Tuesday 4 September 2012

RE: [wanabidii] YANAYOENDELEA IRINGA,MAFINGA NA TUKUYU

Inasikitisha san asana sana  si jambo la kufungia mdomo je watanzania jamani mbona tunayaacha mambo yaendelee hatuamki?? Jamani wale wenye kujua sheria hebu tuongozeni katika hili tumechoshwa na mauaji haya !! Nadhani tuungane na wenzetu wa LHRC tuishtaki serikali palipofika pabaya kesho kwangu ama kwako!!

 

 

The revolution is not an apple that falls when it is ripe. You have to make it fall

 

Lillian L.F.kitunga
Assistant Programme Officer
Gender Training Institute

P.O.Box 8921
Tel: +2552443450;2443205;
Mob: +255 713 321981/ 0683 318105


Email: lkitunga@tgnp.org
url: www.tgnp.org

 

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of mutabaazi lugaziya
Sent: Tuesday, September 04, 2012 10:01 AM
To: Mabadilikotanzania; wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] YANAYOENDELEA IRINGA,MAFINGA NA TUKUYU

 

Wanandugu,

Kwa kipindi sikuwa kwenye mtandao. Nilikuwa Ileje kwa shughuli za kidini.

Nikiwa huko, nikapigiwa simu kuhusu "vurugu" za Mafinga eneo la Nyololo kwenye uzinduzi wa tawi la CDM. Hilo lilikuwa tawi la pili, baada ya kuwa wmefungua tawi jingine kabla kwa eneo lililo kwa ndani toka barabara kuu iendayo Mbeya.

Baadae nikataarifiwa kuwa kuna wanachama wawili wa CDM wamewekwa ndani, na kwamba niliombwa kutoka Ileje ili kusaidia kuwaombea dhamana endapo watapelekwa mahakamani. Niliondoka Ileje saa 6 za usiku na kufika Mafinga saa 12.00 asubuhi.

Baada ya mapumziko mafupi, nikiwa na wakili mwenzangu Basil Mkwata, tuliekea kituo cha polisi, Mafinga, ambapo tulielezwa na Afande mwanamama Furaha Mwakajila kuwa ni kweli watuhumiwa wapo, na kuwa hawangeweza kufanya lolote kwa vile IGP alikuwa njiana kuja huko, hivyo tusubiri. Tukasubiri.

Tukaelezwa kwamba kulikuwa na mazungumzo "chanya" kati ya IGP na Dr. Slaa kuhusu hatma ya mahabusu wa CDM. Mbali ya wale viongozi wawili, polisi waliwarejesha Mafinga vijana 31 wa Red Brigade waliokuwa wameletwa kuongeza ulinzi huko Mafinga. Hawa walikamatiwa eneo la Igawa mkoani Njombe mbali kabisa na eneo la tukio.

Tulishinda hapo Mafinga, tukiaminishwa kuwa IGP na timu yake wanakuja, na kwamba sisi tulikuwa pia tukutane naye, kwa hivyo tuendelee kusubiri. Tukasubiri, zaidi. Mpaka saa 12.30 jioni, hakukuwa na taarifa zozote za IGP kfika, hivyo tukalazimika kuondoka jioni hiyo kurudi Iringa.

Huku Iringa, taarifa kutoka IPC na wanafamilia walitoa taarifa kuwa mwili ungeletwa asubuhi ya leo kwa ajili ya kuagwa. Hata hivyo, bila kutoa taarifa, mwili uliletwa usiku wa manane na shughuli ya kuaga ikafanyika chap chap usiku huo. Na msafara wa kwenda Tukuyu usiku huo huo. Shughuli hii ilifanyika bila kumtaarifu kiongozi yoyote wa CDM.

Hata hivyo, wakati msafara ukiondoka, viongozi wa CDM walipata taarifa, na "waratibu" wa safari, bila kutegemea, wakajikuta wanaongozana na Dr. Slaa na timu yake. Ninapoandika sasa hivi, msafara huo umefika tayari Tukuyu.

Wakati huo huo, tunasubiri taarifa kutoka Mafinga ili kujua watuhumiwa watapelekwa mahakamani ili tuweze kuwahi huko kwa ajili ya masuala ya udhamini.

NB. Mbali ya watuhumiwa wawili walio mahabusu, kuna wanachama 8 wa CDM waliopata majeraha na wamelazwa hospitali ya wilaya ya Mafinga. Kati ya hao, 2 hali zao sio nzuri na hawa wamelazwa huku wakiwa wametiwa pingu. Tunafuatilia hatima yao kisheria ili kama nao watapelekwa mahakamani ili tukawasimamie.

Tukipata taarifa zaidi tutawajuza.

Niliuliza mara ya mwisho: Quo vadis Tanzania?

MJK

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment