Saturday 22 September 2012

Re: [wanabidii] UVAMIZI NA UNYANG'ANYI ULIOFANYWA NA POLISI HUKO KIGOMA

...Imenisikitisha sana! POLISI; badala ya kuwa walinzi wa "uslama wa raia na mali zao" wanakuwa wanyang'anyi! Nadhani kuna kila sababu kwa sasa tufanye UHAKIKI wa POLISI wa Tanzania ili kujiridhish kama wanazo SIFA za kuwa POLISI. Vinginevyo; nchi inaweza kuingia kwenye "MGOGORO" mkubwa wa usalama wa raia na mali zao.
 
Pole sana Mwalimu Mbanyi kwa yote yaliyotkea Kibondo (nyumbani kwetu); na watumie salamu zangu za pole wananchi wa huko! Tanzania ni nchi yetu sote tushirikiane kuilinda...tusiwaache watu wachache wenye CHOYO, UROHO. ROHO MBAYA, na ULAFI kuiharibu.
 
Bakari M Mohamed, BBA [PLM], CPSP [T], MSc (PSCM), Reg. PSP (AU 0005)
  1. Lecturer in Procurement and Supply Chain Management
  2. Procurement and Supply Chain Auditor
  3. Procurement and Supply Chain Specialist, Consultant, Researcher and Trainer in Procurement Contracts Management
  4. Doctor of Alternative Medicines [DAM] & Natural Healing Therapist
Department of Procurement and Logistics Management
Mzumbe University Box 6 Tel (Office): + 255 23 2604381/3/4
Mobile      : + 255 713 593347
MZUMBE, Tanzania.

From: godfred mbanyi <mbanyibg@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, September 22, 2012 9:46 AM
Subject: [wanabidii] UVAMIZI NA UNYANG'ANYI ULIOFANYWA NA POLISI HUKO KIGOMA
Ndugu wanabidii,
 
Kama mlivyosikia na kuona kwenye vyombo vya habari, mama mmoja katika wilaya ya Kibondo huko Kigoma, amevamiwa usiku na askari polisi wanne, wakampiga sana  na kumnyang'anya shilingi milioni mbili na simu zake nne! Kwasa mama huyo amelazwa hospitali ya wilaya kutokana na kipigo hicho na askari wamekamatwa na kuwekwa selo.
Matukio ya aina hii ni mengi mkoani Kigoma yakiwamo ya vitisho na kubambizwa kesi!
 
Nawaomba wanaharakati, wanasheria, wanahabari pamoja na wadau wengine mfuatilie suala hili ili haki itendeke. La sivyo, polisi hao wataachiwa bila hata ya uchunguzi wowote!
 
Nawasilisha;
 
Mwl.Mbanyi
 
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment