Kwa elimu yake na weledi wake sidhani kama amekurupuka, nimuulize happy kuwania uspika lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa?
On Nov 14, 2015 8:50 PM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Naweza kukitafsiri kitendo hicho kuwa huyu sio mwanaCCM bali katumwa na maadui wa CCM kufanya hiv yo. Kama haitoshi naweza kutoa maelezo lakini nadhani nimeeleweka.
> --------------------------------------------
> On Sat, 11/14/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] DK.TULIA ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
> To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Saturday, November 14, 2015, 6:28 PM
>
>
>
>
>
> DK.TULIA
> ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA
> SERIKALI
>
> Na
> Happiness Katabazi
> NAIBU
> Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Dk.Tulia Ackson Novemba
> 11 Mwaka huu, amechukua fomu ya Kugombea nafasi ya Spika
> kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
> Ieleweke
> kwamba Cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ni Cheo
> Che kiutendaji na hivyo anayeshikilia Cheo hicho ni mtumishi
> wa Umma kwa maana Kuwa ni Wakili wa Serikali ambaye Sheria
> ya Utumishi wa Umma ha imruhusu Kuwa mwanasiasa wala
> kujiunga na vyama vya Vya siasa.
> Lakini
> Dk.Tulia amejidhihirisha wazi Kuwa licha ni mtumishi wa umma
> mwenye Cheo cha juu serikali ni mwanasiasa wa CCM. Na
> Watendaji wa idara za Utoaji wa Haki kama Wanasheria wa
> serikali, Mahakimu na Majaji hawapaswi Kuwa wanasiasa wala
> kujiunga na vyama Vya siasa kwa Sababu ya kukwepa kukosa
> kuaminiwa na umma Kuwa hawawezi Kutenda haki
> .
> Naibu
> Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.Tulia alipoenda kuchukua
> fomu ya Uspika mapema wiki hii ametudhihirishia yeye ni
> mwanasiasa na wakati huo huo ni mtumishi wa umma .
> Ni
> wazi hafai kuendelea kushika Cheo hicho endapo akikosa
> Uspika kwasababu Tayari Utendaji wake umeanza kutiliwa
> Mashaka Kuwa hawezi Kutenda Haki kwa wananchi ambao
> siyo wana CCM na ukweli ni kwamba amepoteza '
> Public Confidence'.
> Ibara
> ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
> mwaka 1977, inatoa haki kwa wananchi wake ya kuchagua,
> kuchaguliwa,au kuteuliwa kushiriki katika shughuli za
> utawala".
> Hivyo Dk. Ackson ambaye ni miongoni
> mwa wagombea Nafasi ya Uspika kupitia Chama cha
> Mapinduzi(CCM) , Ana Haki hiyo ya Kikatiba ya Kugombea
> nafasi hiyo ya Uspika licha ni Mtumishi wa serikali tena
> Mwandamizi.
> Itakumbukwa
> Kuwa Septemba 9 Mwaka huu, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
> alimteua Dk, Ackson Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa
> Serikali.Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao
> anaushikiria hadi sasa alikuwa ni Mhadhiri wa Sheria wa Chuo
> Kikuu cha Dar Es Salaam.
> Dk.Ackson
> kwa sasa siyo Mbunge ila anagombea nafasi ya Spika
> kwasababu Ibara ya 84(1) ya Katiba ya nchi
> inatoa haki kwa mwananchi kugombea nafasi hiyo ya uspika
> hata kama siyo Mbunge na inasomeka hivi ;
> "
> Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na
> Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye
> sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na
> atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje
> ya Bunge."..
> Nimelazimika
> kuandika makala hii Leo kwasababu uamuzi wa Dk.Ackson
> Kugombea nafasi ya Uspika wakati akiwa na wadhifa wa Naibu
> Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye Moja ya jukumu la
> Mwanasheria Mkuu wa serikali kuishauri serikali Katika
> masuala yote ya Sheria.
> Kwanza
> napenda kumpongeza Dk.Ackson kwa kuteuliwa Naibu Mwanasheria
> Mkuu wa serikali mwanamke mwanamke wa kwanza Tanzania tena
> mwenye umri Mdogo .Hongera sana .
> Pili
> nampongeza kwa ujasiri wake wa kuamua kujianika hadharani
> bila kujali madaraka makubwa aliyonayo wala miiko ya Kazi
> yake ya Mwanasheria wa Serikali Kuwa yeye ni
> Mwanachama wa CCM na mwanasiasa.
> Tatu
> nampongeza Dk.Acksonkwa uwazi wake wa kuamua Kugombea
> nafasi ya Uspika ikiwa ni siku Chache tu tangu alipoteuliwa
> Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9 Mwaka
> huu. Hatari sana.
> Nne,
> Nampongeza sana Dk.Ackson kwa kuchukua fomu ya Uspika
> kwasababu ni wazi sasa umedhiirishia umma Kuwa hiyo Nafasi
> ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,haitaki na Cheo
> hicho ni kidogo sana kwake hivyo unataka Cheo kingine
> kikubwa Uspika.Yangu macho.
> Tuelezane
> ukweli ,licha Dk.Ackson Ana Haki ya Kugombea nafasi
> hiyo nanina mgombea ashinde licha kwa asilimia
> 99 hawezi kushinda nafasi ya Spika .Na ikitokea Akakosa hiyo
> nafasi umma hasa vyama Vya upinzani utamwamini tena
> Katika Utendaji wake?
> Maana
> siyo Siri Dk.Ackson alipoenda kuchukua fomu Tayari
> Yale maneno yaliyokuwa yakisemwa na wapinzani Kuwa Ofisi ya
> Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ina baadhi ya Wanasheria wa
> serikali wanatumiwa na CCM kwa maslahi ya CCM licha
> wapinzani Hao hawakuwahi kutoa vielelezo vinavyoonyesha ni
> Mwanasheria yupi wa serikali ni Mwana CCM.
> Lakini
> kupitia Mgombea Uspika ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa
> Serikali sasa wapinzani wamepata ushahidi Kuwa Naibu
> Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye ni mtumishi Mwandamizi
> wa serikali Mwana CCM na uthibitisho ni kwamba
> ametumia Kadi yake ya uaachama wa CCM kwenda Kugombea nafasi
> ya Uspika.
> Hivyo
> ni wazi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi sasa
> imebaki Ukitazamwa ndivyo sivyo kwasababu ya Naibu
> Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda Kugombea nafasi ya
> Uspika kwa tiketi ya CCM .
> Kama
> hivyo ndivyo, huyu Dk.Ackson uchaguzi wa Spika
> ukimalizika na ikatokea akashindwa hivi akirudi ofisini
> kwake wananchi tutakuwa tunamtazamaje zaidi ya kubaki na
> hisia na maswali dhidi yake Kuwa hawezi Kutenda Haki sawa
> kwa wote kwasababu Tayari ameishaonyesha yeye ni Mwanachama
> wa CCM wakati hapaswi Kuwa mwanasiasa ?
> Uchaguzi
> Mkuu umekwisha ,Kesi za kupinga Matokeo ya Ubunge lazima
> zitafunguliwa Katika baadhi ya Mahakama zetu na Kesi hizo
> mdaiwa wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbunge
> aliyeshinda na Msimamizi Wa uchaguzi.
> Enzi
> zake Mwanasheria Mkuu wa sasa George Masaju akiwa na wadhifa
> wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa akienda
> Mahakamani Mwenyewe kuiwakilisha serikali pindi
> iliposhitakiwa au serikali ilipofungua Kesi dhidi ya mtu,au
> Taasisi Fulani.
> Hata
> sasa hivi Mwanasheria Mkuu wa serikali hazuiwi kwenda
> mahakamani kuendesha baadhi ya Kesi ila kutokana na jukumu
> zito anaamua kukasimu majukumu Mawakili wa serikali na
> Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
> Na
> Mfano hai ni Oktoba Mwaka huu, Kada wa Chadema alifungua
> Kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiomba
> Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam itoe Tafsiri ya mita 200
> Katika Kesi maarufu ya mita 200 .
> Masaju
> alimtwisha jukumu hiyo Naibu wake Dk.Tulia na Wanasheria
> wengine wa serikali kwenda kutetea Kesi hiyo hiyo na
> hatimaye walishinda.
> Swali
> langu Je , itokee siku aliyekuwa mgombea Ubunge wa vyama Vya
> upinzani Kufungua Kesi ya kupinga Ubunge wa Mbunge wa CCM
> halafu Dk.Ackson aende kuitetea hiyo Kesi
> mahakamani.
> Je
> Yule mlalamikaji ambaye alikuwa mgombea toka vyama Vya
> upinzani akiiambia Mahakama Kuwa Hana Imani na
> Dk.Ackson Katika Kesi hiyo kwasababu ni Kada wa CCM na
> hivyo hatoweza kusaidia Mahakama Kutenda Haki Atakuwa
> amekosea?
> Sina
> Chuki na Dk.Ackson na sina Sababu ya Kujenga Chuki
> naye ,ila tu napenda kumweleza kijana mwenzangu Kuwa Kabla
> ya kuchukua uamuzi aliouchukua wa Kugombea Uspika
> akijitafakari kwanza yeye kwasasa ni nani?Ana wadhifa
> gani?Anafahamu Jamii itamtafsiri vipi?
> Je
> anapoenda Kugombea Uspika awe na uhakika Kuwa atashinda na
> asiposhinda basi atakuwa amejipunguzia asilimia za
> kutoaminiwa Katika suala zima za Utoaji Haki hasa Katika
> vyombo vyetu Vya Sheria hata kama Atakuwa anatenda Haki
> kweli kwasababu Tayari ameishauthibitishia umma yeye ni
> Mwanachama wa Chama Fulani.
> Hivi
> Leo hii itokee Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mgonjwa au
> amesafiri nje ya nchi au amefariki ghafla na hivyo
> kusababisha Naibu Mwanasheria wa Serikali Dk.Tulia kukaimu
> Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ,awe Bungeni anatoa
> ushauri wa kisheria ndani ya Bunge kuhusu muswaada Fulani au
> jambo Fulani ambalo wabunge wa upinzani hawalitaki hata kama
> ni kweli Dk.Tulia yupo sahihi kisheria, wale Wabunge wa
> upinzani wakiamua kumpinga kwa Kigezo yeye anatetea huo
> muswaada kwasababu pia ni Mwanachama wa CCM, at akasirika au
> sisi wananchi na viongozi wa serikali hiyo Hali
> watachukuliaje?
> Kwa
> mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya nchi inasema
> Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifa
> .
> Ibara
> hiyo haijasema Mwanasheria Mkuu wa serikali atakuwa mbunge
> wa
> Chama Fulani cha siasa.
> Ieleweke
> kwamba uteuzi wa Dk.Ackson ulizua minong'ono
> na maswali mengi chini kwa chini kutoka Katika Kada ya
> Wanasheria hasa wa serikali licha ana elimu nzuri licha tu
> hajawahi Kuwa Wakili wa serikali na Hana udhoefu wa
> uendeshaji wa Mashitaka.
> Baadhi
> ya watu wa Kada ya Sheria Walisema licha Rais anayo mamlaka
> ya Kumteua mtu yoyote kushika wadhifa wowote ,Walisema
> aikuwa busara kwa Rais Kikwete kuacha kuteua
> Mawakili wa serikali kushika Nafasi ya Naibu Mwanasheria
> Mkuu wa Serikali na kwenda kumteua Dk.Ackson ambaye
> hata miiko ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali hajaijua
> .
> Kumbe
> sasa wale waliokuwa wakipata Mashaka kuhusu Utendaji wa
> Dk.Ackson kwa upande Fulani sasa tunaweza Kusema walikuwa
> sahihi kwasababu kitendo cha Dk.Ackson Kugombea nafasi ya
> Uspika wakati yeye ni mtumishi wa umma na hapaswi Kuwa
> mwanasiasa tena katika kipindi kifupi tu ni dhahiri sasa
> miiko ya Kazi yake haifahamu na hakutaka kuifahamu
> akaamua kukurupuka na kufanya hicho alichokifanya
> ambacho kimesababisha watu kutulia mashaka utendaji
> wake.Aibu sana.
> Kuna
> taarifa zisizo rasmi Kuwa Dk.Ackson ametumwa kwa makusudi na
> kiongozi mmoja Mwanamke ambaye ni Waziri na ana nafasi kubwa
> ndani ya CCM agombee nafasi hiyo ili aende kuwaganya
> kura za baadhi ya wagombea Uspika ambao ni tisho kwa hao
> waliomtuma Dk.Ackson.
> Kwa
> Kuwa sina ushahidi na taarifa hizo Mimi nitabaki kuamini
> Dk.Ackson amegombea Uspika bila kutumwa na mtu.
> Ila
> taarifa hizo ziwe za kweli au siyo za uzushi,
> zinazidi kujengea Mashaka Utendaji wa Dk.Ackson
> kutokana na Cheo Chake na yote hayo yanampata na yatazidi
> kumpata kwasababu ameamua kuingia Kwenye siasa
> ,asingeingia huko yasingemfika.
>
> Hakuna
> ubishi Kuwa Dk.Ackson kwa kitendo chake cha kugombea
> uspika licha ana haki ya Kikatiba kugombea, amedhihirisha
> kuwa yeye ana papara ya kupata madaraka makubwa tena kwa
> vipindi vifupivifupi ili Hali bado Ana umri Mdogo.
> Ushahidi
> ni huu Septemba 9 kateuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa
> Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Novemba 11 Mwaka huu,
> kachukua fomu ya Kugombea Uspika.
> Hivi
> tukisema Dk.Ackson ameudharau,aupendi na autaki uteuzi
> Rais Kikwete wa alipomteua yeye Kuwa Naibu Mwanasheria
> Mkuu wa serikali tutakuwa Tunakosea?
> Maana
> Aiingii akilini kwa Kipindi kifupi hicho alichoteuliwa
> kushika nafasi hiyo nzito serikali halafu aamue kwenda
> kuwania nafasi ya Uspika halafu tuache kuamini kuwa
> Dk.Ackson ile nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa
> Serikali anaipenda?
> Aipendi
> na ninatabiri anaweza asidumu Katika wadhifa huo kwa muda
> mrefu kwasababu Tayari ameishaonyesha wazi Ana tamaa ya
> kupata madaraka makubwa kwa harakahara na hataki kujifunza
> Kazi kutoka Kwa waiomtangulia na akae akijua baadhi ya
> watendaji wake wa chini wamekerwa na yeye kiongozi wao
> kujiingiza Kwenye siasa wakati haruhusiwi Kuwa Mwanachama wa
> Chama cha siasa.
> Hivi
> wewe Dk.Ackson kama umegombea Uspika sasa ,nikuulize
> Je umepata muda saa ngapi ya kukaa na Mawakili wa serikali
> wakawa wana kufundisha jinsi ya kuendesha hiyo Ofisi na wewe
> ukapata uzoefu ?
> Ni
> wazi bado unaitaji kupikwa na Wanasheria wa serikali ili
> uive lakini ni wazi sasa umeonyesha hata huo muda wa
> kukaa kitako upikwe na watangulizi wako katika hiyo ofisi ya
> Mwanasheria Mkuu wa serikali huna unawaza Kugombea madaraka
> ya kisiasa.Huzuni.
> Minakushauri,
> kuliko kuendelea kushikilia nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu
> wa serikali wakati matamanio yako ni Kugombea Uspika na
> siasa, ni vyema ungeandika barua ya kujihudhuru wadhifa huo
> mapema ili Rais mpya Dk.John Magufuli ateue mtu mwingine
> ambaye kwanza ana uzoefu na kazi ya wakili wa serikali
> ambaye akili zake zimetulia,maana wewe bado hujatulia ili
> afanyekazi.
> Wewe
> Dk,Ackson tayari umeishaonekana mguu mmoja upo Ofisi
> ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mguu mwingine upo CCM
> Kugombea madaraka makubwa ya kisiasa.
> Sasa
> mtu wa aina ya Dk. Tulia ni wazi Utendaji wake katika
> madaraka aliyonayo hautakuwa mzuri maana muda mwingi atakuwa
> fikra za kupanga mikakati ya jinsi ya kupata nafasi nyingine
> kubwa zaidi ya hiyo tena kwa chap chap.
> Dk.Tulia
> unapaswa utambue jambo Moja Kuwa wanasiasa siyo watu wa
> kuaminika sana.Wakikupa ushauri wa kufanya jambo lolote hata
> hili la Kugombea Uspika ulitakiwa ulitafakari sana kwamba
> endapo ukikosa nafasi hiyo wewe hadhi yako Mbele ya Jamii
> inakuwaje.
> Umeanza
> kutiliwa Mashaka na baadhi ya Jamii,lakini waliokushauri
> ugombee Uspika hawatakusaidia kuminya fikra za watu na
> baadhi ya watendaji wako wasikuone wewe ufahai tena
> kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa
> kitendo Chako cha Kugombea Uspika kupitia CCM licha siyo
> kosa la jinai.
> Niitimishe
> kwa Kusema Kuwa Dk.Ackson endapo ukikosa nafasi ya Spika
> ,hufai kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
> kwasababu Tayari umeonyesha wewe ni mwanasiasa hivyo
> Utendaji wako unatiliwa Mashaka.
> Pia
> nakushauri acha pupa ya kuwania madaraka ili Hali wewe
> ni msomi na bado ni binti Mdogo sana licha una elimu kubwa
> lakini bado unaitaji kuelewa,kupikwa na waliokutangulia na
> wenye uzoefu Katika eneo la Mawakili wa Serikali ,siasa
> utafanikiwa.
> Au
> kama fikra na moyo wako hautaki uendelee Kuwa na Cheo
> cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,zinakutuma kwenda
> kufanya siasa ni vyema basi ukaomba Kibali cha kumuona Rais
> Magufuli ili umeombe akutoe Katika Cheo hicho au wewe
> Mwenyewe andika barua ujiudhuru kuliko kufanya hili
> uliofanya ambalo linakatazwa kabisa Kuwa Mwanasheria
> wa serikali Kuwa mwanasiasa lakini wewe mwenzetu bila woga
> tena hadharani umeonyesha wewe ni mwanasiasa wakati huo huo
> ni mtumishi wa umma.
> Dk.Ackson
> nakupenda ebu punguza kasi kidogo ya matamanio ya kupata
> madaraka inakusaidia Kwani Mtaka yote ukosa yote Waswahili
> Walisema.Nakutakia kila la kheri Katika mbiyo zako za
> Uspika.
> Mungu
> ibariki Tanzania
> Chanzo:
> Blogg: www.katabazihappy.blogspot.comFacebook:
> Happy Katabazi0716 77449414/11/2015
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment