Friday 20 December 2013

Re: [wanabidii] TAARIFA YA AWALI KUHUSIANA NA TUKIO LILILOTOKEA MALINYI MKOANI MOROGORO.

Gaston,
Naona umetumia maneno "wasukuma" wasukuma" mpaka mwisho wa story yako lakini wasukuma ni jamii inayojulikana kama jamii ya watu wapole na wakarimu Kitaifa. kama kuna uhalifu inawezekana unafanywa kwa level ya individual na sio kama unavyo jaribu kutuaminisha hapa na swala la ukabila sio vizuri madhara yake ni makubwa kuliko unachojaribu kukitafuta hapa. jamani tuhubili misingi ya sheria kufuatwa maana ni ahueni ya wengi kuliko tukikaa bila kufuata sheria watakao nufaika na hiyo misingi ya bila sheria ni wachache

2013/12/19 Gaston Kikuwi <kikuwigg@gmail.com>
Wanaopaswa kukamatwa kwanza ni Polisi.  Polisi wa kituo kilichounguzwa ni sababu ya kutokea kwa matatizo hayo.  Ni mara nyingi sana  Askari wameletewa malalamiko ya wenyeji kufanyiwa unyama na wafugaji, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.  Wiki iliyopita tu, Bwana Mmoja anaitwa Ngangari alipigwa na kuumizwa vibaya na jamii hii ya wafugaji wa Kisukuma.  Pasingekuwepo na wapita njia, bila shaka umauti ungeweza kumkuta.  Wahalifu hao baada ya kukuta watu wakakimbia. Baada ya kuokolewa na wapita njia na kupelekwa kituo cha polisi na kupewa PF3, alipelekwa hospital ya Lugala ambako amelazwa.  Pamoja na kutajwa kwa wahalifu hao, polisi wa kituo hicho hawakuchukua hatua yoyote, na inasemekana kwamba, wamepata kitu kidogo na wanasema kwamba wala hawajawaona ingawaweje wahalifu wapo na wanaendelea na maisha kama kawaida.

Miaka kama mitatu au minne hivi iliyopita, kuna mwalimu mmoja wa Dini, anajulikana kama kazimoto, alipigwa na wasukuma baada ya wasukuma hao kuingiza mifugo kwenye shamba lake na kula mazao.  Baada ya kuona hivyo, aliamua kuwakamata ng'ombe ili awafikishe kwenye vyombe vya sheria.  Lakini wasukuma wale baada ya kuona hivyo waliamua kumpiga sana na kuokolewa na majirani, alipelekwa hospital na kupwea PF3 na kukimbizwa hospital ambao amepata tatizo la bandama mpaka leo hii.  Kwa mshangao wa wengi hakuna kesi na wala hata wale wafugaji kuchukuliwa hatu ya aina yoyote

Hii ni mifano michache sana, lakini yako matukio mengi sana ya aina hiyo.  Chanzo kikubwa cha uhasama huo ni idara ya usalama na serikali za kijiji.  lakini lawama kubwa sana ni kwa idara ya usalama, haiko kwa ajili ya usalama wa raia, isipokuwa ni kwa ajili ya usalama wa walionacho.

Watu wa Malinyi, na wa Wilaya ya Ulanga kwa Ujumla ni wakarimu sana.  Kama mtakumbuka, wafugaji wa kwanza kufika katika Wilaya na Tarafa ya Malinyi walikuwa Wamasai ambao waliingia mnamo mwaka 1978.  Lakini kulikuwa hakuna matukio ya uhasama wa aina hii.  Kwa hiyo kama kweli serikali ina nia ya kweli na bwana  Chagonja yupo kwa ajili ya kutatua matatizo kama hayo, anapaswa kusimamia ukweli na wala si kauli za watu zinazosema kwamba "UONGO WA ASKARI SI UKWELI WA RAIA"  Kwa kufanya hivyo itakuwa si kumaliza tatizo bado kuongeza ukubwa wa tatizo.

Na kama ikiwezekana, askari waliopo katika kituo hicho kwa sasa wakaondolewa na kuletwa wengine

Kikuwi

2013/12/19 mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>

'There has never been a good war, nor a bad peace"
 
Do human beings subject themselves to be killed without reason?
 
Taarifa hizo za kwenda kujichunguza zitoe pia maelezo ya upande wa pili. Katika matukio mengi ambayo Chagonja amewahi kuteuliwa kuongoza tume, zile taarifa chache zilizopatikana, zilikuwa na maelezo ya uongo, mara kwa mara zikiwatetea askari na kuwalaani raia.
 
Tangazo linasema "ameenda kuongeza nguvu ili kuwakamata wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria". Kwa uzoefu, maeneno yanaeleka yanamaanisha nini!!
 
Mungu atubariki na nchi yetu, busara zaidi itumike, badala ya kupeleka timu ambayo tayari ni "judgemental"-iliyokwisha amua.
 
Lakini ngoja tusubiri tuone.
 
MJL

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Gaston G Kikuwi
SIDO Small Business House
Bibi Titi Mohamed Road
Block B, 3rd Floor Room No:-34
P O Box 15877, Dar es Salaam-Tanzania
Tel:- +255 22 2152 359
Cell:-+255 784 546 122
       +255 713 294 318
       +255 768 633 685
e-mail:-kikuwigg@gmail.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Athanace Motega
P.O.Box 6134,
Mwanza
Tanzania
Cel. +255 784 643 150
AMotega@gmail.com
"Successful people are successful because they form the habit of doing those things that failures don't like to do"

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment