Rais Msaafu Mzee Mkapa atoa ya Moyoni kuhusu Rais Ajaye.
Mwisho wa Siku Wenye Busara Hujiuliza Ni Nani Anakubalika? - Benjamin William Mkapa
Salaam;
Kama kawaida yake Rais Jasiri na asiyemumunya maneno leo kazungumza mengi sana wakati akihojiwa na Runinga ya Citizen kwa njia ya simu.Rais Msataafu Benjamin Mkapa alikuwa akihojiwa juu ya kifo cha Rais wa Zambia Hayati Michael Chilufya Satta aliyefariki leo huko jijini London.
Mkapa alisema namnukuu "Satta hakuitwa King Cobra kimakosa alistahili kutokana na uwezo wake ama wa kimaamuzi au wa kimsimamo. I am very sure that Zambians and we as African Nations will always remember Mr. Satta. Satta was always there for his people and our Continent at large. He said and stand for what he believed to be true and achievable; hesitation was never a good term to Satta.
So the pain I (We) faced when we lost Mzee Nyerere, Mzee Nkhurumah, Mzee Mandela, Mzee Kenyatta is the same we are facing today when we talk about Mr. Satta (Suffice it to say that we lost another hero in our Continent) May His Soul Rest in Eternal Peace.........."
Baada ya salaam hizo mwandishi alimuuliza Mhe. Mkapa vipi siasa zetu Afrika kama Rais mstaafu anaziona je?
Mkapa; Kawaida na sina kubwa la kusema japo kuna mengi yanatokea mengine ya hovyo mathalan waafrika wazee wetu walipigania sana ukombozi wetu ila nadhani wengi bado wana matatizo na wanahitaji kukombolewa kifikra manake kuna wenzetu wanatumika pasipo kujua na kusababishia Nchi zao kuingia ktk matatizo kama vita na wengi wao wameanza kujuta.
Hivyo ni lazma ifikie mahali watu waweze kujitambua na kujua ni yepi malengo mema kwa Bara letu ni yepi tunashinizwa......
Mwandishi kaendele kumuuliza Mhe. Rais Mstaafu Nchi yako mapema mwakani mnatazamia kufanya uchaguzi na mengi yamesikika hasa kwa wanaojitokeza na wengine kupewa adhabu kama Mwenyekiti wa CCM Mstaafu una lipi la kusema manake hata Mwl. Nyerere naye nyakati kama hizi hakusita kusema neno....
Mkapa; (Kicheko) nachelea kupata jibu sahihi ila niseme CCM ni Chama kikongwe na kina hazina kubwa ya kutosha. Na Katiba ya Chama chetu inaelezea kuhusu dhumuni ya Chama chetu kubwa ikiwa ni kuhakikisha tunakamata dola kuanzia Serikali za mitaa mpaka Serikali kuu.Sasa swali ni kwamva dola inakamatwa je?
Chama kama chama lazma muwe mtu anayeuzika na kukubalika ktk jamii kwa utendaji wake, haiba yake, wasifu wake (ndani ya chama na serikali) lakini vile vile ushawishi wake......Haya mambo ya umri na kadhalika sisi hatukutazama wakati huo ila si dhambi Vijana wakijitokeza manake hata wakati wangu Rais wa Sasa Mhe. Kikwete na kina Lowassa walijitokeza na leo unaona Kikwete ndiye Rais.
Wakati wangu Viongozi wenzangu wengi walihisi na kuamini kuwa sikuwa namuunga n mkono lakini mwandishi nataka nikuhakikishie hata kama mimi Ben Mkapa siko na Kikwete mwisho wa siku Wananchama ndio watakaosema wewe humtaki ila sisi tuachie huyo huyo......
Na hayo yalijitokeza mwaka 2005 Watu walimtaka Mhe. Kikwete sasa mimi kuwa Mwenyekiti wa Chama hakunipi Mandate ya kushindana na walio wengi na mliona alishinda kwa asilimia kubwa kweli kweli.Hivyo CCM ina taratibu zake na wanajua nani anafaa manake siasa hizi tuhuma zingine za kipuuzi kweli kweli sasa mkiendekeza tuhuma mwishowe mnakuta mnabaki bila chama na kwenye Siasa mkianza kutuhumiana hakuna wa kusimama....
Hivyo binafsi naamini Chama kitapata mtu safi na mwenye nguvu yai kukisaidia Chama na serikali na kuendeleza yale aliyoyaacha Mhe. Kikwete hakuna Chama duniani ambacho kinaona kabisa flani atatuvusha halafu kimwache hakuna manake huko ni kukiua Chama.Hivyo hata sisi vyombo vyetu vya ndani vilikuwa vinatueleza kabisa kwamba flani yuko vizuri sana ila labda kuna haka katatizo sasa hako katatizo tunakafanyia kazi kwa maslahi ya chama ya kwa maslahi ya huyo ajaye. Naamini ndivyo ilivyo hata mpaka sasa tafiti zimefanyika na naamini wamesikia watu wakisema wanamtaka nani na wakati wangu mimi Mgombea alikuwa amaeshatungiwa nyimbo na watu mbali mbali wenye mapenzi naye. Hivyo labda hata sasa yaweza kuwa hivyo....Waswahili walisema nyota njema huonekana asubuhi.
Nimalizie kama nilivyosema ukongwe wa CCM na viongozi wake naamini watapata mtu bora na mwenye nia njema na Taifa hili.....
Mwandishi Mhe. Mkapa katika waliotajwa naamini yupo mmona ama wawili ambao umeona wanaweza ama viatu vyako ama vya Mwinyi au vya Mwalimu au vya Mhe. Kikwete shirikiana nasi Mhe......
Mkapa (Kicheko) Hapa kwetu kuna kamati ya maadili (Mwandishi Kicheko) Mkapa anaendele mimi na wenzangu sasa Kikatiba ni wazee washauri hivyo Vikao vya Chama ndivyo vitakavyotuongoza......... Baada ya hapo nasi tunaenda na huyo huyo
Mhe. Mkapa naomba nikuulize swali la mwisho tumepata kusikia kumetokea muunganiko wa Vyama huko Tanzania kama hapa Kenya hilo unaliona je??
Mkapa; Sijajua sera zao na makubalinao yao yakoje na bado sijaelewa kama muungano ww COARD na JUBILEE twaweza kuufananisha na huu....... Otherwise I'd like to wish them all the best.....Mwandishi (Kicheko)
Nakushukuru sana Mhe. Mkapa kwa muda wako na tunakutakia afya njema..
Mkapa; Ahsante sana
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment