Tuesday 18 September 2012

Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA

Mngonge,
 
Unapochambua mada kwa ufasaha na upembuzi yakinifu namna hii,unamtesa bure Tambwe! Hana uwezo wa ku-analyse mambo, amekaririshwa ya kusema ili apate mkate wa kila siku!!! Nadhani Tambwe ni mmoja kati ya wale aliowasema Mhe. Dr. Masaburi, siamini kama anatumia kichwa kufikiri!!!



--- On Mon, 9/17/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 17, 2012, 9:57 AM

Ndugu Tambwe pamoja na Chacha
Mmejitahidi kulinda vibarua vyenu kwa upeo wenu. Mimi naanze kumuunga mkono mtoa hoja mmoja aliyesema ni makosa kujibu na kujadili hoja zako kwamba ni uchafu (rubbishes).  Kwa vile ni hoja inayotugusa na inayojaribu kuudanganya umma inabidi tuelimishane kidogo. Tambwe na Chacha ni waganga njaa tu. Tambwe tulikuona sana ukiwa na NCCR miaka ya 1995 ulikuwa mstari wa mbele na kuongoza maandamano na mikutano mingi ambayo serikali ya CCM haikupenda iwepo. Kila mara polisi walijitahidi kuwazuia lakini ulikahidi amri zao. Hivi ndo wewe Tambwe yuleyule au ninaota?

Huku ni kuganga njaa tu, Tambwe umehamia CCM wewe pamoja na Mzee Mtevu si kwa mapenzi bali kupata chochote. Labda maneno yako uwaeleze vijana ambao wamezaliwa juzi juzi au wametoka mikoani hawafahamu historia yako kisiasa. Yote haya ni makosa ya CCM kumpa nafasi mtu anayetangatanga kisiasa na pengine kukufanya think tank yao. Na ndo wewe uliyetoa wazo kwamba ili kupunguza upinzani ni vyema kuwaambia polisi waue watu na kuwatisha na mabomu ili kupunguza kasi ya upinzani. Upinzani unatokana na matatizo ya kiuchumi na kijamii ambayo watu wanaona serikali ya CCM imeyasababisha na ata Chadema ikitoweka bado tatizo litabaki pale pale

Anachojaribu kutetea Tambwe ni upuuzi mtupu kwamba Chadema ndo inaua watu. Swali, je kama Chadema ndo wauaji ya nini kumfikisha polisi muuaji mahakamani?  Tambwe watanzania wa sasa si wapumbavu kiasi hicho? Acha siasa za maji taka, kafanye utafiti upate kujua vizuri nini watanzania wa kawaida wanasema na wanaelewa kuhusu jeshi la polisi. Pamoja na kumuua Mwangosi zipo kasoro na kero nyingi wazipatazo wanapotaka huduma ya polisi, Tambwe ujue penye moshi pana moto.

Tukiachia mauaji ya waislamu wa mwembechai na pemba, wafuasi wa Chadema huko Arusha na Morogoro, mauaji ya wafanyabiashara wa Mahenge yaliyofanyika msitu wa Pande na mauaji mengine mengi. Je ata hayo mauaji ya makusudi ya David Mwangosi bado unataka watanzania wenye akili timamu waamini uwongo wako kwamba Mwangosi kauwa akiwa kwenye maandamano? Uliwahi kuona wapi mwandamanaji aliyewekwa chini ya ulinzi wa polisi kama kumi hivi akiwa hana siraha wala kumbia anapigwa bomu na kusambaratishwa mwili wote?  Naomba nikuulize maswali yafuatayo?
- mwangosi aliuawa akiwa anapambana na polisi kama kumi hivi kwa siraha gani?
- laptop na kamera walivyomnyanganya Mwangosi walikuwa na shughuli gani navyo?
- mbali na Mwangosi ni watuhumiwa wangapi walioshikiliwa katika tukio hilo ili tujue ukubwa wa maandamano hayo?
- mbali na mauaji ya mwangosi ni matukio gani makubwa yenye madhara waliyosababisha waandamanaji?
- je ndugu Tambwe unajua tofauti kati ya waandamanaji wasiokuwa na siraha na adui wa  kivita?
- Je Tambwe ulitaka wanahabari wamkaribishe waziri Nchimbi badala ya Lwaitama kwa sababu gani? Kwani ule ulikuwa ni mkutano wa kiserikali?

Tafakari kabla ya kuwasilisha hoja afifu kama hizo, inaelekea unashangilia mauaji hayo kwa kufikiri kwamba ndo dawa ya kupunguza kasi ya hao Chadema kumbe ndo munawapa nguvu zaidi na hoja za kuwasilisha kwa wananchi. Polisi yetu si ya serikali ya mkoloni kama unataka iwe kama ya mkoloni nafikiri umefilisika kimawazo maana siku hizi tuna ukoloni mambo leo.

2012/9/17 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Chacha Wambura-Sio hii ya kuuawa mwandishi wa habari tu (Mungu amrehemu) imeanza nyingine ya CUF ya kusema kuwa-kuwaondoa wananchi wakazi wa jangwani mabondeni haikuwa sahihi. Mbona serikali inajenga kituo cha bus? kama bondeni ni hatari kituo cha basi kinaweka kufanya nini kama ni a hatari. Ni msifia mvua tu ambaye itakuwa imenyea (anayeona ubaya wa kukaa mabondeni itakuwa imemfika dhahama na hasara pia).Ambae haoni ubaya-hajaonja joto ya jiwe.
 
Fikiria kifo au vifo vinavyoweza kutokea usiku watu wakiwa wamelala hawaoni maji yajayo nyumbani. Jee, hakuna tofauti ya Kituo cha muda na nyumba ya kulala. Kuwa mtu halali kituoni bali anakaa kwa muda na zaidi mchana sio usiku wa manane wamelala hapo. Na kuwa hata nyumba za NHC za raia viwanja vyake viliishia juu kwenye roundabout sio bondeni.
 
Na wale wa kinondoni Mkwajuni walipata msaadawa UNDP-habitat, Halmashauri ya kinondoni na ILO kujenga mitaro ya kupitisha maji yaingie Salander bridge baharini in late 1990s. Maana maji yakijaa ndani ya nyumba yakifurika kutoka mto ng'ombe utokao Tandale na kinyesi cha ng'ombe na mifugo mingine-mbuzi, nguruwe etc na kinyesi cha binadamu(mto Ubungo). Wakazi wakisimulia jinsi walivyokuwa wakiweka watoto darini na kupanda juu ya bati mvua ya mafuriko na mafuriko yikija. Ila  kwa tamaa ya hela, waliowengi waliuza plots wakahamia bondeni kwenye maji ya kinyesi na uchafu mwingine. Iliyopita Dec 2011 ilikuwa babu kubwa ya maisha kupotea, mali n.k Cheap politics zinazema-walionewa kuhamishwa. Hawa watarudi na wanarudi.
 
Jee kama mvua ikija na mafuriko serikali iwaache isiende kuwaopoa kwa vile wamejitakia? Populist approach ya siasa zetu kwa kutaka sifa bila kuangalia essence na mantiki ya kitu itatuumaliza. Ni sawa haya unayoongea hapa mtu ni kulaumu upande mmoja iwe chama tawala au upinzani hii haitufai. Tuangalie na kulichanganua jambo kama afanyavyo P.Lawala hapa it is educative.
 
Mimi ninaona, iwe sasa vyama kujituma na kujipendekeza kwa wananchi na kufanya ushindani kimatendo sio kimaneno. Vyama vya upinzani kuchangisha, kutafuta misaada ya kuwajengea wale wa Mabwepande, kuwawekea miundo mbinu ili kuipiku CCM iliyolala na kuwaacha taabuni. Yaani action-oriented unafanyakazi inaonekana wanakugeukia wewe kukupenda na kukuona Mungu mtu na kura zote toka kwao zitakuwa zako.
 
Lakini ukiwaunga mkono warudikatika madhara na ukishabikia vitu visivyowasaidia, iko siku watakushitukia kuona ni maneno tupu matendo hakuna ni sawa ile ya kumchangia sana marehemu (kesha kufa) kuliko kumchangia kumuuguza apate afya. Waje wazolewe tena jangwani na Merk Sadick Mzee wa ukweli kesha kuwaambia hatopeleka mitumbwi tena kuwaopoa, utakuwa umeunga mkono kitu cha hatari. Ni sawa na wale wanaoziba njia za kupita mitaani na kuweka kiosk, kujenga vibanda chini ya transfoma za umeme na majumba ya kifahari mahala ambapo wanajua hairusiwi na kutumia mbinu za kuhonga ikibidi ajenge hapo. Tingatinga likiingia-uonevu. Moto ukiwaka hakuna njia ya gari kupita-fire vehicle inapigwa mawe. bado hao wajengao majumba ya maghorofa 20-50 ktk nchi ambayo moto ukiwaka huko juu solution wachupe chini au wasubili mpaka helikopta ya zima moto itoke south Afrika. Na majumba yetu tunaweka grili madirishani. Mzungu mmoja aliuliza kama nyumba zote DSM ni benki maana kila aionayo ina vyuma mkangoni na dirishani kuonyesha usalama wa hali ya juu kama utakiwao kwa bank. Tuna mengi ya kujifunza toka kwa wenzetu pia. Ni mifano michache kuonyesha jinsi gani Populist-cheap politics zitatumaliza.
 

From: Chacha Wambura <wamburacm@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, 17 September 2012, 13:47

Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
Bw. Tambwe,
 
Umenena. Kinachinisikitisha ni kwamba Watanzania sasa tumenyweshwa maji ya mzizi wa 'kama nongwa na iwe nongwa'. Tunajifanya sikio la kufa. Tunadhani Tanzania bila CCM itakuwa ni kama kuwa Mbinguni. Tumeziba macho, wala hatujifunzi kutoka kwa wenzetu. Tunakimbilia kule tunasikitishwa nako tukikutazama matukio yake katika TV. Tunadhani ingekuwa vyema polisi wote wauawe, serikali yote ife, sheria zote za nchi zizikwe kaburini, utawala wa nchi upewe upande mmoja ambao baadhi yetu tunafikiri ndio watakaotuletea neema ya asali na maziwa. Tunadhani ni kwa kupayuka huku tumetoa macho, kauli za jeuri, kebehi na za kuudhi dhidi ya viongozi wetu, huku tukiifanya hiyo ndio kazi ya kutwa, basi maisha yetu yatanyooka. Sivyo, hata kidogo.
 
Tunadhani tukiongea kauli mbadala, tofauti na wanazotaka hata wamiliki wa mtandao huu wa wanabidii, basi sisi sio wenzao. Zikiruhusiwa hizo kauli mbadala, kinachofuatia ni comment za kebehi bila kujali mantiki zilizomo. Nina mwaka sasa kila comment ninayoitoa wala sioni ikirushwa, na wala sijapewa masharti ya aina ya kuandika katika jukwaa hili. Ninapata hisia kuwa nalo linatumiwa na walewale wanaoiona serikali yetu na mifumo na viongozi wake kama mashetani. Lakini sikio hili la kupenda kusikia kile linachochagua, sio sikio la mambo endelevu. Ni sikio la giza, lisiloshirikiana na ubongo wake kuona mema katika hali anuwai.--- On Mon, 9/17/12, paul lawala <pasamila292000@gmail.com> wrote:

From: paul lawala <pasamila292000@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] UJUMBE WA RICHARD TAMBWE HIZZA KWA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 17, 2012, 9:05 AM

Tambwe + Kibajaji + Nape = hali ngumu2012/9/17 Abdalah Hamis <http://us.mc447.mail.yahoo.com/mc/compose?to=hamisznz@gmail.com>:> NA RICHARD TAMBWE HIZZA>> WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini> waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha> Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa> mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana> kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.>> Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika> kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la> polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa> yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na> kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa> vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya> majimbo 239).>> Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana> na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi> waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa> habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa> kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote> hatukuyategemea.>> Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na> msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki> baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania> ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo.> Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania> wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa> na nini/nani?>> Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri> sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea> na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la> polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia> wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo> walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je,> uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?>> Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la> kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa,> najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano> na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo> inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi> kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).>> Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima> wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha> kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi?> Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa> mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria> dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo> Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa> ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na> mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua> ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.>> Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya> nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo> kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu> ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria> viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata> upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria> inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.>> Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha> mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je,> ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza> sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha> kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu> Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka> katika taasisi zetu za habari?>> Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko> lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini> wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na> kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani> tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao> wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na> vyombo vyake?>> Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea> kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko> ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida> sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa> katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama> zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.>> Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji> ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika> shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira> hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.>> --> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com>> Kujiondoa Tuma Email kwenda> wanabidii+http://us.mc447.mail.yahoo.com/mc/compose?to=unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma>> Disclaimer:> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.>>-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.comKujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+http://us.mc447.mail.yahoo.com/mc/compose?to=unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment