Thursday 19 December 2013

Re: [wanabidii] KUONDOA KODI YA SIMU NI UWOGA NA UNAFIKI

Yona,
Naona umekuwa extreme sana katika hoja yako hasa kwa kuanza kuponda badala ya kuonesha jinsi kodi hiyo itakavyoathiri bajeti ya serikali. Mimi binafsi naona rais yuko sahihi kuliko hata wabunge ambao wanaogelea katika utajiri kuliko watumishi wote wa umma. Ni vigumu sana kwa mbunge kuona madhara ya kodi ya simu ukilinganisha na mamalishe au mpiga rangi au mwanafunzi. Kimsingi kwangu mimi siyo kodi ila kigezo cha kodi moja kwa watu wote. Ingekuwa inaendana na kipato kama ilivyo PAYE basi ingekuwa sawa. Ila kwa kulipisha wote sawa siyo sawa.
Naamini kabisa rais wetu siyo mwoga wala mnafiki bali naye amefanya utafiti na ameshauriwa pia. Siamini kama hajui yanayoendelea kuhusiana na kodi ya simu. Pengine hoja yako ya maandalizi ya 2015 ina ukweli fulani ila JK hategemei kugombea kwa hiyo haiwezi kuwa sababu ya yeye kufuta kodi. Pengine anafagilia njia chama chake ambayo inaweza kuwa mkakati wa kisiasa na hakuna mbaya maana ndio siasa kujenga mazingira ya kugusa wananchi na hatimaye kupima maoni na kuondoa kama namna ya kuonesha kwamba serikali yao inasikiliza. Hilo nalo ni poa.
 
Kwa hiyo mimi nampa big up JK kwa kuwa msikivu kwa kilio cha machinga wengi.


On Thursday, 19 December 2013, 7:16, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
KUONDOA KODI YA SIMU NI UWOGA NA UNAFIKI 

Ndugu zangu ,

Nimepata taarifa kwamba rais jakaya kikwete ameamua kuondoa kodi ya simu iliyopitishwa na bunge miezi michache iliyopita kwa kutumia kofia yake ya urais na ameshasaini hati ya dharura .

Mie nasema uamuzi huu wa rais jakaya kikwete ni wa kioga , unafiki na hajiamini kwa maamuzi yake mwenyewe na haamini wabunge wa chama chake walioafiki hili wala wataalamu wa wizara waliotafiti na kupitisha suala hili kwa moyo wa kizalendo .
Hivi rais anajua kwamba kuna kampuni moja ya simu ya mkononi kupitia huduma yake ya huduma za pesa inatengeneza karibu trilioni 20 kwa mwaka ? wakati serikali yake bajeti yake ni trilioni 7 tu tena karibu nusu ni mikopo ya kutoka nje ?

Kwanini watu wanakuwa wanafiki na waoga kiasi hichi na kuangalia maslahi yao ya kisiasa haswa uchaguzi wa mwaka 2015 badala ya maisha marefu ya watoto wa kitanzania na maisha yao ya baadaye ? .

Tuache unafiki , serikali haswa rais aheshimu maamuzi ya bunge  na wataalamu wa kodi waliojadili na kuafikiana kuhusu hii kodi ni kwa maslahi yetu wananchi kwa maendeleo yetu kama taifa na kila mwananchi bila kujali nani anatakiwa alipe kodi kwa maendeleo ya taifa .

Sasa nyie wabunge na mawaziri mnaofikiria kwamba kodi hii ikiondolewa basi itakuwa ahueni kwenu kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 mmenoa , kila nchi duniani inategeneza vyanzo mbalimbali vya mapato ya serikali huku ikipunguza kodi kwa vitu vingine kama vyakula , madawa , vifaa vya shule etc .
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment