Tuesday 18 April 2017

[wanabidii] NMB yapata faida ya shilingi bilioni 153.7

NMB yapata faida ya shilingi bilioni 153.7 kwa mwaka 2016


[caption id="attachment_78670" align="aligncenter" width="675"]<img class="size-full wp-image-78670" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/04/Mkurugenzi-Mkuu-wa-Benki-ya-NMB-Ineke-Bussemaker-akizungumza..jpg" alt="" width="675" height="600" /> Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza.[/caption]

&nbsp;

<strong>• Ni ongezeko la asilimia 2.4 la faida
• Kwa miaka 10 mfululizo, NMB imeendelea kuongoza kwa faida nchini</strong>

<strong>BENKI</strong> ya NMB imepata ongezeko la faida la asilimia 2.4 baada ya kodi kwa mwaka 2016. Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NMB - Ineke Bussemaker amesema kwamba licha ya changamoto zilizoikabili sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla kwa mwaka 2016, benki ya NMB iliweza kufanya vizuri.

"Faida ya benki kwa ujumla iliongezeka kutoka shilling billioni 150.3 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 153.7 kwa mwaka 2016. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa pato linalotokana na Biashara ya benki lililokuwa kwa asilimia 16," alisema Bussemaker.

Riba katika mikopo ilikua kutoka shilingi bilioni 438.7 kwa mwaka 2015 hadi billioni 551.0 mwaka 2016 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 25.6. Pia Rasilimali za benki ziliongezeka kwa asilimia 8 kutoka shilingi bilioni 4,580 kwa mwaka 2015 hadi shilingi Bilioni 4,951 mwaka 2016.
Mikopo kwa wateja iliongezeka hadi shilingi 2,794 billioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13% kutoka shilingi bilioni 2,482 kwa mwaka uliotangulia.
Ongezeko hili la mikopo ilitokana kwa kiasi kikubwa na ongezeko la mikopo kwa wafanyakazi kwa asilimia 16 kwa mwaka 2015 hadi kufikia shillingi bilioni 1,698 kwa mwaka 2016.

Pamoja na ukata wa fedha uliozikumba benki nyingi mwaka 2016, ongezeko la amana za benki lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la amana za wateja kwa shilingi bilioni 172 billioni, fedha ambayo benki ilikopa kiasi cha shilingi bilioni 312 pamoja na hati fungani ambayo ilipatikana kiasi cha shilingi bilioni 41.

Gharama za riba ziliongezeka kwa asilimia 49 kutoka shilingi bilioni 68.5 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 102.2 kwa mwaka 2016.
"Amana za wateja ambazo kwa kiasi kikubwa ziliwekwa katika akaunti zisizokuwa na riba ziliongezeka kwa asilimia 4.8% kutoka shilingi bilioni 3, 568 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 3,737 kwa mwaka 2016," alisema.

Aliongeza, "Idadi ya wateja wetu iliathiriwa sana na hali ya kibiashara kwa mwaka 2016, hali ambayo iliathiri ubora wa mikopo na kuchangia ongezeko la mikopo mibovu (NPL) hadi asilimia 4.8 kwa mwaka 2016 kutoka asilimia 2.4 mwaka 2015,"

Ikishikilia asilimia 20% ya soko kwa mikopo na amana za wateja, benki ya NMB ni ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa mizania ya Rasilimali za kibenki nchini, kwa miaka 10 mfulululizo benki imekuwa ikiongoza kwa kupata faida kubwa kuliko benki zote nchini.


___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment