Tuesday 18 September 2012

Re: [wanabidii] MADAKTARI WAMWOMBA RADHI RAIS NA WATANZANIA

Niliisoma habari hiyo jana usiku na nikamshauri Yona atujuze habari hiyo kwa undani lakini hajafanya hivyo hadi muda huu ninapoandika ujumbe huu. Kwa vyovyote vile Yona amejua kwamba tumekwishasoma magazeti na kuujua ukweli. Nimesoma gazeti la majira Habari leo na Mtanzania  na kukuta kichwa kikubwa sana cha habari kinachosema " madaktari waiangukia/waomba radhi serikali kwa madhara ya mgomo" Na kwamba wameapa kutorudia tena.

Yona nina imani kubwa sana na wewe lakini kuna wakati unabughi stepu. Ukiwa kama mwandishi au mtanzania wa kawaida ni vyema uwe unajaribu kuanzisha na kutoa hoja zilizokamilika. Sakata la madaktari na serikali tumelishuhudi wote hadi likampelekea Dk.Ulimboka kutendewa unyama uliopindukia, iweje leo ulichukulie kimzaha mzaha hivi? Sijui ulikuwa na maana gani kutujuza kwamba madaktari wameiangukia serikali huku ukijua ni kakikundi tu na wala si wawakilishi wanaotambuliwa na madaktari kwa mujibu wa taratibu na kanuni zao?

Tangu jana usiku kabla ya kuchangia hoja nilitaka kujua kama ni madaktari wale wale waliogoma au ni mamluki. Baada ya kusoma habari yenyewe nikagundua kwamba tamko hilo lilitolewa na mtu aliyetambulishwa kwamba ni mwenyekiti wa jumuia ya madaktari walioathirika na mgomo. Swali je jumuiya hiyo iliandikishwa lini na wapi? Hapana shaka imeundwa harakaharaka kwa lengo la kutupiga changa la macho. Kwa nini viongozi wa jumuiya iliyoongoza mgomo wasijitokeze kuomba radhi tena siyo kwa rais bali kwa watanzania wote na badala yake waonekane hao waathirika tu?

Kundi lililojitokeza na kuomba radhi kweli ni waathirika, inawezekana wamepatwa na tatizo la msongo wa mawazo ndiyo maana wamekurupuka bila kuwahusisha wenzao na kujifanya ni wasemaji wa madaktari wote. Kuhusu hilo sina ubishi. Lakini tujiulize hao ndo wawakilishi sahihi wa madaktari?

Naungana na Kigwangalla kusema hizo ni propaganda za kipolitiki na hazitatusaidia kutatua matatizo yanayoikumba sekta ya afya. Ni bora tukae chini na madaktari pamoja na watoa huduma wote katika sekta hiyo na kuona ni namna gani tutaboresha huduma. Ni ndoto za mchana kweupe kufikiri kwamba tutaudanganya umma. Siku zote mficha maradhi msiba umkuta.

2012/9/18 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Ubarikiwe HK kwa kapande ka elimu hako

--- On Mon, 9/17/12, hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> wrote:

From: hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com>

Subject: Re: [wanabidii] MADAKTARI WAMWOMBA RADHI RAIS NA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, September 17, 2012, 3:48 PM

Yona, mi ninashaka sana na ulichokiandika hapa maana nimo kwenye eGroup ya madaktari inayokwenda kwa jina la muxalumni na sijaona kitu kama hicho...ama hii ni propaganda inayolenga kuwatawanya kabisa wanafani hawa???! Nakushauri uwe makini sana na kuwachokonoa maDk ambao bado wana majeruhi mioyoni mwao na wengine wameacha kazi kwa hasira. Fahamu kuwa propaganda hazisaidii sana kutatua tatizo la huduma mbovu za afya nchini...wewe si Mbunge wala mtafiti wa mfumo wa afya kama nilivyo mimi, naomba nikuelimishe tu kuwa 'kuna tatizo kubwa kwenye mfumo mzima wa afya nchini' na ufumbuzi si siasa, vitisho ama propaganda kama hizi! Wanaoumia si wewe na mimi na familia zetu, wao wahanga halisi, ambao hawaandiki emails za props kama zako!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Date: Mon, 17 Sep 2012 15:29:58 -0700 (PDT)
Subject: Re: [wanabidii] MADAKTARI WAMWOMBA RADHI RAIS NA WATANZANIA

Kama ni kweli basi hili ndilo kosa.
Kuwaomba msamaha watanzania kwa kuwa walifanya kosa la kuwatafutia mazingira bora ya kutibiwa wanayonyimwa na mipango mibaya na wanasiasa.

--- On Mon, 9/17/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] MADAKTARI WAMWOMBA RADHI RAIS NA WATANZANIA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, September 17, 2012, 9:49 AM

Ndugu zangu

Nasikia Baadhi ya madaktari waliokuwemo kwenye mgomo wamewaomba radhi
watanzania na rais wa tanzania mhe jakaya mrisho kikwete kutokana na
mgomo uliotokea .

Mimi kama mtanzania nimewasamehe na nawatia moyo waendelee na kazi zao
kama kawaida na wale waliofunguliwa mashtaka mbalimbali yanayohusiana
na mgomo , wafutiwe kesi hizo warudi makazini na hata wale wanafunzi
pia wasamehewe warudi makazini kama kawaida .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment