Monday 3 September 2012

Re: [wanabidii] Majibu ya Samwel Sitta Kuhusu Tuhuma alizozushiwa na Dr Slaa

Weka hapa hilo tamko la  Mbeya

Sent from my iPhone

On Sep 3, 2012, at 23:43, Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com> wrote:

Ninaamini wote mnaochangia hapa mko majumbani mwenu na wengine mkienelea kupata kinywaji chenu huku mkikazana damu iliyomwagika haitawaacha huru wale waliomtendea unyama ule, wote hup ni unafiki.

Mbona siwaoni mkiwa mtari wa mbele kupigani hicho mnachokihubiri humu kwenye majukwaa, niwaone basi mko barabarani mkipambambana kutokubaliana na damu ya yule mbeba mizigo wa Morogoro au mdogo wangu Mwangosi, tuache unafiki!!!

Mbona hao CHADEMA siwaoni wakizipigania hizo damu za kina Mwangosi na wenzao waliopoteza maisha kwa ajili yao.

Naelewa hamtonielewa katika msimamo huu, but ukweli utabaki pale pale, wananchi wasio hatia wanapoteza maisha yao kwa ajili ya wanasiasa ambao siku wakifika kwenye huo utukufu hawatawakumbuka, ni ukweli mchungu, lakini huo ndio ukweli.

Wengi tunabebwa na ushabiki kwa CHADEMA, kwa wasomi sio sahihi kabisa.

Asbert, wewe unao upande lazima utete.

Mkitaka kufahamu msimamo wetu kama waandishi wa habari Mbeya someni tamko letu, linabeba uhalisia wa hisia zetu na sio msukumo wa kiitikadi.

Felix

2012/9/3 Deogratias Kawonga <deogratias.kawonga@gmail.com>
Felix,

Pitia mara ya Pili Tamko la TEF na IPC. 
Umesema unashirikisha ubongo wako lakini kumbuka si mara zote Ubongo unatoa Majibu sahihi, kwa hiyo ni vyema kufikiri mara mbili mbili kabla ya kuandika na pengine omba ushauri kabla ya kupost humu. Nasema tena kwa respected person kama wewe hukupaswa kuandika vile hata kama ni kada wa chama.
Na amini Felix damu ya comrade D MWANGOSI haitawaacha huru wale wote waliomtendea Unyama huu.

 Mungu ibariki Tanzania

Sent from my iPhone

On Sep 3, 2012, at 20:52, moses <mosesgasana@yahoo.com> wrote:

Felix,
Hatia wanayo watawala wetu wanaowaza daily namna ya kuviua vyama ktk opposition camp.Hatia wanayo wale watu wanaoamuru Polisi kuwapiga watu wasio na silaha na hata kufikia kuua!
Sifa ya chama hai cha siasa kilichoko ktk opposition ni kuonesha shauku ya kushika hatamu za uongozi wa nchi huku kikionesha vitendo vinavyoonesha mwelekeo Hali hii watawala wetu hawaipendi kabisa.Inawakosesha usingizi kabisa!! 
Ndipo nguvu za Polisi zinapoanza kutumika vibaya!!!!! 
Hiyo ni HATIA!!
Moses

Sent from my iPhone

On Sep 3, 2012, at 5:37 PM, Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com> wrote:

Kupokea na kubwia kila jambo sio utaratibu wangu, kila jambo huliangalia katika pande zake mbili. Iwapo viongozi wa CDM wangetathmini kuhusu hayo mauaji ya raia wasio na hatia kwenye hiyo M4C wangeweza epusha mauaji hayo. Huo ni mtazamo wangu, kuhusisha na chombo nachofanyia kazi ni upo mwingine.

Nina reason kwa kutumia ubongo wangu badala ya kusukumwa na mkumbo.

CHADEMA lazima wajitathmini, hii hadi damu ya mwisho huku inayomwagika ni ya wananchi wasio na hatia hapana.

Felix

2012/9/3 Deogratias Kawonga <deogratias.kawonga@gmail.com>
Huyu Mwakyembe si ndio mwandishi gazeti fulani, kwa hizi comments na huu mtazamo wake nahisi gazeti lake liko kwenye Market risk.

Ni mtazamo tu.

Sent from my iPhone

On Sep 3, 2012, at 16:22, Apilike Gordon <apilike@gmail.com> wrote:

Kusema mwenyekiti wa chama ni DJ ndio kukosoa??

2012/9/3 denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Kaka Mwakyembe umepotoka kabisa. Hamna justification yoyote ya kufanya hiki kilichotokea! HAMNA...................

2012/9/3 Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
CHADEMA pokeeni na upande wa pili wa shilingi yenu, msipende kusifiwa tu mtashindwa kujitathmini.

Leo kelele za ufisadi zimelekezwa CCM lakini katika Bunge lililopita tumeshuhudia baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakitajwa kwenye ufisadi kwenye sakata la TANESCO, kwa hiyo hamjawa malaika nanyi ni binadamu wa kawaida, kuna mapungufu mengi tu.

Leo kwenye hiyo M4C, zinatokea vurugu, sijasikia kiongozi wa CDM akikamatwa or kuawa, bali ni wananchi wasio na hatia, tena wasiohusika, nanyi mnaendelea pasipo kuijihoji kuhusu movement yenu na maisha ya wananchi wasio na hatia yanayopotea.

Hata kama ni polisi ndio wenye kuua, lkn chanzo ni M4C!!

Kubalini kukosolewa mtafika mnakotaka kwenda,sifa ndizo zilizoifikisha CCM hapo ICU ilipo.

Ni mtazamo tu!

Felix

2012/9/3 mngonge <mngonge@gmail.com>
Mzee Sitta tumekupata vilivyo kwanza nikushukuru kwa kujitokeza
waziwazi kutoa maoni yako hadharani. Nakubaliana na wewe mambo kadhaa
lakini pia natofautiana na wewe kama nitakavyoeleza hapo chini. Mambo
hayo ni pale unaposisitiza kwamba Chadema wanayo safu nyembamba ya
uongozi na kwamba hawana uwezo wa kubuni mikakati ya kuinua uchumi,
hivyo wasikabidhiwe nchi. Ninasema maoni yako ni ya juu juu tu
ukichambua mambo hayo kwa undani hadithi inakuwa kinyume kwa sababu
zifuatazo:
1. Safu ya uongozi nyembamba- Ni kweli ukiangalia safu ya uongozi wa
Chadema haina watu wengi wenye CVs (vyeti) zinazotisha, wengi ni watu
wa kawaida sana. Na hilo ndo linaifanya Chadema kukubalika kwa watu,
ebu mzee jikumbushe kilichotokea katika chaguzi ndogo za ubunge huko
Igunga na Arumeru . Hao viongozi waliopo CCM wenye CVs kubwa
kimaandishi ndio hao waliotufikisha tulipo, mzee Sitta usifikiri
wananchi hawako objective, wanaelewa wanachokitaka na ata
wanachikifanya. Viongozi wenye CVs ni watu wanaoishi dunia nyingine
tofauti na ya wapiga kura. Naomba nimuelimishe Mzee Sitta kwamba
watanzania wengi wenye CVs ni woga wa kujiunga na siasa wazi wazi kwa
vile mfumo uliopo unaonyesha kwamba mtu akijiunga na opposition
parties kuna favours na mambo kadha wa kadha atayakosa na ata
kufukuzwa kazi au kunyimwa fursa za kibiashara. Hivyo wanabaki kuwa
neutral au kujiunga na CCM si kwa mapenzi yao bali kuweza kufanikisha
malengo yao kiuchumi pengine ata mzee Sitta yuko kundi hilo.

Mzee Sitta naomba ukumbuke kwamba wataalamu wa nyanja zote wanaofanya
kazi serikalini si mali ya CCM. Hawa ni waajiriwa wa serikali na ata
kama Chadema kitakuwa madarakani bado wataendelea kuwepo kazini. Labda
kama kwenye sera za Chadema kuna hilo la kuvunja mikataba na
wafanyakazi wote hapo nitaomba kuelimishwa. Hao ndo watu
wanaofanyakazi zote za kuinua uchumi na maendeleo ya jamii nchini
kwetu siyo kwa sababu wako CCM. Kinachotakiwa ni wanasiasa wachache tu
wenye uzalendo na akili ya kuwatumia vizuri hao waajiriwa wa serikali.

Sera zote zinazotumika katika wizara, idara na mashirika ya serikali
zimetengenezwa na wataalam ambao ni waajiriwa wa serikali wala siyo
CCM. CCM inachokifanya ni kusimamia tu na ata wakati mwingine
kukologa. Kwa vyovyote vile nchi zote zilizoendelea si kwa sababu ya
safu kubwa ya wanasiasa bali ni kwa sababu ya wataalamu katika nyanja
mbalimbali ( wachumi, wahandisi, walimu, madaktari, mafundi, wakulima
wakubwa nk). Kama ni utaalamu wa mambo ya siasa basi ata hao walio
CCM siku Chadema kikichukua madaraka wengi wao watakuwa upande wa
Chadema. Naomba nikutoe wasiwasi huo kwamba swala la safu ya uongozi
kuwa nyembamba si tatizo kama wananchi wataamua kuipa madaraka
Chadema.

2. Dr.Slaa kuwa dikteita
Ni kweli inawezekana Dr.Slaa kama binadamu akawa dikteita kwa hulka
yake lakini ata Mlm Nyerere alikuwa na kaelement ka udkiteita ili
mambo yaende na kwa manufaa ya taifa. Kama kiongozi atakuwa na
udikteita kwa manufaa ya wengi nasema huyo anatufaa. Ukitaka kumuua
nyani usimtazame usoni, mambo ya kumtazama mtu usoni ndiyo
yaliyotufikisha hapa tulipo. Kwa vile watu tumepigia kelele juu ya
kupunguza madaraka ya rais basi ni vyema tukaliangalia vizuri swala
hilo wakati wa kurekebisha katiba, ili tukimuona  kiongozi an
udikteita usiyo kuwa na manufaa ya wengi tumuondoe madarakani.

3. Chadema hawana sera bali wanatembea nchi nzima kueneza chuki dhidi
ya serikali
Binafsi siamini maneno hayo kwa vile watu wanakuja wenyewe kwenye
mikutano ya Chadema na kusikiliza. Kama wanaeneza chuki ni vyema
serikali ikawapeleka mahakamani lakini kama yanayosemwa yapo hizo si
chuki bali ni ukweli. Siku zote ukweli unauma.
4. Hawaonyeshi vyanzo vya mapato
Mzee Sitta hivi mtu kama wewe unahitaji kuelezwa ni vyanzo vipi vya
mapato tulivyonavyo Tanzania? Binafsi ninachojua ata bila ya kubuni
vyanzo vipya mtu akasimamia vile ambavyo tunavyo sasa maisha ya
mtanzania lazima yataboreka.
Ninaposema hivyo nina maana kwamba kila sehemu ya kazi inayosimamiwa
na serikali moja kwa moja wawekwe watu wenye uwezo na sifa za
kusimamia bila upendeleo. Bila kujali ni dini gani, kabila gani,
mwanachama wa chama gani nk. Bila kusahau kukomesha rushwa na hasa kwa
kuanza na viongozi wa juu. Kuwa na idara ya usalama wa taifa
itakayowezeshwa na kusimamia maslahi ya taifa vilivyo

Nahitimisha kwa kusema kama wananchi wataona Chadema ndo chama cha
kuwaletea maendeleo tuheshimu uamuzi wao. CCM kama munataka kuendelea
kushika hatamu jitahidi kuleta maendeleo ya kweli siyo ya mdomoni.
Watanzania wa leo wanayo akili ya kuchambua pumba na mchele.
Tusiangalie maendeleo ya familia zetu tu tukahisi na wenzetu wa kima
cha chini wanaridhika na hali zao.

Mchana mwema

2012/9/3 denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>:
> Kuzushiwa?
>
>
> 2012/9/2 Pata Habari <patahabari@gmail.com>
>>
>>  Nimesikitishwa na kauli za jazba na mwangwi wa kiwewe za Mhe Dr W
>> Slaa alipokuwa Iringa juzi hadi kuniita mnafiki, mwongo, mtu wa hatari
>> n.k
>>
>> Hali hii inatia mashaka juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa kisiasa
>> kuhimili kukosolewa ambayo ni sifa muhimu ya maisha ya mwanasiasa
>> yeyote hususani anapojinadi  kuwa anaweza kuchukua madaraka ya
>> kuiongoza nchi.
>>
>> Kauli zisizo na staha alizozitoa Dr Slaa dhidi yangu kama vile sifai
>> hata uongozi wa kata zinadhihirisha mambo mawili:
>>
>>     Dr Slaa ni dicteta. Hana uvumilivu. Ana hulka ya kujiskia kwamba
>> mawazo yake hayapingwi.
>>     Ni mzushi asiyeogopa kusema na kupindisha mantiki ya jambo ili tu
>> kushinda hoja. Iweje mtu aliyenibembeleza nigombee uraisi kupitia
>> chama chake mwaka juzi leo aseme sifai kuongoza hata kata kwasababu tu
>> nimetamka ukweli juu ya udhaifu wa chama chake cha siasa?
>>
>> Niliyoyasema pale Karagwe majuzi katika uchambuzi wangu wa vyama vya
>> siasa nchini ni kwamba CHADEMA wamekuwa hodari wa kukosoa na
>> kuishambulia CCM na serikali zake lakini wanasau kuwa ili wawe mbadala
>> kwa kuiongoza nchi hawana budi kurutubisha safu yao ya uongozi nawe na
>> watu wakutosha kuweza kushika madaraka ya ngazi mbalimbali za uongozi
>> wa Taifa. Kuukataa ukweli kwamba safu ya uongozi wa CHADEMA ni
>> nyembamba ni kujidanganya tu.Kupita mikoani kutangaza kwamba matatizo
>> yote ya wananchi yanatokana na CCM ni kazi rahisi na ina mvuto wake
>> kisiasa lakini mwanasiasa makini hana budi kwenda mbele zaidi ya
>> hapo.
>> Hana budi kutuambia wapiga kura mipango ya chama chake inayoeleweka na
>> inayotekelezeka na iliyo makini kukabiliana na changamoto mbalimbali
>> za maendeleo ya nchi. Ahadi za alinacha za tiba bure, elimu bure bila
>> kuonyesha vyanzo halisi vya mapato ni porojo tu. Kusema kwamba
>> raslimali za nchi kama vile gesi asilia, madini, makaa ya mawe, utalii
>> zinatosha kuondoa umaskini ni nadharia tupu ambayo uhalisia wake hauna
>> budi kubainishwa kwa mikakati dhahiri na thabiti ya kiutawala
>> (uendeshaji) inayoweza kuchuma utajiri huo kwa ufanisi, kwa uendelevu
>> na kwa faida ya wengi1. Kuhusu mwenyekiti Mh Mbowe – MB
>>
>> Katika hotuba yangu sikukejeli uzoefu wa Mhe Mbowe, wala sijasema Mhe
>> Mbowe ni mcheza disko. Niliuchambua wasifu wa viongozi wa CHADEMA na
>> kutamka uzoefu  wa Mhe Mbowe katika vitega uchumi vya burudani hii
>> siyo kudharau bali ni kutamka ukweli tu.Huwezi kuuelezea wasifu wa Mhe
>> Mbowe bila kuelezea mchango wake mkubwa katika tasnia ya
>> burudani.Mmoja wa maraisi maarufu wa marekani (USA)alikuwa ni mcheza
>> sinema Ronald Reagan.Na hapa Tanzania tulikuwa na mzee R. Kawawa
>> ambaye alianzia katika tasnia ya uigizaji, kwa hiyo Mhe Mbowe au Dr.W.
>> Slaa anaweza akawa Rais wetu kwa maana ya kupigiwa kura za uchaguzi wa
>> demokrasia.Kumudu au kutoyamudu madaraka hayo ni suala tofauti.
>> Tathmini yangu ilihusu safu nzima ya uongozi wa CHADEMA kwa ujumla
>> wao.Ni safu nyembamba mno.2. Kujiunga na CHADEMA
>>
>> Kama alivyosema Dr. Slaa Chadema walifanya jitihada ya kunishawishi
>> niingie CHADEMA 2010 na niwe mgombea wao wa Urais. Jambo hili
>> nililitafakari na kutafuta ushauri kwa watu wangu wa karibu na
>> nikabaini kwamba:-
>>
>>     CHADEMA wana migawanyiko yao ya uongozi tena ni ya hatari
>> kwasababu ni ya kikanda za nchi – yaani nani anatoka wapi.
>>
>>     Kutokana na yaliomo katika ilani yao ya uchaguzi 2010 – 2015
>> nilibaini mambo ya kiitikadi ambayo siyakubali kama vile sera ya
>> majimbo. Sera ya majimbo inawezekana katika nchi ambazo ni tajiri na
>> pia isiyo na tofauti kubwa ya hali ya maisha baina ya kanda mbalimbali
>> za nchi kama vile Marekani (USA). Kuleta majimbo Tanzania ambako kuna
>> tofauti kubwa za kimaendeleo baina ya Kaskazini, Mashariki, kati,
>> Kusini na Magharibi ni kusababisha nchi ichanike vipande vipande.
>>
>>      Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma
>> bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe
>> siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa
>> umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza
>> wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo
>> nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za
>> msingi sikubaliani nazo.
>>
>> Baada ya hapo nisingeweza eti baada ya uchaguzi Mkuu niombe kugombea
>> Uspika kupitia chama cha CHADEMA.3. Kuhusu CCJ
>>
>> Kama ilivyo kawaida kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea bora, CCJ ni
>> miongoni mwa vyama vilivyonifuata mimi na baadhi ya wanasiasa wakati
>> wa maandilizi ya uchaguzi mkuu. jambo hili si la siri wala la ajabu na
>> Nimelizungumza hili mara nyingi. Isitokee katika mfumo wa vyama vingi
>> vya siasa mtu kutoka chama kumoja cha siasa na kujiunga na chama
>> kingine haiwezi kusemwa kuwa ni uhaini. Na kama Ningeridhika na mambo
>> yao ningejiunga na CCJ mwaka 2010 lakini sikufanya hivyo. Pia ni
>> uzushi usio na msingi kunihusisha na uanzishaji wa chama hicho.
>> Waanzilishi wa chama hicho cha siasa wanajulikana na wapo hai, ni haki
>> ya kikatiba ya kila Mtanzania kuanzisha au kujiunga Binafsi na chama
>> chochote cha siasa.4. Madai mengine
>>
>> Eti nilitamka kwamba ningehamia chadema na Wabunge wa CCM 55 ni porojo
>> za Dr. Slaa kama ulivyo usemi ningeihama CCM siku chache kabla ya
>> kuvunjwa Bunge la 9.
>>
>> Inashangaza kwa Dr Slaa kukejeli uendeshaji wa bunge la 9 ambalo ndilo
>> lililowapa fursa watu kama yeye kujulikana na kujipatia umaarufu.
>>
>> Haya madai ya mimi nikiwa Spika kukwamisha uchunguzi wa Meremeta na
>> Richmond ni kutokana na hisia tu za chuki. Taratibu za Kibunge
>> hazimwezeshi Spika kuwa Dikteta anayeamua nini kijadiliwe na nini
>> kisijadiliwe. Yote yapo katika kanunu za Bunge. Maamuzi ya Bunge si
>> lazima yawe ni ya Spika.
>>
>> Kuhusu ofisi ya Mbunge jimboni Urambo mahasimu wangu ndani ya CCM na
>> nje yake wameng'ang'ania kwa makusudi maalum kuiita ofisi ile kuwa ni
>> ya Spika. Michoro yake na gharama zake hata ukijumuisha samani
>> haifikii tarakimu za ajabu wanazotaja mahasimu wangu kujenga hoja
>> istoshe ofisi hiyo haina maslahi yeyote binafsi kwangu Aidha viongozi
>> wengine waliofikia hadhi za juu mathlani ya uwaziri mkuu nao
>> wamejengewa majimboni ofisi zinazolingana na hiyo
>>
>> Porojo nyingine binafsi kama vile kumuhusisha mke wangu kumpigia simu
>> Dr Slaa kumsihi anisaidie kisiasa ni upuuzi wa aina yake
>> unaodhihirisha umahiri wa Dr.Slaa katika siasa za kiwango cha chini.
>>
>> 5. HITIMISHO
>>
>> Mimi nikiwa mwanasiasa mzoefu na mkongwe nimetoa ushauri na
>> nitaendelea kutoa ushauri kwa makundi mbalimbali nchini.Kuniambia
>> naingilia mambo ya CHADEMA ni kichekesho.Wakiwa wao ni chama cha siasa
>> kinachoendesha harakati za kuwania kuchukua madaraka ya kuongoza nchi
>> ambayo mimi ni raia wasitazamie kuwa sisi wapiga kura tutaacha
>> kuwachambua.Wanalo tatizo kubwa la safu nyembamba mno ya uongozi,
>> Kulingana na majukumu ya kuendesha nchi.
>>
>> Kujilinganisha na safu ya uongozi ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere
>> ni mzaha wako wapi akina R.M Kawawa, Pauli Bomani, George Kahama, Amir
>> Jamal, Solomoni Eliufoo, Tewa Saidi, Tewa Abdallah, Fundikira wa
>> CHADEMA? Kutembea nchi nzima kuhamasisha chuki dhidi ya serikali
>> iliopo madarakani ni jambo jepesi lakini Watanzania walio  makini
>> wanahitaji maelezo ya mipango mbadala ya uchumi kuinua hali za maisha
>> yao na kuiona safu ya uongozi itakayowezesha kwa dhati kubuni na
>> kusimamia mikakati endelevu ya kuondoa umaskini kujenga uchumi imara
>> na kuimarisha umoja wa watanzania
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
>
>
> --
> Wasalaam
>
> Denis Matanda,
> Mine Supt,
> Nzega - Tanzania.
>
> " Low aim, not failure, is a crime"
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

0 comments:

Post a Comment