Friday 20 December 2013

[wanabidii] Taarifa kuhusu hafla ya kumkabidhi Rais Kikwete rasimu ya Katiba Mpya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed 
Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.

Imetolewa na:

Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
Desemba 19, 2013.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment