Aliyefyatua risasi alitumwa na nani, walaumiwe walioshindwa kutumia midomo na njia nyingine za mawasiliano kisaha wakatumia risasi na mabomu. Uchambuzi unaoelemea kusema watu wote wakiri makosa ni kujaribu kugawanya kosa kwa watu wasiohusika na hii inaweza kumfanya mkosaji halisi akaendelea na tabia hii. CCM kupitia chombo cha dola imeua.
--- On Tue, 9/18/12, hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> wrote:
From: hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA To: wanabidii@googlegroups.com Date: Tuesday, September 18, 2012, 1:44 PM
Bariki, umechambua vizuri sana, very fairly and squarely! Wengi hapa wamejaa ushabiki na chuki dhidi ya CCM na serikali yake na hivyo hata hoja nzuri za Hizza hawawezi kuziona, hata hoja potofu zenye mapungufu, za Hizza hawawezi kuziona! Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com> Sender: wanabidii@googlegroups.com Date: Mon, 17 Sep 2012 12:02:53 +0300 To: <wanabidii@googlegroups.com> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
Ni tamko zuri ila limejaa kasoro nyingi mojawapo ni ile ya kusema kufanya mkutano/maandamano. Kwa mujibu wa hali halisi ilivyokuwa, kilichofanyika ni ufunguzi wa tawi jipya na pia suala halikuwa kusubiri Sensa iishe bali suala lilikuwa ni wao chadema kuendelea na shughuli zao za kisiasa ambazo zilipangwa mapema zaidi kama ambavyo Sensa ilivyokuwa imepangwa. Tofauti kubwa ni kwamba Serikali ilisahau kutoa kauli ya kuzuia shughuli za kisiasa wakati wa Sensa tangu awali na hivyo kutoa tamko wakati wa Sensa umekaribia inazua tafsiri mbaya zaidi kwa baadhi ya watu. Mimi kama mwananchi ambaye kwa sehemu nimeelimika, lazima wadau wote wakiri makosa....kuanzia wananchi hadi Serikali yenyewe. Hivi nini kilishindikana kwa wahusika kutoa kauli ya kuzuia shughuli zote (mikutano na mikusanyiko yote ikiwemo ya Dini) wakati wa Sensa? Kauli ambayo ilipaswa itolewe hata ingewezekana mwaka jana ili watu wanapopanga shughuli za kila siku wajue kipindi fulani hakipaswi kuingiliwa??? nafikiri tusiangalie tatizo lililotokea bali tuangalie kiini cha tatizo. Kama ni watu wa mipango mbona tupo tumejaa na wala haiumizi kichwa kupanga. Suala la kupanga ni tatizo hata kwenye uongozi wa michezo ndiyo maana mechi kila siku zinabadilishwa wakati wenzetu Ulaya mechi itabadilishwa kutokana na hali ya hewa kubadilika lakini si vinginevyo. Tubadilike kwanza ili mwingine akikosea tumpe adhabu ya milele 2012/9/17 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> NA RICHARD TAMBWE HIZZA
WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.
Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).
Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.
Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?
Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?
Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).
Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.
Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.
Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?
Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?
Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.
Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Bariki G. Mwasaga, P.O. Box 3021, Dar es Salaam, Tanzania +255 754 812 387 -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
|
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment