---------- Forwarded message ----------
From: Novatus Kambota <novakambota@gmail.com>
Date: Fri, 31 Oct 2014 10:14:48 +0300
Subject: Rais Guy Scott wa Zambia; jaribio lingine kwa wahafidhina wa Afrika
To: Abdallah Sulayman <aboodmsuni@gmail.com>, amichuzi
<amichuzi@gmail.com>, amani masue <kilinyepesi@gmail.com>, MUHIDIN
MICHUZI <issamichuzi@gmail.com>, Mroki Mroki <mrokim@gmail.com>, amani
boniphace <amaniboniphace@gmail.com>, francisgodwin2004
<francisgodwin2004@yahoo.com>
Na Nova Kambota,
Ijumaa, oktoba 31, 2014
Dar es salaam-Tanzania +255712 544237
Alipochaguliwa Barack Obama kuwa rais wa taifa kubwa zaidi duniani
Marekani, waafrika walifurahishwa na hali hiyo huku wakichagiza kuwa
hiyo ilikuwa ni silaha dhidi ya ubaguzi kwa waafrika.
Obama ambaye ana asili ya Kenya alipongezwa hata na wahafidhina wa
Afrika kwa kueleza kuwa hakuna watu wa asili wa Marekani isipokuwa
jamii ya wahindi wekundu pekee, hivyo kulikuwa na kila uhalali wa
mwanasiasa mwenye asili ya Afrika kuliongoza taifa hilo.
Sasa ni kama vile kibao kimegeuka, sasa ni jaribio tosha kwa
wahafidhina na labda waafrika wote, nazungumzia rais mpya wa Zambia Dr
Guy Lindsay Scott ambaye amechukua nafasi baada ya kifo cha rais
Michael Satta.
Hili si jaribio dogo hata kidogo, hasa kwa kuzingatia kuwa bado
waafrika wengi wanajitofautisha na wazungu kwa vigezo kadha wa kadha
lakini uasili, utamaduni na hata rngi zao, na hapa ieleweke kuwa
Zambia kiasili ni nchi ya kiafrika ambayo inapaswa kuongozwa na
waafrika wenyewe, inashangaza si haba kwa mtu mwenye asili ya Uskochi
kuingia Ikulu ya nchi ya Kiafrika akiwakilisha wananchi ambao hafanani
nao kinasaba wala kiutamaduni.
Watu wameanza kujipa matumaini hewa kuwa ni rais wa muda, huu pengine
ni uvivu wa kufikiri na labda ni kipimo cha kushindwa kutambua uafrika
ni nini hasa? Ama rangi au dhana/ideology?
Kwa siasa za Afrika Guy Scott aweza kuwa rais wa kudumu, kujikita
kutazama katiba ni kukimbia ukweli namna katiba za nchi zinavyovunjwa
barani Afrika ili marais kadha wa kadha waendelee kubaki madarakani,
ni muhimu kuzingatia kuwa uzoefu wa siasa za Afrika unaonyesha marais
kama Daniel Arap Moi wa Kenya ama Gudluck Jonothan awali walionekana
wa mpito lakini hali ikaja kugeuka , wakawa marais waliodumu
madarakani, je hili halitatokea kwa Zambia? Tungoje tuone.
Vipi Guy Scott akiwa mwenyekiti wa umoja wa nchi za Afrika (AU),
atakapowaongoza marais wenzake wa Afrika kujadili namna ya kupambana
na unyonyaji wa mabeberu wa magharibi , tusemeje hapa? Hiki si kipimo
kwa vyama vya upinzani barani Afrika kujitafakari namna vinavyojaza
wanachama mpaka nafasi za juu za utawala kwa namna Patriotic Front(PF)
cha Michael Satta kilivyoiweka Zambia kwenye kizungumkuti?
Kuna mengi ya kungoja hapa, lazima tusubiri tuone namna hali ya mambo
itakavyokuwa, dunia inasubiri kuona wahafidhina mithili ya Robert
Mugabe watampokea vipi Guy Scott? Watamkubali kama mwafrika mwenzao au
watampinga? Wapo wanaoona rais wa kwanza wa Zambia mzee Dr Keneth
Kaunda amebarikiwa kuishi muda mrefu kushuhudia nchi yake hiyo
aliyoipigania mpaka kupata uhuru mnamo mwaka 1964 ikipitia wakati
mgumu kama huu katika kitendawili hiki cha rais Guy Scott!
Nova Kambota ni blogger na mchambuzi wa maswala ya kisiasa anayeishi
Dar es salaam nchini Tanzania, anapatikana kwa namba za simu
+255(0)712 544237, barua pepe; novakambota@gmail.com, kwa uchambuzi
zaidi tembelea blog yake www.novakambota.wordpress.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment