Inavyoonekana wengi hatuna historia ya rise and fall ya vyama vya upinzani hapa nchini. Lakini pia hatujui dalili za magonjwa yanaoua kila chama cha upinzani kinachojitahidi kuinua kichwa dhidi ya CCM. Kwanza ijulikane kuwa hata hao CHADEMA tunaowasema si wabunge wake wote na viongozi wenye nia ya dhati kabisa ya kutaka kuking'oa CCM madarakani. Kinachopiganiwa ni mkate wa kila siku na si kingine. NCCR-Mageuzi ilikuwa na dalili zake za kufa, wengine tuliandika mapema na kuonya kiasi cha kuitwa manabii. Kikaja kufa hivyo hivyo. Ikaja CUF na ngangari dhidi ya ngunguri ya Omar Mahita. Hapa pia wachambuzi wakaandika na kuonya kuwa kutokana na misingi thabiti ya nchi hii, ukija na sera yoyote inayoonesha sura na taswira ya vurugu kwa hakika huwezi kufika mbali. Kuna dalili zote kuwa mwisho wa Chadema uko mlangoni. Kauli za kina Peter Msigwa si za kukuza chama cha siasa katika nchi yoyote iliyo na misingi ya ukomunisti ulioyeyuka. Mbowe analijua hili vizuri sana na anafahamu kuwa mwisho wa chama chake ni 2015 maana baada ya kushindwa kutafuatia kukata tamaa kukubwa. Wanabidii, naomba niwape kwa mara nyingine utabiri wangu. NCCR-MAGEUZI ita-gain momentum na itakuja kuwa threat kwa CCM siku chache zijazo kuliko CHADEMA. Uongozi wa James Mbatia unaweza kukuza chama maana Watanzania wa jana, wa leo na wa kesho ni wapenda amani hata kama amani huwa na mwisho kwa muktadha wa uvumilivu. Kinachofanyika bungeni na wabunge wa Chadema ni ulimbukeni wa siasa ambao siku zote huwa na mwisho mbaya. Naamini kuna njia mbalimbali ambazo wabunge wa Chadema wanaweza kufikisha ujumbe bila kutunisha misuli na matusi. Lakini pia ikumbukwe kuwa wabunge wa CCM ni wajanja sana. Wao majimbo yao yanaendelea, Chadema wanasusia. Watakuja kukumbuka shuka kumekucha. Mfano tumeona kwenye uundwaji wa MABARAZA ya Katiba. Ni Chadema hao hao ndio walipitisha utaratibu wa namna ya kuwapata wajumbe wa mabaraza hayo. CCM ikaanza kujipanga mapema, sasa wameingiza watu top. Chadema wao walikuwa wakiandamana na kuzunguka na people's power. Nawaambieni, mwakani kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa. Chadema wameganda kwenye mabaraza ya katiba na tembo wanaoibiwa. CCM tunawaona wanavyozunguka sasa hivi nyumba hadi nyumba kuweka mambo sawa. Chadema inasubiri kampeni mwakani bila kujua ushindi katika siasa ni mahesabu si wingi wa watu na kura. Wakija kupigwa wataanza kudai wameibiwa kura. Yetu macho, wengine hatuna dini wala siasa. --- On Sat, 4/27/13, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment