Tuesday 4 September 2012

Re: [wanabidii] Tafakuri Ya Usiku: Je, Uwezo Wetu Wa Kufikiri Umepungua?

Mjengwa sidhani kama uwezo wa watu kufikiri umepungua! Mwanadamu haachi kufikiri, ila anaweza kuamua kutoshirikisha wengine anachofikiri....mfano uliotoa wa mtu kukurudishia swali unapomtaka maoni yake siyo kuwa huyu hajafikiri. Kuna kitu anakijua, lakini huenda amekata tamaa! Haoni kama fikra zake zinaleta tija akizitoa kwako.
 
Tunachojua ni kuwa Watanzania wengi wanajua tumefika pabaya, tunaelekea pabaya zaidi na matokeo yake ni mabaya kupindukia. Lakini nina hofu kuwa wengi tumekata tamaa hata kanla ya kujaribu kuongea. Sidhani kama ni woga, bali ni hofu tu ya kutosikilizwa. Pengine hatujawa na majukwaa yanayoaminika kubeba hoja za wanaotaka mabadiliko kwa umakini, uaminifu na ujasiri. Mfumo wetu wa kutoa hoja na kubeba mijadala ya kutusogeza kuchukua hatua bado uko kwenye makundi na siyo kwa mtu mmojammoja. Hakuna aliye tayari kumchapa kalumekenge aende shule, ndiyo maana mtu anakurudishia swali. Wakati umefika tupunguze kuulizana maswali na badala yake tupendekeze cha kufanya na jinsi ya kufanya.
 
Maoni yangu:
1: Tuanze na matatizo  ya kiutawala yaliyoko katika uwezo wa watendaji wa serikali za mitaa na vijiji. Kama raia wema tutimize wajibu wetu na tusikubali kuwa sehemu ya wavunja sheria, (kutupa taka ovyo, kuziba mitaa kwa biashara, kukaribisha wageni tusiowafahamu nk). Tujiepushe kutumiwa na viongozi kwa manufaa yao....  na tufanye kazi kwa bidii
2. Tutoe ushirikiano kwa vyombo vinavyotetea haki za raia hata kama itaweza kugharimu masilahi au maisha yetu. Tumewaona wenzetu wanajitoa mhanga.. Hakuna mafanikio yasiyo na gharama.
 
Makongo
 
 
From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, September 4, 2012 9:29 PM
Subject: [wanabidii] Tafakuri Ya Usiku: Je, Uwezo Wetu Wa Kufikiri Umepungua?



Ndugu zangu,

Yanayotokea nchini mwetu yanatutaka sio tu tufikiri, bali, tufikiri kwa bidii. Lakini swali ni hili; Je, uwezo wetu wa kufikiri umepungua?

Yumkini si kwa aliyekuwa na
ujasiri wa kuipiga picha hiyo hapo juu. Alifikiri sana pia. Na si kwa aliyekaa chumba cha habari na kuumiza kichwa, kisha akaamua picha hiyo ipambe sura ya mbele ya gazeti la Mwananchi la juzi. Hapa Iringa gazeti hilo liligombaniwa kama njugu, na bila shaka sehemu nyingine za nchi.

Naam, siku hizi utasikia ikisemwa; " Tumefika pabaya!" Mwingine atasema; " Tunakokwenda ni kubaya!". Lakini, ni Watanzania wangapi wenye kuuliza maswali haya; " Tumefikaje hapa?" Na " Je, tunaendaje?" Maswali hayo yanamtaka mwanadamu afikiri kwa bidii.

Wakati mwingine nafikiri, kuwa Watanzania tumechoka kufikiri. Hata kwenye maswali magumu yenye kutuhusu tunataka wengine wafikiri kwa niaba yetu. Unaweza kukutana na Mtanzania mwenzako ukamwuliza; " E bwana ee, unafikiri nini juu ya jambo hili?". Jibu lake; " Kwani wewe unaonaje?"- Ni moja ya maswali yenye kuashiria anaykujibu swali lako amechoka kufikiri.

Na wakati mwingine tatizo si kutofautiana kifikra, bali kutofautiana namna au jinsi ya kufikiri. Swali moja, lakini unaweza kuona namna tunavyotofautiana katika kuchagua njia ya kulisogelea ( approach) swali husika.

Na kuna wenye kukimbilia kutafuta njia za mkato. Ndio, majawabu ya mkato. Na baadaye itakuwaje? Inshallah na BwanaYesu Asifiwe!

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.com
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment