Ulichosema kiko wazi ndugu. KANU bado inaongoza Kenya. Wamarekani walijaribu kuiondoa kwa kumsaidia laira wakakwama. Zimbabwe waingereza walijaribu kuiondoa ZANU-PF na kumbambikiza TSvangilay wakakwama. Ni hivyo hivyo kwa Tanzania mafisadi papa wanajaribu kumbambikiza Lowasa. Wengine wamemfuata tunaona wanavyotpkwa jasho kujaribu kusema hili na hili. Wamekimbia baada ya kugungua kuwa magufuli hawezi kuwaachia ardhi waliyowanyang'anya wananchi huko Mvomera au kuwaacha waendelee kumiliki ng'ombe walizokwapua Kitengure na kwingineko. Wamejikusanya wanajairbu kujifanya wanamabadiliko
Wameshindwa tarehe 23 October siku mbili kabla ya uchaguzi.
Elisa
--------------------------------------------
On Sun, 9/6/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Siyo lazima kubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, September 6, 2015, 10:28 PM
Siyo
lazima kubadilisha chama ili kuleta
mabadiliko ya Maendeleo
Dhana ya
baadhi ya sisi Wantania ya kwamba kuondoa Mfumo wa utawala
wa nchi ni lazima
kubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo ya
Kiuchumi na maisha bora
kwa kila mwanachi siyo sahihi. Dhana hii imekuwa ikitolewa
mfano wa Kenya na
kwamba imeondoa tabaka la uongozi wa KANU.
Kiuhalisia Kenya haijawahi kubadilisha mfumo wa Utawala ulio
nje ya KANU. MWAI
KIBAKI amekuwa ndani ya KANU tangu Kenya ilipopata uhuru
mpaka mwaka 2002
alipogombea Urais kupitia National Alliance Rainbon
Coalition NARC. Kabla ya
hapo alikuwa Makamu wa Rais wa serikali ya KANU ya Rais
mstaafu DANIEL ARAP MOI.
Rais mstaafu MWAI KIBAKI alidumu na NARC hadi 2005 ambapo
alipokuwa akigombea
kiti hichocha Urais 2007 alipolazimika kupitia chama cha
PNU( Party of National
Unity).
Pia ikumbukwe kwamba wakati MWAI
KIBAKI akiwa
Rais UHURU KENYATTA alikuwa mmoja wa viongozi ndani ya
serikali hiyo. Aidha
viongozi wengine tofauti tofauti ambao ni KANU kiundakindaki
walikuwemo RAILA
ODINGA . ODINGA ambaye hajawahi kuwa KANU.
Mwaka 2013 UHURU KENYATTA alishinda uchaguzi kupitia chama
cha The National
Alliance (TNA). Hivyo mlolongo huu wa uongozi hauonyeshi
moja kwa moja ya
kwamba mfumo huo wa uongozi ulibadilika kutoka ule wa KANU
kwenda kwa ambao
walikuwa hawajapitia KANU.
Hivi sasa inaonyesha dhahiri kwamba
KANU
katika muonekano wa Kimataifa imerejea rasmi .Soma daily
Nation Toleo No18384
Pg la tarehe 11/08/2015.Uhuru's Political Party Catches up
with him as Uganda
army band plays him "KANU YAJENGA NCHI".
Katika
serikali hizo za mpito wakenya hawakuwahi kushawishika
kumpata Rais aliye nje
ya safu ya KANU pamoja na kubadilisha badilisha vyama na
msukumo wa kutoka nje
ya nchi bado walishikamana na kuwa wamoja katika kupata safu
za viongozi.
RAILA ODINGA ambaye ni mpinzani wa
kweli pale
alipoona viongozi ambao asili yao ni wa KANU wamefanya
vizuri alisimamia mazuri
hayo kama raia wa KENYA haijawahi kusikika fununu yoyote
wala uvumi wa kwamba
alitoa fedha interms of billions ili kuupata uongozi wa
kulazimisha,KAMA
AFANYAVYO EDWAR LOWASA HIVI SASA HAPA TANZANIA.
Ninachojifunza ni kwa,mba viongozi bora mpaka sasa, hivi ni
wa kutoka chama
tawala ingawaje pia wapo kwenye vyama vingine vya siasa
.Lakini kiongozi yeyote
aliyeonolewa na chama husika kwa kukiuka maadili ya chama
hicho yaliyo wazi
alafu akakimbilia chama kingine kwa lengo la kutaka kupata
uongozi siyo kama
mlezi wa chama hicho huyo ni MROHO WA MADARAKA.
Nasema hivyo
kwa sababu misingi iliyo muondoa yeye alikuwa miongoni mwa
watu walio iandaa
tena tena akiwa kwenye nafasi ya juu na Mkongwe.
La msingi la kujifunza kutoka kwa wenzetu KENYA ni kuchukia
RUSHWA kutumika kama
njia ya kutupelekea kiongozi IKULU Pia atapata nini
mwendesha bodaboda
anayepewa mafuta na token ya Tsh elfu kumi na kuendelea , Je
akipata ajali
atampa pesa za matibabu ? Mimi nisiye kuwa na elimu ajira
ninayoambiwa kuwa
nitaipata katika ulimwengu huu wa wasomi waliojaa hadi
kijijini kwangu kule
Mbwinde, ajira hii nitaipataje?
Kwa wenzangu waliosoma ni dhahiri
kwamba
tulipofika kwa sasa ni mahali pa kudanganyana cha msingi
tuungane pamoja kwa
nguvu zetu zote kukemea wazi wazi viongozi wanaotumia RUSHWA
ya fedha nyingi
kama barabara ya kwenda IKULU. Pia tuwachukie wafadhili
wanaotoa michango ya
hali na mali Mabilion ya pesa kuhakikisha mlengwa wao
anaingia ikulu.
Hawa ndiyo watakaotufanya tishe maisha
ya
SURVIVAL FOR FITEST, No Fit no Survive . Turudi tujitazame
ili tugundue wapi
tulipojikwaa tuparekebishe ili tuweze kufufua na kuendeleza
nyayo za MWALIMU
JULIUS K NYERERE.
JOHN POMBE MAGUFULI atatufaa kwani hakutumia RUSHWA hata
senti moja , let's
support him ,tuachane na dhana ya vyama ambavyo sasa
vinatupotosha kuanza
kuwakumbatia hata wenye miiba kwa sababu tu ya lita 5 tu za
mafuta ya bodaboda
na usafiri wa kututoa mikoani kuja Dar Es Salaam
kumshangilia . Baadhi ya
mataifa ya nje yaliyo na nia njema yamegundua kuwa Kenya
ilipotea na vivyo
hivyo ndiyo yanavyotuona sisi watanzania tunavyopotea .
DR WILLIBROD SLAA na Prof. IBRAHIMU LIPUMBA ni wa kwanza
kugundua kwamba siasa
za vyama vya siasa ni za kinafiki " Hongera sana kwao hawa
wazee na Mungu awape
uzima zaidi ili waendelee kuwa walezi na mfano wa kuigwa".
Mahali penye
udanganyifu panajionyesha waziwazi toka lini mtu kama LOWASA
akupatie fedha hivihivi
tu, kwani wewe ni mjomba wako!!!! Mtu hawezi kununua wengine
kama yeye
hajanunuliwa kwanza!!!!! Na atakapopata anachokitaka
hatorudi tana kwako bali
atalipa fedha zake zote na faida mara 100 kwa fedha yako
wewe na mimi.
Pindi mambo
yakiharibika hupanda ndege na kukimbilia ULAYa na kutuacha
ndugu tukiuana kwa
kisasi ambacho mimi na wewe hatukijui wala hatuna.
Juhudi zako binafsi ndizo zitakazoboresha maisha yako wewew
binafsi,kikundi
chenu , kijiji chenu , wilaya yenu , mkoa wenu, na hatimaye
Taifa letu kwa
ujumla.
Usikubali kutumiwa na wanasiasa wasakatonge !Waanze kwanza
wao na familia zao
kuandamana na kubeba mabango ya wazazi wao.
TUNAHITAJI MABADILIKO CHANYA YA KIFIKRA KWA KUWAKATAA
WANAOTAKA KUINGIA IKULU
KWA PESA, TUSIJARIBU KUONJA SUMU, SUMU HAIONJWI
INAUA
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment