Saturday 15 April 2017

Re: [wanabidii] NAPE: Kijana Anayepitwa na wakati kirahisi hivi?

Kaka Muhingo

Bado upo. Pole sana.

Walewale.


On Apr 11, 2017 1:09 PM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paulo Makonda alipofanya ziara yenye utata kituo cha matangazo cha Clouds,  aliyekuwa waziri wa wizara husika Nape Nnauye alifanya makosa matatu kwa kupitia matamshi aliyoyatoa kulaani kitendo hicho.
1) Kama kiongozi wa serikali alipaswa kutamka kwa tahadhali katika kuongelea kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam kwa kuzingatia kuwa Makonda ni Mkuu wa Mkoa. Alipaswa kujihoji kama haiwezekani kuwa kitendo haramu cha Makonda kinaweza kuwa na manufaa Fulani kwa serikali anayoitumika.
2) Kosa la pili ni kumhukumu Makonda halafu kuunda tume. Ilibidi atangulie kuunda tume ya kusikiliza pande zote kabla ya kuonyesha msimamo wake; au amlaani Makonda na aachie pale bila kuunda tume ya uchunguzi.
3) Kwa kuzingatia kuwa Mkuu wa Mkoa anawajibika kwa waziri wa TAMISEMI, Nape angekuwa ametumia busara kuwasiliana na wizara husika ili washauriane na kushirikiana kumchunguza Makonda.
Baada ya makosa hayo mwandishi mmoja alitoa makala iliyosema "Ningekuwa rais Nape angesikia mrithi wake radioni". Ndivyo ilivyotokea.

Baada ya hapo Nape alifanya kosa jingine la msingi. Aliongea kwenye vyombo vya habari. Alifanya hivyo siku aliposikia kuwa sasa si waziri tena. Hizi ni tabia za ajabu. Haiwezekani zikawa za ajabu Nape asiwe mtu wa ajabu. Ukiiangalia tabia ya Nape unaweza kudhani nafasi pekee inayomfaa ni kuwa Rais. Chini ya hapo atakuwa anatumiwa na kutimuliwa.
Sasa amekwenda jimboni kwake. Kafanya mikutano kadhaa. Mmoja akina mama walilala chini wakitaka atembee migongoni kwao. Wanampongeza. Ni shujaa. Sijui kwa kufanya nini? Nape kama mhamasishaji (Kama alivyokuwa Moses Nnauye) siwezi kushangaa mbwembwe hizo. Ila siwezi kupinga mtu akisema viliandaliwa viwe hivyo. Nimesoma maelezo fulani yakimnukuu Nape Nnauye katika moja ya mikutano yake. Anasema yeye ndiye alimuweka Magufuli madarakani. Kama ni kweli kasema sijui ina maana gani? Nakumbuka Rais Magufuli kuwahoji wafanya biashara kama kuna aliyemchangia japo shilingi aseme. Sijui kama Nape anataka kutwambia Rais angebadilisha kauli asiseme hela Nape angekuwa mmoja wao kunyosha mkono! Lakini tunajua wakati Nape akiwa Katibu wa CCM idara ya uenezi alifanya kazi kubwa iliyomletea ushindi Rais Magufuli katika kampeni za uchaguzi 2015. Watu wengi walifanya hivyo. Nami nikieleza nilichofanya kuna watakaoshangaa. Wote hao hakuna anayestahili kujiona ni yeye alileta ushindi labda awe wa ajabu. Wote walichangia ushindi huo.
Nakumbuka wakati  Nape, Adulrahman Kinana na Mzee Philip Mangula wanaitwa kuiongoza CCM, ilikuwa hoi na walikuja kujaribu kuifufua na kwa kweli walifanikiwa. Walifanikisha angalau katika mikutano yao (Hasa Mzee Kinana) kuongea lugha iliyokuwa ikitumiwa na wapinzani. Hii ilirudisha moyo wa watanzania wakaamini CCM inaweza kufufuka. Kinana anafahamika misimamo yake. Hata angebadilika hawezi kuupoteza kabisa uNyerere. Nawapongeza sana. Na Nape nampongeza pamoja na hao.
Kipindi hicho CCM ilikumbatia watu fulani. Badala ya kumilikiwa na wanyonge ikawakumbatia matajiri na wanasiasa wengine waliojiona wao ni muhimu. Hata nyimbo kama "CCM ina wenyewe" ziliimbwa na kutafsiriwa 'vile'.
Sasa CCM inafanya mabadiliko. Haitarajiwi siku za usoni kumuona mtu mmoja kuwa muhimu kuliko wengine. Inatarajiwa timu ikifanya kazi mafanikio yanakuwa yao wote. Kumkuta kiongozi leo hii anasema "mimi nilifanya hivi na vile" ni dalili ya kuelekea kupitwa na wakati na kutoiona CCM inakwenda wapi ili kwenda nayo. Hii ni hatari hasa kwa mtu anayeelekea kuamini kuwa siku moja 'atakumbukwa'. Anashindwa kuwaelewa watakaomkumbuka ni watu wa namna gani na kuwashawishi kwa mwenendo wake ili wamkumbuke kweli. Nape anapitwa na hilo bila kuliona. Inaposemwa CCM inafanya mabadiliko, inasemwa wakati Nape bado ni kiongozi wa CCM, na anaelekea kutoona mabadiliko na anaendelea ku-behave kiCCM ya zamani, anaelekea kupitwa na inaweza kuleteleza kutupwa.

La pili linaloonyesha kuwa anaelekea kupitwa na wakati ni kusema " Kama rais hatachukua hatua kuhusiana na watu kutekwa basi 2020 anaweza kupoteza kura". Sitegemei mtu yeyote anayejua sheria na uendeshaji wa nchi aunganishe jinai hiyo na siasa za uchaguzi. Hili ni kosa la kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja. Sasa yeye anasema mpaka 2020 wakati wa uchaguzi? Yaani kama si uchaguzi basi watu waachwe watekwe tu! Lakini jambo la ajabu katika matamshi haya ni kuwa utekaji huu sio kwanza unatokea hapa Tanzania. Dr. Ulimboka akiwa katikati ya kutetea maslahi ya Madaktari alitekwa na kusulubiwa na akatupwa na watekaji mahala atakapookotwa. Kiongozi wa CUF alipozolewa pale Posta na akapotea kwa siku kadhaa na kuja kuonekana mitaani baada ya siku. Dr. Mvungi akiwa kiongozi muhimu wa Tume ya katiba alivamiwa na kuumizwa vibaya sana na akafia Afrika ya Kusini. Kipindi hicho Nape alikuwa Mkuu wa idara ya uenezi ya CCM. Sikuwahi kumsikia akisema haya anayoyasema sasa baada ya matukio mawili ya utekani. Alinyamaza sheria "ichukue mkondo wake" (kama iliuchukua). Maneno haya kwa nini hakuyasema Dr. Ulimboka alipotekwa? Iweje anayasema leo wakati ametimuliwa kazi. Nape (Kwa kumbu kumbu zangu) ni kiongozi wa kwanza kutimuliwa kazi na akaitisha press conference siku hiyo hiyo. Kama angekuwa anasikiliza ushauri basi angezingatia ushauri huu: AKAE KIMYA. Mambo yatajipa huko mbele kama yalivyojipoa kwa wengine. Mwinyi anayemtolea mfano hakusikia baada ya kujiuzuru akiongea. Nape anasahau kuwa silent listeners ndio watakaoichagua CCM iliyobadilika na Magufuli wake aliyeibadilisha au mteule mwingine. Anafikiri wanaofikiwa na habari za kutekwa na kuyapa uzito wa kelele za siasa ni wengi sana mitandaoni na ndio wapiga kura pekee. Lakini ni wachache sana kwa ujumla wake. Bila kupiga hesabu hapo ataendelea kujihangaisha na anachoonekana kutafuta atakikosa kama watangulizi wake.
Ninaamini kama alikuwa mshauri wa busara kwa nafasi aliyonayo ya uanachama wa CCM ushauri wake asingeutoa mitandaoni na hadharani kama wapinzani wa kisiasa. Kuna aliyefikiri kuwa kelele za Nape zilihesabiwa kumsaidia 'kuandaa atakapofikia' (akitimuliwa (maana alijua)). Kama ni hivyo aendelee maana ameishafika.
Elisa Muhingo
0767 187 507
elisamuhingo@yahoo.com
  
     
              --
          
             
          
        
              Send Emails to
 wana...@googlegroups.com
          
             
          
        
               
          
             
          
          
            Kujiondoa Tuma
 Email kwenda
          
             
          
          
            wanabidii+...@
 googlegroups.com 
          
        
             Utapata Email ya
          
        
              kudhibitisha
 ukishatuma
          
             
          
        
               
          
             
          
          
            Disclaimer:
          
             
        
          
              Everyone
         posting to this Forum
 bears
           the sole
          
             responsibility
          
              for any legal
         consequences of his or
           her postings,
          
            and
          
        
             hence
          
              statements and
 facts must be
         presented
           responsibly.
          
        
            Your
          
              continued
 membership signifies that
           you agree to
          
            this
          
              disclaimer and
 pledge to abide by
         our
           Rules and
          
             Guidelines.
          
             
          
          
            ---
          
             
          
              You received
 this
         message because you
           are subscribed
          
            to
          
        
             the
          
              Google Groups
 "Wanabidii"
           group.
          
             
          
          
            To unsubscribe
 from this group and
          
         stop receiving
          
          
          emails
          
              from
         it, send an email to
 wanabidii+...@
          
         googlegroups.com.
          
          
           
          
              For more
         options, visit
          
             https://groups.google.com/d/
           optout.
          
             
          
          
        
          
          
          
        
           --
          
           Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
          
            
          
        
           Kujiondoa Tuma Email
 kwenda
          
           wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
          Utapata Email ya
          
         kudhibitisha
 ukishatuma
          
            
          
          
         Disclaimer:
          
           Everyone
         posting to this Forum
 bears the sole
        
         responsibility
           for any legal
 consequences
         of his or her postings,
 and
          hence
           statements and facts
 must be presented
         responsibly. Your
           continued
 membership
         signifies that you
 agree to this
          
         disclaimer and pledge
 to abide by our Rules
   and
           Guidelines.
          
           ---
          
          
         You received this
 message because you are
     subscribed
       to
          the
           Google Groups
         "Wanabidii" group.
          
           To unsubscribe from
 this group and stop
         receiving emails
           from it, send an
 email
         to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
          
           For more options,
         visit
        
        
 https://groups.google.com/d/optout.
          
        
           
        
      
       --
       Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
      
       Kujiondoa Tuma Email
 kwenda
       wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
       Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma
      
       Disclaimer:
       Everyone posting to this
 Forum bears the sole
      responsibility
       for any legal consequences
 of his or her
   postings,
     and
      hence
       statements and facts must
 be presented
   responsibly.
     Your
       continued membership
 signifies that you agree to
     this
       disclaimer and pledge to
 abide by our Rules and
      Guidelines.
       ---
       You received this message
 because you are
   subscribed
     to
      the
       Google Groups "Wanabidii"
 group.
       To unsubscribe from this
 group and stop receiving
     emails
       from it, send an email to
 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
       For more options, visit
      
 https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment