Thursday 5 December 2013

Re: [wanabidii] MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA AJIUZURU

Huko chichiemu ndo kabisaaaaa


2013/12/5 mngonge <mngonge@gmail.com>
Wengine ndo tunatafuta chama cha kujiunga ambapo hakuna ndiyo Mzee au mangumashi, je CCM ndipo hakuna ndiyo mzee au chama gani? Nisaidieni mwenzenu nipo njia panda

2013/12/4 lesian mollel <aramakurias@yahoo.com>
mh lissu hapo pia umekosea,kwanini hadi mtu aondoke ndio aonekane mbaya, basi chadema uchafu upo mwingi,kama mzee tu moani kala pesa na hamjamwajibisha basi hadi taifa hapo kuna jambo na zitto might be right alivyokua anawakomalia mpeleke hesabu za ukaguzi kwa CAG.
Cjapenda hii hali ya majibu yako hata kidogo, ni kuonyesha namna uchafu ulivyo na ni advantage kubwa kwa your rivals.......kuna kazi kwa demokrasia yetu, hii ni sawa na taarabu, akiimba huyu hivi kesho majibu kwa kuibua nawe majibu.
nawashaur cdm mkae mjitathmini na mpen makene kaz ya usemaji , uongozi  ktk siasa ni uvumilivu...igeni mfano wa mh Edward  Nguyai ole lowasa anavyojua kuvulia na akijibu hoja anajibu kwa busara kabisa, na ndio maana mimi namuunga mkono kama Rais mtarajiwa, tho sina chama yet
busara ktk uongozi ni muhimu
si kila jambo mtolee majibu




On Wednesday, December 4, 2013 2:10 PM, Magora Hassan <magorah15@gmail.com> wrote:
Hawa chadema wanatoa siri zao za wizi wa pesa za kampeni.Vita ya panzi.............,
majibu yote 2015 ,TUTAJUA CHAMA KINACHOPENDWA ZAIDI NA WANANCHI,NANI FISADI,NAZI MSAFI,NANI MWANA DEMOKRASIA WA KWELI.
Rgrds
Magora
On Dec 4, 2013 11:14 AM, "Abdalah Hamis" <hamisznz@gmail.com> wrote:
Kwenye barua ya kujizuru mwenyekiti wa Singida amemtaja Tundu Lissu kuwa sehemu ya wavamizi wanao iua CHADEMA haya ndio majibu ya TUNDU LISSU:-

Kwa vile aliyejiuzulu ni Mwenyekiti wangu wa Mkoa, na kwa vile amenituhumu specifically kuwa ni mmoja wa 'wavamizi' ndani ya CHADEMA ambao ndio 'vinara' wa migogoro ndani ya chama chetu, nafikiri nitasemehewa nikiweka utetezi wangu hapa jukwaani.

Wilfred Kitundu is probably the longest serving regional chairman wa CHADEMA katika nchi hii. Na ni kweli, Kama anavyosema, kwamba kwa muda wa karibu miaka ishirini ya uenyekiti wake, sebule ya nyumba yake ilikuwa ndio Ofisi ya chama ya Mkoa. Which is another way of saying, kwa miaka yote hiyo, chama hakikukua. 

CHADEMA haikuwa na Mwenyekiti wa kitongoji, wala wa kijiji, wala Diwani, achilia mbali Wabunge. In fact, viongozi wetu wa kwanza wa kuchaguliwa - wenyeviti wa vitongoji na wa vijiji - walichaguliwa mwaka 2009, mwaka mmoja baada ya mimi kuvamia na/au kuhamia CHADEMA Singida. Mwaka 2010 tulipata, kwa Mara ya kwanza tangu mungu aumbe mbingu na nchi, Wabunge na Madiwani wasiokuwa maCCM. 

Sitaki kujisemea sana katika hili, lakini nafikiri mchango wangu katika kuijenga CHADEMA Singida ni mdogo. On the other hand, zaidi ya kutuwekea Ofisi ya Mkoa sebuleni kwake, sidhani kama Mzee Kitundu ametoa mchango mwingine wowote katika mafanikio haya. Zaidi ya kula pesa zetu za kampeni ya udiwani katika Kata ya Urughu mwaka 2011 wakati wengine tukiwa kwenye mapambano ya uchaguzi mdogo wa Igunga, sidhani kama nitakuwa namsingizia Mzee huyu nikisema kwamba hatujamwona akishiriki kwa maana yoyote katika harakati za kisiasa za CHADEMA Singida. Mtu aliyemwokoa kutokana na hasira ya wanachama baada ya kula hela za kampeni kata ya Urughu ni ....... Jaza mwenyewe!!!

Mwaka huo huo wa uchaguzi, kulikuwa na skandali ya mgombea ubunge wetu wa Singida mjini kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi kwa maelekezo ya Mh. Zitto Kabwe. Mtu aliyetumiwa kuweka pingamizi ili mgombea wetu aenguliwe alikuwa wakati Mwenyekiti wa CHADEMA Singida mjini Wazaeli Nakamia. Tulipambana hadi tukamrudisha mgombea wetu kwa kushinda rufaa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mzee Kitundu hakuwahi kusema chochote, either way, kilichokuwa kinaendelea kwa sababu Mhusika Mkuu wa skandali hiyo, kama alivyo Mhusika Mkuu aka MM wa Mkakati wa Mapinduzi 2013, alikuwa mfadhili wake yaani Zitto Kabwe.

CHADEMA imekuwa sana katika Mkoa wa Singida tangu 2010. Kwa kiasi kikubwa, pengine kuliko mtu mwingine yeyote katika Mkoa wetu, ni mvamizi na mhamiaji Tundu Lissu. I can say with a straight face kwamba Jimbo pekee ambalo sijawahi kufanya mikutano ya hadhara ni Iramba Magharibi. Mengine yote nimefanya mikutano ya hadhara hata kabla sijawa Mwenyekiti wa M4C Kanda ya Kati. 

In brief, naweza kusema, as a matter of fact, kwamba Mzee Kitundu amejiuzulu kwa sababu mfadhili wake ameng'olewa madarakani na Kamati Kuu. I also can say with clear conscience kwamba Mzee Kitundu ataondoka peke yake CHADEMA Singida. Hana following yoyote Mkoa ule. Hata mkutano wa Mtaa hawezi kuitisha akapata watu. Kuondoka kwake ni good riddance, at least inatupunguzia mizigo ambayo tumeibeba kwa miaka mingi!

One final point: kwa vile amemtaja marehemu Chacha Wangwe kama mmoja wa wasaliti waliong'olewa CHADEMA siku za nyuma, ni vizuri wananchi wafahamu kwamba Mzee Kitundu, kama Zitto Kabwe, alikuwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati Kuu 'iliyowaaminisha' Watanzania kwamba Chacha Wangwe alikuwa msaliti mwaka 2007! Kama anabisha mwuulizeni jamaa yake anayempigania sasa hivi!

Kama ilivyo katika historia ya mapambano ya ukombozi ya zama zote, hakuna mapambano yasiyokuwa na akina Yuda Iskariote wake, yaani wale wanaosaliti cause kwa vipande thelathini vya fedha! Haijaanza jana wala juzi. Na haitaisha kesho. Kitu muhimu zaidi ni kwamba wasaliti wa aina hii hawajawahi kuzuia jua la haki kuchomoza na giza la ufisadi na uonevu kutoweka. Haitakuwa tofauti kwa CHADEMA. We, too, shall overcome. Tutashinda. Kama anavyosema mwanafasihi Shaffi Adam Shaffi katika kitabu chake Kuli: 'Yana mwisho haya'!

Tundu

On Tuesday, December 3, 2013 10:08:54 PM UTC+3, James wrote:
Halafu cha kufurahisha, yeye amekuwa mwenyekiti wa mkoa tangu 1992. Kwa nini kama ni mwana demokrasia wa kweli, hakuomba kuachia ngazibu haguzi ufanyike kutafuta mwenyekiti mwingine? Au kwa sababu alitoa nyumba?

Sent from my iPhone

On 3 Des 2013, at 20:01, Vincent Mhangwa <vmha...@gmail.com> wrote:

Naunga mkono kwamba waendelee kutoka woooote kwenye vyeo vyao ili CHADEMA ipange safu mpya mapema asibaki kirusi hata mmoja. The!


2013/12/3 Joseph Ludovick <josephl...@gmail.com>
Nilimaanisha heche,au mwikabe. si unaujua wewe mgogoro wa chadema tarime? ofisi ya chama ilifungwa na wapambe wa mwikabe na akaitwa msaliti na kundi la heche.Magesa kama unajua practice za chadema na siasa za hapo kuwa makini na kauli zako.


2013/12/3 Johale Magere <joha...@gmail.com>
Wewe unaesema aondoke na virusi vyake hujawahi kuchangia chama hata nguvu kazi zaidi ya maneno tu humu kwenye mitandao.watu wametoa nyumba na kuigeuza ofisi ya chama unadhani ni kiasi gani mtu huyu anauchungu na chama ?
Magere  J.
On Dec 3, 2013 7:36 PM, "Boniface Magessa" <mage...@gmail.com> wrote:
Aondoke na virusi vyake. Mpaka Wassira anadai chadema itakufa mwaka huu unadhani alikuwa anatania?!anajua fika kabisa kuwa kulikuwa na mamluki wa kutosha ndani ya chadema hivyo siku wakiamua kufanya timbwili chama kitakufa...aaah wapi..hakifi ng`oooo wao ndo watakufa..wakazikane na ccm yao..byeeee


2013/12/3 Paul Lawala <pasamil...@gmail.com>
Kuondoka siyo jambo baya,ila iwe ni kwa sababu zinazotokana na mtu mwenyewe,isiwe ya ushawishi wa kimaslahi


2013/12/3 F Kitigwa <kit...@gmail.com>
Kama mtu unajiuzuru kuna haja gani ya kutoa msururu wa shutumaaa za nini,
Ondokeni mnaoondoka CHADEMA itaendelea kuwepo tu, na huu ni ujinga wa hali ya juu kweli, yaani mtu kusimamishwa uongozi wewe huko unajiuzuru kumbe nyoote nyie mlikuwa nyuma ya huo uhaini wa akina zitto sasa mmeshitukiwa mnaanza kukimbia hovyo,
hata mkiondoka bado CHADEMA itakuwepo na itaendelea kuwepo,



2013/12/3 Johale Magere <joha...@gmail.com>
Ivi zitto ni adui au rafiki wa demokrasia ?
Magere  J.
On Dec 3, 2013 2:48 PM, "Bariki Mwasaga" <bmwa...@gmail.com> wrote:
Keneth
Nimeshauri mahali kwamba wataalam ambao ni wanachama na wapenzi waliopo humu kwenye majukwaa wachukue hatua za kuchukua uongozi wa chama badala ya kupambana na kuweka misimamo ya chama humu ktk majukwaa. Matamko yamezidi sana inawezekana ndiyo uthibitisho wa demokrasia bora ila tatizo sasa yanatufanya tuizungumzie Chadema weee.
Jambo lingine la msingi wahusika 3 waondolewe chamani ili kuwe na msimamo wa moja kwa moja.
On Dec 3, 2013 2:33 PM, "Kenneth Masuki" <kenny...@gmail.com> wrote:
Duh sasa naona taarifa zimezidi kipimo. Halafu huyu jamaa kutoa takwimu za kujiunga na CDM ina mashiko kweli?

Sent from my iPad

On Dec 3, 2013, at 13:15, Chadema Tanga <mabadili...@gmail.com> wrote:

WILFRED NOEL KITUNDU
MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza

Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.

Kwa barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.

Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.

Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.

Kusimamia haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.


Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.

………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
0764619335/0786215181


________________________

MSIMAMO WA MWENYEKITI CHADEMA MKOA WA SINGIDA DHIDI YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



UTANGULIZI
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mtu wa 300 kitaifa kujiunga na Chama hiki. Nimejiunga mwaka 1992 siku ya mkutano mkuu kwanza wa uzinduzi chama uliofanyika mnazi mmoja.

Nimekuwa nikijitolea vya kutosha nguvu, muda na akili zangu nyingi kukijenga na kukilinda chama hiki mpaka sasa mkoa wetu wa singida umepata wabunge watatu mmoja wa kuchaguliwa na wawili wa viti maalum.

Tangu mwaka 1992 mpaka 2011, chadema imekuwa ikitumia nyumba yangu kama ofisi, nimekuwa nikifanya hivyo kama kielelezo change cha kudai na kupigania demokrasia ya kweli ndani ya nchi kwa kuijenga CHADEMA imara.

Kwa kipindi chote hicho nimekubali kujibana na kuipunja familia yangu stahili zake ili chama chetu kikue kwa kasi mkoani kwetu, nashukuru mungu wanasingida waliitikia ombi nletu na kutufuta majozi yaliyotokana na jasho langu kwa kutupatia mbunge mwaka 2010.

Hivyo nimehudhunika sana kwa kitendo kilichofanywa na wajumbe wa kamati kuu cha kukiuka utaratibu na kujivalisha mamlaka yasiyowahusu.


HISTORIA YA USALITI KWENYE CHADEMA
Viongozi wa chama chetu wamekuwa na historian a tabia ya kutubadilishia wasaliti na kuwapachika kila aina ya shutuma kila kunapokaribia uchaguzi ndani ya chama.

Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa KABURU ni msaliti mkubwa ndani ya chama.

Tukaambiwa na kuaminishwa kuwa CHACHA WANGWE alikuwa msaliti, tukafanyishwa vikao vya ndani, tukaanzishiwa mikakati mbali mbali kuwa wangwe ni msaliti na kwamba anatumika.

WANGWE alipofariki hali ikatulia kidogo, tukaanza kuimba na kumsifia kwamba ni kamanda, tukamuita majina yote ya kishujaa lakini haikuwa na faida yoyote.

Sasa hivi tumeanza kuaminishwa wasaliti wengine wapya, safari hii wasaliti hawa wamevuka usaliti na kuwa WAHAINI, masikitiko yangu ni hawa wahaini ndio wale wale wengine waliokuwa wakikitetea chama kipindi kinapingwa na waliokuwa wasaliti.
Bahati mbaya sana na cha kufurahisha kama si cha kusikitisha hakujawahi kutokea Msaliti, Mhaini Wala kiongozi yeyote anayetuhumiwa kukihujumu chama mwenye asili ya KILIMANJARO ama KASKAZINI kwa ujumla, wahaini na wasaliti wote wanatokea mikoa yetu sisi wanyonge.

WAVAMIZI NDANI YA CHAMA
Bahati mbaya sana, harakati hizi za kuibua na kuwashuhulikia hawa wanaoitwa wasaliti zinafanywa na wavamizi ama wahamiaji ndani ya chama, nitatoa mifano michache muda huu.

1. GODBLESS LEMA tulimpokea kwenye chama hiki mwaka 2009 akitokea TLP aliposhindwa kufanya siasa za ushindani baada ya kushiriki kukiua chama hicho, lema alikwenda TLP akitokea NCCR-mageuzi aliposhindwa kutimiza malengo yake ya kisiasa na kushuhudia akikiua chama hicho. Leo LEMA ndio mpambanaji mkuu dhidi ya Zitto Kabwe, Dokta Kitila mkumbo na demokrasia ya kweli ndani ya chama chetu, anaambatana na kijana mwengine anaitwa MAWAZO, huyu wakati sisi tunapambana na CCM mwaka 2010 kuwanadi wagombea wetu wa ubunge urais na udiwani, yeye alikuwa anagombea udiwani kupitia CCM tuliyokuwa tunaipinga, ameingia chadema na sasa wale waliokuwa wanampinga akiwa huko leo anawaita WASALITI na WAHAINI.

2. MCH. MSIGWA naye huyu ni hivyo hivyo tulimpokea CHADEMA baada ya kushindwa na kuigombanisha NCCR na baadae TLP. Baada ya kuvimaliza vyama hivyo sasa wamehamia chadema kutugombanisha na kutuharibia chama chetu kwa makusudi kabisa.

3. Wengine vinara kwenye mgogoro huu ni Tundu Lissu, bensoni kigaila, john mrema na wengineo hawa ni vijana tuliowapokea kuja kujenga chama na sio kukibomoa chama kama wanavyofanya

4. TUNDU LISSU yeye ni kinara sana wa kumshambulia zitto kwenye hili, lakini ninasikitika kusema kuwa Tangu nimekuwa mwanachadema na Tangu nimemfahamu Lissu alipohamia CHADEMA hajawahi kufanya mkutano hata mmoja wa kujenga chama ndani ya mkoa wa SINGIDA ukiondoa jimboni kwake. Tumemuona Zitto akitoka bungeni na mara nyingine hata kigoma kuja kufanya mikitunano maeneo mbali mbali hapa singida ikiwemo iramba, singida mjini na kwingineko, na mtakumbuka zitto amewahi kukamatwa na polisi mkoni singida akikinadi chama, hakuwa lissu. Sasa leo anapotoka mbele na kujinadi kuwa ana mapenzi mazuri na chama kushinda zitto kabwe ni upuuzi unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa sana.

Ninasikitika sana kuona Mwenyekiti Mbowe na Katibu mkuu Slaa wanawakumbatia hawa, ninashangaa sana kuona viongozi hawa wanakubali kuwa sehemu ya ubakaji huu mkubwa wa demokrasia.

Ninaamini kabisa vijana hawa wanatumiwa na mwenyekiti na katibu mkuu kuutumia uzoefu wao walioutumia kwenye vyama vyao vya awali mpaka kuviua.


KUHUSU KAMATI KUU NA MAAMUZI YAKE.

Uamuzi wa kuwavua nyadhifa zitto kabwe na wenzake kwa madai ya kuwa na mkakati wa siri wa uchaguzi, ni uamuzi wa kipuuzi na wa kupuuzwa, kwenye hili kamati kuu imedhihirisha namna gani inaundwa na watu wasio na weledi na hawaongozwi na misingi na taratibu za chama.

Katika chama chochote kile, kamati kuu haiwezi kuwa mshitaki mkuu, hiyo hiyo iwe mwendesha mashitaka, hiyo hiyo iwe shahidi, hiyo hiyo iwe hakiku na hiyo hiyo iwe muandika hukumu. Hapa wamedhihirisha ni namna gani wanaongozwa na Hisia na chuki zinazotawaliwa na hofu ya uchaguzi ndani ya chama.

Kamati kuu hii ya sasa haipo kwa ajili ya maslahi ya wanachama na chama kwa ujumla, ipo kwa maslahi ya mbowe na slaa pengine na watu wa kaskazini.

Kwa hiyo kuwazuia watu wenye mawazo tofauti na wao na kuwaita wasaliti na wahaini ni sawa kuasisi na kuimiza mpasuko ndani ya chama, maana kuna mambo kamati kuu inaweza kufanya na kuna mengine haiwezi, hii haiwezi kufanya hili walilolifanya sasa hawawezi kulifanya.

Nionavyo mimi na wanachama ninaowaongoza hapa singida ni kwamba kamati kuu imekurupuka na kufanya maamuzi yaliyotawaliwa na hofu, chuki na uroho wa madaraka dhidi ya zitto kabwe na wenzake walioonyesha nia thabiti ya kukivusha chama kwenye harakati za kuilikomboa Taifa.

MSIMAMO WA CHAMA SINGIDA
(i) Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

(ii) Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.


(iii) Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.

(iv) Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa kuwa asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.


(v) Tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa Chama, Kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.



MWISHO

Kutokutii maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki, 

Singida tunasema kuwa '' kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA CHADEMA.'' 




Kwa kuzingatia utangulizi wangu hapo mwanzo, na kwa kuona ukweli kwamba chama chetu sasa kimevamiwa na kuwa na vyama viwili ndani ya chama kimoja, 

Nimeonelea ni vyema sasa niilinde na kuithibitisha dhamira yangu ya demokrasia ya kweli, nimeona ni vema nihakikishe demokrasia tunayoiimba tunaitenda kwa vitendo.

Kwa misingi hiyo sasa, nimeamua kukaa pembeni ya udhalimu huu wa demokrasia unaoasisiwa na viongozi wakuu wa chama wanaoogopa kivuli cha uchaguzi mkuu wa ndani ya chama, 

Nimeona ni vema sasa niuthibitishie umma wa Tanzania kuwa kwenye chadema unaruhusiwa kugombea vyeo na nafasi zote isipokuwa uenyekiti wa Taifa ndio maana zitto tuliyemuunga mkono leo hii anashambuliwa kwa dhamira yake safi ya kidemokrasia.

Nimechoka sasa, nimebadili mawazo, sipo tayari tena kuwa msukule wa fikra mbele ya watu wanaopenda kuigiza na kujifanya watetezi wa wanyonge kumbe ni wanafiki wa kutupwa.

Nimememuandikia barua katibu wangu wa mkoa kumueleza maamuzi yangu ya kujiudhuru uenyekiti wa mkoa, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho hakitendi kinachoyasema, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho dakika na saa yoyote unaweza ukageuzwa na ukaitwa msaliti na muhaini
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment