Monday, 13 October 2014

Re: [wanabidii] Katiba Pendekezwa itachapishwa upya

wani orodha ya walipoiga kura iliongezeka mmoja? kama sio atakayeongezwa badala ya huyu wa NCCR ahojiwe nao wahojiwe ilikuwaje asiwemo toka mwanzo. Kuna upuuzi humu
--------------------------------------------
On Mon, 10/13/14, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Katiba Pendekezwa itachapishwa upya
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, October 13, 2014, 6:13 AM

Hilo jina la huyo
mbunge liliingiaje huko kama huo siyo uchakachuaji tu? Mbona
halikukosewa herufi au chama? Hakuna kudanganyika hapa!

2014-10-12 17:09
GMT+03:00 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:
Uongozi
wa Bunge Maalumu la Katiba, umemuagiza Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali, kupiga chapa upya Katiba Inayopendekezwa, baada ya
kubaini makosa ya uchapaji, ikiwemo kuandikwa kwa makosa kwa
mjumbe wa bunge hilo kupitia NCCR-Mageuzi Zanzibar, Haji
Ambar Khamis. 

Katika
chapisho la Katiba Inayopendekezwa, mjumbe Khamis ameonekana
kama vile alishiriki katika awamu ya pili ya Bunge Maalumu
la Katiba, wakati hakushiriki. 

Kosa
hilo na mengine ya uchapaji, yamekuwa yakitumika kwa
makusudi kupotosha umma kuwa Katiba Inayopendekezwa, ilipita
katika mazingira ya kuchakachua kura za wajumbe, ili
kuiondolea uhalali wake wakati wa kupiga kura ya
maoni. 

Moja
ya jitihada hizo ni pamoja na hatua ya mjumbe Khamis,
kuangua kilio 
juzi
mbele ya waandishi wa habari na kukimbizwa hospitalini kwa
matibabu, baada ya kukiri chini ya kiapo cha chama chake cha
NCCR-Mageuzi, kuwa hakushiriki kuipitisha Katiba
Inayopendekezwa. 

Akizungumza
na mwandishi jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Dar es Salaam, Naibu Katibu wa Bunge Maalumu
la Katiba, Dk Thomas Kashililah, alisema jina la Khamis
kuwepo katika orodha hiyo, ni moja kati ya makosa kadhaa
yaliyobainika. 

"Sisi
tulibaini kasoro hiyo na mengine ya uchapaji siku ya
kukabidhi Katiba hiyo Pendekezwa na kuelekeza Katiba hiyo
ichapishwe upya baada ya kufanyiwa marekebisho," alisema
Dk Kashililah. 

Alifafanua
kuwa kuna vitabu vya aina mbili, kimoja kinachotumika kwa
ajili ya kumbukumbu, ambacho kina majina ya wajumbe wote wa
Bunge Maalumu la Katiba, wakiwemo wajumbe wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (UKAWA) na wajumbe wengine ambao si wa Ukawa,
lakini hawakushiriki kupiga kura. 

Kitabu
cha pili kwa mujibu Dk Kashililah, kimeorodhesha majina ya
washiriki wa Bunge hilo katika awamu zote, ambacho wajumbe
wa UKAWA na wengine ambao si wa kundi hilo hawapo kwa kuwa
hawakushiriki mpaka mwisho. 

"Baada
ya kurekebisha (kile kitabu cha kumbukumbu) ili kupata
kitabu kinachoeleza wajumbe waliopitisha Katiba
Inayopendekezwa, jina hilo lilipita kimakosa wakati hakupiga
kura, tunathibitisha hilo kosa kwa kuwa ni kweli hakuwepo
kupitisha Katiba hiyo," alisema. 

Alifafanua
kuwa katika orodha ya wapigakura, Mjumbe huyo wa
NCCR-Mageuzi, alikuwa namba 63 lakini hakupigakura jambo
ambalo haliathiri hata kidogo kura zilizopitisha Katiba
Inayopendekezwa. 

Pia
Dk Kashililah alitoa ufafanuzi kuhusu wajumbe waliopiga kura
kwa kusema jumla walikuwa 631, lakini baada ya mmoja
kufariki walibaki 630 na kati yao, 411 walikuwa wa Tanzania
Bara na 219 wa Zanzibar. 

Alisema
idadi hiyo ilipatikana baada ya mjumbe Salim Suleiman Ally
kuondolewa Zanzibar na kuwekwa upande wa Tanzania Bara baada
ya kuwekwa Zanzibar kimakosa. 

Katika
upande wa Zanzibar theluthi mbili ya kura zilizotakiwa
kupitisha Katiba Inayopendekezwa, zilipaswa kuwa 146, hata
hivyo Katiba hiyo kila ibara ilipitishwa kwa wastani wa kura
146 na 148. 

Kwa
upande wa Tanzania Bara, wajumbe 335 walipiga kura ambapo
kila ibara ilipata wastani wa kura 331 mpaka 334, na hivyo
kuzidi theluthi mbili iliyokuwa ikihitajika ya
274.

Katika
hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania
kupuuza watu wachache wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa
ni mbaya, na badala yake wajiandae kuipigia kura ya
kuikubali wakati ukiwadia. 

Rais
Kikwete alitoa ushauri huo kwa nyakati tofauti juzi kwa
wananchi mkoani Mwanza ambako yupo katika ziara ya kikazi ya
siku tatu, kukagua na kuzindua miradi ya
maendeleo. 

"Watakuja
watu kuwashawishi kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya,
wasikilizeni lakini tumieni akili yenu, kama ile hadithi ya
mbayuwayu. Jiandaeni tu kupiga kura na kuunga mkono Katiba
Inayopendekezwa kwa sababu hii ni Katiba nzuri sana,"
alisema Rais Kikwete. 

Alishangaa
watu wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, akiuliza
kuwa kama Katiba hiyo ni mbaya basi hiyo nzuri
ikoje? 

Aliisifu
Katiba Inayopendekezwa kwa kujali makundi yote ndani ya
jamii na kusisitiza kwamba kamwe haiwezi kuwa Katiba
mbaya. 

"Sijui
Katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani
ya jamii kama hii Katiba Inayopendekezwa. Hakuna aliyeachwa
– wavuvi wamo, wajane wamo, wafanyabiashara ndogo wamo,
akinamama lishe wamo, wakulima wamo, wafungaji wamo….kila
mtu yumo. Akinamama ndio usiseme kabisa wao wamepata hata
asilimia 50 kwa 50 ndani ya Bunge," alisema Rais
Kikwete. 

Aliongeza
Rais Kikwete: "Hivi katiba mbaya inakuwa kama
inayopendekezwa na kama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa
hivi nzuri ikoje?"

Imenukuliwa
kutoka kwenye gazeti la HabariLeo




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment