Thursday 12 December 2013

[wanabidii] Sheria kumsulubu Zitto kwa kukiri hana majina ya wenye mabilioni Uswisi

Na Beda Msimbe, Dodoma — MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema amesema wanashughulikia kisheria suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto kudanganya Bunge na Kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi. 

Werema ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kuchunguza madai ya mabilioni hayo amesema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Naibu  Spika wa Bunge kuiongezea kamati hiyo miezi sita.

Akitoa majumuisho ya  taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Werema alisema
alishangaa kitendo cha Zitto kutaka suala hilo liangalie mfumo na siyo majina ya watu walioficha mabilioni hayo.

Alisema awali yeye alishauri kuangalia mfumo wa uwekaji wa fedha hizo lakini Zitto alikataa na kusema anataka kutoa dukuduku kwa kutaja majina ya watu walioficha hizo.

Alisema mwezi Februari, Kamati ilikutana na Zitto na kuwaeleza kuwa ana taarifa na nyaraka na kutoa masharti lakini aliondoka ka kwenda katika kambi ya jeshi kwa mafunzo ambako kamati ilimfuata lakini bado aliwataka kukutana Dar.

Alisema Mei mwaka huu amekuwa akiichenga kamati hiyo hadi Oktoba ndipo alipokiri kwa kiapo maalumu kuwa hakuwa na jina wala akaunti ya mtu yeyote ambaye ana fedha nchini Uswisi.

"Jambo la kushangaza ni leo kudai serikali haina dhamira na suala la walioficha fedha Uswisi? Kwa keli Zitto Kabwe ni mzigo na sasa tunaingia kufanya kazi hiyo ya uchunguzi kama serikali kwa kutafuta taarifa bila kumuonea mtu," alisema Werema.

via Lukwangule blog

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment