Nimependa hii
achievement based progression, lkn kwa hali ilivyo sasa hivi mtoto anaweza kukaririshwa miaka hata mitatu bado hajajua K 3
2013/3/30 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Joseph J.Mungai MB (mstf)--
P.O.BOX 34 Mafinga
S: 0753 192999
BP: jjmungai@tatepa.com
BARUA YA WAZI KWA TUME YA ELIMU YA KUFELI 60% MTIHANI WA KVI 12012 ILIYOTEULIWA NA MHE WAZIRI MKUU
29/03/2013
Kumb Na. JJM/2013/ELIMU/19
Kwa Mwenyekiti
Tume ya Elimu ya Kufeli KIV
Ofisi ya Waziri Mkuu
DAR ES SALAAM
Ndugu Mwenyekiti
KUONGEZEKA WANAOFELI KIV KUTOKA 9.7% MWKA 2007 HADI 60% 2012
1.1 Nnawapongeza kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau fwa elimu kuwaletea maoni na au/ushauri.
2.0 Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya Mufindi na kuziendesha kwa mika zaidi ya 10 Sekondari 9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani (3) Itengule (4) Igowole (5) Itandula (6) Mgololo (7) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni mwaka 2000 hadi 2005.
3.0 Kabla ya kutoa ushauri naoba kuipa Tume yako ufahamu wa ukweli ufuatao:
3.1 Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio lililoibuka ghafla bali waliofeli (Divisio 0) mtihani huo waliongezeka kutoka mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa 2012:60%!!!!!
3.2 Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka 1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%, 2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi 2007 ni 10%. Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka 2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST (Basic Statics in Education, National Data) ya miaka husika.
3.3 Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne walikuwa wastani wa 10% ambayo inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008 kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge zeka kila mwaka hadi kufikia 60% ya mwaka huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada ya matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya "utafiti kudadisi sababu za ufaulu huo mbaya" na taarifa yake ipo kwenye maktaba a Wizara" na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni", lakini hadi leo haikusomwa. Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja isiyo ya siri ya ndani ya wizara ya Elimu.
4.0 Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo yanaweza kusomwa katika maandiko mawili ya Wizara ya Elimu yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi 2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa maboresho hayo uzito wa kisheria yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla ya wakati wake. Maboresho yamewekwa kando moja baada ya jingine au hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi ilivyokuwa kabla ya mwaka 2000.
USHAURI:
5.0 Kwa kuwa Elimu ni nyenzo muhimu sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na kucho cchea maendeleo ya nchi nimeamua kutonyamaza na kuwa muwazi kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa niliyestaafu. Kwa hiyo NASHAURI mambo yafuatayo:
5.1 Utaratibu sahihi wa kupanda madarasa kwa ufaulu ( achievement based progression) uliowekwa na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe bila kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza, la pili na la Tatu ambayo Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka ya kukalilisha, kama mwanafunzi hajazijua "K" 3: kusoma, kuandika na kuhesabu.
5.2 Tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya Elimu niliyoyataja akatika 4(a) na (b) hapo juu yaliyomo maboresho ya elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha kufaulu vizuri katika Elimu ya Msingi na Sekondari miaka ya 2004-2007; badala ya kutumia muda mwingi na fedha n=yingi kugundua upya gurudumu.
5.3 Taasisi ya Elimu Tanzania ( Tanzania Institute of Education –TIE) iagizwe na iachiwe kutekeleza wajibu wake wa kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.
5.4 Wanasiasa tuache kuamua bila kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.
Kutokana na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu imerudi ilikokuwa kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha kuingilia na kuamua bila kuzingatia utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo mabaya kama hayo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia " anayeficha maradhi kifo kitamuumbua"
Wasalamu
Joseph J Mungai MB mstf
MDAU WA ELIMU
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment