Saturday 21 December 2013

Re: [wanabidii] Kurudi kwa Edward Lowassa

Na ukiwa unasema sana na kukosoa kila wakati watu ndani ya familia warekebike au kurekebisha vitu; uwe msemaji kijijini au  ofisini, mtaani ambapo kuna uzembe; au mtaani jirani yako anamwaga maji  yanaelekea kwako, au kaweka bar jirani na watu wanajaa barazani kwako, makelele hamlali-utachukiwa na utaadhibiwa kama si wewe watoto wako au jamaa uishio nawe. Na huu mfumo, itikadi, mitazamo na upeo wetu WA-AFRICA ndio tuliuza nchi tukatawaliwa, na sasa wamerudi kututawala na tunawauzia nchi wenyewe; ndio unaoleta vita africa nzima nchi nyingi vita kila wakati inazuka mpaka mzungu aje kutusaidia. Ubinafsi, fikra zisizokubali kubadilika, kupenda sifa na lawama sio kukubali ukweli na kujirekebisha. Na Ujinga huu upo mkubwa TZ maana jirani anahamia kwetu na mifugo tunamkaribisha lakini hatukaribishwi nchi jirani. Mhamiaji haram tunamkaribisha na anahamia na mifugo tele, tunamuoza, kumopa makazi na anatutumia kukata miti na tunasema ndio soko la bidhaa zetu. sasa wanyarwanda wamerudi upya na silaha kuchukua maeneo na kufukuza waTZ kutoka vijiji hivyo waliokaa zamani. Operesheni Tomokeza tumeitokomeza na waziri wake; tusubiri kutokomezwa na majirani wenye umoja na silaha-wanaingia. Sio tu wanachukua ardhi kujaa na kukata miti-watateka mabasi ya abiria, kutuibia na kututia kilema. Sisi tupo intesive care ktk masuala mengi ila vinara wa malumbano kuharibu vyetu wenyewe kisha-visingizio kibao. Tukubali kuona mbali na kubadilika wote.

On Saturday, 21 December 2013, 22:10, Sylvanus Kessy <frkessy@yahoo.com> wrote:
Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa. Tatizo wala siyo viongozi tatizo ni mfumo. Mfumo ndio umeoza. Na wooote wameathirika na mfumo huo. They are rotten to the marrows. We need healing. A healer is the leader who will dare for changes. Most of those in the posts, they fear it. They know that they will loose if they make changes. Because they fear for changes, they do nothing and at the end they seems to be hopeless. So we will continue to have HOPELESS LEADERS.
 
We need Mandelas' type of leaders. Who are ready even to be prisoned. Who is that? That is the major question. We must be very watchful. Those who are claiming to manage for sure they are not. For me a real leader is in SILENCE. We must look for him/her. And he is there! Ask me then I will tell you! 
BRAVO KIWASILA. You are in the right track!

From: Joseph Hella <jp_hella@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, December 21, 2013 8:30 PM
Subject: Re: [wanabidii] Kurudi kwa Edward Lowassa

Sijui kama watu tunapata nafasi ya kusoma maandiko ya huyu dada Hildegrada Kiwasila. Huwa namfuatilizia na kusoma mada zake kwa karibu zaidi. Namuunga mkono Bernard Ulaya kuwa tatizo sio viongozi wetu tatizo ni sisi. Mimi na wewe. Tunahitaji utekelezaji sio hotuba ya kulindana. Baada ya kagasheki, kama alivyosema Hildegrada, subiri uone. Mali za asili zimeisha. Baada ya Matayo subiri uone Mnazi mmoja bustani tutaanza kulishia ng'ombe kwa kunenepesha. Bila utawala wa sheria tumeisha. Kama hujatunza mazingira kisheria hata hao masikini wanotetewa kuwa wamehamishwa bila ridhaa ya haki za binadamu watakuwa masikini wa kutupwa maana hata hiyo hela chache za mkaa watapata wapi. Watatumia muda wao kutafuta maji manna vyanzo nya maji vimeharibiwa na wavimizi tuliowatetea japo waliingia bila ridhaa. Rwanda wanatuwashia taa wanapita tena kwa jeuri sisi hata kulipia nusu ya bajeti ni mgogoro. Inayopitishwa ni ya uongo kwa makofi na mbwembwe bungeni lakini haitekelezwi hata asilia 40. Tunajiona tuko vizuri
Poleni  

On Saturday, 21 December 2013, 18:11, Bernard Ulaya <nyalukolo@yahoo.com> wrote:
Kiwasila!
YOU HAVE SPOKEN WELL, VERY WELL!

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Kurudi kwa Edward Lowassa
Sent: Sat, Dec 21, 2013 9:39:59 AM

Hii ni nchi iliyopo intensive care. Ondoa Rais, Mawaziri, wabunge-kama watanzania wote kuanzia kaya hatutokubali kubadilika kiakili, kimatendo, kuwajibika kwetu wenyewe na kwa jamii na nchi-itakuwa biashara kichaa
Arudu Mh Lowasa na tabia yake ya kufika jukwaani na kufukuza kiongozi na kutoa amri; aondolewe Mh Kagasheki na operesheni tokomeza aje Zitto kabwe-hatutafika kokote. Aliyebaka wanawake, aliyeamlisha mtu kubaka mtu ni mtumishi wa umma sio Waziri, mtanzania mwanajamii. Mume na baba wa mtu ana mila na desturi za kabila yake na sheria ya nchi anazijua. anayevibaka vizee vijijini na kulawiti vitoto vya kiume, kubaka wasichana na akina mama wakienda shamba au mtoni-ni mtanzania, mwanakijiji mwenye akili timamu , mila na desturi. sawa na anayepitisha majambazi na wahamiaji haramu. Anayeua mwenye bodaboda, taxi, gari na kuyajaza uani kwake yanakarabatiwa na kubadilishwa-mke, watoto, ndugu wakifahamu. Wabakaji, wauaji albino, vikongwe na wezi wauaji hawa huwekewa dhamana na ndugu zao. Kesi zinaandikwa magazetini. Shehere za ukeketaji wali wanatembezwa mtaani na ngariba waliazimia kuwakeketa staff wa Wizara ya Maendeleo waliokwenda Tarime kuongea na Ngariba hao. na sherehe mgeni rasmi Diwani au kiongozi fulani wa Mila in public. Hawazuii na wananchi hawasemi Mbunge ajiururu hawasaidii. Ila watamchagua tena asipokemea mila. Operesheni kihamo vijijini iliyokamata watu na mafuvu, fisi, tunguli, majoka na kukutwa watoto 2 Magu wachawi wakabondwa vibaya na mgambo/jeshi lilikokuwa likilazimisha watu kuhamia vijijini-Mh Mzee Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi aliambiwa kujihudhuru na baba wa taifa. yeye hakutoa amri ya kupiga na kuua walioshukiwa uchawi au kukutwa na mafuvu na Rais Mh baba wa taifa alisema-wabebwe na Fisi zao, majoka wakae nayo mpaka watakapoelimika kuona hayawasaidii kitu na kuyatupa. Leo baada ya kumuondoa waziri H. Mwinyi wakati ule jee mauaji ya albino, kukata watu viganja na kuviuza, ubakaji vitoto, mauaji ya vikongwe na kuchomea nyumba wachawi kumeisha??? Ndio kumekua kwa ubaya na kunaendeshwa na wanafamilia bila kujali sheria na tunahonga hela kesi isahaulike. Tuna hata matangazo magazetini ya uganga wa chuma ulete, dawa ya kushinda kesi mahakamani, uganga wa zindiko la jini anayekusaka asikupate etc bila ya kujali maadili tunajali gazeti linunulike mkono uende tumboni. wanaotoa matangazo haya hatuwakamati wala magazeti yao kufungwa kwa kutangaza uovu.
Kama unamficha kaka, ndugu, baba yako mwenye meno ya tembo na bunduki na magari ya wizi ambapo wamiliki waliuawa-Lowasa akija bila ya wewe mtanzania kubadilika atafanya nini? kama unamiliki kumuoza binti kwa mzungu mchina mgeni na kumsaidia apate ardhi kwa kumpa au kwa jina lako-usipokubali kubadilika Lowasa au mwingine yoyote atafanya nini? Sasa kuondoka Kagasheki na wengineo-kuzuia 'operesheni tokomera', tusubiri wimbia na mauaji tembo, faru; ujambazi vijijini; kuchoma moto vituo vya polisi wanapokamata wahalifu tutaona tunaita polisi tumevamiwa-hawatokuja. Sijui tunaelekea wapi waTZ. Hatukai tukapanda kikapangika na tukafanya kikafanyika kwa ushirikiano. Tumeweka malumbano yasiyoisha kama tija.
 
On Friday, 20 December 2013, 20:01, Pauline Mengi <paulinemengi@gmail.com> wrote:
Na MM Mwanakijiji

Dalili zote zinaoonesha kuwa kilio cha wabunge kutaka Pinda ajiuzulu na hivyo Baraza la Mawaziri livunjike lina dalili moja kubwa; Lowassa's comeback. Sidhani kama kuna mwanasiasa mwingine yeyote ambaye anaweza kupata kuungwa mkono na wabunge wa CCM kama Lowassa. Kurudi kwake itakuwa ni kupata second chance na kujipanga vilivyo kwa ajili ya 2015. Kama siyo Lowassa ni mbunge gani mwingine wa CCM kutoka majimbo ya kuchaguliwa anayeweza kupata support na heshima ya kuwa Waziri Mkuu? Haitakuwa mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu kurudia kiti chake mara ya pili. 

Yetu macho.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment