Thursday, 24 September 2015

Re: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] Tukumbushane: Ndoto Ya Seif Sharif Hamad Kuingia Ikulu Ya Zanzibar..

Kazi aliyoifanya DR Sheid kwa muda huu mfupi alioshika madaraka katika kuendeleza aliyoyaacha Abeid Aman Karume Rais wa Kwanza (Karume =Gadafi No 1 katika maendeleo ya wananchi) itamfanya Seif Sharrif Hamad awe na uzoefu mkubwa wa kugombea tena 2020.

--------------------------------------------
On Wed, 23/9/15, 'Nico M' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] Tukumbushane: Ndoto Ya Seif Sharif Hamad Kuingia Ikulu Ya Zanzibar..
To: Wanazuoni@yahoogroups.com, "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 23 September, 2015, 23:40

Safi
sana Maggid, 
Umepatia sana. Natumai umesoma kitabu cha .
G.Thomas Burgess - Race, Revolution, and the Struggle for
human rights in Zanzibar detailing the memoirs of Ali Sultan
Issa and Seif Sharif Hamad. Ukisoma section ya Maalim utaona
yote hayo. 
Asante kwa kumbukumbu hii. 
Nico Sent from Samsung
Mobile

-------- Original message --------From:
"Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com
[Wanazuoni]" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date:23/09/2015 23:17 (GMT+03:00)
To: mabadilikotanzania
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>,wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>,Wanazuoni@yahoogroups.com
Cc: Subject: [Wanazuoni]
Tukumbushane: Ndoto Ya Seif Sharif Hamad Kuingia Ikulu Ya
Zanzibar..

 










Ndugu zangu, Historia ni Mwalimu Mzuri.
Nimelisema hilo mara kadhaa. Nina bahati, ya tangu utotoni,
kupenda kufuatilia masuala ya kisiasa. Wakati fulani
mwaka 1984, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM zanzibar
walikutana pale Kisiwandui chini ya Alhaj Aboud Jumbe,
aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa JMT.
Ndani ya kikao kile walikuwamo wanasiasa wa aina ya Ramadhan
Haji Fakhi, huyu alikuwa Waziri Kiongozi, alikuwamo pia
Hamad Rashid, Hamis Shabaan Mloo, na Seif Sharif Hamad.
Wajumbe walizungumza jasho likiwatoka juu ya hali
isiyo sawa kwenye Muungano yakiwemo madai kuwa Zanzibar
haikuwa hata na fursa ya kukopa nje ya nchi kwa vile imo
ndani ya Muungano. Ikajengwa hoja ya Serikali Tatu.
Wajumbe wote wakaafiki. Ikafika siku ya kuwasilisha hoja
Dodoma. Ajabu ya jambo lile, Julius Nyerere,
alionekana kulijua hilo mapema sana. Alhaj Jumbe mkutanoni
Dodoma akawa na wakati mgumu. Wenzake wote akiwamo
Seif Sharif Hamad waliikana hoja isipokuwa Ramadhan Haji
Fakhi, Waziri Kiongozi. Inasemwa, Julius Nyerere
alimuuliza Ramadhan Haji Fakhi;
" Moja jumlisha moja ni ngapi?"
Jibu: " Tatu!" Inasemwa pia, Julius
Nyerere aliwachekesha wajumbe alipohoji ni shule gani
aliyesoma Ramadhan Haji Fakhi yenye kufundisha hesabu kwa
namna hiyo! Hatma ya kikao kile cha Dodoma ni Alhaj
Jumbe kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama ikiwamo
kuachia Urais wa zanzibar. Ramadhan Haji Fakhi pia
akunusurika, alikwenda na maji. Ali Hassan Mwinyi
akafanywa kuwa Rais wa Zanzibar na Seif Sharif Hamad akawa
Waziri Kiongozi. Mwaka mmoja na nusu baadae, mwaka
1985, Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano na akawa Rais kwa kuchaguliwa na
Wananchi. Inasemwa, kwa vile Ali Hassan Mwinyi
alipata fursa hiyo, basi, Seif Sharif Hamad alitumaini
angekuwa Rais wa Zanzibar. Hapana, CCM ikamteua
Idrissa Abdul Wakil kugombea nafasi ya Rais wa Zanzibar.
Seif Sharif Hamad akawa ameukosa Urais na akafanywa kuwa
Waziri Kiongozi. Kukawa na minong'ono ya Seif kulalamika
chini chini. Ikafika wakati kukawa na ' Hali ya
Hewa ya kisiasa Iliyochafuka Visiwani'. Nilikuwa
mwanafunzi pale Tambaza Sekondari. Ilinong'onwa mjini
kuwa Rais wa Zanzibar, Abdul Wakil, kutokana na hali ya hewa
kuchafuka, akawa anafanya kazi Unguja na anarudi kulala Dar
es Salaam. Siku moja wakati nikitoka shule na kupita
maeneo ya Upanga kuelekea kituo cha mabasi cha Palm Beach,
kwenye moja ya nyumba za eneo hilo, nikamwona kwa macho
yangu Rais wa Zanzibar, Idrissa Abdul Wakil. Nikafahamu
baadae, kuwa aliishi kwenye moja ya nyumba za eneo
hilo. Mwaka 1988, akina Seif Sharif Hamad , Hamad
Rashid na wenzao, walitaka hoja ya Serikali Tatu ipelekwe
tena Dodoma. Safari hii Idrissa Abdul Wakil aliipinga
kutokana na uzoefu wa 1984. Seif Sharif Hamad naye
akaishia kupokonywa kadi yake ya uanachama CCM. Vuguvugu la
mageuzi ya kisiasa duniani likaanza kwenye kipindi hicho.
Lilitokea Ulaya Mashariki. Ndipo akina Seif Sharif
Hamad wakapata fursa ya kuanzisha KAMAHURU. Na baadae CUF
ikaja pia. Na ndoto ya Seif Sharif Hamad ikabaki hai, ndoto
ya siku moja kuwa Rais wa Visiwa vya Zanzibar. Mwaka
huu wa 2015, Seif Sharif Hamad amerusha tena karata yake.
Anaweka rekodi, ya kuwa mgombea mkongwe kushinda wote, na
mwenye uzoefu wa kugombea Urais kwa zaidi ya miaka 20. Kuna
tunachojifunza. Ndugu zangu Wajumbe,
Nimejaribu kukumbuka nikiandika, na bila kusoma popote.
Nilipokosea nisahihisheni. Nakaribisha maoni yenu
pia... Maggid.






__._,_.___










Posted by: Maggid Mjengwa
<mjengwamaggid@gmail.com>







Reply
via web post




Reply to sender




Reply to group



Start a New
Topic



Messages in this
topic
(1)



















Visit Your Group



New Members
2







• Privacy • Unsubscribe • Terms of Use






















.







__,_._,___



















--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment