Tuesday 3 December 2013

Re: [wanabidii] TAMKO LA CHASO TAWI LA MOROGORO KUHUSU ZITTO KABWE NA KITILA MKUMBO

ebeneza KWAYU. wale wale wa machame investment. Duh


On Monday, December 2, 2013 12:09 AM, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO 

CHASO MKOA

S. L. P 1976,

MOROGORO

30 November, 2013


TAARIFA RASMI YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA CHADEMA VYUO VIKUU (CHASO) MKOA WA MOROGORO KWA VYOMBO VYA HABARI. 


Ndugu Wanahabari,


Ni matumaini yangu kuwa mu wazima na hongereni kwa kazi ya kupasha habari kwa umma wa watanzania. 
Tumewaita hapa kuzungumza na umma wa Watanzania kupitia ninyi, na tuna mambo machache ya kuzungumza na kupasha umma kuhusu yanayoendelea ndani ya chama chetu.


Kufuatia kikao cha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHASO Mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 30.11.2013, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi 8.00 mchana katika ofisi za CHADEMA Mkoa wa Morogoro, kilichohudhuriwa na viongozi wa vyuo vikuu vya Mkoa wa Morogoro (Wenyeviti, Makatibu,na makatibu wenezi), wajumbe wa mkutano kwa kauli moja wameunga mkono maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya Chama dhidi ya Zitto Zuber Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama makini na umakini wake umethibitishwa na maamuzi yake dhidi ya wahujumu chama na wanaojiona miungu watu ndani ya chama chenye sura na matendo ya kidemokrasia, na kinachomthamini kila mtanzania.


Kwa mantiki hii na kwa tukio hili lililofanywa mbele ya watanzania, ni dhahiri kwamba CHADEMA kimekomaa na kinafaa kupewa jukumu la kuiongoza nchi kwani maamuzi magumu (na yenye manufaa kwa umma) ndiyo maamuzi stahiki kwa chama chochote cha siasa nchini na kote ulimwenguni.


Vipo vyama vingi vya siasa nchini (mathalan CCM) ambavyo vimekuwa vikiwaingiza wananchi kwenye nyakati ngumu na dimbwi la umaskini kwa kuwa tu, wanawalinda mafisadi, wasaliti, na watu wenye maslahi yao binafsi.
Taswira aliyoionesha Zitto Kabwe ni taswira mbaya na haifai kuigwa na kijana au mtu yeyote kwani kinachoonekana ni kwamba ameyatanguliza mbele maslahi yake binafsi na kuyaacha ya taifa na chama chake.


Zitto Kabwe amehasi chama na taifa kwa ujumla na ameshindwa kutekeleza majukumu yake sawia kama chama kilivyokusudia hadi kumpa jukumu la Naibu Katibu Mkuu Bara, nafasi ambayo ni nyeti sana ndani ya chama kinachokuwa kwa kasi kama CHADEMA. 


Kama kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya chama, alikuwa na uwezo wa kuwashauri viongozi wenzake wa ngazi ya juu ndani ya chama pale walipokosea (kama kweli makosa yapo) na siyo kutumia nafasi hiyo kujitafutia mtaji binafsi wa kisiasa (personal political capital).


Kwa misingi ya hoja hii, hata kama kuna makosa yaliyofanywa na viongozi wenzake ndani ya chama, bado Zitto Kabwe hafai kuendelea kupewa jukumu lolote kwani kushauri mfumo (system) unapokosea ni jukumu la mwanachama yeyote na siyo kutafuta umaarufu ndani ya chama kwa kuombea viongozi kufanya kosa.


Wapo wanachama wanaokesha kwenye mitandao ya kijamii kuandika kwenye kurasa (pages) za viongozi waandamizi wa chama, wakiwa na lengo la kurekebisha au kutoa taarifa ya kukikuza chama hiki na kukilinda. 


Hii ni kutokana na kutokuwa na ukaribu wa kutosha na viongozi hawa ili wawashauri. Tunamsikitikia ndugu Zitto Kabwe mwenye ukaribu na access ya kuonana na kiongozi mwenzake yeyote anayemhitaji na wakati wowote anayahifadhi mapungufu ya chama mfukoni ili kesho anunue umaarufu binafsi yeye na familia yake.


Pia CHASO Mkoa wa Morogoro kupitia viongozi na wawakilishi wa vyuo vikuu, tunawataka wanachama wa CHADEMA kuwa na subira na utulivu katika kipindi hiki cha mpito ndani ya chama kwani chama kinategemea nguvu ya umma katika kufanya maamuzi yake na CHADEMA ndilo tumaini jipya kwa Watanzania. 


Pia tunawasisitiza wanachama na viongozi kutoterereka na kutumika kwa maslahi ya mtu binafsi au kikundi chochote chenye itikadi kinzani na ya chama na kuepukana na propaganda za wapinzani kwamba hoja giza katika maamuzi haya ni Hofu ya uongozi wa juu ndani ya chama (uenyekiti) jambo ambalo halina ukweli wala haliwezi kusadikika kuwa na ukweli wowote kwani yeye (Zitto) siyo mtu wa kwanza kuadabishwa na chama kwa utovu wa nidhamu binafsi na ya umma, wapo wakina David Kafulila, Danda Mjuju na wengine wengi ambao waliwajibishwa pale tu walipokwenda kinyume na chama na matakwa ya kanuni na katiba ya chama.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza,

Wenu katika Mapambano, 

Ebenezer F. Kwayu.

Mwenyekiti CHASO, Mkoa wa Morogoro 

Na

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa BAVICHA, CHADEMA 

0764013330

ekwayu@ymail.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment