Kuna wenye macho ambao ni vipofu. Mifano wanaonyeshwa jinsi gani mtu amezungukwa na misitu, maji, udongo lakini nyumbae ipo wazi hakandiki. Kuna nyoka, wanyama pori. anakata miti, anauza mkaa na mbao-hela apatayo hajiletei mabadiliko-pombe, kuoa wake wengi, kutwa kilabuni. Kikija chama kimya kitamjengea choo, kumkandikia nyumba? Wamepewa viwanja, bati, cement-wameuza na wamerudi kutoka mabwepande wanaishi katika maji ya kinyesi. Barabara ya mabasi mwendo kazi na vituo vyake-kageuza pa kutupa taka kituo cha bus alichangie uzoaji taka. Kipindupindu kinaua na anaona wanaokufa jirani au ndugu zake-bado anatiririsha maji ya kinyesi mtaani, anauza vyakula hapo, ana sanduku la samaki, chips hafungi mlango wa wavu anaachawazi nzi zinajaa.
Yupo hapo kijijini hafanyi lolote kama diwani au mbunge lakini anaona kuhama chama ndio kutaleta maendeleo. Mbona yeye hapo hahamasishi wananchi kufanya maendeleo yao? Semina anazohudhuria za kujenga uwezo na yeye ndio anamiliki bar ya pombe ya , video ya simena za matusi kijijini (ana hela). Hata kukiwa na land use plan-hasisitizi wananchi kutekeleza wajibu wao. Tunasema ni sisi sote tubadilike. Ukifika hapo katani kwake Diwani anawaambia wananchi wasihudhurie kikao hicho kama hawatapewa posho. Anakuwa wakwanza kuulizia posho ya kikao eti mliokuja mnalipwa posho ya kazi hiyo. Hiyo kisha anahama chama-mtu huyo? Mwache ahame-akafie mbele. Anaangalia makosa ya CCM kwani CCm ni nani? Ni pamoja na yeye kuhakikisha anazingatia maadili, matakwa ya kazi yake, mwananchi kujituma ipasavyo bila kubweteka, kutetea uozo (mtoto anabakwa mnakaa kikao kuongea kufuta kesi na kuchukua rushwa kuficha fedheha ya familia bila ya kuangalia haki ya mtoto); mtu fisadi akirudi
kijijini mnajikomba kumpokea kwa shangwe na vifijo kisha-CCM ina mafisadi na kumuwekea dhamana ya mamilioni juu. Lakini mkiambiwa kijiji mchangie madawati na kunjenga shule ya Kata au bomba la maji 20% ya capital cost hamtaki. Lakini ni ninyi pia mnaochimba mto kukoshea dhahabu; mnaingiza mifugo, mnakata msitu ambao ni chanzo cha mto na mito inakauka hakuna maji. Mkiondolewa msiharibu na kujiumiza wenyewe maji hampati na mnakunywa kemikali mnazoingiza zina madhara- CCM mbaya tunaganga njaa! Ganga njaa kwa kulinda afya na mazingira. Tumia hela kwa maendeleo yako.
CCM imefanya mengi lakini ili nchi iwe na maendeleo kona zote, sekta zote muhimu ni sisi watanzania kubadilika kiakili na kimatendo ili tufanye ya maendeleo. Pili-serikali ijayo ihakikishe imefanya kwa gharama zote Village and Urban Land Use Planning and Certification kwa kuwapa wamiliki hati miliki ardhi. Hati zipigwe muhuri wa Haihamishiki bila ya kibali cha serikali (non transferable without GVT permit) ili kuondoa ule uhuni wafanyao watu masikini kuuza ardhi kisha kuhamia maeneo hatarishi hela zote anakunywia pombe au kutoroka familia.
Hao waliohama wanajua Mangufuli anakuja kuwanyanganya ardhi waliyochukua za mashamba ya magereza, mamlaka mbali mbali. Watafirisiwa walipimiwa viwanja vya uwekezaji wakapewa hati miliki wakachukua mikopo wao hawakujenga viwanda wakajenga hall za arusi, kuweka frame za kupangisha kuuza imported items, watu wanafua vyuma na kutengeneza fanisha. Gharama za umpimaji maeneo hayo ni mkopo wa World Bank!! Imefika wakati wa kuwafirisi!! Waanze kuhama na walioweka frame Urafiki textile tumpe mchina anununue pamba isio mawe na michanga achakacue nguo tuvae. Mbongo unapewa mkataba kama mwekezaji mjasiriamali mzawa-ukisha kununua pamba au mchele uuzie serikali ulipwe unajaza mawe na kokoto!! Ni sisi WAJINGA kubadilika na kuwa na upendo na nchi yetu.
Anayempa tender ya kupika kulisha semina ya ofisi au warsha na kupamba na kulipwa mihela ya serikali mke wake abadilike awape vijana wajasiriamali. waliojiajiri na kujiandikisha. Tuache upendeleo.
Semina au warsha ni kitu cha kawaida. Fulana, kofia, bag, writing pad yenye nembo ya nini kikao hata kama ya wiki. Hela za hizo sare ni jinsi ya kuiibia serikali hapo una 10+% yaani bila sare maelezo hayatoingia kichani? Hivi vyote vikomeshwe na mangufuli. Ni Mbinu ya sisi wabongo kuiibia serikali inapofanya hivi tunageuza hivi kama inzi anavyofanya miguu yake. Ni sisi WANGA wakubwa kutafuta mbinu ya kujifaidisha daima na kumnyima mtu haki anapokataa kutoa rushwa. Kwa tabia hizi mbaya-hata kije kipya kitakwama. Na hao wanaotaka kipoya ndio hao wanaotangaza utengano ili wafaidike zaidi eti ZNZ iwe huru, kuwe na Tanganyika na Jamuhuri ya Muungano!! Hela zote hizo za management utatoa wapi na unasema hutotoza kodi. Hela za investment na hata za kujenga vyoo jimboni kwako watu wasinye porini huna au unazo hukutoa. Unataka urudishe ukoloni na utumwa?
Anayesema Nooo big no hebu nenda kwao kwa wazazi wao uone amefanya nini-yupo mjini anakula keki. Hata mkifika kwao anakupeleka nyumba ya mjomba sio ya wazazi wao. Huyu ndio anaona mageuzi yanamchengea nyumba bora na choo? Hata likizo harudi kwao anaona shida kwenda porini au choo jirani anapepesa jicho anakuona-makuti na nyasi zipo lakini hawana muda wa kujengea hifadhi yao. Fukuza mpaka extesion staff ambae hakai kituoni, hana analofanya katika eneo lake yupo yupo tu anauza sura na kuzaa na visichana kila kijiji ana mbuto-kidume mbegu na mdada kutwa magari yanakuja kumchukua anakwenda mjini.
Tunataka wachapakazi wamsaidie Mangufuri kuleta mageuzi ya uhakika kwa KUTUPELEKESHA tufanye na kutimiza wajibu wetu. Hivi kweli unayaona mapungufu na matatizo hata jimboni kwako ulikokuwa mbunge karne, unamipesa kibao unagawa lakini matatizo madogo jimboni huwezi kusaidia halafu-CCM haijafanya kitu 54 years? Wewe nawe ukiwa mtendaji umefanya nini kwako? Jibu-tuhamie kwingine ndio tutafanya utendaji!
Kama kawa, ninakuwekea tena kumbukumbu ya hali halisi nchini halafu uone kama yatashuka kama mvua maendeleo tutakayo!!
--------------------------------------------
On Wed, 9/9/15, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Siyo lazima ubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, 9 September, 2015, 16:59
Kwa asiyeangalia CCM wamefanya nini,
bali anaangalia hawakufanya nini tu atakubaliana nawewe.
najua wapo ambao wanaadika humu lakini isingekuwa CCM
wasingepata nafasi ya kuandika hata humu. Nenda nchi jirani
utawakuta. Hatuitetei wala hatusemi haina makosa au
haikuharibu lakini si sahih kusema miaka 54 haikufanya kitu.
Tafakari hilo kwanza.
--------------------------------------------
On Sun, 9/6/15, 'Flano' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Siyo lazima kubadilisha chama ili
kuleta mabadiliko ya Maendeleo
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, September 6, 2015, 11:36 PM
Kwa Tanzania na tulipofikia noooo big
noooo impractical. ccm wameshindwa kufanya vzr miaka 54
unasema wabaki? haipogo
'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>
>-Nchi ambayo UKAWA wataleta mabadiliko kwa kuondoa
kodi zote kwa kuwa tuna gas, madini makaa ya mawe,
tanzanite, gold, almasi, mbuga za wanyama, ruby, no kodi.
>
>-Mishahara ya walimu haitokatwa kodi.
>
>-Mkulima ambaye mpaka achuke madaraka Oct 25 atakuwa
hajalipwa hela zake za mazao stakabadhi gharani atalipwa
mara 2. Kwa mfano wapo wakulima mia kila kijiji Tanzania
zidisha huyu milioni 20 mara mbili yule mil 30 mara 2 kama
fidia na hakuna kuwatoza kodi.
>
>-Kuukataa masikini na nyumba za nyasi ambapo nyumba za
kaya au maboma za aina ya manyata Monduli, manyara ni za
fito zilizokandikwa kwa udongo uliochanganywa na kinyesi
cha
ng'ombe na kuelekwa kwa nyasi lakini hazijaondolewa karne.
Kuukataa umasikini ambapo gender NGOs zinapambana na elimu
na ufuatiliaji kutokomeza ndoa za utotoni kuoza mtoto wa
miaka 12 kwa jibaba la miaka 60 ili wazazi wapate mifugo
ya
kulimbikiza. Wanafunzi kukosa uji shule mpaka kupata
misaada
ya World Food Progeam unga wa USAID ulaya ulilimwa
kulishia
mifugo. Leo hauondoi umasikini uliopo ndani ya utajiri wa
kulimbikiza mifugo iletayo land degradation, kukausha mito
lakini anaukataa umasikini kimaneno sio kimatendo jimboni
ambalo sio la mfano kitaifa ktk maendeleo wakati mbunge wa
miaka kenda plus anamwaga mindoo ya hela.
>
>-Urafiki na mama, baba ntilie na bodaboda-kaeni popote
mtakako hakuna wa kuwasumbua na kodi msitoe nchii tajiri
ni
CCM ndio wabadhirifu.
>-Mkulima lima na uuze mazao yako kokote utakako ndani
na
nje ya nchi hakuna masharti ya serikali. Kukukataza na
kukutoza kodi ni uonevu.
>
>Ama kweli kuleta maendeleo kwa sasa hakuhitaji
Economists. Rais mtarajiwa ameachwa kuongea haya ya
economists wapo hata kumshauri. Public health specialists
na
wanasheria wapo kusema Ruksa kila kitu kaa popote fanya
utakalo hakuna bugha wala kodi. Sio tu kipindupindu
kitamaliza watu, malori yatapata raha ya kukanyaga miili
ya
wafanyabiashara barabarani. Kihamo kutoka vijijini kuja
mijini kufanya biashara kitaongezeka. Ujenzi holela utapaa
300% plus kwani uhuru bila kuzingatia sheria ni ukichaa.
Misaada yetu toka nje ni kodi za walipakodi huko itokako.
kama hapa TZ matajiri waliopewa viwanda, mashamba
hawaendeshi; wanaziona sekta za uchumi wao wanauza soda za
rangi na kuingiza mitumba malori kwa malori na used
cars-hela ya kila kitu bure itatoka wapi iwapo local
investors wenyewe ni dhulumati katika kuendesha uchumi na
kulipa mishahara ni magumashi tu?
>
>Kuleta mabadiliko si lazima kubadilisha chama. Wote
tunahusuka wananchi, watumishi wa umma na makampuni
binafsi
y wabongo. Kufanya efficiently na effectively yale ya
wajibu
wetu bila udugu, ukabila, urafiti na tamaa ya kutajirika
haraka haraka bali kuzingatia wajibu wa kazi, sera,
mikakati
na sheria ya sekta husika.Tubadilike kiakili na kimatendo
tusitegemee vishuke kama mvua. Wanaoahidi vya
kusadikika-tusiwape kura. Hata kama nchi tajiri ina kila
kitu KODI lazima ikusanywe, ikatwe katika mauzo na
biashara
ili huduma za bure zipatikane. Bure ilikuwa wakati ule
China, Urusi, Scandinavian countries, UK inatulipia
wakitaka
aidha tuwe wajamaa (ujamaa-Socialism) au tuwe capitalists
wakipambara. Sasa ni liberal economy ili tujitegemee budi
tugharimie maendeleo yetu kwa juhudi zetu. Bure aghali!!
Budi uwe mtumwa wa mtu ndani au nje ya mnchi. Wagombea
wengine Tabula Rasa!!
>--------------------------------------------
>On Sun, 6/9/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>
> Subject: [wanabidii] Siyo lazima kubadilisha chama
ili
kuleta mabadiliko ya Maendeleo
> To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Sunday, 6 September, 2015, 22:28
>
>
>
> Siyo
> lazima kubadilisha chama ili kuleta
> mabadiliko ya Maendeleo
>
>
>
> Dhana ya
> baadhi ya sisi Wantania ya kwamba kuondoa Mfumo wa
utawala
> wa nchi ni lazima
> kubadilisha chama ili kuleta mabadiliko ya Maendeleo
ya
> Kiuchumi na maisha bora
> kwa kila mwanachi siyo sahihi. Dhana hii imekuwa
ikitolewa
> mfano wa Kenya na
> kwamba imeondoa tabaka la uongozi wa KANU.
>
>
>
> Kiuhalisia Kenya haijawahi kubadilisha mfumo wa
Utawala
ulio
> nje ya KANU. MWAI
> KIBAKI amekuwa ndani ya KANU tangu Kenya ilipopata
uhuru
> mpaka mwaka 2002
> alipogombea Urais kupitia National Alliance Rainbon
> Coalition NARC. Kabla ya
> hapo alikuwa Makamu wa Rais wa serikali ya KANU ya
Rais
> mstaafu DANIEL ARAP MOI.
> Rais mstaafu MWAI KIBAKI alidumu na NARC hadi 2005
ambapo
> alipokuwa akigombea
> kiti hichocha Urais 2007 alipolazimika kupitia chama
cha
> PNU( Party of National
> Unity).
>
> Pia ikumbukwe kwamba wakati MWAI
> KIBAKI akiwa
> Rais UHURU KENYATTA alikuwa mmoja wa viongozi ndani
ya
> serikali hiyo. Aidha
> viongozi wengine tofauti tofauti ambao ni KANU
kiundakindaki
> walikuwemo RAILA
> ODINGA . ODINGA ambaye hajawahi kuwa KANU.
>
>
>
> Mwaka 2013 UHURU KENYATTA alishinda uchaguzi kupitia
chama
> cha The National
> Alliance (TNA). Hivyo mlolongo huu wa uongozi
hauonyeshi
> moja kwa moja ya
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment