Friday 20 December 2013

Re: [wanabidii] Ujumbe wa Edward Ngoyai Lowasa Katika Kutumiza Miaka 52 ya Uhuru

Ukiona mtu amepita umri na bado anahangaika kutaka madaraka ujue kuna lake analotaka kutetea kwa kificho. Na ndio afrika vita haziishi, watu kuwa viongozi kama rais miaka 23-50 na bado anataka kuendelea kwa kubadili katiba au afanye ujanja achukue mwanae, nduguye, rafikiye, kabila lake. Ingefurahisha kama akina Mugabe wa TZ wangekaa pembeni kufanya shughuli za kuhamasisha maendeleo katika majimbo yao badala ya kuhangaikia uongozi wa juu wa nchi. Utakapoangushwa baada ya kutumia mihela mingi sijui utafanyaje. Ndio haya ya vijembe na majungu bungeni TZ na vita visivyoisha nchi jirani; Sudan sasa ipo tena kulekule ilikotoka vitani wanauana. Hapa yanazuka ya kikabila, pale ya maliasili kule ya udini mradi tu wanaotaka vyeo daima wasikose la kufanya kwa maslahi yao binafsi.Mabadiliko unaweza ukaleta kwa kushauri chama chako na viongozi wake ukiwa ktk hizo kamati sio lazima ushike hatamu kwani pale ujimboni umeleta maendeleo gani mpaka ukawe exceptional. Kusifu na undumakuwili ndio culture yetu ya kujipendekeza na ya tumboni street. lakini issue sio mtu fulani tu-jee wewe na familia, mtaa, kata yako manaleta mabadiliko gani pale mlipo hata huyo akija itakuwa change kubwa. kama ni kulimbikiza mifugo-unafanya makusudi hutaki kubadilika; kuoza vichanga-mwenyewe na sheria zipo; akibaka unashitaki kisha hufiki mahakamani unapokea blood money-wewe; unapanga biashara barabarani hukai sokoni-wewe; huchangii madeski au kuzoa takataka lakini unaingia video, kilabuni, mpira wa simba na yanga kwa mihela mara 500% ya mchango wa deski-wewe; unakata miti na kuchafua maji unywayo-wewe; unayemuunganishia mtu au kuunganisha bomba limwage uchafu barabarani usiite gari ay kunyonya-wewe; unayelewa pombe kutwa hujali hata kukandika nyumba tole la bure na pori limuekuzunguka-wewe; unanunua ardhi kubwa kwa jina lako lakini unamnunulia mhindi au mchina na kujifanya lako-wewe kisha unalilia umiliki raslimali-ni wewe mbongo; hulimi ngano within TZ unaagiza nje utuuzie mikate ni wewe kisha unalalama na umiliki raslimali wageni wananchi hawawezeshwi ni wewe ambae huwawezeshi kwa kulima ngano kimkataba wakulimie Monduli, Babati, Loliondo, Iringa, Njombe. Ni wewe tajiri wa madawa ya kulevya unayepiga kele nchi ina umasikini na mihela unajenga mijengo ya kupanda juu, malori yanayozidisha mizigo kuharibu barabara na hutaki kulipa kodi husika unatumia janja ni wewe mbongo. Kuja Lowasa kutabadili nini kama hatubadiliki wote kiakili kuwa na mitazamo ya maendeleo sio ufisadi kusubiri vishuke kama mvua.

Atakuja yeye Lowasa, na wengine TZ ktk uongozi-bado tutakuwa hapa hapa tunajifisadi hadi wabunge kufikia ufisadi wa daily allowance na unaona ukumbi wabunge mtupu, mweupe- hawapo; twasikia kuwa hela za safari kikazi-wanakwenda kuvinjari Dubai kula maraha badala ya kazi waliyopewa. Kisha-wakiwa bungeni hao hao kelele huyu ajiuzuru, yule hivi!!
Vijijini na mijini wananchi nao kuchukua sheria mkononi kwa jambo wakati mwingine ni jema likadhibitiwa kuzuia uharibifu mazingira au kuoneana-haikubaliki-ni mauaji, kuchoma vituo vya polisi ndio inakuwa solution. Tujipime-solution huenda sio Lowasa-attitude of mind yetu wote toka kaya hadi juu na orientation yetu ktk kutenda haki, kukubali ukweli na kutendea wengine haki na kujituma kwa maendeleo endelevu sio ubabaishaji ndani na nje ya kaya. Tuache na unduma kuwili.

On Wednesday, 18 December 2013, 13:44, Kenneth Masuki <kennymasuki@gmail.com> wrote:
Mollel

Mh Lowasa siyo "Waziri Mkuu Mstaafu" bali "Waziri Mkuu Aliyejiuzulu" kuna tatizo la kutofautisha kati ya hizi status mbili.

Sent from my iPad

On 16 Des 2013, at 19:42, lesian mollel <aramakurias@yahoo.com> wrote:

hao kina mh nanyaro sijui tuwaeleje, mh lowassa ndio kiongozi pekee aliekua ktk ile ndege, na pole anazopata anawawakilisha wale abiria woote walionusurika, its a simple mathematic, ila wao ni kila kitu against.
au hawajui huyu ni mh waziri mkuu msaafu na hadi leo ana ulinzi wa kiserikali, na still taifa linamtumia na litamtumia?
Tuwe fair wakubwa ktk kuangalia mambo

On Monday, December 16, 2013 6:33 PM, Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk> wrote:
----- Forwarded Message -----

Boxbe This message is eligible for Automatic Cleanup! (ngupula@yahoo.co.uk) Add cleanup rule | More info
When people fights you,sometime  is a good sign that you are at the top or heading there...Lowasa must be a threat to many at the moment specially those who think can positively compete him by hypocrisy...and the like...Americans said,Obama is an unseen hard worker,let him be a president. Lowasa is a wonderful hard worker,and thus nature has chosen him for presidency..am glad that I love him..There is nothing bad like fighting with nature...I think Jk too knows this...Ngupula

On Monday, 16 December 2013, 16:50, lesian mollel <aramakurias@yahoo.com> wrote:
hawa kina muhingo wametumwa, chuki tu za ajab ajabu.
acheni hizo, ngupula lowasa atapeta ti despite hawa wanaotumwa kumtuhumu bila ushahidi.
baba lowasa watanzania kibao wako nyuma yako, no retreat no surrender, till better is best

On Thursday, December 12, 2013 11:48 PM, Jeremiah Kibwengo <jerrykibwe@gmail.com> wrote:
Mgonge shida tuliyonayo ni kwamba kuna baadhi ya Watanzania wenzetu, ni vugugu yaani wanafiki. Wanapiga kelele pembeni siku viroboto wakijitokeza na kwennda kwenye majimbo yao kuomba kura kipindi cha uchaguzi, huku wakiwa wamebeba Mchele,Sukari, kanga, Kofia na T-shirt. Hapo utashangaa wale wapiga kelele wakiwa kimyaaaaaa huku wakifurahia zawadi hizo, na kuuza utu wao. Baada ya viroboto kupata kura na kushinda, utawasikia hao hao Wanafiki wakianza tena kupiga kelele, kuwa tunaishi maisha shida.
Watanzania kazi tunayo kubwa mbele yetu, sijui lini tutakuwa na Fikra Pevu.

2013/12/12 mngonge <mngonge@gmail.com>
Watanzania wanajitahidi kuchapa kazi kwa ajili ya maisha yao tatizo ni viroboto waliomo ndani ya nguo zao. Kila juhudi inafanyiwa hujuma na hao viroboto. Miili yetu lazima itazoofu tu kama hatutatambua na kujiweka mbali na viroboto hao

2013/12/11 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Tunu haza si Amani, Mshikamano na utulivu bali hayo ni mazao ya haki ambayo sasa kwa kuikosa vinajaribu kulazimishwa na matumizi ya Polisi. Lakini vitaweza kudumu kaka mafisadi wanaolinyonya taifa watadhibitiwa. Hapo wala hatutahitaji kuvihubiri ila vitakuja vyenyewe

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, December 9, 2013 11:49 AM
Subject: [wanabidii] Ujumbe wa Edward Ngoyai Lowasa Katika Kutumiza Miaka 52 ya Uhuru

LEO HII TAIFA LETU LINATIMIZA MIAKA 52 YA UHURU.

Kama taifa tuna kila sababu ya kujivunia Amani, Mshikamano, na Utulivu vitu ambavyo ni tunu pekee tuliyorithi kwa waasisi wa taifa letu.

Kwa sasa kila Mtanzania lazima awajibike na kutimiza wajibu wake ili Taifa lizidi kusonga mbele na kuwashinda maadui zetu Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Kwa pamoja lazima tumuunge mkono Mh Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika jitihada zake mbali mbali za kuliletea taifa letu maendeleo makubwa na ustawi wa kijamii.

Na pia lazima tukiri kwa dhati toka moyoni kwamba Mh Rais ameitangaza vyema Tanzania katika medani ya kimataifa na kwa sasa tumepata heshima kubwa kama taifa na kuaminika katika uso wa kimataifa (Hongera sana Mh Rais)

Pia kama taifa lazima tuendelee kujivunia rasilimali watu tuliyonayo na tuitumie vyema katika kuleta manufaa kwa taifa na hasa nguvu kazi ya VIJANA WA TAIFA LETU.

NAWATAKIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA UHURU WA TAIFA LETU

Edward Ngoyai Lowasa
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment