Surmendia,
Maswali yako pengine hayalingani sana na alichokuwa anakizungumzia mama Nkya, nilivyomwelewa mimi hakuwa na maana ya kuwagawa watu ni yupi ni mwananchi na nani siyo mwananchi. Kama hufahamu au umesahau labda nikukumbushe. Je, unafahamu jinsi sheria za nchi yetu zilivyo legelege inapokuja kushughulikia watu waliopo madarakani au vyombo vya usalama.
Kwa kipengele hicho tu bila shaka mawazo yako yatakukumbuka baadhi ya matukio ya kinyama yaliyofanya na vyombo vya kulinda usalama, moja wapo ni tukio la wafanya biashara waliouawa kinyama kwa agizo la wakuu na wakasingiziwa ni majambazi. Miaka siyo mingi mwandishi wa habari alipigwa bomu utadhani ni jasusi, na kama achukuliwa kama jasusi, basi ujasusi wake ulikuwa ni kuwekuwepo pahala akitaka kupata habari za matukio yanayotokea ili ujumbe uwafikie watu wengine ambao hawakuwepe kwenye eneo la matukio. Hayo ni baadhi tu ya kati mengi yanayofnana na hayo.
Kwa hayo machache wewe fikiria Rais akitoa ruhusa ya kuua, hufikirii kwa akili ya wa wetu walivyo wanaweza wakaua halafu wakasingia wameua jambazi? Kama umetoa uhuru inamaana hakuna hata haja ya uchunguzi wa ukweli wa tukio, mind! Mtu anaweza akauliwa na kuwekea silaha karibu yake wakasema alikuwa anatishia maisha yao kumbe ameuawa kwa sababu nyingine tu, kwa vile kuna loop hole ya ujambazi basi ikatolewa sababu hiyo?
Hakuna mtu anayeshabikia majambazi, ila tu kwa taarifa yako mimi , wewe au jamii zetu tunaweza siku moja tukakumbwa na balaa kamalo, usifikirie kisa hicho ni maalumu kwa ajili ya nani, tunaweza tukakumbwa na balaa kama hilo. Hivyo kauli isingelikuwa wild kiasi hicho, angelitumia kauli za kama vile dawa ya majambazi iko jikoni, nitakula chungu kimoja na majambazi, au kauli zingine ambazo zitaonyesha kuna uangalifu wa aina fulani ya utoaji kauli. Je unakumbuka pale Mrema alipowatoa pangoni majambazi wakanza kurudisha sila, je alirusha risasi au ni kauli yenye mbinu ya kumtoa nyoka pangoni?
Miaka kadhaa ya nyuma kidogo serikali ya Uingereza walitaka mapolisi wawe wanabeba bunduki wanapokuwa kwenye doria, kwa taarifa yako walikataa kata kata. Kisa ukibeba silaha kwa vile madui/majambazi kwa vile huishi kwa hofu saa zote, wanaweza wakawahi maasikari kabla hata hawajaamua kutumia silaha, maana yake unataka kuzima moto wa petrol kwa mafuta ya ndege. Kabla hata ya mahojiano majambazi wataanza kurusha risasi maana kwa nanma yoyote watakapowekwa nguvuni, atakuwa amepatikana.
On Friday, 25 September 2015, 20:15, Surumedia <majiydsuru@gmail.com> wrote:
Sijakuelewa vizuri dada Ananilea. Una maanisha kuwa polisi siyo wananchi? Una maana ya kuwa wanachama wa CCM siyo wananchi? Una maana kuwa viongozi siyo wananchi? Una maana kwamba wananchi ni majambazi? Nisaidie dada yangu!
..........................................................................
"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".
Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa

From: ananilea nkya ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]
Sent: 25/09/2015 17:57
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: WANA BIDII; Wanazuoni - Informal Network of Tanzanian Intellectuals
Subject: [Wanazuoni] MAGUFULI NA MAJAMBAZI [1 Attachment]
[Attachment(s) from ananilea nkya included below]
MAGUFULI NA MAJAMBAZI
Ananilea Nkya
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr John Magufuli akichaguliwa huenda nchi yetu ikashuhudia mapambano dhidi ya polisi na wananchi yakiongezeka kwa sababu serikali yake itaruhusu polisi kuuwa wananchi kwa kisingizio cha ujambazi.
Dr Magufuli katika kampeni zake kwenye uwanja wa Mashujaa mkoni Mtwara 02 Septemba 2015 alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa serikali yake haitamshitaki polisi yoyote atakayemuua jambazi mwenye silaha.
Dr Magufuli alikaririrwa akisema ''serikali yangu askari akipiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona hawavamii kambi za jeshi, jeshi la kujenga taifa au Ukonga FFU maana polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua''.
Wapiga kura wanajiuliza, kama kabla hajachaguliwa Dr Magufuli anaanza kuwaweka wananchi roho juu kiasi hiki, je akichaguliwa mapambano kati ya wananchi na vyombo vya dola yataongezeka kiasi gani?
Wananchi wanauliza swali hili kwa sababu ingawa hivi sasa hakuna polisi anayeruhusiwa kuhukumu watuhumiwa wa makosa mbali mbali ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa ujambazi, lakini umma umeshuhudia polisi wakiwauwa watu hovyo hovyo kwa tuhuma za ujambazi.
Wanauliza je Dr Magufuli akichaguliwa na polisi wakiruhusiwa rasmi kuwauwa watuhumiwa wa ujambazi—ni wananchi wangapi wasio na hatia watakaosukiwa zengwe la ujambazi na kuishia kuuwawa kikatili na polisi?
Hivi Magufuli ambaye amekuwa kiongozi wa serikali kwa zaidi ya mika 20 hajui kwamba polisi siyo mahakama na kwamba polisi haipaswi kutoa hukumu ya kifo kwa raia?
Wakati mgombea Dr Magufuli akitoa ahadi kwamba kwenye serikali yake polisi ndio watakaotoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa wa ujambazi; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa ni mahakama kuu ndiyo yenye mamlaha ya kutoa hukumu ya kifo.
Zaidi wananchi wanajiuliza, nchi itakuwa katika hatari kubwa kiasi gani Dr Magufuli akichaguliwa ambapo ataruhusu polisi kujichukulia sheria mkononi kuwauwa wananchi ambao pengine maisha magumu yametumbukiza kwenye ujambazi?
Lakini pia wananchi wanajiuliza je Dr Magufuli uchambuzi wake wa masuala ya kijamii umempa jibu kwamba polisi wakiwauwa ''majambazi wenye silaha'' ndio utakuwa mwisho wa mapambano kati ya wananchi na polisi?
Pengine Dr Magufuli anapaswa kujielimisha kujua kuwa chanzo cha ujambazi siyo wananchi na wala siyo polisi. Kadhalika chanzo cha mapambano katika ya polisi na wananchi siyo polisi wala wananchi
Dr Magufuli anapaswa mapambano kati ya polisi na wananchi wa ni kiashiria kimoja cha kuonyesha athari ya mfumo wa serikali ya CCM wa kutajirisha watawala na kufukarisha wananchi wengi.
Anapaswa kufahamu kwamba CCM baada ya kulitupa Azimiao la Arusha bila kuweka mbadala wake katika zama hizi mpya za utandawazi wizi ambapo mfumo wa uchumi unaotamba duniani baada ya ukomunisti kufa ni wa upebari ambao unaruhusu mtu uwezo wa kupata apate hata kama kwa wizi na wa kukosa afie mbali.
Matokeo yake sasa nchi yetu Tanzania ina kikundi kidogo cha watawala waliotajirika vya kutisha kwa kujigawia kibepari fedha za wananchi na mali za nchi (kutumia ujambazi wa kalamu na sheria) huku mamilioni ya wananchi wakiwepo polisi ambao hali zao za maisha ni mbaya wakitumia mbinu mbali mbali safi na chafu ukiwepo ujambazi ili maisha yaende.
Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu. Lakini cha kushangaza ni kwamba Dr Magufuli hajui kwamba hata pale mamilioni ya wananchi walipotaka kuisaidia nchi kuondoa mfumo huu wa utawala unaozalisha makundi mengi ya kihalifu katika jamii—majambazi, panya road, wezi wa kutumia kalamu na sheria na kadhalika, CCM na serikali yake walikataa.
Wananchi walipendekeza Katiba Mpya CCM na serikali yake ikakataa kata kata na kuyazika maoni hayo pale Dodoma tena kwa mbwembwe na kutukana wananchi mwaka 2014.
Kiburi na jeuri ya watawala wa serikali ya CCM kukataa ushauri wa wananchi kutengeneza Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ili kupunguza pengo la utajiri kati ya watawala na wananchi ndiyo sababu ya wananchi kuikataa CCM hata kama CCM itafanya propaganda na ufisadi kuonyesha inapendwa.
Tena wananchi wanajua kuwa Dr Magufuli akichaguliwa kuwa Rais maana yake ni kwamba serikali ya CCM kuendelea kuwa madarakani na hivyo ujambazi hautakwisha kwa kuuwa majambazi.
Badala yake amani ya nchi itawekwa rehani kwa sababu kwa polisi kuua majambazi—hasira ya wananchi itaongezeka siyo tu dhidi ya polisi bali dhidi ya kila chombo ambacho serikali itakitumia kudhibiti umma unaotamani madadiliko ya mfumo wa uongozi unaowafanya wananchi kuwa maskini na kudhalilishwa na vyombo vinavyopaswa kuwalinda raia.
Kwa hiyo vema CCM wakati huu wa kampeni isijidanganye, iwe ni kwa kutumia tafiti za kimkakati ama propaganda nyingine zozote kuwa wanakubalika kwa mamilioni ya wananchi wanaoteseka kwa umaskini na hivyo eti watashinda uchaguzi.
CCM na mgombea wao wa Urais Dr Magufuli wanapaswa kuwa na miwani itakayowaelekeza kuona kuwa kitendo cha wananchi wenye silaha (majambazi) kuvamia kituo cha polisi na kuuwa polisi, ni ishara tosha ya amani kutoweka nchini –maana ni mwanzo wa vita kati ya wananchi na polisi—kati ya wananchi na serikali yao.
Hii ni ishara tosha kwamba wananchi wameichoka serikali ya CCM iwe inaongozwa na Dr Magufuli au mwanamuziki maarufu nchini Diamond au mwana CCM yeyote mwingine atakayedhaniwa ni kivutio kwa wananchi.
Kadhalika CCM wanapaswa kufahamu kuwa kwa wananchi wengi kushabikia upinzani ni ishara nyingine tosha kwamba wananchi wameichoka CCM na serikali yake. Hivyo suluhisho siyo kuuwa upinzani, bali nchi kuweka mfumo mpya wa utawala ambao misingi yake wananchi wamependekeza kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.
Kwa hiyo kama kweli CCM na serikali yake wanaitakia mema Tanzania yetu ---hasa amani ya kweli unaotokana na wananchi wengi kuridhika na maisha badala ya viongozi peke yake kuwa matajiri wa kukufuru, ni vema na ni muhimu sana wakaheshimu maamuzi ya wananchi watakayoyafanya kupitia sanduku huru la kura hapo tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015. Mungu ibariki Tanzania.
Note: Ninaruhusu yeyote mwenye kutaka kuisambaza, kuichapisha Makala hii afanye hivyo. Lengo sote tushiriki kuijenga Tanzania yetu.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

__._,_.___
Attachment(s) from ananilea nkya | View attachments on the web
1 of 1 File(s)
Posted by: ananilea nkya <ananilea_nkya@yahoo.com>
| Reply via web post | • | Reply to sender | • | Reply to group | • | Start a New Topic | • | Messages in this topic (1) |
.
__,_._,___
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment