Idriss Mussa
Sent from my BlackBerry® smartphone from Orange Botswana
From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 26 Mar 2013 19:11:10 +0000
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] " Njiani Kwenda Kwa Rais!"
Ndugu zangu,
Leo mchana wakati nikipata kikombe changu cha chai na andazi pale Tea Room ya kona ya Jamhuri na Morogoro nilipitia kitabu cha mwandishi wa Kisweden Stig Holmqvist kiitwacho; Pa Vag Till Presidenten- Njiani kwenda kwa Rais.
Mwandishi kwa lugha ya Kisweden anaipitia historia yetu huku mwenyewe akiwa mshiriki kwenye simulizi yake.
Wakati nikimsoma Holmqvist nikatafakari ujio wa Xi Jinping, Rais wa China hapa kwetu Tanzania.
Mwandishi anatukumbusha pia mahusiano ya Tanzania na China na Soviet Union wakati ule wa Vita Baridi ( Kiitikadi) vya Dunia. Mahusiano ambayo yalimweka Julius Nyerere kwenye wakati mgumu sana.
Naam, Wachina wamerudi tena, safari hii si kiitikadi, bali kiuchumi zaidi. Wakati ule wa kiitikadi Tanzania ilikuwa mshiriki muhimu kwenye harakati. Na sasa kwenye Vita Baridi ya Kiuchumi, ujio wa Wachina Afrika unaofuatiliwa kwa karibu na Marekani na Uingereza.
Si ajabu nilimwona Balozi wa Marekani siku ile Xi Jinping alipotoa hotuba ya mwelekeo wa sera za China kwa Afrika akiwa Dar. Naam, Wamarekani wanafuatilia.
Na ndivyo ilivyokuwa miaka ya 60 hadi 70. Mwaka 1964 ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwa uongozi wa Julius Nyerere kuliko wakati mwingine wowote. Kulikuwa na matukio makubwa yaliyomtikisa Julius Nyerere na Tanzania kama taifa changa.
Mapinduzi ya Januari 12, Zanzibar na Army Mutiny ( Uasi wa jeshi) wa Januari 20, 1964.
Wachina na WaCuba waliingia kwa kasi Zanzibar mara baada ya Mapinduzi. Hali hii iliwatisha Wamarekani. Ikaja taarifa ya kupandikizwa ya kiintelijensia. Ni katika miezi hiyo hiyo. Kwamba Marekani na Uingereza wanapanga njama za kumwangusha Karume. Nyerere akaridhia Karume amfukuze Balozi Mdogo wa Marekani kutoka Unguja.
Julius Nyerere akagundua baadae kuwa alikosea. Akaenda mwenyewe kwa Balozi wa Marekani kufafanua kilichotokea.
Kwenye telegramu ambayo Balozi wa Marekani aliituma White House na CIA Januari 1965 , Balozi huyo, Bw. Leonhart anauelezea mkutano wake na Julius kwa kusema, " Haukuwa mzuri...."
" Nyerere bekglagade djupt att han kunde inte andra sitt beslut"- ( Swedish) Kwamba Nyerere alisikitika lakini hakuwa tayari kubadili uamuzi wake ( Kumfukuza Balozi mdogo wa USA) ( Pa Vag Mot Presidenten, Ukurasa wa 196)
Mengine yaliyojiri kwenye mkutano wa Julius Nyerere na Balozi Leonhart ni vema yakabaki kwenye maandishi ya mwandishi Holmqvist na kwa lugha yake, maana, kuyaweka bayana hapa haiwezi kuwa ni kwa maslahi ya taifa letu.
Nikipata muda nitawasimulia mengine kutoka kwenye kitabu hiki.
Maggid Mjengwa,
Dar es salaam
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/ --
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment