Friday 20 December 2013

Re: [wanabidii] TAARIFA YA REGINALD A. MENGI KUJIBU MAELEZO YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUHUSU HODHI YA VITALU

Mzee, mpuuze tu, mkiendelea kulumbana mtaonekana wapuuzi wote, na kama kuna hoja ya msingi ni vyema kutumia vyama kama chama cha waagizaji mafuta, tccia, tic.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, December 20, 2013 6:40:47 PM GMT+0300
Subject: [wanabidii] TAARIFA YA REGINALD A. MENGI KUJIBU MAELEZO YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUHUSU HODHI YA VITALU

Baada ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe
16 Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza
mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na
mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya
Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho nimekuwa nikipigania. Hivyo basi,
kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013,
zimenishtua na kunisikitisha sana.

Ningependa kuwaeleza Watanzania wenzangu yafuatayo.

*Profesa Muhongo ni muongo*
Imefika wakati wa Watanzania kubaini kwamba Mhe. Profesa Muhongo ni mtu
mwenye hulka ya kusema uongo. Kwa mfano:

1. Kwenye kongamano la tarehe 8 Desemba 2013, Mhe. Profesa Muhongo
alisema kwamba moja ya kazi yake, alipokuwa akifanya kazi kama mwanasayansi
huko nje, ilikuwa kutabiri umuhimu wa sayansi katika uchumi wa dunia miaka
3,000 ijayo. Huu ni uongo wa mchana kweupe.

2. Mnamo Julai 2012 Mhe. Profesa Muhongo aliwaahidi Watanzania kwamba
hakutakuwa na mgawo wa umeme tena. Sote tunashuhudia mgao wa umeme
ukiendelea hadi sasa.

3. Mnamo mwezi Septemba 2012, Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa
akizungumzia mikataba ianayohusiana na vitalu vya gesi akisema kwamba
"baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa" na "sitovumilia
mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache". Baada ya
hapo, Mhe. Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji
wa vitalu vya gesi uliopangwa kufanyika mwezi huo na kupitia upya mikataba
yote iliyokuwepo awali. Sasa zaidi ya mwaka umepita na Mhe. Profesa Muhongo
hajarekebisha mkataba hata mmoja.

*Profesa Muhongo na takwimu zake za maeneo ya madini*

1. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu
kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Profesa Muhongo alitoa takwimu
za kuonyesha kwamba mimi ninamiliki eneo kubwa mara tatu ya Dar es Salaam
kupitia kampuni zangu tanzu.

2. Jumapili iliyopita mimi nilimjibu Mhe. Profesa Muhongo kwa
kumueleza kwamba takwimu zake kuhusu mimi ni za uongo, na vilevile hizo
alizotoa Bungeni pia ni za uongo na nilimweleza kwamba swali la Mhe. Tundu
Lissu lilikuwa ni "nani anamiliki maeneo ya migodi".

3. Katika eneo la kutafuta madini unaweza ukapata au ukakosa – ni
bahati nasibu, ndiyo maana maeneo ya utafutaji yanakuwa makubwa. Vilevile
wakati unatafuta madini shughuli nyingine za wananchi waliopo katika eneo
hilo huwa zinaendelea, kwa mfano kilimo, makazi, uchimbaji mdogo mdogo nk.
Unapopewa leseni ya mgodi inamaana kwamba tayari umeshapata bingo – madini
yapo na unaanza kuchimba. Kwa mantiki hiyo maeneo ya migodi inakuwa midogo
– isiyozidi kilomita 10 za mraba, na shughuli zote za wananchi katika eneo
hilo zinasitishwa.

4. Sasa kwenye maelezo yangu ya Jumapili iliyopita nilitamka wazi
kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja tu wa
uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja
ya mraba. Profesa Muhongo hajakanusha hili, badala yake anaturudisha
Watanzania kule kule kwenye maeneo ya utafutaji badala ya migodi.

5. Siyo hilo tu. Mhe. Profesa Muhongo anafahamu kwamba kuna aina 6
za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini. Lakini kwa makusudi kabisa
Mhe. Profesa Muhongo anafananisha leseni ya Mtanzania anayetafuta au
kuchimba kokoto na leseni ya mwekezaji wa kigeni anayetafuta au kuchimba
urani au dhahabu. Kweli unaweza kufananisha kokoto na dhahabu?

6. Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa utafutaji madini (mineral
prospecting) ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta ya madini kwa sababu bila
utafutaji hakuna ugunduzi na uendelezaji wa migodi hapa nchini. Lakini
kuanzia Julai mwaka jana Waziri Muhongo alipandisha tozo za vitalu kwa
asilimia kati ya 100 na 500. Matokeo yake Watanzania wengi wanarudisha
leseni zao na kasi ya ugunduzi wa migodi imepungua.

7. Nia ya mtu inajionyesha siyo tu kwa yale anayosema lakini bali pia
kwa yale anayoacha kusema. Sasa kama kweli nia ya Mhe. Profesa Muhongo ni
nzuri, kwa nini hatoi takwimu zinazohusu gesi? Kwa mfano, kwa nini
hawaambii Watanzania kwamba:

a. Eneo ambalo limeshatolewa kwa ajili ya mafuta na gesi lina ukubwa
wa kilomita za mraba 243,000 ambalo ni sawa na karibu robo ya eneo la
Tanzania nzima au mara 175 ya eneo la mkoa wa Dar es Salaam au eneo la
mikoa 9 ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha,
Shinyanga na Kagera.

b. Kwa nini Mhe. Profesa Muhongo hataki kuwaambia Watanzania kwamba
hakuna hata mzawa mmoja anayemiliki kitalu cha kutafuta au kuchimba mafuta
na gesi?
c. Kwa nini Mhe Profesa Muhongo hataki kuweka wazi kwamba vitalu
vyote 27 vya gesi ambavyo vinaanzia katika mpaka wetu na Kenya hadi mpaka
wetu na Msumbiji, vimegawiwa kwa wageni? Je, kugawa vitalu vyote vya gesi
kwa wageni siyo hatari kwa mustakabali wa usalama wa taifa letu?

d. Lakini cha muhimu ni kwamba Watanzania wafahamu kwamba gesi ambayo
imeshagunduliwa Tanzania inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 500 bilioni
wakati dhahabu yote iliyokwishagunduliwa hadi sasa na bado haijachimbwa
inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 60 bilioni kwa bei ya sasa ya dhahabu.

Kwanini Profesa Muhongo hawaambii Watanzania takwimu hizi?

*Profesa Muhongo na kauli zake kwamba Watanzania hawawezi kushiriki katika
mchakato wa mafuta na gesi*


1. Mara nyingi tumesikia kauli za Mhe. Profesa Muhongo kwamba
Watanzania hatuwezi kufanya biashara ya mafuta na gesi kwa sababu biashara
hiyo inahitaji mtaji mkubwa na utaalamu, vitu ambavyo Watanzania hawana.
Mhe. Profesa Muhongo amewahi kusema kwamba Watanzania ni wavivu wa
kufikiri, wavivu wa kusoma na washamba sana katika masuala ya uwekezaji na
kwamba uwezo walionao Watanzania ni kuuza juisi au soda. Huu ni uongo.
Watanzania wanajua wanachokisema na gesi yetu ni mtaji mkubwa sana.

2. Kwanza kabisa katika karne ya 21 utalaamu ni bidhaa ambayo mtu
asiye nayo anaweza kuinunua. Mhe. Profesa Muhongo anaweza asilifahamu hili
kwa sababu yeye mwenyewe hajawahi kufanya biashara katika maisha yake –
anayasoma masuala ya biashara kwenye makaratasi tu.

3. Namsihi Mhe. Profesa Muhongo akumbuke kwamba gesi ni mali ya
Watanzania na wana haki ya kuzaliwa ya kumiliki rasilimali yao ya gesi.

4. Mhe. Profesa Muhongo anataka Watanzania waamini kwamba kuna
mwekezaji wa nje anaweza kumiliki na kuendesha kitalu kwa fedha zake yeye
mwenyewe. Hii si kweli. Fedha zinazotumika ni za watu wengi waliowekeza
katika masoko ya hisa. Sisi pia tungehamasishwa na kuwezeshwa, tunaweza
kuunganisha nguvu zetu hivyo hivyo na kuwekeza katika gesi yetu kwa
kushirikiana na wageni. Mimi sipingi uwekezaji wa wageni. Watanzania nao
washirikishwe katika umilikaji. Mgeni aje mwenyeji apone, siyo mgeni aje
mwenyeji akose fursa ya kushiriki katika umiliki wa uchumi wake.

*Profesa Muhongo hana nia nzuri kuhusu ushirikishwaji wa Watanzania katika
gesi ?*

1. Katika kongamano lilofanyika tarehe 8 Desemba 2013 Mhe. Profesa
Muhongo alisema Watanzania wenye uwezo wa kifedha wazipeleke TPDC tarehe 10
Desemba 2013 na watapewa vitalu vya gesi. Vilevile alisema kwamba baada ya
tarehe hiyo, hoja ya suala la wazawa kumiliki vitalu litafungwa. Watu
waliokuwepo kwenye hilo kongamano walipigwa butwaa kwa sababu Profesa
Muhongo alishanukuliwa akisema kwamba kwenye uongozi wake wazawa hawatapewa
vitalu vya gesi na kwamba "suala la vitalu halina mambo ya uzawa".

2. Kwa kuzingatia kwamba maagizo ya Mhe. Profesa Muhongo yalikuwa ni
batilii (huwezi kutangaza zabuni kwenye kongamano) wafanyabiashara wa
Tanzania walimpuuza na hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Lakini kikubwa
zaidi ni kwamba haya mazingaombwe ya Mhe. Profesa Muhongo yalitufumbua
macho Watanzania kung'amua kwamba kumbe kazi ya TPDC ni kupokea maagizo tu
na anayegawa vitalu vya gesi ni Profesa Muhongo mwenyewe.

3. Nimekuwa nikirudia mara kwa mara kwamba mtaji sio tu fedha hata
rasilimali kama gesi ni mtaji.

*Hitimisho*

1. Ningependa kutofautiana na Mhe. Profesa Muhongo na kusema kwamba
adui wa maendeleo ya Watanzania siyo Watanzania wenyewe kama alivyosema ila
ni Watanzania wachache sana wenye kauli za dharau za kutuambia kwamba
Watanzania hatuwezi.

2. Katika suala la gesi mimi sipiganii mambo yangu binafsi, kwa
sababu mimi nimeshafanikiwa kibiashara. Ninachopigania ni Watanzania
wenzangu nao wapate fursa. Naomba nieleweke kwamba ninaposema Watanzania
nina maana kuanzia yule mfanyabiashara mdogo wa sekta isyo rasmi,
mfanyabiashara wa kati na wafanyabiashara wakubwa. Nataka kuwepo sera
ambayo itahakikisha kwamba wanawezeshwa na siyo kusema tu kwamba hawawezi.
Nafanya hivyo kwa sababu ninaamini kwamba utajiri uliobarikiwa ni ule
uliopatikana kwa njia halali na unatumika kusaidia wanaohitaji msaada.

3. Ni wazi kwamba Mhe. Profesa Muhongo anachuki binafsi na mimi. Hii
ni utashi wake, siyo lazima anipende na mimi siyo lazima nimpende. Lakini
suala la gesi ni kubwa mno kuliko mahusiano kati ya Mhe. Profesa Muhongo na
mimi – linagusa kila Mtanzania wa leo na wa vizazi vijavyo. Kwahiyo napenda
kumsihi ndugu yangu Mhe. Profesa Muhongo aache kuchanganya chuki zake
binafsi kwenye suala la gesi.


*Dr. Reginald Mengi*
*Dar es Salaam*

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment