Thursday, 10 September 2015

Re: [wanabidii] Wanaharakati, wasomi wamshukia Magufuli kuhusu mabadiliko

Ushauri kwa viongozi wa UKAWA na Watanzania wasomi na Wazalendo kwa ujumla: Wakati Magufuli anatoa ahadi mpya mpya kwa Watanzania, orodhesheni ahadi za JK (CCM) 2000 - 2005, na 2010 - 2015 ili Watanzania wajue ni yapi yametekelezwa na yapi yameota mbawa. Baada ya hapo, watanzania tuanze sasa kuzipitia ahadi mpya za Magufulu na kuziamini ama kuzikataa kutokana na tathmini ya japo ahadi za miaka 10 iliyopita zilizotolewa na CCM.

Kupoteza muda mwiiiingi kusema mgombea wa upinzani yupo hivi, mara mdhaifu mara ana kashfa ni kama kulazimisha maji kupanda mlima. Hadithi marudio za mara Rose Kamili si kamili, mara Slaa ambaye kashachukua njia yake mpya ya maisha ya kumalizia uzee wake hapa duniani kasema hivi, mara yupo sawa, mara .... NADHANI KOTE HUKO NI KUTUTOA NJE YA RELI! Tung'ang'ane na kuiuliza CCM, japo kwa ahadi ya miaka 10 tu iliyopita dhidi ya ahadi mpya za 2015 -2020.

Kama CCM imetekeleza ahadi zake kwa Watanzania kwa japo miaka 10 iliyopita, na utawala umezidi kuimarika na kuwa bora, na uchumi wetu unalipa sasa kuliko tulikotoka, na wabadhirifu wa mali ya umma wapo kifungoni na mali walizotuibia zimetaifishwa/zimerudishwa katika hazina ya taifa, na watoto wa viongozi wanamiliki wanachomilik kihalali kabisa sawa na kila Mtanzania mtafutaji, na ya kwamba rasilimali alizotujalia Muumba zinawafaidisha Watanzania kwa ujumla wao pasipo mikataba yenye hila, then kelele za nini na kulazimisha mara sura ya huyu yafaa, mara huyu ana nyumba ndogo... haina maana kwani hakuna aliyemkamilifu. Tangu tusikie habari za afya ya Lowassa, mimi na ninyi tumezika ndugu zetu kibao, na hatujui mchana huu ama kesho ni zamu ya nani. Yaweza kuwa mimi ama wewe! Tukamwacha unayemtuhumu afya yake (japo huna vipimo vya mapungufu ya afya yake) akiendelea kudunda. Inanikumbusha babu yangu aliyeuguzwa kwa miaka 40! Mpaka mkewe aliyekuwa anamuhudumia akatwaliwa, hapo ndipo naye akafuata mwaka mmoja baadae.

Kama CCM wapo safi kiasi hicho, tutawapa nchi hata kama kwa miaka mingine 50 ijayo!
La, Watanzania watapima! Tusilazimishe maji kupanda mlima. CCM yaweza kushinda sana, lakini tuwe wakweli.
Lakini waandishi mlio humu ndani, wengine mnalazimisha mambo mno, na wengine mna agenda ya kututoa nje ya mstari kwa propaganda zisizo na tija kwa wakati tulio nao. MUONE AIBU, Watanzania wa leo wameelimika sana, wanataka data, basi, unachukua chako. Njaa zenu wengine zisilete tabu namna hii. Waambieni mabwana zenu jamaa mbona kama vile hawaelewi? Badillisheni mwelekeo, tutawaelewa. Viji-heading uchwara vinadhalilisha taaluma zenu! Mnaturudisha nyuma kila wakati. Nendeni kwa hoja za msingi na za maana ya kampeni. Wengine mnonyesha wazi kuendeshwa na njaa na malipo ya vipande 30 vya fedha. TANZANIA YETU KWANZA, mtusaidie Watanzania kujua tulipo na tunapoelekea. Ndiyo, ni wakati wenu vyombo vya habari kuvuna sana, ni wakati wenu wa mavuno, lakini, tupeni vitu vyenye ladha ya kuponya nchi, elimu sahihi pasipo ushabiki wa vijisenti.

nitangulize msamaha kama nimegusa tumbo la mtu.

2015-09-09 18:21 GMT+03:00 'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
CCM hawana jipya, wameanza kutapatapa. Kwanza kabla ya kutoa ahadi mpya wanapaswa wawaambie watanzania wamewafanyia nini tangu mwaka 1961 walipoingia madrakani. sio kila mwaka wanaturundikia ahadi ambazo hazitekelezeki.

On Wednesday, September 9, 2015 5:59 PM, 'Mike Zunzu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Uzuri wa wale wanaokemea kauli za uchochezi, hawawezi kusema chochote pale kinapotamkwa na mtu wa kutoka upande wao,
Mwbari hii kazungumza vizuri sana, kwamba mabadiliko yanayozungumziwa ni mabadiliko ya kidemokrasia, yaani mkwenda mpiga kura, mshindi aliyechaguliwa na wengi anapatikana, ambapo atakayeshinda si lazike CHADEMA au CCM, anaweza kutoka chama chochote. Kwani nani kasema kiongozi mwinginkuja sha kidikkideta? Hayo ni mawazo tu, tema mawazo finyu, cha msingi ni kupanda jukwaani na kumwaga sera zako, tena usizungumzie kwa kirefu kuhusu wapinzani wako.

Leo hii nimesoma kuna issue nyingine imezuka, eti kwa nini Lowasa anakuja nyuma alikopita Magufuli, hiyo ni hoja ya kushindwa kuzifikia ndizi mbivu, kama wakiweza wabadilishe iwe Lowasa Maguli afuate, kwanzababishwa na Serikali wenyewe, kinyume chake siku CCM wana launch kapeini yao owasa angelikuwa barabarani, lakin wakawachelewesha  ndiyo maana yupo nyuma.yo nayo ni issue, hapo ni dalili za kuona anazidiwa kete..

Mimi bado masubiri kuona moto wa mabua ukizimika le wa makaa ya mawe, au miujiza itatokea,ule wa makaa ya mawe utazimika na kuucha wa mabua?
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment