Viwanda vinavyotengeneza nondo (reinforcing Bars) ni vya washikaji. TBS hawawagusi na hata BRU nao kimya! Nondo zinazotengenezwa Tanzania ni sawa na bisquit, haiwezi kukunjwa mara mbili bila kukatika. Utadhani sio mild steel, utadhani ni cast iron vile.
Majengo yote yanayojengwa na makampuni ya nje hayatumii nondo za bongo kwa kulijua hili na kuamua kuachana nazo. Sio kwavile uzalishaji hautoshi, la, hasha, ni ubora. Nondo zinatengenezwa tokana na mifuniko ya maji machafu, mitaro na hata wakati mwingine injini chakavu za magari! Hatupo serious!
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.
From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 30 Mar 2013 04:45:04 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] JENGO LA GHOROFA LAPOROMOKA KATIKATI YA JIJI LA DSM
Madam Kiwasila,
Nikweli tumekua tunalalamika sana juu ya ujenzi holela usio fuata sheria. Nakumbuka ile mada ya Waziiri wa Mazingira Dr. Huvisa baada ya kuamua kuzifungia zile hotel zilizokua zinatiririsha kinyesi baharini ulivyokua moto hapa jamvini, na jinsi tulivyo gusia suala la kuzingatia sheria za ujenzi, michoro na ukaguzi wa majengo kabla hayajaanza kutumia.
Nashukuru kitu kimoja, nimeona miongoni mwa watu walioenda kuangalia hili tukio la kuporomoka kwa jengo ni pamoja na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Sadiki.
Naamini wamejifunza kitu na ninamatumaini makubwa kwao kua sasa watafanya kitu; kwa maana ya kuzibana sector na idara zinazo shughulikia ujenzi.
Tofauti na hapo waheshimiwa hao wategemee kuendelea kutoa mkono wa pole kwa wahanga wa hizo ajali; maana kama unavyosema zitaongezeka huko mbeleni ni kweli.
Alexander
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, March 30, 2013 11:55 AM
Subject: Re: [wanabidii] JENGO LA GHOROFA LAPOROMOKA KATIKATI YA JIJI LA DSM
Mungu awasaidie waokolewe wale ambao bado wazima. lakini daima twalalama humu wengine kuhusu ujenzi wa sasa na mabalaa yajayo. Vyuma chakavu na uharibifu wa miundombinu na kuomba ikiwezekama kiwanda cha chuma chalavu kifungwe kukomesha uharibihu huo. Hizo nondo watengenezao zitumikazo katka ujenzi huenda ni chelema hazifai.Cement wajenzi wanakwenda kununua re-bagged cement ndio wanajengea kupunguza gharama. Na bado yataporomoka mengi na kuuwa wengi kutokana na kutokuzingatia kanuni za ujenzi. Yatakuja mengine kutitia au kutumbukia ardhini hulalamikaga daima nikichangia humu kulalama kuondoka katika zile nyumba za NHC na kujenga kisasa bila ya kuzingatia magonjwa-hewa na usalama wa wakazi. Ghorofa zimezunguka na vijumba vya chini hewa hakuna. Vighorofa uchara vinajengwa kati ya nyumba ambazo ni fupi. Mpango wa DSM wa mji 1979 hauendelezwi na kujali tu maendeleo ya sasa mtu ajenge popote aina yoyote ya nyumba atakayo kwa urefu wowote ule bila kuangalia vifaa gani tunavyo vya mima moto na uokoaji. Hii ni ghorofa 16 to jee hizo 50 hadi mia itakuwaje. pale Mwenge DSM kila mtu anaongezea kachumba juu ya kaghorofa fulani na chama cha maijinia wajenzi, Serikali ya Mtaa na halmashauri wanaona vighorofa uchwara hivyo kisha juu ofisi za watu chini watu wanakula ktk retaurant, kuna majiko ya moto na hatari nyinginezo. Wengine juu wamekodisha ukumbi wa sherehe za arusi au wana maombi. Aina ya ujenzi haihimiri uzito ibebayo. Kila ghorofa limechimba kisima kirefu na wanapampu maji wanatengeneza mifereji chini na pia kuweka vacuum apapo ardhi hushindwa kuhimili mzigo. Jengo litakatika na kutumbukia ardhini. Wanaonekana watu Mwanza wanavyojenga kando ya mawe ktk peninsula ya ziwa victoria. Wanapasua mawe, kuwasha moto na kuyatia joto na nyufa. Ipo siku ya mvua kubwa mawe yatabiringita na watu na kuwamwaga ziwani au barabarani. Kama hii ya kujenga bondeni haijatufunza wanaendelea kujenga na kuzama kupoteza mali na unawaona wakilia kuhaha matatizo ktk TV na magazeti, tunaona majumba yakiporomoka mtoni tuchimbako mchanga na hatukatazi hao vijana na wajengao maporomokoni; hatujifunzi kutokana na ujenzi wa mabilioni wa baranara ambapo inakatika kabla ya kukabidhiwa na madarasa yanakatika kabla ya kukabidhiwa- kwa nini tuwape hao wakandarasi feki nyumba. Badala yake bora kuchukua kampuni za Kigeni-Chinese, Japanese, Noremco (norwegian) Denish, Germany. kampuni isiyotaka kutumia viwango-ifutwe na ilipe gharama ya uharibifu jengo au barabara iliyopasuka kabla ya kukabidhiwa au kutumika. Fundi mjenzi budi aangalie wabongo-mafundi wadogo na vibarua ni wezi. Ukimpa dakika 2 tayari na wenzake wameondoa mfuko wa siment kuficha vichochoroni wakauze. Wanajaza michanga mingi bila ya kuwa na utu/ubinadamu na jengo linaanguka. Budi uwe na msimamizi kona zote za ujenzi na ufunge uzio kuzunguka nyumba hakuna kutoka bila kusachiwa ama sivyo watauza vifaa na kujenga mbambiko. Wanajali kupata tu na pesa zote huishia anasa na ndio maana huishi kama vibarua maisha yote licha ya kuuza cement na nondo za wizi. Hebu fikiria jengo kama hilo manzese inaangukia nyumba ndogo kadhaa usiku au hata mchana na ndani kuna watu na nyumba nyingine zina TV kuonyesha cinema za video, zina madrasa, mama ntilie na moto unawaka wanapika wakati zinaporomokewa. Tusipojipenda na kutii sheria mbalimbali za usafi, ujenzi, makazi, viwango vya mpaka nondo na cement-tutaendelea kijiuua wenyewe daina na uwezo wa kujiokoa ni mdogo. --- On Sat, 30/3/13, nevilletz@gmail.com <nevilletz@gmail.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment