Saturday 28 November 2015

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] NAOMBA LEO NIWATAJE WABUNGE HAWA WAWILI...


Mageed,
Hongera kwa nia yako hiyo, ila, ila kabla hujachangia pato lako kwa serikali ya kijiji chako nakuomba wewe Mageed kama mwanamabadiliko anza kwa kuichangia mabadiliko forums kwani kuna uzi ulirushwa hapa kwa wanamabadiliko kuchangia gharama za uendeshaji wa jukwaa letu pendwa na linalokuwa siku hadi siku.

Natanguliza shukrani.

On Nov 29, 2015 6:57 AM, "Maggid Mjengwa" <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:


Ndugu zangu,

Hali ya uchumi wa nchi yetu ni ngumu kwa sasa. Hatua zote za Serikali za kubana matumizi ni za kuungwa mkono kwa nguvu zote na kila Mtanzania anayeitakia mema nchi yetu.

Watanzania tumeguswa na hatua za Wabunge Zitto Kabwe na Elibariki Kingu za kujitolea posho za vikao vyao vya Bunge kwa bajeti za maendeleo ya majimbo yao.

Ingependekezwa hapa, walau katika kikao cha bajeti ya Serikali 2016-2017, Wabunge na Madiwani, kwa hiyari, wajitolee posho za vikao hivyo vya bajeti kwenye kuchangia kwenye Hazina Kuu, kwa Wabunge na Mawaziri, na Halmashauri, kwa Madiwani.

Mimi kama ' Mwenyekiti' wa Kijiji Mjengwablog.com  naahidi , katika kipindi cha bajeti ya Serikali 2016-2017 , nitajitolea malipo yangu yote nitakayopokea kwa kazi za kiuandishi, kwa kuchangia kwenye bajeti ya maendeleo ya halmashauri yangu ninakoishi sasa.

Nianze leo, kwa heshima, kwa kuwataja Wabunge hawa wawili waliojitolea posho zao, mbali ya mambo mengine, kuchangia pia bajeti ya Serikali ya 2016-17;

1. Zitto Zuberi Kabwe , ACT
2. Eliakim Kingu, CCM

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye5gCuKrELa12dk2MfH6b3USqJ2C9wuOj5rak1AHOYCQow%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment