Hapana. Kiii si kubombea madaraka. Kiini ni mwelekeo wa kuuvunja Muungano kwa kuiongezea nguvu Serikali ya Zanzibar ikaelekea kuwa Nchi badala ya ilivyokuwa toka mwanzo wakati wa uasisi wake. kwa kupima mambo. na kuona ugumu wa kuirekebisha serikali ya zanzibar kurudi mahala pake zikiwa mbili tu, mazingira ambayo yamemfanya rais wa Zanzibar amuone wa Muungano kama 'mwenzake ikapendekezwa ziundwe tatu ili mbili kwa kadri tunavyosonga mbele itafikia mahala itagundua mwenzao ni Tnganyika. Ukweli ni kuwa ni hatari sana kuendelea kuimarisha nguvu ya Zanzibar huku Tanganyika unainyamazia. Vijana wa Tanganyika watakapokuja hawatakuja kudai kurekebisha muungano ila Tanganyika yao. Njia pekee salama ya kulinda muungano ni Serikali tatu ambazo zitaharakisha kuingia serikali moja. na itakuwa hivi: Wazanzibari wana mambo mengi wanayafaidi ndani ya mfumo wa serikali mbili. ambayo kwa ukubwa wake Watanganyika hawajai (sasa wameanza kujali) Siku wakiyakosa kwa sababu
ya kuwepo Tang\anyika haiweekani wakaamua kuuvunja muungano ila watarufi kujadiliana na tanganyika ndani ya Mfumo ulio katika Rasimu ya pili ya Tume ya warioba. Wanaweza kuja kwa kuomba zirudishwe serikali mbili na wakaambiwa hapana. Ama Tatu ama moja. hawawezi kupinga labda kama hawaoni udogo wa visiwa vyao
Hekima hiyo inawezekana ndani ya mfumo wa serikali tatu (maana katikaq huu wa mbili imeshindikana.
Ieleweke muungano umekuwa dhaifu sasa.
1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano aliweza kuchanganya udongo wa Zanzibar na tanganyika peke yake huku wa Zanzibar akiwa anaangalia. Ilikuwa hivyo kwa sababu yeye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano akiwawakilisha wazanzibari na watanganyika.
Jumatano iliyopita tumemkosa mtu mmoja kupokea katiba pendekezwa mpaka Shein akaipokea kwa niaba ya waZanzibari na Kikwete sijui alipokea kwa niaba ya nani maana bila kuwawaqkilisha wazanzibari hata watanganyika hawawakilishi. Ni jambo dogo sana kijuu juu lakini lipimeni muone linaashiria nini
--------------------------------------------
On Mon, 10/13/14, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Jaji Warioba: Tusidanganyane, kutaka Serikali tatu ni kuvunja Muungano
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, October 13, 2014, 6:10 AM
"...kuna watu
wanafikiri kuimarisha Muungano ni kuwa na serikali tatu,
unaimarishaje? Sasa
hivi kiini ni ugomvi wa madaraka kati ya Serikali ya
Muungano na
Serikali ya Zanzibar. Hivi ukileta serikali tatu, ugomvi huu
hautakuwapo? Ukileta Serikali ya Tanganyika yenyewe haitadai
madaraka?
Mwisho wataomba madaraka hadi Serikali ya Muungano isiwe na
chochote. Hivi
Serikali ya Tanganyika kwa mfano ikawapo, ikataka iwe na
wimbo wake wa
Taifa, bendera yake, nembo yake, kisha inadai ifanye
biashara ya nje,
unafikiri tutakuwa tumefika wapi? Ni kwamba tutakuwa
tunaondoa Muungano na kurudisha Tanganyika na Zanzibar.
Lakini kama wananchi wanataka hivyo, sawa. Lakini
tukivunja Muungano madhara yake ni makubwa sana kwa pande
zote mbili.
Mimi naamini wale wanaotaka serikali tatu wanajua nia yao ni
kuvunja
Muungano na huu ndio ukweli. Ukianzisha serikali tatu, maana
yake
unavunja Muungano." Haya maneno yananipa shida. Si hivi
ambavyo huwa tunamsikia Warioba akielezea kwa nini tume
iliweka muungano wa serikali tatu kama ilivyoelezwa kwenye
rasimu na bango kitita. Huenda mwandishi amefanya tafsiri
yake. Ninasema hivi kwa sababu muundo wa serikali tatu
unaonekana kwenye uhalisia wenyewe wa utendaji wa serikali.
Mfano tu, ni muundo wa mahakama. 1) Kuna Mahakama Kuu ya
Tanzania (ambayo haina mamlaka Zanzibar). 2) Kuna Mahakama
Kuu ya Zanzibar (ambayo haina mamlaka Tanzania Bara) 3) Kuna
Mahakama ya Rufaa (ambayo ina mamlaka Tanzania Bara na
Zanzibar). Muundo huu upo na haujavunja muungano. Pia kuna
mifano mingine, ambayo kiutendaji inaonyesha wazi kwamba
tuna serikali tatu ingawa kinadharia zinasemwa mbili. Kwamba
nchi mbili zinapounga ni ama zinaunda serikali moja (siyo
mbili), ama zinaunda serikali tatu za shirikisho. Hivyo,
tuwe makini sana tusiwapotoshe wananchi as if hatujamsikia
Warioba akizungumzia serikali 2 na 3 na kwamba haya
mahojiano ndiyo tu yameibua kile ambacho Warioba anakiamini.
2014-10-12 20:02
GMT+03:00 Jane Mwakalukwa <mwakalukwa@gmail.com>:
Raia
Mwema: Unazungumziaje suala la Katiba mpya?Jaji
Warioba: Sina hakika kama viongozi wetu wanaelewa
ni kitu gani kilicho muhimu. Nadhani tunaingia katika tatizo
hili la kila mmoja anatazama manufaa yake.Katiba
hii msingi wake ulikuwa ni chama kimoja. Tumefanya
mabadiliko kuna mambo ambayo yametokana na chama kimoja
lakini ni ya msingi katika kuendesha nchi. Ni muhimu
tuyatazame na kati ya hayo ni Tanzania ya aina gani
tunayotaka kuijenga.Moja
ambalo limetokana na mfumo wa chama kimoja ni kwamba TANU,
ASP na CCM vilikuwa na itikadi ambayo ilikuwa inafafanua
tunataka Tanzania ya aina gani na wananchi wakaielewa.Bila
kujali ulikuwa unakubaliana na Ujamaa na Kujitegemea ulijua
huu ndio mwelekeo wetu tunataka Tanzania ya Ujamaa na
Kujitegemea. Ni Ujamaa na Kujitegemea na miiko yake ilikuwa
inaeleweka nchi nzima. Wananchi walikuwa wanatoa uamuzi
kulingana na itikadi.Sasa
hakuna. Hatujui ni Tanzania gani tunayotaka kuijenga na hapo
nadhani tunapokwenda kwa wananchi tutarajie hilo kwamba
kubwa tunalotaka kutoka kwa wanannchi ni Tanzania gani
wanataka tuijenge.Tusiende
kwamba kulazimisha kuyazungumza haya tunayoona ni makubwa
kwa sababu watazungumza kwa jinsi wanavyoona mambo yao.
Unaweza kwenda sehemu ukakuta tatizo lao ni ardhi. Wengine
wanaweza kuzungumzia madini. Tuyasikilize yote haya na
kutokana na hayo utaona Watanzania wanataka Tanzania ya aina
gani.Katika
kile kifungu cha malengo muhimu ya Taifa haya yaelezwe ndani
ya Katiba kwamba Watanzania malengo waliyonayo ni
haya.Kwa
hiyo, kwangu hili ni muhimu la sivyo tutabaki katika yale
yale ya kujidanganya kwamba Tanzania ni nchi ya Ujamaa na
Kujitegemea wakati ile misingi haipo. Lazima tujipange
kuhakikisha tunajenga Tanzania tunayotaka. Katiba ni
wananchi na wananchi waachwe waamue mambo yao muhimu.Tusipofafanua
Tanzania tunayoitaka bado tutakuwa na mgogoro kwa sababu
hapatakuwa na yard stick ya kuwapima viongozi na
Tanzania tunayotaka kuijenga.Kuna
suala la msingi kuwa wananchi ndiyo wenye madaraka. Lazima
tueleze ni madaraka gani yako kwa wananchi, kwamba wana
uwezo upi wa kukataa viongozi.Saa
hivi kuna kujichanganya, unakuta tunasema madaraka yako kwa
wananchi lakini tumeyahamisha kwa kiwango kikubwa kwenda
kwenye dola au kwenye vyama vya siasa.Serikali
utakuta imepewa madaraka makubwa lakini wanasema ni kwa
niaba ya wananchi. Vyama vya siasa navyo ni hivyo, vimepewa
madaraka makubwa nao wanasema ni kwa manufaa ya
wananchi.Sasa
hivi pamoja na Katiba kusema kwamba msingi wa madaraka ni
wananchi kwa hiyo wanachagua wawakilishi lakini bado msingi
huo unabanwa kwamba unawaambia kama unataka mwakilishi
lazima ufuate taratibu hizi. Kama wewe si mwanachama wa
chama cha siasa basi huna nafasi hiyo.Kwamba
watu wanaweza kumchagua mwakilishi lakini chama cha siasa
kinaweza kumfukuza huyu mwakilishi. Wanakorofishana ndani ya
chama wanamfukuza na anapoteza mandate ya
wananchi kama vile mwakilishi huyo alichaguliwa na chama.
Lazima mipaka iwekwe ndani ya Katiba.Baada
ya hapo tuangalie zile taasisi muhimu, Bunge, Serikali na
Mahakama tuangalie upya mgawanyo wa madaraka haya,
ile separation of powers iwepo lakini pia lazima
kuwapo checks and balances.
Sasa hivi nadhani itabidi
tuimarishe Mahakama. Iwe na uhuru wa kifedha, wasitegemee
hisani ya Katibu Mkuu wa Hazina.Kama
tumefika mahali unasema Bunge litapata bajeti kiwango fulani
na vyama vya siasa vinapata bajeti fulani, Mahakama nayo
lazima tuseme wanapata asilimia fulani.Tuingie
kwenye utendaji, tuangalie mgawanyo wa madaraka kati ya Rais
na taasisi za utendaji. Najua Rais lazima atakuwa na
madaraka lakini kuna mahali pengine ama madaraka haya
yanaweza kwenda kwenye taasisi au utendaji wake Rais lazima
ashauriwe.Inawezekana
tukaamua, je, kuna umuhimu wa kumpa Rais madaraka ya kuteua
mawaziri lakini wawe wanathibitishwa mahali? Ateue majaji
lakini wathibitishwe mahali.Sasa
hivi naona kuna watu hawataki Rais awe na madaraka makubwa
lakini mimi nafikiri Rais lazima awe na madaraka isipokuwa
tuangalie yale mengine awe nayo lakini kwa kushauriwa.
Lazima katika Taifa kuwe na mtu mnasema lazima awe na
madaraka haya, isipokuwa ni kutengeneza utaratibu.Hata
kama tunataka Rais wa kikatiba tu ingawa sioni hilo kama ni
zuri katika nchi, kama tunataka awe waziri mkuu sawa. Lakini
suala la madaraka ni muhimu.Katika
mabadiliko ya mwaka 1984 nia ilikuwa kupunguza madaraka ya
Rais, Waziri Mkuu asimamie zaidi utendaji lakini sasa hivi
unaona kama Waziri Mkuu hana madaraka ya kusimamia
utendaji.Imejitokeza
Rais anasimamia utendaji, anakwenda wizara kwa wizara,
anatoa maagizo ya utendaji, Katiba haijamzuia lakini
imemuwekea mtu wa kumsaidia, nimeona kwenye Bunge Waziri
Mkuu anaulizwa maswali ya papo kwa papo anazumgumzia sera.
Sera si ya kwake, iko chini ya Rais.Kwa
hiyo tutakapozungumza Katiba ni lazima hapa tufafanue nini
kazi za waziri mkuu au kama kuna sababu ya kuwa na waziri
mkuu. Tuzungumze, je, mawaziri wawe kama walivyo kutokana na
Bunge?Bunge
nalo liangaliwe, madaraka yake yafafanuliwe. Unajua wakati
mwingine Bunge limeingilia mambo ya utendaji, lazima sasa
iwepo mipaka kati ya Serikali na Bunge na tujue nani
anastahili kuchaguliwa kwenda bungeni, tujue utaratibu wa
kupiga kura.Sasa
hivi wanazungumzia sana Tume ya Uchaguzi. Tuzungumzie hili.
Kuna watu wanafikiri lazima iwakilishe makundi fulani
fulani. Zanzibar wanazungumzia uwakilishi wa vyama.
Kwingine, Afrika Kusini wanaye kamishna. Ghana wanayo tume
ambayo mwenyekiti ni yule yule, amekuwapo kwa muda kwa
sababu yuko huru.Naamini
Tume yetu ikiwa na wajumbe kutoka vyama vya siasa haitakuwa
huru. Nadhani utaratibu wa Katiba mpya utuwezeshe kupata
maoni ya wananchi.Ninachokiona
sasa ni kila kundi kwa maslahi yake linatumia hoja ya
wananchi kuwa wanataka utaratibu fulani. Vivyo hivyo,
Serikali nayo inataka kuweka mipaka fulani kwa maslahi ya
wananchi.Tusiweke
mipaka. Wananchi watoe mawazo yao. Kuna vyama vya siasa
vinasema kwa manufaa ya wananchi tuwe na Bunge la Katiba
ambalo litachagua Tume na kutoa hadidu za rejea na kusimamia
mchakato na baada ya kupitisha watakwenda kwa
wananchi.Sikubaliani
na hilo. Wananchi waachwe wazungumze yote wanayotaka, Katiba
yao iweje. Wakishakuzungumza, hiyo tume itengeneze muswada
wa katiba urudi kwa wananchi. Wazungumze, kusiwe na kikundi
hapa katikati kinasema kwa manufaa ya wananchi.
Hapana.Wananchi
wazungumze muswada na chombo cha kupitisha kipitishe
baadaye. Wasilete vikao hapa katikati huku wanajitafutia
nafasi. Mchakato huu uende moja kwa moja kwa wananchi.
Tusiwawekee mawazo.Kuna
wanaharakati wanataka kuleta mambo ya kuwajaza wananchi.
Nina hakika wananchi wakiachiwa uhuru, watasema na wataalamu
watapanga vizuri. Nasisitiza la msingi ni kuwaacha wananchi
waseme wanataka nchi ya namna gani.Suala
la Muungano pia liwe katika Katiba. Tusipokuwa makini kwa
maneno yanayozungumswa sasa tutavunja Muungano.Muungano
huu una misingi yake na upo kwa manufaa ya wananchi.
Tufafanue manufaa hayo ni nini kwa mwananchi wa
kawaida.Wakati
wote kwa mwananchi wa kawaida, kumekuwa hakuna matatizo ya
Muungano. Matatizo yanatoka kwenye midomo ya viongozi.Shughuli
za wananchi wa kawaida haziangalii orodha ya mambo ya
Muungano, bali haki yao kama raia. Wanajiona ni raia katika
shughuli zao za kibiashara au nyingine. Mwananchi wa kawaida
anaona anayo haki ya kufanya biashara mahali popote.
Wananchi wamezoa hivyo. Msiwafikishe mahali wakajiona kuwa
kwenda Zanzibar au kuja Bara inabidi wafuate taratibu za
kwenda Kenya au Uganda.Tunayo
matatizo ya madaraka, kwamba unazo Serikali mbili kwa hiyo
yale yaliyomo kwenye orodha ya Muungano ni kuonyesha
Serikali hii ina madaraka gani. Wanagombania madaraka.Kama
suala ni mafuta au mengine tuzungumze. Inategemea
mnavyokubaliana, tusije kuongeza au kupunguza kwenye orodha
mambo ambayo yatakuja kuwatenganisha wananchi. Kama kwa
mfano, kuna watu wanafikiri kuimarisha Muungano ni kuwa na
serikali tatu, unaimarishaje?Sasa
hivi kiini ni ugomvi wa madaraka kati ya Serikali ya
Muungano na Serikali ya Zanzibar. Hivi ukileta serikali
tatu, ugomvi huu hautakuwapo? Ukileta Serikali ya Tanganyika
yenyewe haitadai madaraka? Mwisho wataomba madaraka hadi
Serikali ya Muungano isiwe na chochote.Hivi
Serikali ya Tanganyika kwa mfano ikawapo, ikataka iwe na
wimbo wake wa Taifa, bendera yake, nembo yake, kisha inadai
ifanye biashara ya nje, unafikiri tutakuwa tumefika
wapi?Ni
kwamba tutakuwa tunaondoa Muungano na kurudisha Tanganyika
na Zanzibar. Lakini kama wananchi wanataka hivyo,
sawa.Lakini
tukivunja Muungano madhara yake ni makubwa sana kwa pande
zote mbili. Mimi naamini wale wanaotaka serikali tatu
wanajua nia yao ni kuvunja Muungano na huu ndio ukweli.
Ukianzisha serikali tatu, maana yake unavunja
Muungano.-
See more at: http://www.raiamwema.co.tz/jaji-warioba-tusidanganyane-kutaka-serikali-tatu-ni-kuvunja-muungano#sthash.pzEssMWC.EFRLlLub.dpuf
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment