Unalindaje KURA wakati kuna Mawakala ambao wanacheki jina la kila anayeingia kupiga kura. Watu zaidi ya kumi wajae hapo na kusoma majina kila anayeingia na kutoka na kila kura iliyopigwa? Hata hivyo-kila mgombea anajiaminisha ni yeye mshindi kutokana na wananchi wadanganyika na wadanganya wafanyavyo kwa wagombea. Unamkuta mgombea ana watu 100 ktk mtutano hao 100 wanamuimbia...Rais! Raisi! Raisi!! Anakuja Lowasa wanajaa milioni 2 na Mangufuri milioni 2 na sare zao wanaimba hivyo hivyo. Anakuja Mghwila ni idadi hiyo na wanaimba Mama Raisi! mama Raisi huyoo!. Ukija kwenye Kura waliomuaminisha kuwa anapendwa na atashinda mfano Rungwer jimbo hilo anakura 100, wenzake millioni 3 hadi 5 mwingine Chief fulani anazo 30 tu. Halafu kila mmoja ana amini kuwa ameibiwa kura kwa vile walisema wanampenda waliimba Raisi Raisi!! Kwa hiyo kura za Chama chao zimeibiwa. Wakala amesaini walipohesabu-unalindaje ukiwa nje? kama mji au jimbo lina watu laki 5 na hao laki tano walivaa sare za vyama mbali mbali wakishakilia hivyo hivyo. Huoni kuwa ni changa la macho kudai umeibiwa? Ni hao hao tu vi T-shirt, hela ya mafuta na madela wanaserebura pande hii anapata hiki pande ile hiki anaweka sandukunu. Wewe umeliwa, wanampigia wamtakae au aliyeyetoa hela nyingi kwao kwa faida binafsi. Sijui kama kusingekuwa na mawakala mpambano wa kuvamia vituo na wasimamizi ungekuaje!
Kama si jeshi kupewa vifaa na kuzagaa kila kona-kweli uchaguzi wa mwaka huu ungekuwa vita vingeanzishwa na wapenda madaraka. Fikiria kura imepiwa kilometa 120 lakini wanatoka hapo kwenda kuchoma nyumba ya mgombea aliyeshinda kilometa hizo 120 mbali sana. Wengine wakifahamu kuwa kufika vijiji vya milimani huko Njombe, Morogoro si mchezo na usafiri ni miguu mpaka ufike pale pikipiki zinapoishia. Wanaona wanachelewesha kupewa matokeo nafanika kuchoma kituo cha kata, polisi na nyumba ya chama fulani-tawala. Wakati yeye hata kutembelea nduguze milimani huko mbali mpaka kuwe na kilio labda kutokana na umbali na njia mbaya. Ila wakusanya matokeo ndi wajinga labda watafute kitunga waruke nacho juu raia hawana subira kusubiri 2 days. Na wanapochoma ofisi ya Kata, kituo cha polisi-wanachoma mafaili ya ndugu zao, jirani zao kama si yao wenye kesi mbalimbali na vidhibiti humo. Huu si ukichaa chini ya kisingizio cha haki ya binadamu ya Kura?
Ukiangalia police wa Marekani au UK na vivalo vyao-huwezi kuamini na utawaona wanavyotwangana na wananchi wanaoandamana na kuvunja sheria wengine kuvunja maduka na kupora. Police wanapigwa, wanauawa nao kuvunja watu na kuua. Ila polisi wa TZ wawaache wananchi wafanye watakavyo, kuvunja sheria under the mwamvuli wa demokrasia? Mbona huko demokrasia ilikoiva makari ya washawasha yanatumika na ndio wao wanatengeneza, wanatumia na wanatuuzia? Na kisha pamoja na kuwa na demokrasia kuna Camera barabara zote, kwenye majumba ya biashara na ya serikali, bank, mataa ya barabarani, nyumba za kuishi mwenye uwezo na vyuoni. Likitokea la kutokea ni police kukusanya vifaa vya camera tukio nilipotokea na kuwafuatilia wahusika. Sisi hapa watu watarusha mitandaoni tukio la kumchoma mtu moto, mwanamke kupigwa uchi au watu wamefumaniwa wanatembezwa bila nguo na watu kuwarushia mawe-hakuna linalofanyika kuwakamata wale na yule mume aliyemtembeza mke uchi na kumweka ndani, kumshitaki, kumwadhibu. Hata NGO huoni zikaandamana kuwa yume mtembeza mfumaniwa wake (me) na mkewe akamatwe na kumfuatilia mpaka ofisini/nyumbani kwake. Hapa demokrasia ipo ila ya Kura tu na mawakala wamesaini-HAIPO. Excuse me! Kuna lililotakiwa litokee la machafuko kama kisingizio lakini halikuwezekana kwa kiwango kilichotakiwa. MTAJI UMEINGIA NUKSI, KIKWETE ALIJIANDAA ILA KWA MANUFAA YETU WOTE. Tunapo pa kukimbilia? Mifano nchi za wenzetu hatuioni? Kura zimepita-tujenge nchi kwa upendo na Amani. Mtaji wa Vurugu ilele ulaji utarudi tena 2020.
--------------------------------------------
On Tue, 10/11/15, 'dani killo' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] KIKWETE KAULI HATARI UCHAGUZI
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "Wanazuoni - Informal Network of Tanzanian Intellectuals" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Tuesday, 10 November, 2015, 9:42
Hii
ndo nchi ya demokrasia? nina
makengeza God created men in LOVE ,let us live with
LOVE
On Saturday, October
17, 2015 4:50 PM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Ni haki kwa watanzania
kubaki vituoni kusubiri matokeo. Lengo ni kujua matokeo na
kujua kiongozi wako ngazi fulani na kujua mwelekeo wa
kiongozi ambaye kura zake zinahitaji jumba toka sehemu
nyingine.
Huko nyuma tumeshuhudia hayo. mara
kadha nimekuwa nawapigia vijana wangu waliolala vituoni
kutaka kujua nani kashinda.
Siku hizo
makundi yote yalisimama na kusubiri matokeo. Aliposhinda wa
chama fulani wote na wa chama kingine waliungana
kushngilia.
Mwaka huu ni tofauti.
Kuna vyama vimetamka wazi kuwa hsi kwamba
wanaenda kusubiri matokeo bali wanakwenda kulinda kura.
Wanasema kama matokeo yataonesha chama chao kimeshindwa basi
kura zao zimeibiwa. Hapa ndio Rais anasema hakuna kulinda
kura. Maana yake kuna chama kikitangazwa kushindwa wakati
wananchama walioshinda wamesimama pembeni basi hapo ngumi na
mateke vinaanza. Wote tunajua kuwa rais anaendesha nchi kwa
vyombo vya dola. Ni uelewa gani tena kuwa rais anatishiwa
kushitakiwa ICC kwa sababu ya kutumia vyombo vyake vya dola.
Kuna kila dalili kuwa kuna watanzania hawathamini tena nchi
yao; uongozi wa nchi kwa kudhani kuwa watakwenda kulalamika
ICC. WATU HAO WAMECHELEWA. hakuna kugombana. Hakuna
kupigana. Wala hakuna kwenda ICC. Kama mtu anafikiri
atawapiga mawe Polisi na wasifanywe lolote. HUU NAO NI
UPUMBAVU MPYA.
--------------------------------------------
On Fri, 10/16/15, 'ananilea nkya' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject:
[wanabidii] KIKWETE KAULI HATARI UCHAGUZI
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com,
"WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "Wanazuoni - Informal Network of
Tanzanian Intellectuals" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Friday, October 16, 2015, 11:42 AM
RAIS KIKWETE WANANCHI
KULINDA KURA
UTAEPUKA KUSHTAKIWA
Na Ananilea Nkya
Uchaguzi mkuu utakaofanyika
Jumapili tarehe 25 Oktoba mwaka
huu 2015
huenda vyombo vya dola vikatumika kifisadi kupora
mamlaka ya wananchi kuchagua kiongozi
wanayemtaka katika ngazi ya Urais, ubunge na
udiwani.
Hii ni kwa
sababu Rais Kikwete siku
alipozima
mwenge wa Uhuru huko Dodoma alitoa kauli
hatari kwamba vyombo vya dola
vitawashughulikia wananchi ambao watakuwa wako karibu na
vituo vya kura kulinda kura zao na
kushuhudia
kuwa atakayeshinda atakuwa
ameshinda kihalali na
siyo kwa 'goli la
mkono' (wizi).
Kinachoshangaza Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa
kauli hii huku akijua wazi kuwa sheria
ya
uchaguzi inawaruhusu wananchi kukaa
mita 200 kutoka
kituo cha kupigia kura kwa
lengo la kushuhudia upigaji
kura,
kuhesabu kura na kutanga matokeo.
Vyama vya upinzani vikiwepo vinavyounda
Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA)
–CHADEMA, CUF, NCCR-
Mageuzi na NLD
ambavyo vimeamua
kusimamisha mgombea
mmoja mmoja kwenye nafasi ya urais,
ubunge
na udiwani vimekuwa
vikiwahimiza
wananchi kulinda kura.
Kufuatia kauli hiyo ya Rais Kikwete wananchi
wanauliza: Rais ambaye anapaswa kuwa mlinzi
namba moja
wa sheria za nchi inakuwaje
ametoa kauli inayoashiria kuwa
anakusudia kuvunja sheria ya uchaguzi?
Wananchi wanauliza swali hili kwa sababu
Rais
kutumia vyombo vya umma
vinavyopaswa
kulinda usalama wa
wananchi kama
vile jeshi la polisi
au
jeshi la wananchi kunyanyasa
wananchi
siku ya kupiga kura kinyume na
sheria ya
uchaguzi ni sawa na
kufanya ufisadi katika
mchakato
wa kupata viongozi wa nchi.
Kufanya ufisadi huo siyo tu
ni kuvuruga amani na demokrasia ya
uchaguzi unaohusisha vyama vingi vya
siasa bali pia ni kukwamisha
juhudi za kukomesha umaskini unaowatafuna
wananchi wengi
kutokana ambao chanzo
chake ni ufisadi.
Rais
Kikwete kutumia vibaya nguvu ya
kimamlaka aliyopewa na
umma kwa
kuagiza vyombo
vya
dola kunyima wananchi kulinda
kura
zao ni kutaka viongozi
wan chi yetu wapatikane kwa njia za ufisadi na
wizi wa kura
na hivyo wakiingia
madarakani wataendelea
ufisadi huo huo
katika chaguzi zijazo.
Hii ni hatari kubwa kwa taifa kwa sababu madhara yake
ni makubwa kwa maendeleo ya nchi
yetu kudumu kwa amani ya kweli
inayotokana
na haki kutendeka kwenye
uchaguzi.
Ndiyo sababu
wananchi wanauliza lengo
la Rais
Kikwete lilikuwa ni nini kutaka
kuvunja sheria ya uchaguzi kama siyo anafanya
hivyo kuandaa mazingira ya kutekeleza
azma
ya chama chake ---Chama cha
Mapinduzi
(CCM) kutumia 'goli la
mkono' kupata ushindi
kwa gharama
yoyote kama wanavyozungumza kwenye majukwaa ya
kampeni?
Maswali haya ya wananchi yanatokana na ukweli
kwamba kauli ya Rais
Kikwete kuzuia wananchi kuwa karibu na
vituo vya kupiga kura kinyume na sheria ya
uchaguzi ilianza kutolewa kwa
msisitizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya
Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Damian
Lubuva.
Lubuva
alinukuliwa akihoji: "Tume inashangaa kwa
nini vyama vinang'ang'ania kubaki katika
vituo vya
kupigia kura''.
Kadhalika, jambo
linaloshangaza wananchi ni
kwamba hata
Msajili wa vyama vya siasa ,
Jaji Francis
Mutungi naye ameunga mkono uvunjaji huo wa
sheria ya uchaguzi kwa sababu badala ya
kumshauri Rais kufuta kauli yake hiyo , ameuunga
mkono.
Jaji
Mutungu amenukuliwa akisema ''ni kweli sheria
imeruhusu wananchi kubaki katika kituo cha
kupiga kura kwa
umbali wa mita 200, lakini
sheria hiyo ina upungufu ambao
wameuona
ndio maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa
kauli hiyo ya kuwezesha uchaguzi kufanyika
katika mazingira
ya amani''
Wananchi wanauliza kama
sheria ya uchaguzi
ilikuwa na mapungufu
ni kwa nini serikali haikuipeleka
Bungeni
iweze kufanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi
wakati uchaguzi halikuwa jambo
ghafla?
Kadhalika
wananchi wanauliza: Rais Kikwete
pamoja
na Jaji Lubuva na Jaji Mutungi wamepatwa na
nini gafla kiasi kwamba wameamua
kushabikia uvunjifu wa Katiba ya nchi na
sheria ya
uchaguzi kunakoweka rehani
amani, usalama na
heshima kubwa ambayo
Tanzania imejijengea mbele ya mataifa?
Pengine kinachowafanya wananchi kuamini
kuwa
huenda Rais
Kikwete na na CCM yake wanakusudia
kutumia 'goli la mkono' kupata viongozi wa
nchi yetu kwa kutumia ufisadi wa kura ni
kwamba
Jaji Lubuva na Jaji Mutungi
wote ni
mwanasheria waliobobea na
kwa nyadhifa
zao wanapaswa kuitiii
Jamhuri ya Muungano
kama walivyoapa
siku walipoteuliwa kushika
nyadhifa hizo
na siyo vinginevyo.
Kutii Jamhuri maana yake siyo kusema ndiyo
kwa kila analosema, kuagiza au analotaka Rais
wa Jamhuri
yetu, bali ni kutumia
busara na
kuheshimu kiapo cha utii
kwa Jamhuri
kumshauri Rais kuepuka
kutoa
kauli au kupanga mambo
maovu
yanayoweza kufanya uchaguzi
kultumbukiza nchi yetu
kwenye machafuko.
Hebu jiulize ni wanawake
wangapi, watoto wangapi, wazee
wangapi na
vijana wangapi wataathirika ikitokea hii kauli
hatari ya Rais Kikwete ikitekelezwa na nchi
yetu ikakumbwa
na machafuko kwenye uchaguzi
mwaka huu?
Rais Kikwete
ajue kwamba kwa kauli alioyoitoa kama
atatekeleza hiyo azma yake ni lazima katika uchaguzi wa
mwaka huu kutokee umwagaji mkubwa wa damu kwa
sababu kauli
yake imewafanya wananchi
kuamini kuwa haki yao ya
kulinda kura
inapokonywa na Rais kwa kuamua kuivunja sheria
ya uchaguzi.
Muhimu, wananchi hasa katika wakati
huu
nchi inaelekea kwenye siku ya
uchaguzi mkuu tarehe
25,
wanategemea Jaji Lubuva kuonyesha
hekima, busara na ujasiri wa hali ya kuu kuhakikisha NEC
inasimamia na kutenda ili wananchi
waridhike kwa dhati kabisa kwamba haki
imetendeka kwenye
uchaguzi maana bila haki
kutendeka hakuna amani ya kweli nay
a
kudumu Tanzania.
Aidha wananchi wanatarajia pia kuwa
wadau wakubwa wa amani vikiwepo vyombo vya habari na
hususan wahariri , viongozi wa dini zote,
wakuu
wa vyombo vya usalama hususana
jeshi la polisi
na jeshi la wananchi,
viongozi wa vyama vya siasa,
mashirika ya
kiraia NGOs mfano TAMWA, TGNP na LHRC
wasomi, wahanahakati na kila mtu mwenye nia njema na
Tanzania anachukua hatua bila
woga kumtahadharisha Rais Kikwete
kwamba kuvunja sheria ya uchaguzi kwa
kuwazuia
wananchi kulinda kura zao ni
ufisadi mbaya
utakaoigharimu nchi yetu
.
Bila kumtaadharisha
Rais Kikwete, ikitokea
vyombo vya dola
vikapambana na wananchi walioamua kutumia
haki yao ya kisheria kulinda kura, Jaji
Lubuva na Mutungi hawatakwepa mkono wa
sheria za
kimataifa kwa kushiriki
jinai
ya kufisadi uchaguzi wa mwaka
huu
kwa kuamua kuwasaidia
watawala wa
CCM wanaotaka chama chao
kung'ang'ania madaraka
kwa gharama
yoyote hata kama kitakuwa
kimekataliwa
na wananchi.
Tukumbuke
kuwa kauli ya kwamba CCM itashinda kwa gharama
yoyote imekuwa ikitolewa na viongozi mbali
mbali waandamizi
wa CCM akiwepo Katibu Mkuu
wao, Abrahamani Kinana.
Hivi sasa baada ya Jaji Lubuva na Jaji
Mutungi kuungana na Rais Kikwete kutaka
kuvunja Katiba ya nchi yetu na
kukiuka sheria ya uchaguzi ili
kuwanyima wananchi haki ya kukaa karibu na
vituo vyao vya kura hadi mwisho kujua
hatma ya
kura yao kumewafanya wananchi
kuuliza :
Hivi Tanzania
imebinafsishwa
lini na
lini na
kugeuzwa kuwa mali
binafsi ya
Rais Kikwete na
watawala wachache wa
CCM kiasi kwamba
wanaweza kufanya lolote
na Watanzania
wengine wote hawana tena mamlaka juu ya
nchi yao?
Hivi Tanzania
imebinafsishwa kwa
hivyo hivi
sasa nchi hii ni
mali binafsi
ya Rais KIkwete na
watawala wachache wa
CCM kwa hivyo wanaweza
kufanya watakavyo
na wananchi hawana tena mamlaka juu
ya
nchi yao?
Wananchi
wanauliza kama Tanzania
haijabinafsishwa kifisadi Rais Kikwete, Jaji Lubuva na
Jaji Mutungi wanapata wapi kile
Dakta Harrison Mwakyembe alichokiita
'jeuri ya
kifisadi' ya kutaka
kuvunja sheria za
uchaguzi kuruhusu
vyombo vya dola kunyanyasa
wananchi siku
ya uchaguzi ili sauti ya umma inayotaka
mabadiliko ya uongozi isisikike kupitia sanduku huru
la kura?
Wananchi wanauliza maswali haya kwa sababu wanaona kauli
iliyotolewa na Rais Kikwete kwamba ataamuru
vyombo vya
dola kushughulikia wananchi
watakaokuwa karibu na vituo vya
kupigia
kura na kisha kauli hiyo kushabikiwa na Jaji Lubuva
na Jaji Mutungi kunaashiria wanataka
Tanzania
iingie kwenye balaa
zililozikumba
nchi kadhaa za
Afrika ikiwepo nchi
jirani ya Burundi.
Kwa Rais Kikwete kutaka
kuivunja sheria ya uchaguzi
juu ya haki
ya wananchi, tafsiri yake ni
kwamba anataka kuweka historia mbaya
ya kuingiza Tanzania kwenye machafuko kwa
kulaka kulazimisha CCM kubaki madarakani
kwa
'goli la mkono' ambalo ni
sawa ni sawa
na uhaini.
Je kwa Rais Kikwete kwa kutaka
kuvunja sheria ya uchaguzi inayoruhusu
wananchi kukaa
mita 200 kutoka kituo
cha uchaguzi anataka
kuwaambia Watanzania
kuwa tarehe 25 Oktoba
2015
amejiandaa kutumia vyombo
vya dola
kuwapora wananchi Watanzania mamlaka ya
kuamua nani awe kiongozi wao?
Kama Kikwete ndivyo anataka ni vema ajiandae
kushtakiwa
kwenye mahakama ya
Kimataifa ya makosa ya
jinai.
Akiamua kutekeleza jinai
hiyo siyo tu atakuwa
amejidhalilisha
mwenyewe na CCM yake bali pia Wanzania
wote na Tanzania ambayo inaheshimika
duniani kote kutokana na misingi ya haki na
kuheshimu wananchi kulikojengwa na muasisi
wa taifa
hili Juliua Nyerere.
Lakini zaidi itakuwa ni aibu
kwa CCM ambayo imeongoza
nchi hii
miongo mitano kuonekana kuwa
serikali
yake haikuanzisha vyama vingi kwa nia
ya dhali kuleta ushindani wa kisiasa kukomesha umaskini
unaotafuna mamilioni ya Watanzania.
Hii ni kwa sababu Rais
wa serikali ya CCM kujaribu
kuvunja
sheria ya uchaguzi kulazimisha
CCM
kubaki madarakani ni kukataa mfumo wa vyama vingi
usifanye kazi kuondoa umaskini.
Huku ni kukataa mabadiliko
wakati mmoja wa
waasisi mashuhuri wa
CCM, Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru
ambaye ameamua kuondoka CCM kwa
tuhuma za
kukiukwa kwa Kanuni na Katiba ya chama hicho
wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais,
amekiri
hatadhani kuwa chama hicho sasa
kimechoka, kimekosa
pumzi, uchumi wa
nchi umekwama, kinakodisha
mavuvuzela
kutukana watu , hivyo madadiliko ni
lazima mwaka huu 2015.
Lakini zaidi Rais Kikwete asipoacha kutekeleza kauli
yake atakuwa ameuthibitishia
ulimwengu
kwamba Tanzania ni miongoni
mwa nchi
ambazo wanazuoni Daron
Acemoglu and James Robinson
kwenye kitabu
chao ''Why Nations Fail ''
wanadai kwamba chanzo kundi
kubwa la
wananchi kubaki maskini na kikundi kidogo cha
watawala kujajirika kufuru ni chama
kinapokuwa
madarakani serikali kukataa
mabadiliko ya
uongozi hivyo kutumia
vibaya vyombo
vya dola kung'ang'ania
madaraka.
Hii itakuwa
ni aibu kwa CCM iliyoongoza Tanzania
miongo mitano kuonekana kuwa serikali yake
haikuanzisha vyama vingi vya siasa
kwa nia ya dhati ya kuleta ushindani wa
kisiasa
kukomesha umaskini unaotafuna
mamilioni ya Watanzania.
Mungu ibariki
Tanzania.
Note:
Nimeridhia yeyote anayetaka kuchapisha au kusambaza
andiko hili afanye hivyo. Tuwasiliane: ananilea_nkya@yahoo.com
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed to the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment