What is wrong with maandamano, if I may ask.
em
2016-12-20 13:01 GMT-05:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Najua nimechelewa kuleta mada hii humu lakini haiepukiki kuletwa kwa mjadala kwa kila anayeziangalia kwa umakini siasa za Tanzania. Si wote waliisoma kwenye Facebook yangu.
Yapata wiki tatu hivi zilizopita katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV kulikuwa na mgeni mmoja. Mgeni huyo ni Ndugu Wilfred Rwakatare, Mbunge wa jiji Tarajiwa la Bukoba (kwa sasa ni manispaa lakini ndoto yake ya 2005 ni kulikuza kuwa jiji). Rwakatare ni Waziri kivuli wa wizara inayohusika na ardhi na nyuma.
Katika kipindi hicho alifufua matumaini yangu kuwa upinzani ungali unaishi Tanzania na ni kwa sababu watu wenye mawazo kama yake hawapati nafasi za mbele katika taasisi walizomo.
Katika kipindi hicho Rwakatare anamsifu waziri Lukuvi lakini anaikosoa serikali kwa kutotoa fedha zilizoahidiwa kwenye bajeti za wizara.
Akijibu swali kuwa kama yeye (Rwakatare) angekuwa waziri angefanya nini kuhusiana na migogoro ya viwanja katika mazingira ya sasa, anajibu swali kwa kusema: angetoka nje ya Dar Es salaam na kutafuta maeneo Kibaha. Angewachukua wananchi wanaotaka viwanja kutoka Dar Es Salaam na kuwaonyesha maeneo hayo na kuwataka waeleze mahitaji yao ya viwanja. Watu hao wanaombwa kutoa fedha za kupima viwanja na kila mtu anapimiwa eneo analotaka. Kwa sababu tayari maafisa ardhi wapo, garama za upimaji zinastahili kuwa ndogo. Na kwa sababu wanaohitaji viwanja wanagarimia basi serikali haitahitaji kutoa fedha nyingi. Anaendelea Rwakatare kuwa angehakikisha serikali inapanua mradi wa mabasi ya mwendo kasi na reli kutoa huduma mpaka huko na kuhakikisha inachukua dakika 40 kutoka maeneo mapya mpaka Dar Es Salaam. Hii ingeondoa msongamano wa watu Dar Es salaam.
Ukichunguza usemi huu unaona sera mbadala ya tatizo la viwanja na usafiri Dar Es Salaam. Unaona jinsi ambavyo viwanja vinaweza kupatikana kirahisi kwa sababu mara zote serikali inasema haina fedha za kupima viwanja huku watu wakitumia fedha nyingi kununua viwanja hivyo.
Hapa mimi nataka kuongelea "sera mbadala". Naweza kusema toka Dr. Slaa ameondoka upinzani, vyama vyetu vya upinzani havielezi sera mbadala kwa matatizo ya wananchi bali vinapiga kelele ya kutetea uhuru wake wa kufanya fujo na kuchelewesha maendeleo ya wananchi. Utasikia wakitaka bunge live. Ili mwananchi aondokewe na tatizo gani kati ya kero alizo nazo? Wanataka bunge lisiendelee na vikao kwa sababu wao wametoka nje kupinga Speaker kuwakumbusha kanuni. Wanataka waruhusiwe kuandamana wakati wengine wanakazana kuzalisha. Maandamano yanakuja kusaidiaje kuongeza uwajibikaji serikalini; au kudhibiti rushwa na ufisadi mambo ambayo hasa ndiyo kero za wananchi wanaowawakilisha? Wapinzani wakafikia hatua ya kusahau kuwa wanawakilisha wananchi na kero zao wanaanza kutetea haki zao za kucheza michezo ya kuigiza barabarani na kwa hiyo huduma kwa wananchi zisimame. Imefika mahala wengine wakaona upinzani ni kama mchezo wa watoto kwa hiyo wanapodhibitiwa ni halali ili watu wazima waendelee na mambo ya ,maendeleo. Ile hali ya watanzania kuunga mkono hoja za upinzani zilielekea kusahaulika.
Lakini kama taasisi hizi zikiweza kujiambia ukweli na kuwapa vipaza sauti akina Rwakatare huenda na serikali na chama tawala vikazidi kuwa macho. Vyama hivi vinahitaji kuachana na watu waliojichokea au kushindwa kazi, na viwape watu wenye mwelekeo wa kujua wananchi wanataka nini. Haina maana yoyote kumchukua mtu aliyeshindwa na kuharibu unamleta mbele za watu na kutarajia mwishoni mwa 2017 au 2020 atauongoza upinzani eti kwa sababu mchawi fulani kabashiri hivyo. Kuna mambo mengine hayahitaji kukubali kudanganyana. Kinyume chake ni kuuimarisha mfumo wa chama kimoja ndani ya vyama vingi vya siasa kama Botswana.
Elisa Muhingo
0767 187 507
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment