Thursday 26 December 2013

[wanabidii] Mwaka 2014 amua kufanikiwa. Jilinde. Jipende. “Don't Die a Copy”

Ndugu zangu, tunapoelekea kuaga mwaka huu wa 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, nimepata muda wa kukaa na kumshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea, ninamshukuru Mungu pia kwa kupata marafiki wapya kupitia mitandao ya kijamii na pia kupitia mtandao huu wa WAVUTI. Kuna walionipigia simu na kuniandika barua pepe na kuna walionitembelea nyumbani Iringa kujifunza Kilimo cha Mboga na kile cha miti. Ninawashukuru sana wote. Karibuni tena na ninawatakia mafanikio mema kwa mwaka ujao. 

Mwaka ujao wa 2014 Usikubali watu wenye mtazamo hasi, watu wanao haribu majina ya wenzao, wenye viburi, watu wasiokuwa na shukrani kwa wenzao ama kwa serkali, ama ajira inayo kupotezea muda bila kutimiza malengo yako iendelee kukupotezea muda wako na kukuumiza kisaikolojia na kurudisha nyuma ndoto yako...  Jilinde, Jipende. "Don't die a copy."

Mwaka huu ujao, Jitengeneze kiasi ambacho utapendwa na kuzungukwa na watu watakaokusaidia kuyafikia uyatakayo (Malengo yako ama ndoto ya maisha yako)  na wafanye wafurahi kuwa na wewe. Wanaweza kuwa wateja wako, marafiki 
zako, waajiri wako, wafanyakazi wako,wasaidizi wako,nduguzako, wajasiriamali wenzako. wafanyabiashara wenzako mahali popote ulipo.

Fanya mambo ambayo yatawafanya wajue kuwa bila wewe yasingetokea. Uwezekano huo upo kwasababu wapo wengine wanafanya hivyo na tunawaona na kuwasikia. Mwimbaji mmoja wa nyimbo za njili wa hapa Tanzania ameimba kwa kusema ' katika yale yale yanayowatoa roho watu ndiyo hayohayo wengine wanafanikiwa.'

Hakikisha kuwa unatumia muda wako vizuri. Ishi maisha kwa manufaa usipoteze muda duniani. Muda ndio maisha yako ya kuishi duniani, wengine wanaendelea amka na wewe ufanye kitu. 

Jifunze na fanya mambo mapya kila siku ambayo hujawahi fanya hata kama ni mapya duniano.Kumbuka kuwa dunia hii itabaki kuwa na mapungufu siku zote kama hutafanya cha kwako cha kipekee ulichonacho. Jisukume kwenda mbele na kuwa huru kuishi kimanufaa. Na jifunze kutafuta uwezekano katika kila kitu kwani kila kitu kinawezekana kwa atakayetafuta njia ya uwezekano. Fursa zipo Tanzania na hakuna nchi yenye fursa za kufanikiwa kama Tanzania amua kufumbua macho uzione, zipo hata ukibisha zipo. Moyo wako, akili yako na mwili wako vikubali na kupenda kitu hicho hutachoka kufanya Na lazima utasababisha kitu.

Na kwa kipindi cha mwaka huu ujao, acha kuwanyooshea vidole wengine wewe fanya kwa nafasi yako na kwa muda wako kwa kuwa msaada kwa wengine. KUMBUKA Tanzania inarudishwa nyuma na watanzania wanaowanyooshea wengine vidole wakati wao hawajafanya kitu chochote. Kuwa 'role model' na 'mentor' wa watu. Jitolee ikibidi. 

Ukifanya hayo lazima dunia itageukia upande wako.Na ukumbuke kuwa ipo nafasi duniani kwa binadamu atakayeamua kujitengenezea nafasi yake. Kumbuka kuwa Tanzania haiwezi kutambulika bila wewe,haiwezi kuheshimika bila wewe na heshima ya Tanzania inaanza na wewe kimafanikio,kitabia,kiutamaduni, kielimu, kibiashara  na kimtazamo.  Jifunze kusema kuwa Tanzania ni yako na bila wewe Tanzania haiwezi kuitwa Tanzania.

Ninawatakiwa mafanikio mema kwa kwa mwaka huu ujao wa 2014, tufanye kazi, tuanzishe miradi, tununue mashamba ama viwanja, tuwe wapya, tuache lawama, AMUA KUFANIKIWA 2014.

meshackmaganga@gmail.com 0713 48 66 36/ 0767 48 66 36.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment