Friday 20 December 2013

Re: [wanabidii] KUONDOA KODI YA SIMU NI UWOGA NA UNAFIKI

Yona.
Ngoja tukuseme kidogo na wewe.
Mtu anayefuatilia comments zako za siku hizi kwanza atagundua kuwa unaikandia serikali ya Kikwete. Tena atagundua kuwa umeanza kutumikia uchaguzi wa 2015.
Kupitia kuitaka saerikali ikubaliane na wabunge wa chama tawala haimaanishi kuwa huelewi kuwa taasisi hizi mbili zina haki ya kutofautiana bali ndani unasomeka kuwa una mtu kwa ajili ya 2015. tafadhali acha hata kama kakuahidi cheo. Kutakutesa huko tuendako.
Ninaamini unaelewa kuwa kodi aliyoondoa rais hakuwapunguzia wenye makampuni wanaopata trilioni 20 baliamewapunguzia wanyonge.
Unaelewa kuwa kodi hii haipingwi kawanbabu tu ni mzigo kwa mlipaji bali kwa sababu serikali inawasamehe wakubwa kodi na kuwatoza wanyonge.
Rais wetu kuanza kuliona hili halafu ukamshambulia na kusema anajiandaalia uchaguzi 2015 unafikiri Jk atagombea udiwani au ujumbe wa mtaa? Anamaliza urais
Unajua kuwa huwa simlengi mtu katika maandishi yangu. katika hili nimekulenga. Nimekosea???
Elisa

From: Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, December 19, 2013 10:16 AM
Subject: [wanabidii] KUONDOA KODI YA SIMU NI UWOGA NA UNAFIKI

KUONDOA KODI YA SIMU NI UWOGA NA UNAFIKI 

Ndugu zangu ,

Nimepata taarifa kwamba rais jakaya kikwete ameamua kuondoa kodi ya simu iliyopitishwa na bunge miezi michache iliyopita kwa kutumia kofia yake ya urais na ameshasaini hati ya dharura .

Mie nasema uamuzi huu wa rais jakaya kikwete ni wa kioga , unafiki na hajiamini kwa maamuzi yake mwenyewe na haamini wabunge wa chama chake walioafiki hili wala wataalamu wa wizara waliotafiti na kupitisha suala hili kwa moyo wa kizalendo .
Hivi rais anajua kwamba kuna kampuni moja ya simu ya mkononi kupitia huduma yake ya huduma za pesa inatengeneza karibu trilioni 20 kwa mwaka ? wakati serikali yake bajeti yake ni trilioni 7 tu tena karibu nusu ni mikopo ya kutoka nje ?

Kwanini watu wanakuwa wanafiki na waoga kiasi hichi na kuangalia maslahi yao ya kisiasa haswa uchaguzi wa mwaka 2015 badala ya maisha marefu ya watoto wa kitanzania na maisha yao ya baadaye ? .

Tuache unafiki , serikali haswa rais aheshimu maamuzi ya bunge  na wataalamu wa kodi waliojadili na kuafikiana kuhusu hii kodi ni kwa maslahi yetu wananchi kwa maendeleo yetu kama taifa na kila mwananchi bila kujali nani anatakiwa alipe kodi kwa maendeleo ya taifa .

Sasa nyie wabunge na mawaziri mnaofikiria kwamba kodi hii ikiondolewa basi itakuwa ahueni kwenu kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 mmenoa , kila nchi duniani inategeneza vyanzo mbalimbali vya mapato ya serikali huku ikipunguza kodi kwa vitu vingine kama vyakula , madawa , vifaa vya shule etc .
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment