Baada ya tarehe 11 Julai, Lowassa alipokatwa mshenga wa
 Lowassa,
 Askofu Josephat Gwajima alinipigia simu kuniambia sasa kule
 Dodoma mambo
  yameisha, nikamwambia awasiliane na Mwenyekiti (Mbowe),
 tukawasiliana
 na naye baadaye tukakutana naye, nikawaeleza msimamo wangu
 kwamba ni
 lazima kusikia mtu ana nini, tukakutana na vijana wake ili
 tujue ana
 nini," alisema na kuongeza; "Nikasema msingi wa kwanza
 ni lazima
 atangaze kutoka CCM, akijiondoa aseme anakwenda chama gani,
 na atumie
 nafasi hiyo kujisafisha na tuhuma zote zinazomkabili katika
 nchi hii,
 kwa sababu Chadema kimeaminika, ukipokea mtu ambaye
 hajajisafisha
 unakuwa unapokea na uchafu wake. Hilo halikufanyika mpaka
 alipopokewa
 Julai 28. Siwezi kumsafisha mtu ninayekaa naye meza
 moja."



   Dk. Slaa anasema msingi wa pili aliokipa chama chake kabla
 ya kumpokea
  ni kupima kama Lowassa ni rasilimali (asset) au mzigo
 (liability) kwa
 chama hicho, kwa kuwa walikuwa wameambiwa kwamba angekuja na
 viongozi
 wengi kutoka CCM. "Nikawauliza anakuja na nani, yeye peke
 yake au na
 wafuasi, na kama wafuasi ni wa aina gani, vijana wa boda
 boda
 wanaoshabikia tu au ni viongozi serious (makini). Nikaambiwa
 anakuja na
 wabunge 50, wenyeviti wa CCM mikoa 22 na wenyeviti wa wilaya
 88,
 nikakiri hili litakuwa tetemeko, nikahitaji kupewa majina,
 Katibu Mkuu
 makini hawezi kupokea idadi tu, na tulikuwa tunakwenda
 kwenye uchaguzi
 wa kura za maoni, ilikuwa lazima nijue nani anagombea wapi,
 vinginevyo
 uta – destabilize (utayumbisha) chama," alisema na
 kuongeza kwamba;
 mpaka chama hicho kinampokea Lowassa hakuna hata moja kati
 ya misingi
 hiyo iliyotekelezwa.



 Kuhusu ushiriki wake katika kikao cha kumpokea Lowassa,
 alisema aliombwa
  kuitisha kikao cha Kamati Kuu ya dharura, lakini akaeleza
 msimamo wake
 kwamba hajapata jibu la upembuzi kama Lowassa ni mtaji au
 mzigo.



   "Asubuhi ya Julai 27, Mwenyekiti alinipigia simu
 kunieleza sijaridhika
  akaomba tukutane asubuhi tuzungumze ili tusije
 tukatofautiana na
 Mwenyekiti, kwangu mimi tangu mwaka 2004 sijawahi
 kutofautiana na
 mwenyekiti, tulifika pale akiwepo Tundu Lissu, na mshenga
 wake Gwajima,
 tukabishana tangu saa 3 asubuhi mpaka saa 9 alasiri, wapo
 hapa waseme
 kweli, mimi sikukubaliana nao tangu mwanzo, nawaomba
 viongozi wangu wawe
  wanyoofu na wenye hofu ya Mungu," alisema.



 Kwa mujibu wa Dk. Slaa, baadaye walitakiwa kwenda nyumbani
 kwa Lowassa
 lakini alikataa akisema hawezi kwenda nyumbani kwa mtu wa
 CCM katika
 mazingira ya u-Katibu Mkuu wa Chadema. Aliongeza kwamba
 baada ya hapo,
 iliundwa kamati ya watu wachache kumshawishi (Slaa), ambayo
 ilikaa tangu
  saa 9 mpaka saa 12 jioni lakini akawapa masharti yale
 yale.



   "Tuliporudi kwenye kikao taarifa ya kikao kile
 haikutolewa. Nikaandika
  barua ya kujiuzulu nikampa Makamu Mwenyekiti Profesa Safari
 akaichana,
 nikaandika nyingine nikampa Makamu Mwenyekiti Zanzibar,
 akaniambia Dokta
  usihangaike mambo haya yamepangwa," alisema.



   Akizungumzia watu waliokuja Chadema, alisema wote wamekuja
 wakiwa
 makapi baada ya kuwa wameshindwa kwanza kwenye mchakato wa
 awali wa CCM
 (kura za maoni) na hata huko walikotoka si wasafi. "Watu
 kama Sumaye
 hawakuwa safi, mimi mwenyewe nilimwita fisadi bungeni,
 alichukua Shamba
 la Magereza Kibaigwa, na yeye mwenyewe alifikia hatua ya
 kusema CCM
 wakimteua Lowassa yeye atahama chama, sasa yuko naye, najua
 dhambi
 haihalalishiwi na dhambi nyingine, lakini maneno hayo
 yalitamkwa na
 nani, Watanzania walimwita Sumaye ziro," alisema.



 Aliendelea kuwaponda wana CCM waliohamia kuwa ni kama makapi
 ambao
 hawataongeza thamani yoyote kwa chama hicho akiwataja Mgana
 Msindai na
 Matson Chizii kuwa ni sehemu ya makapi ambayo hayataongeza
 thamani
 yoyote kwa Chadema. "Kuna watu wanasema ondoa CCM kwanza
 hata
 ikiwezekana kuweka mkataba na shetani, mimi ni Padri
 Mkatoliki, hata
 kama nimestaafu, nikubali kuweka mkataba na shetani mradi tu
 niondoe
 CCM. Unaondoa CCM kwa program serious na watu makini au
 unaondoa na watu
  wale wale?" alihoja Dk. Slaa.



 Chadema na tuhuma za ufisadi Mbali na kuhoji endapo
 waliohamia Chadema
 kutoka CCM wameongeza thamani yoyote kisiasa; Dk. Slaa
 aliyesimama imara
  akizungumza kwa saa 1.32 alisema; "Chadema iliaminika
 miongoni mwa
 Watanzania kwa kutoyumbishwa na kusimamia uadilifu. Sasa leo
 Chadema
 wanathubutu kusema etu usimtuhumu mtu? Upuuzi mtupu! Kama
 tusingemtuhumu
  Mramba (Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba) leo
 angekuwa Segerea?



 "Kama tusingemtuhumu Yona (Waziri wa Viwanda wa Nishati na
 Madini,
 Daniel Yona) leo angekuwa Segerea? Ni lazima tuhuma zitolewe
 ndipo
 serikali iwajibike. Kwa kawaida binadamu lazima kwanza awe
 na
 'reasonable doubt' sio 'absolute doubt'," alisema
 Dk. Slaa. Alinukuu
 kifungu kimoja cha Biblia kinachosisitiza kuwa ni makosa na
 dhambi
 kupotosha watu huku akiitupia lawama Serikali ya CCM kwa
 kumlea Lowassa
 kwa miaka mingi bila kumshughulikia akisema: "CCM ni waoga
 na ndio maana
  wamlea mtu huyu na leo wanatuletea matatizo."



 Dk. Slaa ambaye alisema hajawahi kutofautiana na Mwenyekiti
 wa Chadema,
 Mbowe, vikaoni tangu mwaka 2004, aliwashangaa viongozi wa
 Chadema kwa
 majaribio yao ya kuwapotosha Watanzania kwa kutaka waamini
 kuwa kwa
 Lowassa na watu wake kuhamia Chadema, wamekuwa watu
 wasafi.



   "Ni kama vile choo; kwetu Watanzania choo ni sehemu
 chafu ingawa kwa
 wenzetu ukiingia chooni unakuta kuna glasi ya 'wine'.
 Samahani kwa mfano
  huo lakini sina mfano mwingine. Sasa leo mtu aende chooni
 achote kile
 kilichomo ndani ya choo na kukihamishia chumani anakolala,
 utasemaje? Ni
  kwamba choo kimehamia chumbani. "Na kwa kuwa ili aweze
 kuchota kinyesi
 kilichomo chooni atalazimika kwanza kukikoroga, basi kile
 kilichomo
 chumbani kitakuwa kinanuka zaidi ya hata choo chenyewe,"
 alisema Dk.
 Slaa.



   Suala la kashfa ya Richmond



 Kuhusu kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond,
 kashfa ambayo
 aghalabu Lowassa na wapambe wake hawapendi kuisikia hata
 kidogo, Mbunge
 huyo wa zamani wa Karatu alisema yeye na wabunge wengine wa
 Bunge la
 Tisa wanalifahamu zaidi kwa kuwa waliiishi kashfa hiyo.



   Dk. Slaa aliwatupia lawama wabunge wa CCM kwa kutopenda
 kusoma nyaraka
  mbalimbali huku pia akiwalaumu waandishi wa habari kwa
 kutokufanya
 utafiti na kuandika habari za kina.



   "Hebu mwambieni Lowassa aache kulalamika. Ajitokeza
 hadharani na
 kusema Richmond ni ya nani? Amtaje hadharani huyo mkubwa
 anayedai kuwa
 alimzuia kuvunja mkataba, ni nani. Juu ya Waziri Mkuu kuna
 Makamu wa
 Rais na Rais, sasa ni nani kati ya hao,

 "Juzi juzi hata leo walikuwa wakinitisha eti nisizungumzie
 masuala haya
 wakidai kuwa nitapotea kisiasa; nini kupotea kisiasa, niko
 tayari
 kupotea katika siasa za Tanzania hata nipotee kabisa duniani
 kuliko
 kuikana dhamira yangu.



   "Msingi wa Richmond ukitaka kuujua ni ripoti ya Kamati
 ya Mwakyembe
 (Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison
 Mwakyembe)," alisema
 Dk. Slaa Alisema kamati hiyo iliomba ridhaa ya Rais iweze
 kupitia
 nyaraka za Baraza la Mawaziri na kufahamu kwamba katika
 Kikao cha Baraza
  la Mawaziri kilichoketi Februari 2, 2006 (takriban mwezi
 mmoja na nusu
 tangu Lowassa ateuliwe kuwa Waziri Mkuu), kilitoa
 mapendekezo ya namna
 ya kushughulikia kwa dharuala tatizo la umeme lililokuwa
 limeikumba
 Tanzania.



 Alisema suala hilo lilianzia tangu wakati wa Rais Benjamin
 Mkapa ambapo
 Baraza la Mawaziri lilielekeza namna ya kulitatua, kisha
 suala hilo
 likarithishwa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.



   "Kwa mujibu wa kifungu cha 112 cha Katiba, Waziri Mkuu
 ndiye mwenye
 nguvu katika utendaji wa serikali na baada ya kikao cha
 Februari 2,
 2006, saaa 10 jioni ya siku hiyo hiyo, Ibrahim Msabaha
 (aliyekuwa Waziri
  wa Nishati na Madini wakati huo), akafuta mchakato
 ulioanzia kwenye
 Serikali ya Mkapa na kubarikiwa na Baraza la Mawaziri.



   "Tujiulize Msabaha alipata wapi nguvu ya kufanya hivyo
 kama si kwa
 bosi wake (Waziri Mkuu)? Mimi mwenyewe, Februari 5 au 6
 mwaka 2008
 wakati wa kashfa ya Richmond, nililetewa rushwa hotelini
 kwangu saa 12
 asubuhi. Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 8,
 2008.



   "Nililetewa Sh. milioni 500 ili ripoti isipitishwe.
 Nikamuuliza
 aliyeniletea, kama mimi unanipa Sh. milioni 500, wewe una
 shilingi
 ngapi?" alisema huku akihoji Dk. Slaa na kumtaka Lowassa
 ajitokeze na
 kueleza jinsi ripoti ile ilivyoibiwa, ingawa hakufafanua
 zaidi akisema
 hizo 'ni silaha za akiba'. Alisema amewahi kuwaambia
 wote wawili,
 Lowassa na Sumaye kwamba rushwa huanzia kichwani, moyoni
 kabla ya
 kutolewa mikononi na kwamba katika sakata la Richmond,
 Lowassa
 aliingilia mchakato kwa kumtumia msaidizi wake binafsi
 kupeleka
 maelekezo kwa Msabaha.





 "Leo anasema mwenye ushahidi apeleke mahakamani la sivyo
 afunge mdomo
 wake; mimi ninasema Lowassa anatafuta urais wa nchi hii
 nafasi ambayo
 hawezi kupewa mtu mwongo; mwongo hakubaliki kuwa Rais,"
 alisema.

   Dk. Slaa alikumbushia pia ufisadi wa Kampuni ya Meremeta
 iliyodaiwa
 kuwa ni mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla
 wajanja
 'hawajaidaka' na kuitumia kuibia fedha za umma akisema
 Lowassa alimuonya
  akimwambia nyaraka anazoziandika na kuziwasilisha bungeni
 zinaiaibisha
 serikali.



 "Nikamjibu, nikasema hapana. Tuwatafute kwanza wanaoiba
 Meremeta hapo
 itatusaidia hata kufahamu nani alisababisha mradi wa magari
 wa Nyumbu
 ukafilisika. "Baadaye akaniita kule Speaker's Lounge
 bungeni, tukawa
 wawili, akaja na mtu mwingine ambaye leo sitamtaja, wakaanza

 kunitishatisha na nikawaona na wale vijana wao, nikaogopa.
 Nikawaambia
 nyie ni mafisadi vichwani, moyoni na ndani ya nafsi zenu.
 "Baada ya hapo
  nikafungua mlango nikakimbia kuokoa maisha yangu. Nani
 anaweza
 kumwambia Lowassa wewe ni fisadi? Ni watu wachache sana
 wenye ujasiri
 huo lakini mimi nilimwambia," alisema.



   Dk. Slaa aliwashangaa wananchi wanaoshabikia ujio wa
 Lowassa kutaka
 urais kupitia Chadema akidai kuwa atawasaidia kutatua shida
 mbalimbali,
 akisema: "Nendeni Monduli (Jimbo la Lowassa), hakuna maji
 kule! Sasa
 atawaletea vipi maji Watanzania wote? Nendeni Karatu (Jimbo
 ambalo Slaa
 alikuwa Mbunge kwa miaka 15) mfananishe na Monduli ."Watu
 wa Karatu
 watakwambia ukweli kuwa akiwa Waziri Mkuu, alibadili hata
 mpaka wa
 Monduli na Karatu na hadi leo kuna ugomvi. Mtu kama huyo
 atawezaji
 kutatua matatizo ya wakulima na wafugaji kama yeye mwenyewe
 ni chanzo?"



   Dk. Slaa pia liponda ujenzi wa shule za kata ambao wapambe
 wa Lowassa
 huutumia kama kete ya mafanikio yake kiuendaji, akisema
 mpango huo
 ulibuniwa mwaka 1990 nchini Thailand naye akiwa ni mmoja wa
 wajumbe
 walioshiriki wakati huo ukiitwa Education For All (EFA).
 Urafiki wa
 Lowassa na Lawrence Masha Kuhusu uhusiano uliopo kati ya
 Lowassa na
 aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha,
 ambaye naye kwa
  sasa yupo Chadema, Dk. Slaa alisema ulianzia wakati wa
 mchakato wa
 kuhalalisha zabuni ya Richmond.



   Alisema Lowassa, Msabaha na Masha walishiriki kikamilifu
 kusimamia
 mchakato uliorudiwa zaidi ya mara tatu kuiwezesha Richmond
 kupata zabuni
  ya kufua umeme wa dharura nchini kinyume cha sheria ya
 ununuzi. Alisema
  kampuni nane zilizoomba zabuni hiyo zote hazikuwa na sifa
 lakini
 wakubwa hao wakalazimisha Richmond kupewa mkataba ndani ya
 siku 10
 badala ya siku 45, kwa mujibu wa sheria na kwamba uetetezi
 wa Lowassa
 kwamba alichukua hatua, si kweli na mtu mwongo hafai kuwa
 Rais.



   Alisema hata baada ya kashfa ya Richmond kujulikana,
 Lowassa na Rostam
  Aziz walishinikiza kampuni hiyo irithiwe na Dowans, kampuni
 nyingine
 feki kutoka Costa Rica. "Kamati ya Mwakyembe ilipotaka
 kuifahamu Dowans
 ya Costa Rica, iliambiwa kuwa Mkurugenzi wake aitwaye Zamora
 aliisajiri
 siku moja pamoja na kampuni zake nyingine 99 huku pia akiwa
 ni
 mwenyekiti wa kampuni nyingine 52 tofauti. "Hadi leo
 Dowans wanalipwa
 Sh. milioni 153 kila siku. Lowassa aje kutuambia ni nani
 anayepokea
 fedha hizo. Ninafahamu kuwa hata fedha za kampeni sasa
 zinatolewa na
 Rostam Azizi, mtu aliyewahi kunipigia simu akiniambia;
 'dokta, omba
 Mungu ndani ya dakika tano hautakuwapo duniani'.



 "Lowassa aje atuambie kwa nini Scotland Yard wanamtafuta
 kwa utoroshaji
 wa Pauni milioni 400. Mtu huyu leo anataka kuwa Rais!
 Haikubaliki na
 niseme wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote lakini
 ni
 Mtanzania na nitapiga kelele watu hawa wajulikane.



 "Lowassa aje hadharani aseme ana hisa kiasi gani kwenye
 kampuni
 mbalimbali nchini ambazo hakuziandikisha kwenye Sekretarieti
 ya Maadili
 ya Viongozi wa Umma," alisema. Alihoji uadilifu wa Sumaye
 aliyepora eneo
  la ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Mvomero huko Morogoro
 na kuihodhi
  ardhi ambayo hadi leo haitumiki na sasa makao hayo makuu
 yamejengwa
 pembebi ya Barabara ya Dodoma – Morogoro.



 Ahitimisha hoja zake



   Katika kuhitimisha hotuba yake hiyo ya saa moja na nusu,
 Dk. Slaa
 aliwasihi vijana aliowaimarisha ndani ya Chadema kutopiga
 kura kwa
 ushabiki bali watafakari na kufanya uamuzi sahihi huku
 akiponda hoja za
 kufunguliwa kwa babu Seya na watuhumiwa wa ugaidi Zanzibar,
 akisema si
 za msingi kwa Watanzania wa sasa.

 "Nilisema tangu awali kuwa nimestaafu siasa. Kwa sasa sina
 chama, bali
 nina nchi. Nimeombwa na vyama vitano tofauti nijiunge
 nigombee uraisa,
 lakini nikasema hapana, tatizo la Watanzania si urais wa Dk.
 Slaa; ni
 uadilifu wa viongozi.



 "Ndio maana nitaendelea kupiga kelele nje ya vyama vya
 siasa kwa kuwa
 kuna viongozi ambao si waadilifu wanataka kuchukua taifa
 letu. Kwa mfano
  mshenda wa Lowassa (Askofu Gwajima) alikuja kwangu,
 akaniambia
 ninapaswa kumuunga mkono Lowassa kwa sababu anaungwa mkono
 na wengi.
 "Nikamuuliza akina nani hao? Akanijibu kuwa kuna fedha
 kutoka kwa Rostam
  Aziz, anaungwa mkono na KKKT na kwamba kati ya maaskofu 34
 wa Katoliki,
  30 wamehongwa!



 "Nikamwambia akili yake imepumbazwa. Nikawasikitikia
 maaskofu wangu
 kwamba kama ni kweli wamehongwa, basi taifa letu
 linaangamia. Mshenga
 (Gwajima) akaniambia kuna askofu alitaka gari zuri la
 kiaaskofu, ndani
 ya dakika 20, akapewa. "Nikajiuliza hawa watu wanatoa wapi
 fedha?
 Inamaana hata hawaziweke benki kwa sababu huwezi ndani ya
 dakika 20
 ukanunua gari la Sh. milioni 60," alimaliza Dk. Slaa
 hotuba hiyo huku
 akisisitiza kuwa zipo silaha nyingine za akiba atazitumia
 mara baada ya
 Lowassa na Sumaye kujibu hoja hizo.



 Dk. Slaa alisema huenda maneno yake yakaonekana kuegemea
 upande fulani
 kwa sasa, lakini hiyo ni kutokana na ukweli kuwa ukweli
 lazima utakuwa
 upande tofauti na uongo.



   Chanzo Raia Mwema



   Toleo la 421, 2 Sep 2015

























 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment