Naweza kukitafsiri kitendo hicho kuwa huyu sio mwanaCCM bali katumwa na maadui wa CCM kufanya hiv yo. Kama haitoshi naweza kutoa maelezo lakini nadhani nimeeleweka.
--------------------------------------------
On Sat, 11/14/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] DK.TULIA ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, November 14, 2015, 6:28 PM
DK.TULIA
ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA
SERIKALI
Na
Happiness Katabazi
NAIBU
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Dk.Tulia Ackson Novemba
11 Mwaka huu, amechukua fomu ya Kugombea nafasi ya Spika
kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Ieleweke
kwamba Cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ni Cheo
Che kiutendaji na hivyo anayeshikilia Cheo hicho ni mtumishi
wa Umma kwa maana Kuwa ni Wakili wa Serikali ambaye Sheria
ya Utumishi wa Umma ha imruhusu Kuwa mwanasiasa wala
kujiunga na vyama vya Vya siasa.
Lakini
Dk.Tulia amejidhihirisha wazi Kuwa licha ni mtumishi wa umma
mwenye Cheo cha juu serikali ni mwanasiasa wa CCM. Na
Watendaji wa idara za Utoaji wa Haki kama Wanasheria wa
serikali, Mahakimu na Majaji hawapaswi Kuwa wanasiasa wala
kujiunga na vyama Vya siasa kwa Sababu ya kukwepa kukosa
kuaminiwa na umma Kuwa hawawezi Kutenda haki
.
Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.Tulia alipoenda kuchukua
fomu ya Uspika mapema wiki hii ametudhihirishia yeye ni
mwanasiasa na wakati huo huo ni mtumishi wa umma .
Ni
wazi hafai kuendelea kushika Cheo hicho endapo akikosa
Uspika kwasababu Tayari Utendaji wake umeanza kutiliwa
Mashaka Kuwa hawezi Kutenda Haki kwa wananchi ambao
siyo wana CCM na ukweli ni kwamba amepoteza '
Public Confidence'.
Ibara
ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977, inatoa haki kwa wananchi wake ya kuchagua,
kuchaguliwa,au kuteuliwa kushiriki katika shughuli za
utawala".
Hivyo Dk. Ackson ambaye ni miongoni
mwa wagombea Nafasi ya Uspika kupitia Chama cha
Mapinduzi(CCM) , Ana Haki hiyo ya Kikatiba ya Kugombea
nafasi hiyo ya Uspika licha ni Mtumishi wa serikali tena
Mwandamizi.
Itakumbukwa
Kuwa Septemba 9 Mwaka huu, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
alimteua Dk, Ackson Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao
anaushikiria hadi sasa alikuwa ni Mhadhiri wa Sheria wa Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam.
Dk.Ackson
kwa sasa siyo Mbunge ila anagombea nafasi ya Spika
kwasababu Ibara ya 84(1) ya Katiba ya nchi
inatoa haki kwa mwananchi kugombea nafasi hiyo ya uspika
hata kama siyo Mbunge na inasomeka hivi ;
"
Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na
Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye
sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na
atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje
ya Bunge."..
Nimelazimika
kuandika makala hii Leo kwasababu uamuzi wa Dk.Ackson
Kugombea nafasi ya Uspika wakati akiwa na wadhifa wa Naibu
Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye Moja ya jukumu la
Mwanasheria Mkuu wa serikali kuishauri serikali Katika
masuala yote ya Sheria.
Kwanza
napenda kumpongeza Dk.Ackson kwa kuteuliwa Naibu Mwanasheria
Mkuu wa serikali mwanamke mwanamke wa kwanza Tanzania tena
mwenye umri Mdogo .Hongera sana .
Pili
nampongeza kwa ujasiri wake wa kuamua kujianika hadharani
bila kujali madaraka makubwa aliyonayo wala miiko ya Kazi
yake ya Mwanasheria wa Serikali Kuwa yeye ni
Mwanachama wa CCM na mwanasiasa.
Tatu
nampongeza Dk.Acksonkwa uwazi wake wa kuamua Kugombea
nafasi ya Uspika ikiwa ni siku Chache tu tangu alipoteuliwa
Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9 Mwaka
huu. Hatari sana.
Nne,
Nampongeza sana Dk.Ackson kwa kuchukua fomu ya Uspika
kwasababu ni wazi sasa umedhiirishia umma Kuwa hiyo Nafasi
ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,haitaki na Cheo
hicho ni kidogo sana kwake hivyo unataka Cheo kingine
kikubwa Uspika.Yangu macho.
Tuelezane
ukweli ,licha Dk.Ackson Ana Haki ya Kugombea nafasi
hiyo nanina mgombea ashinde licha kwa asilimia
99 hawezi kushinda nafasi ya Spika .Na ikitokea Akakosa hiyo
nafasi umma hasa vyama Vya upinzani utamwamini tena
Katika Utendaji wake?
Maana
siyo Siri Dk.Ackson alipoenda kuchukua fomu Tayari
Yale maneno yaliyokuwa yakisemwa na wapinzani Kuwa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ina baadhi ya Wanasheria wa
serikali wanatumiwa na CCM kwa maslahi ya CCM licha
wapinzani Hao hawakuwahi kutoa vielelezo vinavyoonyesha ni
Mwanasheria yupi wa serikali ni Mwana CCM.
Lakini
kupitia Mgombea Uspika ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali sasa wapinzani wamepata ushahidi Kuwa Naibu
Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye ni mtumishi Mwandamizi
wa serikali Mwana CCM na uthibitisho ni kwamba
ametumia Kadi yake ya uaachama wa CCM kwenda Kugombea nafasi
ya Uspika.
Hivyo
ni wazi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi sasa
imebaki Ukitazamwa ndivyo sivyo kwasababu ya Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda Kugombea nafasi ya
Uspika kwa tiketi ya CCM .
Kama
hivyo ndivyo, huyu Dk.Ackson uchaguzi wa Spika
ukimalizika na ikatokea akashindwa hivi akirudi ofisini
kwake wananchi tutakuwa tunamtazamaje zaidi ya kubaki na
hisia na maswali dhidi yake Kuwa hawezi Kutenda Haki sawa
kwa wote kwasababu Tayari ameishaonyesha yeye ni Mwanachama
wa CCM wakati hapaswi Kuwa mwanasiasa ?
Uchaguzi
Mkuu umekwisha ,Kesi za kupinga Matokeo ya Ubunge lazima
zitafunguliwa Katika baadhi ya Mahakama zetu na Kesi hizo
mdaiwa wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbunge
aliyeshinda na Msimamizi Wa uchaguzi.
Enzi
zake Mwanasheria Mkuu wa sasa George Masaju akiwa na wadhifa
wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa akienda
Mahakamani Mwenyewe kuiwakilisha serikali pindi
iliposhitakiwa au serikali ilipofungua Kesi dhidi ya mtu,au
Taasisi Fulani.
Hata
sasa hivi Mwanasheria Mkuu wa serikali hazuiwi kwenda
mahakamani kuendesha baadhi ya Kesi ila kutokana na jukumu
zito anaamua kukasimu majukumu Mawakili wa serikali na
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Na
Mfano hai ni Oktoba Mwaka huu, Kada wa Chadema alifungua
Kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiomba
Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam itoe Tafsiri ya mita 200
Katika Kesi maarufu ya mita 200 .
Masaju
alimtwisha jukumu hiyo Naibu wake Dk.Tulia na Wanasheria
wengine wa serikali kwenda kutetea Kesi hiyo hiyo na
hatimaye walishinda.
Swali
langu Je , itokee siku aliyekuwa mgombea Ubunge wa vyama Vya
upinzani Kufungua Kesi ya kupinga Ubunge wa Mbunge wa CCM
halafu Dk.Ackson aende kuitetea hiyo Kesi
mahakamani.
Je
Yule mlalamikaji ambaye alikuwa mgombea toka vyama Vya
upinzani akiiambia Mahakama Kuwa Hana Imani na
Dk.Ackson Katika Kesi hiyo kwasababu ni Kada wa CCM na
hivyo hatoweza kusaidia Mahakama Kutenda Haki Atakuwa
amekosea?
Sina
Chuki na Dk.Ackson na sina Sababu ya Kujenga Chuki
naye ,ila tu napenda kumweleza kijana mwenzangu Kuwa Kabla
ya kuchukua uamuzi aliouchukua wa Kugombea Uspika
akijitafakari kwanza yeye kwasasa ni nani?Ana wadhifa
gani?Anafahamu Jamii itamtafsiri vipi?
Je
anapoenda Kugombea Uspika awe na uhakika Kuwa atashinda na
asiposhinda basi atakuwa amejipunguzia asilimia za
kutoaminiwa Katika suala zima za Utoaji Haki hasa Katika
vyombo vyetu Vya Sheria hata kama Atakuwa anatenda Haki
kweli kwasababu Tayari ameishauthibitishia umma yeye ni
Mwanachama wa Chama Fulani.
Hivi
Leo hii itokee Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mgonjwa au
amesafiri nje ya nchi au amefariki ghafla na hivyo
kusababisha Naibu Mwanasheria wa Serikali Dk.Tulia kukaimu
Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ,awe Bungeni anatoa
ushauri wa kisheria ndani ya Bunge kuhusu muswaada Fulani au
jambo Fulani ambalo wabunge wa upinzani hawalitaki hata kama
ni kweli Dk.Tulia yupo sahihi kisheria, wale Wabunge wa
upinzani wakiamua kumpinga kwa Kigezo yeye anatetea huo
muswaada kwasababu pia ni Mwanachama wa CCM, at akasirika au
sisi wananchi na viongozi wa serikali hiyo Hali
watachukuliaje?
Kwa
mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya nchi inasema
Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifa
.
Ibara
hiyo haijasema Mwanasheria Mkuu wa serikali atakuwa mbunge
wa
Chama Fulani cha siasa.
Ieleweke
kwamba uteuzi wa Dk.Ackson ulizua minong'ono
na maswali mengi chini kwa chini kutoka Katika Kada ya
Wanasheria hasa wa serikali licha ana elimu nzuri licha tu
hajawahi Kuwa Wakili wa serikali na Hana udhoefu wa
uendeshaji wa Mashitaka.
Baadhi
ya watu wa Kada ya Sheria Walisema licha Rais anayo mamlaka
ya Kumteua mtu yoyote kushika wadhifa wowote ,Walisema
aikuwa busara kwa Rais Kikwete kuacha kuteua
Mawakili wa serikali kushika Nafasi ya Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali na kwenda kumteua Dk.Ackson ambaye
hata miiko ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali hajaijua
.
Kumbe
sasa wale waliokuwa wakipata Mashaka kuhusu Utendaji wa
Dk.Ackson kwa upande Fulani sasa tunaweza Kusema walikuwa
sahihi kwasababu kitendo cha Dk.Ackson Kugombea nafasi ya
Uspika wakati yeye ni mtumishi wa umma na hapaswi Kuwa
mwanasiasa tena katika kipindi kifupi tu ni dhahiri sasa
miiko ya Kazi yake haifahamu na hakutaka kuifahamu
akaamua kukurupuka na kufanya hicho alichokifanya
ambacho kimesababisha watu kutulia mashaka utendaji
wake.Aibu sana.
Kuna
taarifa zisizo rasmi Kuwa Dk.Ackson ametumwa kwa makusudi na
kiongozi mmoja Mwanamke ambaye ni Waziri na ana nafasi kubwa
ndani ya CCM agombee nafasi hiyo ili aende kuwaganya
kura za baadhi ya wagombea Uspika ambao ni tisho kwa hao
waliomtuma Dk.Ackson.
Kwa
Kuwa sina ushahidi na taarifa hizo Mimi nitabaki kuamini
Dk.Ackson amegombea Uspika bila kutumwa na mtu.
Ila
taarifa hizo ziwe za kweli au siyo za uzushi,
zinazidi kujengea Mashaka Utendaji wa Dk.Ackson
kutokana na Cheo Chake na yote hayo yanampata na yatazidi
kumpata kwasababu ameamua kuingia Kwenye siasa
,asingeingia huko yasingemfika.
Hakuna
ubishi Kuwa Dk.Ackson kwa kitendo chake cha kugombea
uspika licha ana haki ya Kikatiba kugombea, amedhihirisha
kuwa yeye ana papara ya kupata madaraka makubwa tena kwa
vipindi vifupivifupi ili Hali bado Ana umri Mdogo.
Ushahidi
ni huu Septemba 9 kateuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Novemba 11 Mwaka huu,
kachukua fomu ya Kugombea Uspika.
Hivi
tukisema Dk.Ackson ameudharau,aupendi na autaki uteuzi
Rais Kikwete wa alipomteua yeye Kuwa Naibu Mwanasheria
Mkuu wa serikali tutakuwa Tunakosea?
Maana
Aiingii akilini kwa Kipindi kifupi hicho alichoteuliwa
kushika nafasi hiyo nzito serikali halafu aamue kwenda
kuwania nafasi ya Uspika halafu tuache kuamini kuwa
Dk.Ackson ile nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali anaipenda?
Aipendi
na ninatabiri anaweza asidumu Katika wadhifa huo kwa muda
mrefu kwasababu Tayari ameishaonyesha wazi Ana tamaa ya
kupata madaraka makubwa kwa harakahara na hataki kujifunza
Kazi kutoka Kwa waiomtangulia na akae akijua baadhi ya
watendaji wake wa chini wamekerwa na yeye kiongozi wao
kujiingiza Kwenye siasa wakati haruhusiwi Kuwa Mwanachama wa
Chama cha siasa.
Hivi
wewe Dk.Ackson kama umegombea Uspika sasa ,nikuulize
Je umepata muda saa ngapi ya kukaa na Mawakili wa serikali
wakawa wana kufundisha jinsi ya kuendesha hiyo Ofisi na wewe
ukapata uzoefu ?
Ni
wazi bado unaitaji kupikwa na Wanasheria wa serikali ili
uive lakini ni wazi sasa umeonyesha hata huo muda wa
kukaa kitako upikwe na watangulizi wako katika hiyo ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa serikali huna unawaza Kugombea madaraka
ya kisiasa.Huzuni.
Minakushauri,
kuliko kuendelea kushikilia nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu
wa serikali wakati matamanio yako ni Kugombea Uspika na
siasa, ni vyema ungeandika barua ya kujihudhuru wadhifa huo
mapema ili Rais mpya Dk.John Magufuli ateue mtu mwingine
ambaye kwanza ana uzoefu na kazi ya wakili wa serikali
ambaye akili zake zimetulia,maana wewe bado hujatulia ili
afanyekazi.
Wewe
Dk,Ackson tayari umeishaonekana mguu mmoja upo Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mguu mwingine upo CCM
Kugombea madaraka makubwa ya kisiasa.
Sasa
mtu wa aina ya Dk. Tulia ni wazi Utendaji wake katika
madaraka aliyonayo hautakuwa mzuri maana muda mwingi atakuwa
fikra za kupanga mikakati ya jinsi ya kupata nafasi nyingine
kubwa zaidi ya hiyo tena kwa chap chap.
Dk.Tulia
unapaswa utambue jambo Moja Kuwa wanasiasa siyo watu wa
kuaminika sana.Wakikupa ushauri wa kufanya jambo lolote hata
hili la Kugombea Uspika ulitakiwa ulitafakari sana kwamba
endapo ukikosa nafasi hiyo wewe hadhi yako Mbele ya Jamii
inakuwaje.
Umeanza
kutiliwa Mashaka na baadhi ya Jamii,lakini waliokushauri
ugombee Uspika hawatakusaidia kuminya fikra za watu na
baadhi ya watendaji wako wasikuone wewe ufahai tena
kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa
kitendo Chako cha Kugombea Uspika kupitia CCM licha siyo
kosa la jinai.
Niitimishe
kwa Kusema Kuwa Dk.Ackson endapo ukikosa nafasi ya Spika
,hufai kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kwasababu Tayari umeonyesha wewe ni mwanasiasa hivyo
Utendaji wako unatiliwa Mashaka.
Pia
nakushauri acha pupa ya kuwania madaraka ili Hali wewe
ni msomi na bado ni binti Mdogo sana licha una elimu kubwa
lakini bado unaitaji kuelewa,kupikwa na waliokutangulia na
wenye uzoefu Katika eneo la Mawakili wa Serikali ,siasa
utafanikiwa.
Au
kama fikra na moyo wako hautaki uendelee Kuwa na Cheo
cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,zinakutuma kwenda
kufanya siasa ni vyema basi ukaomba Kibali cha kumuona Rais
Magufuli ili umeombe akutoe Katika Cheo hicho au wewe
Mwenyewe andika barua ujiudhuru kuliko kufanya hili
uliofanya ambalo linakatazwa kabisa Kuwa Mwanasheria
wa serikali Kuwa mwanasiasa lakini wewe mwenzetu bila woga
tena hadharani umeonyesha wewe ni mwanasiasa wakati huo huo
ni mtumishi wa umma.
Dk.Ackson
nakupenda ebu punguza kasi kidogo ya matamanio ya kupata
madaraka inakusaidia Kwani Mtaka yote ukosa yote Waswahili
Walisema.Nakutakia kila la kheri Katika mbiyo zako za
Uspika.
Mungu
ibariki Tanzania
Chanzo:
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.comFacebook:
Happy Katabazi0716 77449414/11/2015
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment