Monday, 9 December 2013

Re: [wanabidii] Re: ATHARI ZA MVUA ZINAZONYESHA MKOA WA DSM

Tutakapoacha tabia ya uchafu ndipo tutakapoishi katika miji na mazingira masafi. SOMA UKIPENDA HAYA HAPA CHINI KAMA MCHANGO WANGU

Fikiria kampeni za mtu ni Afya baada tu ya kuanzisha vijiji vya ujamaa. Mradi wa Usafi wa mazingira mijini na uenezaji wa vyoo bora vya kisasa vinavyopunguza mazalia ya nzi na mtu wa matende kwa asilimia 80. Kulifanyika utafiti mkali wa mineralization of excreta na kuenea kwa mbu wa matende na mabusha ambao matokeao ya sanitation studies, uchafunzi wa mazingira na tafiri za afya hizi  ukaleta taasisi za NIMR na NEMC. Hela za wazungu misaada na  Mkopo wa World Bank kuboresha usafi wa mazingira DSm na Municipalities TZ (Urban Towns) na kuwekwa maofisa mazingira kusaidiana na Bwana afya. Kuundwa kwa DSD na DSSD ambayo sasa ni DAWASA na DAWASCO na kuruhusu sasa kuzoa taka na kunyonya maji taka iwe under private sector kupunguza gharama kwa public sector.  Shughuli hizi zikaja na mkopo wa choo (VIP latrine) vyoo vya mnfano 100 kila kona ya low income area DSM kumfanya mwananchi wa TZ mijini aishi ktk usafi. Ndio kwanza kinyesi ni tatizo. Mkopo wa world bank kupima viwanja Site and Services sinza, Tangi Bovu, Tegeta, Mbagala etc na Viwanja mediun and Low density maeneo mbali mbali Mijini-Mkopo wa World bank. Leo kaangalie maeneo yaliyopimwa na kuwekewa bomba za maji kila baada ya mita 400 (sinza, low income area, ikiitwa sinza machinjioni harusu ya kinyesi cha ng'ombe)-kuna bomba la maji utaliona? Ndio kwanza wamejenga mpaka juu ya bomba la maji wakabomolewa miaka ya karibvuni na wanarudia tena kujenga. Huko kuna sewer pipe? Ni kuiba manholes za cguma na kujaza takataka ndani ya shimo ambazo kukwama na kufanya kinyesi kifurike.

Jee, miradi ya Buguruni squatter upgrading na kuweka sewer pipe mpaka depot ya vyoo bora mtu unakwenda kununua parts mbali mbali utakazo. Mkopo wa choo bora ulitolewa (walilipa? wakaua mradi). Wakaondolewa Buguruni kupimiwa viwanja high na medium density Mabibo-Makuburi. Leo kaangalie kama unapita kwa gari kunapitika huko. maeneo ya Taasisi taluwekwa mabibo, Kijitonyama, ya viwanda Mbezi-tangibovu kwenda RTD ya Kunduchi. Hela ambayo huenda hadi leo hatujamaliza kulipa. hata hizo nyumba zilizokuwa za NHC Mwanayamala, Tandika, Magomeni yote, Mburahati, Kinondoni you name it, zilipangwa mstari, viwanja vya kucheza watoto, city centres za burudani majengo ya kiwepo na yakiwa pia ni eneo la nursery school. Tanzania -biashara kichaa. Tusipokuwa wakali na kuipenda nchi-mipango yote ya ardhi, afya, maendeleo haitofika popote ni gharama tu. Vinchi vidogo vitatupita kwa maendeleo na usafi. Mji wa DSm ni makorokoro ndani ya maghorofa yapandayo juu.

Kijiji cha MWENGE cha mfano cha Baba wa taifa JK Nyerere alitaka kiwe cha mfano mjini-kikiwa na Cooperative Union, Nyumba mjengo mmoja, viwanja vya michezo, kupumzika, zahanati. Jee hayo maeneo kwa sasa si vurugu tupu, bar kila kona, moto unawaka kila nyumba kuna mapishi, takataka kila kona kuna lundo; wameziba feeder roads hawajali hata hatari za moto ambao unawaka kila nyumba eti kuganga njaa. hapa moyo wa mapishi, nyumba ya pili ni duka la dawa ambapo nyingine ni viripuka, nyumba ya tatu duka linauza gas ya kupikia ipo ktk mitungi, ya nne garage wanachoma vyuma vitoavyo cheche na mataka kibao. haya yote tunayaona na bado unatkuta watu wanauza nyumba kariakoo maghorofa yanajengwa wanahamia bondeni kwenye hatari. pita njia ya kwenda CCBRT-mikocheni uone mapishi kila nyumba na wamivyobananisha njia zilizoachwa wazi ili kupita watu na za msaada wakati wa hatari.

Angalia mto Ubungo ulivyojaa takataka na wanavyouchimba mchanga na hapo hapo ubungo darajani mtu anafuga ng'ombe ambao kinyesi mvua ikinyesha kinaingia mtoni. Mbunge wa ubungo anaona vijana wanavyoharibu mto ambao unatanuka kuangusha nyumba na utaangusha milingoti ya Tanesco ila kelele bungeni na majukwaani sio kuelimisha na kukaa na watu wako waache uchafu, watumie fursa hii ya wakandarasi wa kuzoa tata wawachaguao wenyewe na kushirikiana kuweka usafi maeneo yao na kuchangia hela ili vijana wao wazoao taka walipwe mshahara. Hakuna tena misaada na mikopo ya world bank ya sewerage and sanitation street sweeping activities ni 'Polluter Pay Principle'. Wewe utoae uchafu wa taka ngumu na kinyesi na taka maji ulipie uzoaji na ulinde mazingira yako-participatory env sanitation. wacha watupe taka hovyo, zinakwamba ndani ya open drain na sewer line na kurudisha uchafu wote ndani ya nyumba zetu, kuharibu biashara zetu, kufukuza wateja, kutupa hasara kimaisha na kibiashara. Na bado hatuna mental memory kuona yanavyotokea kila siku ili kujipanga tusiyarudie yakajirudia. Bwana afya au kiongozi wa mtaa akimfuatilia mtu anayechafua-anajitakia kuchomewa nyumba moto, kupigwa au kuadhibiwa vinginevyo. Si mijini hadi vijijini visasi ndio tija. hata vijijini kulikokuwa na donor supported programs za water supply and sanitation-ni hadithi tu alama ya kulikuweko bomba. O &M hatujali. hayo mabwawa funded na TASAF na wananchi kuchangia 20% ndio wafugaji wanaogeshea na kunyweshea mifugo na siasa inaona waachiwe huku magonjwa ya maji machafu yakipamba moto. Wao ni kura tu sio kuhakikisha kuwa mfugaji anafuga sustainably sio beyond land carrying capacity pale kwao alipo.

Hizi athari tuZionazo sasa ni za kujitakia. RC  wa DSM Melk Sadiki alisema 'hana muda na wanaojitakia madhara na wala hawatoona boat ikienda kuwaokoa kama ilivyokuwa miaka uliopita wakapelekwa mabwe pande'. Baadhi wakagoma kuhama.

Huko jangwani ni kinyesi, uchafu na mazingira hayo mtu anasema ameyazoea. Hata UNDP, Kinondoni Municipality, ILO, UCLAS walipoboresha Hananasif (Kinondoni  Mkwajuni) kwa mifereji iliyosakafiwa kuondoa maji majumbani, barabara safi, SACCOS, vituo vya maji wakiuza kuingira hela-wameuza maeneo yaliyoboreshwa na wamehamia bondeni kwenye kinyesi. walikouza ni macassaino, bar, majumba ya matusi. Kiwe na sheria ya kuzuia kuuza eneo linapoboreshwa mpaka ofisi husika na uboreshaji itoe kibari. Na hivyo ndivyo mradi wa CIUP mijini unaoshirikisha wananchi kuboresha maeneo yao yasituame maji, yapangike, yapate hudima muhimu (Mkopo wa World Bank) utakavyoshindwa kuwa na mafanikio ya muda mrefu kutokana na tabia zetu za kipumbavu za kutokujithamini na kuthamini mangira bali hela kisha unamalizia ktk vivalo, sherehe ya arusi uonekane na kurudi kuishi ktk kinyesi.

Tutupe takataka ndani ya mifereji ya majitaka, mtoni, ndani ya sewer line, tuhamie mabondeni kuona tupo mjini hata uuzapo nyumba kwa bilioni huendi nje ya mji. Tunajiangamiza wenyewe kwa kiburi na tabia za uchafu na kutokujali majanga.

Bado janga moja kubwa laja-kutokutenga barabara itokayo bandarini kuipitisha Pungu-Mbezi-Kibaha-Moro-Mbeya au Chalinze ndani kwa ndani itokee Korogwe-Same-Arusha ambayo itakuwa ya Malori tu yaendayo au yatokayo bandarini. Hiyo gari za abiria, ndogo zisizo malori ya mafuga na mizigo yasipite. Hii itapunguza msongamano na hatari endapo tanker na petroli litaripuka katika foleni ndefu ambapo mamilioni watakufa na nyumba kuteketea. injinia wa transport anapokwenda kusoma ulaya na study tours maana yake nini akirudi hatumii mafunzo katika kuweka barabara za kazi tofauti? kama gari ya abilia-bodaboda ikipita huko-inachukuliwa na kuuzwa directly hii ndio itakomesha ule uswahili wetu. Maana kwa sasa njia za miguu bodaboda, bus la abiria, bajaji zinapita na kudhuru watu na mazingira. wacha tuzame, tunajitakia.

Vyuo kama UCLAS, Maji Institute viko ktk mazingira ambapo wananchi wanatupa taka mtoni na madaraja yanachimbika. Hapo wanatoa degree za mazingira, maji, waste water and sanitation engineering. Field practice wanafanyia wapi? Kwa nini mazingira ya hapo jirani ya malundo ya mataka mitobi, mtaani wasishughulikie kwa kutumia wanafunzi wao kuwa na regular field practice and monitoring ya mazingira, kuhusisha wananchi waliozunguka eneo lao la chuo kila mwaka kuwa mfano. haipendezi kuona nje tu ya chuo cha maji au uasafi wa mazingira au kilimo, au school of medicine ndio kuna vinyesi vinafurika, taka malundo, degradation milimani na kiliumo kisicho endelevu a few meters/kilometers kutoka chuo. Hebu vyuo vyetu pale vilipo viwe mfano. Field practice isiwe lazima usafiri ukawatembelee ili upate night allowance-hata pale chuoni mlipo na jirani il;i wananchi nao wawatambue na kuwaheshimu na kuwafanya extension workers wa kata, halmashauri wafanye kazi yao kikamilifu. Sajabu hata ukiingia nyuo vya sanitation engineering utakuta vyoo vya wanafuzi vimefurika na ukizibua utatoa vyupa vya maji ya uhai, mifuko ya plastiki; pale penye civil and construction engineering utakuta hata material testing lab yao imebomoka ceiling board, ngazi zote na mifereji ya chuo kizima cement imebomoka na practical training ktk repair hakuna na consultancies zinafanyika na idara zinaingiza hela.

Pale penye degree za revenue na commerce ndio business zote zilizopo chuoni pamoja na maduka, cafeteria, canteen, bar, photocopy and stationeries vendors hazina mashine ya TRA na wala hawatoi risiti lakini degree za revenue na taxation zinapatikana na kofia zinavaliwa na wanunuzi ni walimu na wanafunzi ambao hawahoji maduka hayo kuwa mfano. Kodi hizi zingesaidia maendeleo ya nchi hata chuo husika.
Hivi, ndio tutahoji watu kukaa mabondeni, ujenzi wa kuzina feeder road za kurahisisha kuzoa takataka, kunyonya vyoo, kuzima moto unapotokea? tutahoji maji kufurika barabarani na waheshimiwa viongozi  na mabalozi wote wanaogelea maji hayo? Hii TZ ni nchi ya ajabu. Tunaona-ila ni vipofu, tunasikia-ila ni viziwi, tunabwata yale ya kupigana piganga tu hakuna anayekuwa mfano halisi-sote dugu moja uwe tawala au mapinduzi kote kuna uharibifu na mtindio wa aina fulani. Tubadilike tuwe wasafi.

Usafi hatuwezi-ndio tutaweza kumiliki raslimali tutazivuna kwa faida? Unauza nyumba kariakoo bilion 3 uliinunua kwa elfu 60,000/= kwa mkopo tena unahamia kinyesisi na mwaka ukisha huna hata senti? Mtindio huu ukomeshwe. una ng'ombe 800, mbuzi 100, ndodoo, 20 punda 5 unaishi kufuata maji klm 5, nyumba duni, kinyesi kila mahala na huna choo wala watoto hawasomi-Mtindio. Mijini kuchafu maji yanajaa, vijijini kuchafu maisha duni. udogo na maji mvua ikinyesha wa bure ila hukandiki nyumba wala kuezeka na nyasi huhunui ni za bure. Manpower unayo watoto 60, wake 5-10. wanasiasa wapo kujinadi sio kubadili maisha ya raia wao kwa kukaa nao kuongea yote haya ili wabadilike. Tubadilike.


On Sunday, 8 December 2013, 13:00, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Hapo ni maeneo ya sinza nimeambiwa 


On Sunday, December 8, 2013 12:39:50 PM UTC+3, Yona Fares Maro wrote:
Ndugu zangu ,

Naomba kujua athari za mvua zinazoendelea kunyesha siku ya leo kwa maeneo mbalimbali ya mkoa wa dare s salaam .

Kwa ufupi hapa Chuo kikuu cha Dar es salaam maji yamejaa kweli kweli maeneo mengi yana maji na baadhi ya mitaro imefurikwa na maji na kuzibwa kabisa .

Huko mwenge nilisikia umeme ulikatika kwa muda pamoja na radi la mara kwa mara 

Maeneo ya mlimani city haswa kwa kutokea kwenye ile njia ya kwenda savei napo maji yamejaa na kuna msongamano wa magari .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment