Monday 16 December 2013

Re: [wanabidii] Clement Mabina auwawa na wananchi wenye hasira , Mwanza


 

Mh Mhingo nakubaliana na wewe 100% kwa 100%!

 

Waingereza wana msemo wao kwamba "The chicken have come home to roost", kwamba hawa sasa wamerudi kudai himaya yao.

 

Si sahihi na wala si vema kuhukumu, lakini mwendo wa marehemu Mabina hauna tofauti na mwenendo wa "wakubwa" wetu wengi. Kwamba wao sio kama sisi, na vyombo vilivyowekwa kusimamia haki na usawa haviwahusu wao kwa sababu wao wako juu ya sheria-"primus inter pares". Kwao usawa mbele ya sheria haupo-" salus animarum suprema lex"-Sina uhakika lakini naweza kuthubutu kudhani kuwa wakati akikaua kale katoto, hakuwa na chembe ya ubinaadamu wala hakuwa anahisi kitisho chochote kwake, maana, ni chombo kipi kingemuwajibisha, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa na Diwani anyezozana na watu wake. Hivi kwanza hata huo udiwani alishindaje??. Raia wale walilijua hilo. Mtoto wao angeishia kufa kibudu, wakaamua kujichukulia sheria mkononi, na kutoa adhabu waliyoona inasadifu ukatili waliofanyiwa.

 

Kwa hili, niwasihi watanzania tufunguke macho. Watanzania wenzetu sio kuku. Ni binadamu. Kadhia hii itukumbushe kuwa sasa watanzania wanataka uwepo wa haki, na kwamba haki hiyo isipopatikana kwenye vyombo tulivyojiwekea, wataitafuta kwingine.

 

Binafsi sina masikitiko, wala sababu ya kumhurumia huyu bwana. Sipepesi macho.Kifo chake kiwakumbushe wakubwa wenzake. Majogoo wamerudi nyumbani, na wanaitaka himaya yao.

 

Tuzidi kutafakari!!

 

MJL 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment