Friday, 29 March 2013

[wanabidii] ' Njiani Kwenda Kwa Rais!'-4

Maggid, nausubiria kwa hamu huo 'mshindo mkuu' ambao Neema Kambona bado hajafanikiwa kuufikisha kwa hadhira japo amekuwa na nia hiyo. Leo nimekutana na huyu mtafiti anayeandika wasifu wa Kambona, naye pia anajaribu kuuvunja huo 'ukimya mkuu': "Oscar Kambona: A Life in Nationalism and Exile" - James Brennan cf. http://www.thecitizen.co.tz/magazines/32-political-platform/11461-1964-army-mutineers-were-inspired-by-the-zanzibar-revolution.html


From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Saturday, March 30, 2013 1:21 AM
Subject: [wanabidii] ' Njiani Kwenda Kwa Rais!'-4

' Njiani Kwenda Kwa Rais!'- 4

Ndugu zangu,

Jana niliandika, kuwa ili  tufahamu zaidi urafiki uliokuwepo wa watatu hawa; Julius, Oscar na Rashid  ni vema tufahamu jinsi walivyokutana;

Nyerere alikutana na Oscar Kambona  wakati Kambona alipokuwa shuleni Tabora mwishoni mwa miaka ya 40. Inasemwa, kuwa Nyerere alimtangulia kiumri  Oscar kwa kupishana miaka mitatu tu. Kule Tabora Nyerere  alikutana pia na Rashid Kawawa, naye alimzidi kiumri kwa miaka mitatu hivi.

Hivyo basi, twaweza kusema, kuwa urafiki wa Julius, Oscar na Rashid ulianzia Tabora, na harakati zao za pamoja za mapambano ya kisiasa zilianzia huko huko Tabora. Endelea....

Julius Nyerere alikuwa Mkatoliki na hodari sana shuleni. Akafika mpaka Uingereza kimasomo. Aliporudi akafanya kazi ya ualimu pale Pugu. Alipoambiwa achague kati ya ualimu na siasa, Julius akachagua siasa.

Oscar naye alikuwa mwumini wa kanisa la Anglican na hodari sana shuleni. Naye akafika mpaka Uingereza kusomea sheria. Hakumaliza masomo yake, .... Soma zaidi..http://mjengwablog.co.tz/siasa/item/1910-njiani-kwenda-kwa-rais-4.html#.UVZ1uTdafx0
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment