Monday 16 December 2013

Re: [wanabidii] Re: JWTZ INUNUE HISA KWENYE MIRADI MIKUBWA


Kununua hisa, kuwa na miradi mikubwa utawafanya wasiangalie kazi na majukumu yao, kuja kujali pesa na wajanja wachache kujaa vitumbo. waache wafanye kazi yao ya ulinzi, walime mashamba na kujenga majumba yao kwa mkataba na GVT.

Tunachokielewa wengine ni kuwa: Ukiliingiza jeshi katika biashara-utapotosha malengo yake ya kazi yake ya kulinda usalama. Pia, kulikuwa na makosa katika sera za Mh Marehemu Nyerere katika kulitaka jeshi kuchanganyika na wananchi/Raia ili tuwe wamoja tofauti na jeshi la kikoloni likikaa makambini na kuogopwa. Likaongezewa jeshi la JKT, Mgambo na sasa ulinzi shirikishi.

Ktk kutanzua utata la JWTZ kuwa uraiani na ikaonekana wanajeshi na wake zao kushiriki zaidi miradi-matuta ya mchicha, mashamba ya mpunga na mifugo pale Lugalo tukiona mpunga kila kona na ming'ombe, mbuzi, vigenge na vioski ktk maghorofa yao (mwenge)- ikaja kubadilishwa.Mashamba yakaondolewa, mageti yakafungwa na miti kupandwa milima na mabonde ya Lugalo, Makongo-Kawe na njia za`kupita raia zikafungwa. Ulinzi wa mazingira ukawa issue.  Wakawekewa eneo maalum la mifugo michache ya maziwa ya watoto na duka lao ambapo watu wa nje hutumia kanjanja kununua mavyombo kwa bei rahisi hapo Lugalo darajani.

Eneo la usalama makubusho (ofisi ya Rais) wakakatazwa kulima mchicha. Ilikuwa biashara ya akina mama tuta moja 15,000/= wanunuzi kibap mijengoni. Mwenge JWTZ maghorofani-vibanda bomoa. JWTZ ikawawekea maduka ya kisasa ya vifaa na manunuzi ya mahitaji yao kwa bei rahisi na ikakodisha maeneo ya mabanda ya kisasa ya biashara hapo ukipita Mwenge darajani kwenda Lugalo. wengine tunahoji ukodishaji wa vibanda vya biashara kwa wengine ndani ya kambi ya JWTZ na usalama wa nchi.

Unapomfanya Mlinzi wa Nchi au wa nyumba yako awe muuza duka, mfanya biashara-atalinda usalama wakazi gani? Si ndio atachoka na kusinzia? Wawekeeni canteen maduka ya mahitaji lakini wasiingie biashara za uchimbaji gesi wala mirahaba ya madini. Jeshi la namna hiyo liwe JKT na Magereza. Kwani hawa wanaweza kuwa na vikosi vya ujenzi wakachukua mikataba, wakatumia makuruta kulima, wale walio katika miaka 2 kama service men and women ambao huwa kama Veta (st leavers wakikaa 2 years na zaidi) wakafanya kazi za mikataba. wafufue yale mashamba ya JKT na magereza walima maelfu ya ekari, kujenga majumba na barabara. wazoe mibaba ya vifua miraba mine inayozurura mjini kuuza used underwear na midoli wajae huko walimbe kwa trkta na power tiller nan kuvuna kwa combine harvesters, kupakia na kujaza maghala ya serikali na kuuza nje pia.

Tumekua tukiona wafungwa wakifanya useremara na kuuza vitanda na viti vizuri, wakijenga majumba ya serikali, kulima na kufyeka majani majumba ya waheshimiwa. hii inaonekana kupotea irudishwe. wakitoka na vyeti vya ufundi, zawadi za charahani na vifaa vya ujenzi-hii iendelee.

JWTZ wakipewa miradi ya serikali ya kujenda madaraja ya muda mfano lile na Msasani ukitoka Kawe na mengineyo maana wana mainjinia wa ujenzi wa madaraja watumikao wakati wa vita kujenga njia za kupitia. hii ni nzuri maana inasaidia baadhi ya maeneo-vijiji. wawe na shule zao za msingi, secondari ambako ni muhimu kwa wanajeshi kuwa na elimu ya juu hata vyuo na wapendao wengine wasome huko. Kuwatumia kujenga irrigation schemes vijijini waliko na makambi maana wanajua miundo mbinu. Ila msiwaingize ktk biashara za kuwapa faida wakubwa wachache wajae vitambi, kuingia ubia-waje wasahau kazi yao muhimu waione kero pesa itawale. Jeshi ni moja hao wa JKT, Magereza wataingiza vipato kwa wizara na majeshi yote.

Kama matajiri wa nchi wanajitetea na kuleta longolongo kuhusu Gas kwa sasa, lakini wamekaa kutokuungana kuunda makampuni makubwa wakachukua viwanda, mashamba makubwa yapo hawafanyi kitu. Viwanda Tanga, Morogoro, DSM, Mtwara vimekufa-mbona wamekula jiwe. kazi kujaza magodown waliyopewa marobota ya mitumba na spare za magari used. Tuone wananunua vifaa na kulima na kuingiza wananchi ktk mikataba wanunue, waendeshe viwanda kuuza nje na ndani ya nchi. Private sekta yetu umekuwa na Vibaka ambao kazi yao kulipa mishahara midogo waachijiwa, kuuzia wananchi madawa yaliyokwisha muda ndio wanaweka ktk private hospital zao, kuibia serikali madawa nan vifaa kupeleka mahospitali yao. Kuchanganya rangi ndio tomato sauce sio kuweka mashamba ya vijana ya nyanya wanunue. Ndio kuuza soda za rangi-matunda yanaoza Ulanga, Lindi, tanga na kwingineko. Kisha kupanda`majukwaani kujidai eti wazawa hawapewi fursa-uletewe kinywani? Mifugo inazurura hovyo-umesaidiaje kuwafanya wafugaji wafuge kisasa ununue mazao yao? Unasaidia kuuwa tembo na ukataji miti na kununua mbao-msitu wako upo wapi wewe muuza mbao binafsi? Huna msitu wa pine au mininga ila unasaidia uharibifu ktk nchi yako.

Miradi Mikukbwa waachie hao tunaowaona wanagombana na Mh Muhongo majukwaani-tuwaone wajivue GAMBA wafanye kweli sio maneno tu na uwekezaji wa gas unataka mamilioni na ukikosa imekula kwako!!  Waachie JWTZ miradi ya ujenzi ya GVT (ya majengo yao na vikosi vingine au nyumba za DC, RC) ili majengo hayo ya GVT yasichakachuliwe-wao na magereza wajenge ghorofa zao badala ya kuwapa wakandarasi uchwara. Wapewe mikataba ya kufundisha majeshi nje ya TZ-italeta kipato. wapewe mazingira masuri na elimu kwa ajiri ya job satisfaction. Wapeni madege mabovu ya ATC na mengineyo ya serikali wayafufue na wataalamu wa nje watumie ktk kazi zao sio yanaoza tu viwanjani. watumieni wastaafu wao ambao wengi bado vijana wawe walimu wa ufundi vyuoni.

Ili ulinzi uwe mzuri na JWTZ na hasa police watekeleze sheria-waondolewe kuishi mitaani ambako wanachanganyika na raia (sera ya baba wa taifa) kuzoeana na wahalifu, kuunda urafiki ambapo wanashindwa kuwakamata watendapo maovu hao wahalifu. nao kuogopa usalama wao ambapo anaweza kufanyiziwa uswahilini akitekeleza sheria. Hivyo anachukua rushwa na kuacha maovu yanaendelea. Kisasi kinafanya wanaotakiwa kutenda haki kuacha kufanya hivyo. Rudisha askari makambini na mahakimu wa serikali katika majumba ya GVT maeneo maalum kwani ule ujamaa na kuishi pamoja umeshindikana ktk akutekeleza sheria kwa KISASi na uswahili kutawala. Mkoloni hakukosea kuweka quarters zao magomeni, oysterbay au maeneo maalum ya GVt na ulinzi.


On Sunday, 15 December 2013, 21:18, Arbo <akihaule@gmail.com> wrote:
......Chunga sana sana umuonapo  Simba akijihusisha na  kilimo cha umwagiliaji maji; hususani wa  majani yaliwayo na swala  mbugani..nyakati za kiangazi.... 

On Sunday, 15 December 2013 10:50:09 UTC+1, Yona Fares Maro wrote:
Ndugu zangu ,

Jeshi la nchi jirani ya Rwanda yaani RPF limenunua Hisa kwenye kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Afrika Kusini ya MTN pia imenunua kampuni kadhaa katika nchi nyingine kama sehemu ya kuboresha kipato cha jeshi hilo la Rwanda .

Hapa kwetu sijawahi kusikia Jeshi likijishugulisha na shuguli za uwekezaji mkubwa au kwenye biashara za ushindani kama wa simu za mikononi , migodi ya dhahabu na Kilimo .Niliwahi kusikia moja ya mchuchuma ambayo ilileta kelele kidogo .

Ni vizuri Jeshi letu kuachwa liwekeze kwenye maeneo mengine yenye faida kwa Jeshi hilo kwa kununua hisa kama kwenye kampuni za simu , migodi ya dhahabu , kwenye vitalu vya gesi na hata kwenye utafiti .

Tunasikia kwa mfano uwekezaji katika gesi ni gharama sana , hivi jeshi linashindwa kuwekeza huko mpaka tuombe mikopo mikubwa mikubwa ? Jeshi linashindwa kuuziwa vifanda na mashamba makubwa kwa ajili ya kuwekeza kweli ?

Hawa vijana wanaoajiriwa kwenye majeshi yetu kila siku wanaenda huko kufanya nini kama hawatumiki kwenye shuguli nyeti na muhimu kwa taifa kama hizi ?

Jeshi lianze kutafuta fedha lenyewe za kujiendesha na kidogo litapewa toka serikali kuu .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment