Tuesday 20 December 2016

[wanabidii] SERIKALI HAIJAPIGA MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA KUKOPA BENKI, VICOBA, SACCOS NA TAASISI NYINGINE ZA FEDHA

Wadau habari za kazi

Kumekuwa na taarifa inasambazwa katika mitandao ya kijamii, makundi ya 'WhatsApp', 'Facebook' na majukwaa mbalimbali ikieleza kuwa Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma   kukopa Benki,SACCOS,VICOBA na  Taasisi mbalimbali za kifedha.

Taarifa hiyo ambayo imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza, na izingatiwe kuwa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote ya Fedha nchini.

Ikumbukwe kuwa, mikopo yote ya watumishi wa umma katika Taasisi za Fedha hutolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza vigezo.

Aidha, natumia fursa hii kuwakumbusha watumishi wa umma kutojihusisha na usambazaji wa taarifa zisizo za kweli na ambazo zina mamlaka husika ya kuzitoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma

Taarifa husika imeambatishwa
Asante
Asiatu Msuya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment