Friday, 25 September 2015

RE: [wanabidii] TWAWEZA UKAKASI

TWAWEZA nmi taasisi ambayo utafiti wake unaheshimika ila wale ambao wanaona haukutoa kile walichotaka huwa wanalalamika.
1. Utafiti wa Twaweza ulipoonyesha kuwa Lowasa alikuwa anaongoza mwaka jana wagombea wengine walilalamika ila Lowasa na wafuasi wake hawakulalamika.
2. Utafiti wa TWAWEZA ulipoonyesha kuwa wananchi wengi walikuwa wanapenda rasimu ya katiba ya Warioba msemaji wa CCM alilalamika akizingizia kuwa ni kwa sababu sample size ilikuwa ndogo. Hakukubali matokeo hayo.
3. Sasa utafiti huu unaonyesha hali ilivyokuwa mwishoni mwa Atgust na mwanzoni mwa September lakini wale ambao hawapendi hayo matokeo hayo wanasema Twaweza imenunuliwa.
Kwa maoni yangu Twaweza wako makini kuchukua random sample. Matokeo hayawezi kuwa mbali sana na hali halisi. Tafiti hizi badala ya kukataliwa na kupuuzwa ingefaa zifanyiwe kazi. Mwezi mmoja uliobaki kufikia siku ya uchaguzi inawezekana kubadilisha matokeo (either way) kutegemea na kila upande utakavyojipanga kuendesha kampeni zao. Changamoto ni kuweka mikakati na mbinu bunifu wala si kukataa utafiti na kutafuta mchawi.

Samuel Wangwe
Executive Director

............................................................
REPOA, undertakes and facilitates research, conducts and coordinates training, and promotes dialogue and development of policy for pro-poor growth and poverty reduction.
Please consider the environment before printing this email.

-----Original Message-----
From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com]
Sent: Friday, September 25, 2015 8:56 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TWAWEZA UKAKASI

Huu ugonjwa wa kutetemeka (Parkisons Disease) ni mbaya sana kama si exposure to chemicals ambazo ni neuro toxic zaidi ni genetically transmitted. Inafikia stage mtu anapoteza kumbukumbu, hawezi kumeza chakula, haja inatoka hawezi kuzuia kutokana na mfumo wa neva na mishipa hauna mawasiliano. Mtu anakuwa mkali kama mbwa wa ulinzi kutokana na stress mishipa ya fahamu na ubongo. Kinasaidia kumpatia Vitamin B1 gram 100 kwa siku au B complex ukikosa Neuroton mpaka utakapopata ushauli ya daktari kwa matibabu maalum. Mwisho wake anakuwa hawezi kumeza hata chakula budi uji kumlisha kupitia tube na haja ndogo mkoba na tube ya haja ndogo. Ni mateso sana sana. Kwa uzuri-utafiti huko USA umefika mbali sana. Kwa sasa wanatumia cells zako kuotesha cells nzuri kuondoa zile mbaya zenye gene ya ugonjwa huo. Lakini muda bado wa sisi kupata matibabu haya kwa haraka. Matajiri wameweka hela katika tafiti za matibabu ya ugonjwa huu.

Tanzania tunakoelekea ni kubaya sana na magonjwa kama haya kutokana na madini yaliyopo nchini. Wachimbaji wakubwa kutokuzingatia sheria ya madini, kazi na mazingira. rushwa katika uanzishaji na ruhusa ya ujenzi wa viwanda vya kemikali na vya kuchakachua madini. Ujenzi wa kiwanda kinachomwaga maji ya sumu, mabaya kiafya na kimazingira unapitishwaje bila ya design kuwa kamilifu na kinaruhusiwajwe kuanza kazi na kuendelea bila ya approval ya final constructed structure na facilities zake? Amesoma wapi huyo anayepitisha kiwanda cha processing ya madini kuanza, textile ya nguo na kiwanda cha sabuni bila ya kiwanda kujenga waste stabilization pond? wafanyakazi kufanyakazi bila ya protective gear. gari la takataka za mjini linapita wazoa taka wamekaa juu ya taka bila ya nguo za kazi bali na zao za kawaida kakalia lead, suphuric acid, DDT iliyotupwa jalalani, matambaya ya zahanati na sindano yametupwa dampo la kawaida na barabarani na anajichoma na sindano zake na kukalia mafuko yenye matambala ya damu na makohozi ya TB anayashika kwa mkono? Tunapita tunaona hatufanyi kitu!! Private firms hizo vibaka kama public firms-bongoland!! Kisha Mabadiliko bila ya sisi wanga kona zote kubadilika kiakili na kimatendo!!

Wote ni wateja wa Parkisons disease kwani-machimbo ya Geita-Mugusu, Nyangarata, Nyamigele; ya Musoma, Kagera yanaingiza madini na kemikali mbali ziwa Victoria kupitia mito iingiayo ziwani na sumu hizo tunakula nchi nzima kutokana na bio-accumulation kwenye samaki, dagaa, maziwa na nyama ya ng'ombe. Tunakula DSM kutoka kutokana na maji ya mto Ruvu kutoka Mgeta, Mkulazi Morogoro; Tunakunywa maji yenye ulanga vijijini ambao unaleta cancer ya koo na utumbo (carcinogenic); madawa ya mazao (agrochemicals) na hizo wanazopiga kuku na kanga wanenepe. Ni wateja wa magonjwa ya kila aina yasiyotibika na kama huu jamaa anaougua. Kuzingatia sheria za chemikali, mazingira, occupational health maafisa mazingira na industrial officers wafanye kazi ya ziada. Elimu haisaidii. Amref wamefundisha kuhusu AIDS na mazingira migodini geita hakuna kinachoendelea hatusikii na ndio kwanza wanahamahama mgodi hadi mgoni na kuoana bila ya kupima au kutumia kondom. akianza kuumwa kutetemeka, nywele kudongoka (kutokana na matumizi mabaya ya kuchezea mercury) anatafuta mchawi. Waganga, mahela, kifo ndugu wanamshika uchawi hawara au mshirika wake kumbe ni mercury anayochezea na kuvuta pumzi kupumua mvuke wake.

Akili za nyani-changanya na zako!!

--------------------------------------------
On Fri, 25/9/15, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] TWAWEZA UKAKASI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 25 September, 2015, 8:05

Ubishi sio kitu muzuri
sana. Hata Omela anajua hiyo. Mmh!!!
Tukisema Edo hayupo vizur kiafya, it
doesn't mean tumesema ni positive, malaria, diabetic or whatever. We are trying to think we are thinking right on what we see.

Sisi sio madaktari, hatujui kutibu iwe mtu au hata kuku tu.
Lakini hata picha hatuoni?
Angalia hiyo video attachment.

Tell me something!!!!!

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
wanabidii+ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
This message has been scanned for viruses and dangerous content by MailScanner, and is believed to be clean.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment