Umasikini wa kujitakia. Watanzania pale tulipo hatujitumi ipasavyo. NGO zifanye kazi ya kuhamasisha hasa zikishirikiana na extension staff na kutumia sheria kama mtu hataki kubadilika mfano kutokujenga nyumba bora na resources zipo mpaka mashine za kutengeneza matofari ya kuchoma ya kuingiliana -interlocking blocks, soil cement block na maeneo mengine wana mawe ya gypsum; kulima na kufuga endelevu, mabwawa ya samaki; kuingia mkataba na mwekezaji wakufaidika na madini achimbe yeye kwa vifaa vya kisasa ili waepuke zinaa machimboni na ukimwi, kushika madini chafuzi ya viungo vya mwili wao hatumie mafao kufanya kujiajiri katika shughuli nyingine endelevu. Kulinda raslimali-ardhi, mito, maziwa, misitu ni muhimu. unapouza mali yako kama nyumba, ardhi tumia hela kiakili badala ya kujitafutia matatizo kimaisha. Ona yanayoonekana na badilika. Jipende na kupenda nchi yako. Jijue na ujitambue na uwe mwaminifu kona zote. Kama ni dereva-zingatia sheria za uendeshaji
salama, wacha kuweka maduka kando ya barabara, vilabu vya pombe, viti barabarani na kila baada ya nyumba 3 ni bar na vitu vya anasa-Tutafika? Mtumishi wa serikali wacha uroho na ubadhirifu timiza wajibu wako. Ogopa Mungu wacha kuibia raia wenzako.
--------------------------------------------
On Thu, 10/9/15, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 10 September, 2015, 12:23
UCHAGUZI 2015: NI KURA YA
MAAMUZI KUHUSU UMASKINI WA WANANCHI
Na Ananilea Nkya
Tanzania ni moja ya nchi chache
barani Afrika ambazo zimejaliwa utajiri mkubwa wa mali
asili yakiwepo madini, ardhi yenye rutuba iliyosheeni
milima mabonde na wanyama lakini mamilioni
ya wananchi ni masikini wa kutisha ingawa
nchi ilipata uhuru zaidi ya miaka 50
iliyopita.
Ili nchi iweze kuondokana na umasikini hata kama inazo
rasilimali nyingi inapaswa kuwa na
rasilimali nyingine muhimu—rasilimali uongozi –uongozi
unaohakikisha kuwa mali za nchi
zinanufaisha wananchi wote na siyo kikundi
kidogo cha viongozi.
Uongozi wa nchi kwa kawaida hupatikana kupitia
vyama vya siasa. Hivyo ni muhimu wanaotafuta
fursa ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka huu
2015, kutambua kuwa mamilioni ya Watanzania hivi
sasa ni maskini ili hali kikundi kidogo cha viongozi
ni matajiri sana.
Kibaya zaidi mamilioni ya Watanzania
wanaotaabika kwa umaskini hivi sasa wametambua
kuwa umaskini wao
unatokana na uongozi unaotoa fursa
kwa viongozi kuwa matajiri wa kupindukia
na mamilioni ya wananchi kubaki maskini.
Mamimioni hayo ya wananchi wanateseka kwa
umaskini mwaka huu wanataka
mabadiliko ya uongozi wa nchi yao.
Wanataka mabadiliko hayo baada ya kutambua kuwa mfumo
wa utawala (Katiba) uliotengenezwa na serikali ya
CCM ndio unawezesha watawala
wachache kuwa matajiri wa kutupa kwa kulipana
fedha nyingi za umma na
kujigawia rasilimali za nchi kujitajirisha wao wenyewe.
Kwa mfano wananchi wanajua kuwa watawala
walijiuzia kwa bei chee nyumba za
umma zilizojengwa kwa mabilioni ya fedha za kodi
ya Watanzania wanaoteseka kwa umaskini.
Kadhalika, wananchi wanafahamu
kuwa viongozi wa serikali
walijigawina fedha za umma zilizoibiwa kwenye akaunti
ya Tegeta escrow mwaka jana 2014.
Vilevile wananchi wanajua kuwa
watawala mfano wabunge
wanalipwa mishahara mikubwa na kiinua
mgongo kikubwa katika muda wa miaka mitano tu huku watumishi
wengine wa umma mfano walimu, wauguzi na madaktari
wakiwa wanalipwa mishahara midogo sana.
Kwa sasa, mtu ambaye haijamuingia akilini kwamba mamilioni
ya wananchi wamechoka na umaskini ambao chanzo
chake ni uongozi mbovu katika nchi
yao—uongozi ambao unatajirisha wachache
na hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi wa nchi yao,
mtu huyo atakuwa anajidanganya.
Jambo jema ni kuwa hata baadhi ya wagombea
Urais kwa mfano mgombea wa CCM, Dr
John Magufuli na mgombea wa CHADEMA, Edward
Lowassa kwa niaba ya vyama
vinavyounda UKAWA wamekuwa wakizungumza wazi
kwenye mikutano yao ya
kampeni kwamba wananchi wanataka
mabadiliko ya uongozi.
Tena wagombea hawa wanatambua wazi kuwa
mabadiliko watayaleta hao
Watanzania wenyewe wanaoteseka
kwa umaskini kwa kutumia sanduku huru la kura hapo
tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015.
Kwa maneno mengine mamilioni ya wapiga kura maskini wanajua
kuwa uchaguzi wa mwaka huu 2015 kura yao ni kura
ya maamuzi juu ya maisha yao. Ni kura muhimu ya
KUAMUA KUENDELEA KUWA MASKINI AU KUUKATAA
UMASKINI.
Ni kura ya kuamua iwapo wanataka watawala
wachache wanaotengenezwa na serikali
ya CCM waendelee kuwa matajiri wa kutisha na mamilioni
ya Watanzania waendelee kuumizwa na umaskini ili hali nchi
yetu ikiwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali za asili za
kuwawezesha Watanzania wote kuwa matajiri na kuishi maisha
ya furaha na yenye hadhi.
Wananchi wenyewe wanajua kuwa mabadiliko
wanayoyataka yanawezekana ingawa kumekuwa na njama za
kujaribu kupunguza nguvu ya umma inayodai mabadiliko
kutumia baadhi ya viongozi wa ngazi za juu kwenye vyama vya
upinzani vinavyounda UKAWA (CUF, CHADEMA, NCCR Mageuzi na
NLD)--vyama vinavyoongoza wananchi katika kutafuta
mabadiliko.
Wananchi wameshuhudia baadhi ya viongozi wa
upinzani wakiamua ghafla kuondoka kwanye uongozi
na kuungana na watawala ambao mfumo wa uongozi
umewafanya kuwa matajiri wa kutisha huku wananchi wengi
wakiwa ni maskini wa kutupa.
Lakini pamoja na viongozi hao
kuachia ngazi, mamilioni ya wananchi hawajabadilika,
hawajayumba, msimamo wao uko pale pale na
wanasonga mbele hadi waweze kufanya
mabadiliko wanayoyataka.
Ni kwa nini wananchi wanataka mabadiliko ya uongozi wa nchi
yao?
Wanataka nao wawe matajiri katika kipindi
cha miaka mitano kama ambavyo wananchi wenyewe
wameshuhudia wanaochaguliwa kuwa viongozi
wakitajirika ghafla baada ya kuchaguliwa kuwa
viongozi!
Wananchi wamechoka kuwa mafukara katika
nchi yao yenye utajiri mwingi wa asili lakini
utajiri huo unatajirisha makundi mawili tu--
watawala wachache na wawekezaji wa kigeni.
Tena baadhi ya mamilioni ya Watanzania wanaotaka
mabadiliko wengi wao hawana vyama vya siasa wanavyofungamana
navyo maana hata fedha za kununua kadi ya chama cha
siasa hawana.
Baadhi waliobahatika kuwa wanachama wa vyama vya siasa
kikiwepo chama kinachotawala nchi kwa sasa CCM, lakini
wengi wa wanachama hao ni mafukara wa kutupa pia
wanaohangaika kwa umaskini kama wananchi wengine.
Kimsingi, mamilioni ya watu maskini (nguvu kubwa
ya umma) ambayo mfumo wa uongozi wa serikali ya CCM
umezalisha, mabadiliko wanayoyataka ya uongozi hayaepukiki
maana hakuna anayeweza kuizuia nguvu ya umma inapoamua
kuleta mabadiliko.
Isitoshe, mamilioni ya wananchi hawa
maskini, ni kama bomu ambalo serikali
ya CCM imelitengeneza kwa kujua au kwa kutokujua
kwa miaka kadhaa sasa na hivi sasa
linasubiri kulipuka lenyewe kwa amani kwenye
sanduku huru la kura tarehe 25 Oktoba
2015.
Jambo la kuzingatia ni kwamba , atakayejaribu kuzuia
kwa mkono bomu hilo lisilipuke kwa amani kwenye sanduku huru
la kura---uwanja wa wazi ambao ndio pekee bomu
hilo linaweza kulipuka bila kuleta madhara ya kuvuruga
amani ya nchi, mtu huyo historia ya taifa
hili itamhukumu. Mungu ibariki Tanzania.
NOTE: Naridhia anayetaka kuichapisha au kusambaza makala hii
isomwe na Watanzania wengi afanye hivyo.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



0 comments:
Post a Comment